Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya Octoba 22
Rais Magufuli Aweka Jiwe La Msingi Mradi Wa Hosteli Za Wanafunzi Katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
21 Oktoba, 2016 ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa mabweni
20 ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 3,840 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mwezi Juni
mwaka huu wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa
ya chuo hicho.
Wakati
Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi la mradi huo, tayari ujenzi
umefikia asilimia 75 ambapo majengo 20 yaliyounganishwa kimuundo
yamefikia ghorofa ya nne na ujenzi huo unaofanywa na Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Desemba, 2016.
Akizungumza
kabla ya kuweka jiwe la msingi Rais Magufuli aliyeambatana na Mkewe
Mama Janeth Magufuli ameipongeza TBA na wadau wote wanaoshiriki katika
ujenzi huo zikiwemo Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa hatua kubwa ya ujenzi iliyofikiwa
tangu ujenzi uanze tarehe 01 Julai, 2016 na amebainisha kuwa kwa kutumia
TBA mradi huo utatumia kiasi kidogo cha fedha.
"Nawapongeza
sana TBA kwa kazi nzuri mliyoifanya mpaka sasa, mradi huu utatumia
Shilingi Bilioni 10 tu, Wakandarasi kutoka nje walitaka kujenga mabweni
haya ya wanafunzi kwa Shilingi Bilioni 100, sasa mtaona wenyewe tumeokoa
Shilingi ngapi" amesema Rais Magufuli.
Aidha,
Rais Magufuli ameahidi kuwa, kwa kuwa majengo hayo yanauwezo wa kubeba
ghorofa sita, Serikali itafanya utaratibu wa kutumia moja ya likizo za
wanafunzi kuongeza ghorofa nyingine mbili ili kuwawezesha wanafunzi
wengi zaidi kupata nafasi.
Kuhusu
mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Dkt. Magufuli amesema Serikali
imetenga Shilingi Bilioni 483 kwa mwaka huu ambapo wanafunzi takribani
93,000 wanaoendelea na masomo na wanafunzi takribani 25,000 watakaoanza
masomo watapatiwa mikopo lakini ameweka bayana kuwa mikopo hiyo
itatolewa kwa wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia masikini.
Rais
Magufuli ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kurekebisha
dosari zilizopo katika mfumo wa utoaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na
upangaji mbaya wa wanafunzi katika vyuo, kutoa mikopo kwa upendeleo,
kutozingatia sifa za mkopaji, kutoa mikopo hewa na kufungua vyuo kabla
ya mikopo ya wanafunzi kutolewa na pia amewaonya wanafunzi kujiepusha na
vitendo visivyofaa wakati Serikali inarekebisha dosari hizo.
"Na
ndio maana wakati mwingine na wabaya wanapitia humo humo, mara fanye
hivi fanyeni vile, wakati wanajua kuwa mkifanya yasiyofaa Serikali
itawafukuza tu ili mkafanyie mambo yenu huko.
"Kwa
sababu huwezi kuwa unahangaika kutafuta fedha za kuwapa mikopo, wakati
huo huo unahitaji kujenga reli, wakati huo huo unahitaji kujenga
barabara, wakati huo huo unahitaji kulipa mishahara, wakati huo huo
unahitaji kutoa elimu bure, wakati huo huo Karagwe kuna njaa, wakati huo
huo watu wanahitaji dawa hospitali, halafu watu wengine wanataka
kukuendesha kana kwamba hela unayokusanya ni kwa ajili yao tu, ni lazima
tuelewane na mimi ninataka kuwaeleza kwa dhati lazima twende katika
njia iliyonyooka, ni bora uwe Rais usiye maarufu lakini utimize
uliyoyaahidi, asitokee mtu wa kukuendesha, ninajua mmenielewa"
amesisitiza Dkt. Magufuli.
Dkt.
Magufuli ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kujipanga
vizuri kukusanya marejesho ya mikopo kwa wote waliokopeshwa na bodi hiyo
ambapo mpaka sasa bodi inadai takribani Shilingi Trilioni 2.6.
Awali
akitoa taarifa ya mradi huo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Prof. Rwekaza Mukandala amesema wakati ujenzi huo ukiendelea chuo
kimetenga Shilingi Bilioni 4.5 kutoka kwenye mapato yake kwa ajili ya
kununua samani ikiwa ni pamoja na vitanda vya wanafunzi na pia Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia itashughulikia ujenzi wa uzio, jiko na
bwalo la chakula.
Hafla
ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imehudhuriwa na viongozi mbalimbali
wakiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako,
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Wabunge, Makatibu Wakuu na Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
21 Oktoba, 2016
Rais Magufuli aagiza HESLB kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni.
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli ameagiza Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutumia Sheria zilizopo kuongeza
kasi ya ukusanyaji wa madeni kwa wahitimu walionufaika na mikopo.
Rais
Magufuli ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akiweka jiwe
la msingi la mradi wa ujenzi wa hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam unajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa
gharama ya shilingi bilioni 10.
Amesema kuwa Serikali inadai takribani shilingi trilioni 2.6 kwa wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu.
“Serikali
inawadai wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu takribani
shilingi trillion 2.6 ambazo wanatakiwa kuzirudisha ili ziweze kutolewa
kama mikopo kwa wanafunzi wapya na waliopo vyuoni” alifafanua Dkt Magufuli.
Aidha
Dkt. Magufuli ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo
ya Ufundi kusimamia ipasavyo suala la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi kwa
kuzingatia vigezo vilivyopo kwani lengo la mikopo hiyo inawalenga
watoto maskini.
Alisema
kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko ya kuwa Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu inafanya zoezi la ugawaji wa mikopo hiyo kwa
upendeleo hivyo kuzitaka uongozi wa Wizara kushughulikia suala hilo.
Mbali
na hayo Rais Magufuli amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutimia mikopo
hilo kwa malengo mazuri katika kujinufaisha na masuala ya Elimu.
Naye
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce
Ndalichako alisema kuwa mradi wa ujenzi wa hosteli hizo utasaidia
kuwahudumia wanafunzi 3,840 ambapo unatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi
Desemba 2016.
Katika
hatua hiyo Prof. Ndalichako alisema kuwa wanafunzi waliodahuiliwa kwa
mwaka huu wapo 58,000 hivyo suala la wanafunzi 66,000 kukosa mikopo hiyo
ni upotoshaji unaofanya na baadhi wa watu.
Mradi
wa Ujenzi wa Hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wenye majengo 20 kila jengo gorofa nne zenye vyumba 12 unatarajiwa
kukamilika mwishoni mwa Desemba mwaka huu.
Alichosema Rais Magufuli kuhusu mikopo ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu
Rais
wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema Serikali imetenga Shilingi
Bilioni 483 kwa mwaka huu kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu ambapo
wanafunzi zaidi ya 118,000 watanufaika.
Akizungumza
katika uwekaji wa jiwe la msingi la hostel za Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam leo, Rais Magufuli amesema miongoni mwa hao watakaonufaika,
wanafunzi 93,000 ni wanaoendelea na masomo na wanafunzi takribani 25,000
ni watakaoanza masomo mwaka huu huku akiweka bayana kuwa mikopo hiyo
itatolewa kwa wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia masikini.
Rais
Magufuli ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kurekebisha
dosari zilizopo katika mfumo wa utoaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na
upangaji mbaya wa wanafunzi katika vyuo, kutoa mikopo kwa upendeleo,
kutozingatia sifa za mkopaji, kutoa mikopo hewa na kufungua vyuo kabla
ya mikopo ya wanafunzi kutolewa na pia amewaonya wanafunzi kujiepusha na
vitendo visivyofaa wakati Serikali inarekebisha dosari hizo.
"Na
ndio maana wakati mwingine na wabaya wanapitia humo humo, mara fanye
hivi fanyeni vile, wakati wanajua kuwa mkifanya yasiyofaa Serikali
itawafukuza tu ili mkafanyie mambo yenu huko.
"Kwa
sababu huwezi kuwa unahangaika kutafuta fedha za kuwapa mikopo, wakati
huo huo unahitaji kujenga reli, wakati huo huo unahitaji kujenga
barabara, wakati huo huo unahitaji kulipa mishahara, wakati huo huo
unahitaji kutoa elimu bure, wakati huo huo Karagwe kuna njaa, wakati huo
huo watu wanahitaji dawa hospitali, halafu watu wengine wanataka
kukuendesha kana kwamba hela unayokusanya ni kwa ajili yao tu, ni lazima
tuelewane na mimi ninataka kuwaeleza kwa dhati lazima twende katika
njia iliyonyooka, ni bora uwe Rais usiye maarufu lakini utimize
uliyoyaahidi, asitokee mtu wa kukuendesha, ninajua mmenielewa" amesisitiza Dkt. Magufuli.
Dkt.
Magufuli ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kujipanga
vizuri kukusanya marejesho ya mikopo kwa wote waliokopeshwa na bodi hiyo
ambapo mpaka sasa bodi inadai takribani Shilingi Trilioni 2.6.
HABARI ZA KIMATAIFAAAA
Habari
| 22.10.2016 | 06:03
Watu 55 wamefariki dunia na wengine takriban 600 wamejeruhiwa baada
ya treni iliyokuwa imejaa watu imeanguka nchini Cameroon hapo jana
ilipokuwa ikisafiri kutoka mji mkuu Yaounde kuelekea mjini Douala.
Waziri wa uchukuzi wa Cameroon Edgar Alain Mebe Ngo'oo amesema mabehewa
kadhaa ya treni hiyo iliyokuwa imejaa watu yaling'oka kutoka njia ya
reli muda mfupi kabla ya kufika katika mji wa Eseka. Watu wengi
walilazimika kutumia usafiri wa treni hiyo kuelekea Douala baada ya mvua
kubwa iliyonyesha usiku wa Alhamisi kusomba daraja muhimu na kukatiza
usafiri wa magari. Kilichosababisha ajali hiyo bado hakijabainika lakini
duru zinaarifu kuwa mabehewa zaidi yaliongezwa kwenye treni hiyo ili
kubeba abiria zaidi. Baadhi ya waliojeruhiwa wako katika hali mahututi.
Uchunguzi wa kimataifa umegundua kuwa majeshi ya serikali ya Syria
ndiyo yaliyohusika katika shambulizi la tatu la silaha za sumu. Hayo ni
kulingana na ripoti ya nne ya faragha iliyowasilishwa kwa Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana baada ya uchunguzi uliodumu kwa
miezi 13.Wataalamu wa Umoja wa Mataifa na wa shirika linalodhibiti na
kupiga marufuku silaha za sumu OPCW wanavilaumu vikosi vya jeshi la
Syria kwa kutumia gesi ya sumu katika mji wa Qmenas katika jimbo la
Idlib mnano mwezi Machi mwaka jana. Jeshi hilo pia linashutumiwa kwa
kutumia sumu katika miji ya Talmenes na Sarmin katika nyakati tofauti.
Wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS
pia wanashutumiwa kwa kutumia gesi aina ya mustard katika vita
vinavyoendelea Syria.
Jumuiya ya kujihami ya NATO imemteua Arndt Freytag von Loringhoven
aliyekuwa naibu wa mkuu wa shirika la ujasusi la Ujerumani kuwa mkuu wa
kwanza wa ujasusi wa NATO. Freytag von Loringhoven atakiongoza kikosi
kilichopewa jukumu la kuratibu shughuli za kijasusi za nchi wanachama wa
NATO ili kufuatilia kwa karibu shughuli za kijeshi za Urusi na
kuimarisha juhudi za kupambana na ugaidi. Freytag von Loringhoven mwenye
umri wa miaka 59 hivi sasa ni balozi wa Ujerumani katika Jamhuri ya
Czech na anatarajiwa kuacha wadhifa huo mwishoni mwa mwaka huu.
Chama kikuu cha upinzani katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
kimekatalia mbali makubaliano yaliyotiwa saini Jumanne wiki hii ambayo
yatamruhusu Rais Joseph Kabila kusalia madarakani hadi 2018 kwa
kuahirishwa chaguzi kuu zilizokuwa zifanyike mwezi ujao hadi mwezi April
2018. Chama cha UDPS kikiongozwa na Etienne Tshisekedi kimesema
kinakataa vikali mpango huo ambao kimeutaja kuwa ni ukiukaji mkubwa wa
katiba.Siku ya Jumanne, viongozi wa makundi yaliyokuwa yakishiriki
mdahalo wa kitaifa walitia saini makubaliano ya kurasa 24 mjini Kinshasa
yanayomruhusu Rais Kabila kusalia madarakani wakati ambapo chaguzi
zimeahirishwa. Kanisa Katoliki Congo limesema makubaliano yoyote kuhusu
uchaguzi wa rais sharti yaeleze bayana kuwa Kabila hatagombea muhula wa
tatu madarakani. Kiongozi huyo alipaswa kuachia madaraka mwezi Desemba
mwaka huu baada ya mihula miwili madarakani kuambatana na katiba ya nchi
hiyo.
Uchunguzi mpya wa maoni umeonya kuwa asilimia hamsini ya Warepublican
nchini Marekani watakubali ushindi wa mgombea urais wa chama cha
Democratic Hillary Clinton huku asilimia 70 ya wapiga kura wa Republican
wakisema iwapo atashinda uchaguzi wa urais itakuwa ni kutokana na wizi
wa kura.Asilimia 70 ya wapiga kura wa Democrats wamesema watakubali
ushindi wa mgombea urais wa Republican Donald Trump. Uchunguzi huo wa
maoni uliotolewa jana na shirika la habari la Reuters na shirika
linaloendesha uchunguzi wa maoni la Ipsos ni kufuatia madai ya mara kwa
mara ya Trump kuwa vyombo vya habari na mfumo wa uchaguzi nchini
Marekani vina njama ya kufanya udanganyifu wa kura ili kumwangusha.Trump
amesema atakubali matokeo ya uchaguzi iwapo tu ataibuka mshindi. Kwa
upande wake Bi Clinton amesema atakubali matokeo jinsi yatakavyokuwa.
Uchaguzi mkuu unatarajiwa tarehe 8 Novemba.
Sudan imeyahimiza mataifa zaidi ya Afrika yaliyo wanachama wa mkataba
wa Roma unaounda mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu
wa kivita ICC kujiondoa kutoka mahakama hiyo ikisisitiza kuwa ICC ni
chombo cha kikoloni kinachowaandama tu viongozi wa Kiafrika.Hapo jana
Afrika Kusini ilitangaza inajiondoa kutoka ICC baada ya kushutumiwa
vikali mwaka jana kwa kutomkamata Rais wa Sudan Omar al Bashir
anayetafutwa na ICC kujibu mashitaka ya mauaji ya halaiki na uhalifu wa
kivita katika jimbo la Darfur. Uamuzi huo wa Afrika Kusini unafuatia ule
wa Burundi ambayo pia imetangaza rasmi inajiondoa kutoka ICC.Burundi
pia imeisifu Afrika Kusini kwa uamuzi wake na kuongeza inatarajia nchi
zaidi kujiondoa. Marekani imesema inatiwa wasiwasi na uamuzi huo wa
Afrika Kusini wa kutaka kujiondoa ICC. Kenya na Namibia pia zimeelezea
nia ya kutaka kujiondoa kama wanachama wa mkataba wa Roma. Mashirika ya
kutetea haki za binadamu yamelaani uamuzi huo. Kati ya kesi 10
zilizochunguzwa na ICC tangu 2002, tisa ni dhidi ya mataifa ya Afrika.
Askari nchini Ufaransa wamefanya mgomo katika mji mkuu wa nchi hiyo
Paris wakidai hawana silaha za kutosha hata za kujihami na kiasi cha
askari 3,000 waliandamana usiku wa Alhamisi. Mamia ya polisi hao
waliandamana pia hapo jana usiku karibu na makao makuu ya polisi ya
Paris, mijini Calais, Lille, Toulon na miji mingine.Akizungumza mjini
Brussels baada ya mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya Rais
wa Ufaransa Francois Hollande amesema atakutana na wawakilishi wa askari
hao ofisini mwake mapema wiki ijayo kusikia malalamiko yao.
Kilichochochea maandamano hayo ni tukio lililotokea katika mji mmoja
ulio karibu na Paris mapema mwezi huu ambapo genge la wahalifu
waliwashambulia askari wanne kwa bomu la kutengezwa na petroli
walipokuwa wakishika doria.
HABRI ZA KIMICHEZOOO .
Na katika michezo, Hamburg SV ilicharazwa mabao 3-0 na Eintracht
Frankfurt katika mechi ya kandanda la ligi kuu ya hapa Ujerumani
Bundesliga iliyosakatwa jana usiku. Hamburg ilijipata pabaya baada ya
mchezaji wake Lewis Holtby kujifunga na kuipa Eintracht Frankfurt bao la
kwanza katika dakika ya 35. Kisha katika kipindi cha pili Shani
Tarashaj na Haris Seferovic wakahakikisha kuwa pointi tatu zinaelekea
Frankfurt.Hamburg haijashinda mechi yoyote msimu huu na mashabiki
waliwazomea kwa kuonyesha mchezo dhaifu hapo jana. Katika mechi ya leo
kati ya Bayern Munich na Borussia Moenchengladbach, Mshambuliaji wa
Bayern Frank Ribberry ndiye mchezaji pekee atakayekosa kucheza kutokana
na maumivu ya misuli.
MWEZI
JULAI, FC Barcelona ilitangaza kuwa Neymar amekubali Dili mpya ya Miaka
Mitano na Jana Mabingwa hao wa Spain wamethibitisha kuwa ameshaini.
Jana
Klabu ya Barcelona iliposti kwenye Mtandao wa Twitter Picha ya Mbrazil
huyo na Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu, wakipeana mikono
kuthibitisha Dili imekamilika.
Neymar, akiongea na Barça TV, alisema anasikia furaha kubwa kwa kusaini Mkataba mpya kwani anajisikia yuko Nyumbani.
Alisema:
“Kabla sijaja Barcelona nilijua ni Klabu kubwa na ina Wachezaji wazuri
sana na hilo lilinipa wasiwasi. Lakini nilipofika tu nikagundua ni Watu
wema na hilo lilinigusa moyoni na kunisaidia kujisikia Nyumbani!”
++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
- Neymar amefunga Mabao 91 katika Mechi 150 tangu 2013.
++++++++++++++++++++++
Mwezi
Julai Barca ilithibitisha kuwa kwenye Mkataba huu Mpya na Neymar, ikiwa
Klabu nyingine itataka kumnunua katika Mwaka wa Kwanza wa Mkataba huo
basi itapaswa kulipa Euro Milioni 200, Mwaka wa Pili wa Mkataba Dau ni
Euro Milioni 222 na kwa Miaka Mitatu iliyobaki kwenye Mkataba Dau
litakuwa Euro Milioni 250.
Neymar
alijiunga na Barca kutoka Santos ya Brazil Mwaka 2013 kwa Mkataba wa
Miaka Mitano na kuweza kutwaa Ubingwa wa La Liga mara 2, Copa del Rey
mara 2 na UEFA CHAMPIONZ LIGI 1.
>CONTE: ‘APOKEWE VYEMA, AMEANDIKA STORI YA KLABU HII!’
>MOU: ‘TUKIFUNGA SITASHANGILIA KAMA MTOTO MWEHU!’
JUMAPILI,
Stamford Bridge Jijini London itakuwepo Mechi ya EPL, Ligi Kuu England
kati ya Wenyeji Chelsea na Manchester United na, mbali ya kuwa ni Mechi
ya Timu zinazovutana na kuleta msisimko kila Msimu, safari hii mvuto
mkubwa ni kurejea kwa mara ya kwanza Uwanjani hapo kwa Jose Mourinho.
Jose
Mourinho alikuwa Meneja wa Chelsea kwa vipindi viwili tofauti na
kutimuliwa Desemba 2015 na kisha, kabla Msimu huu kuanza, kujiunga na
Man United.
Hivi sasa Chelsea ipo chini ya Meneja Mpya kutoka Italy, Antonio Conte, ambae nae alishika hatamu kabla Msimu huu kuanza.
Akiongea kuhusu Mechi yao ya Jumapili, Conte, amewataka Wadau wa Stamford Bridge kumpokea vizuri Jose Mourinho.
Conte
ameeleza: “Namuheshimu sana. Alitwaa Ubingwa mara 3 hapa na ni Mtu
muhimu kwa Klabu hii. Anastahili kupokewa vyema kwa sababu aliandika
Stori ya Klabu hii, sehemu ya Historia ya Klabu hii!”
Kwa
Mourinho, hii itakuwa mara ya pili kwake kutua Stamford Bridge kama
Meneja wa Timu pinzani baada ya Mwaka 2010 kutua na Inter Milan na
kushinda.
++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-MOURINHO alikaa Chelsea kwa Vipindi Viwili kama Meneja, Miaka ya 2004-2007 na 2013-2015.
++++++++++++++++++++++
Mwenyewe Jose Mourinho amesema ‘hatashangilia kama Mtoto mwehu’ ikiwa Timu yake itafunga bao dhidi ya Chelsea.
Pia Mourinho amesema hatafanya lolote ikiwa Mashabiki Uwanjani watampokea kwa kumpinga.
Mbali
ya mvuto huu wa Mourinho, Mechi hii ni muhimu mno kwa Klabu zote mbili
ambapo, baada ya Mechi 8, Chelsea wapo Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 16
na Man United wapo Nafasi ya 7 wakiwa na Pointi 14.
Vinara
wa EPL ni Man City, ambao wamefungana na Arsenal, na wana Pointi 19 na
hivyo ushindi kwa Chelsea au Man United ni muhimu mno ikiwa watataka
kutotupwa mbali toka mbio za Ubingwa hasa kwa vile Msimu uliopita Klabu
zote 2 hazikuwemo 4 Bora.
EPL - LIGI KUU ENGLAND
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 22
1430 Bournemouth v Tottenham
1700 Arsenal v Middlesbrough
1700 Burnley v Everton
1700 Hull v Stoke
1700 Leicester v Crystal Palace
1700 Swansea v Watford
1700 West Ham v Sunderland
1930 Liverpool v West Brom
Jumapili Oktoba 23
1530 Man City v Southampton
1800 Chelsea v Man United
RIPOTI SPESHO
MWENYEKITI
wa Yanga, Yusuf Manji, ameeleza kuwa Wapinzani wote wa mchakato wa
Yanga kukodishwa kwa Kampuni ya Yanga Yetu Limited kwa Miaka 10
wanakaribishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Dharura utakaofanyika Jumapili
Oktoba 23 Uwanja wa Kaunda, Makao Makuu ya Yanga, Jijini Dar es Salaam.
Akiongea
na Wanahabari hapo Jana kwenye Makao Makuu ya Yanga, Mtaa wa Twiga na
Jangwani Jijini Dar es Salaam, Manji amemwelezea Mpinzani Mkuu wa azma
ya Yanga kukodishwa, Mzee Ibrahim Akilimali, kuwa ashapoteza haki ya
kuwa Mwanachama wa Yanga kwa vile alikuwa hajalipia Ada ya Uanachama kwa
Miezi 6 iliyopita.
Manji
amemshauri Mzee Akilimali akitaka kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Jumapili
basi atapaswa kurudi kwenye Tawi lake kuomba upya Uanachama.
Vile
vile, Mwenyekiti Manji amewakaribisha Wapinzani wote wa Yanga
kukodishwa wahudhurie Mkutano Mkuu na kutoa michango yao wakihakikishiwa
ulinzi badala ya kupayuka kwenye Vyombo vya Habari.
Manji
pia alidokeza mipango yake ya maendeleo kwa Yanga na kudokeza kuwa
Uwanja wa Gezaulole huko Kigamboni utakuwa ni wa Mazoezi na Gym wakati
Uwanja wa Kisasa wa kuchezea Mechi utajengwa hapo hapo Jangwani kwenye
Makao Makuu ya Yanga.
WAKATI
HUO HUO, Mdau mmoja mkubwa wa Yanga amedai kuwa wanaopinga Mabadiliko
ndani ya Yanga ni ‘Wapumbavu na Malofa tu’ ambao ni wanyonyaji wa Yanga
badala ya wao kuisaidia Yanga kukua na kujitegemea.
Mdau
huyo amedai zama za Klabu kubwa kutegemea kuzungushwa Kofia kwa
Wanachama na Wadhamini ili kujiendesha zimepitwa na wakati na sasa Watu
wajipange upya kuendesha Klabu kisasa, kitaaluma na kibiashara kwa
ufanisi mkubwa.
++++++++++++++++++++++++++++++++++
AJENDA ZA MKUTANO MKUU WA DHARURA, Oktoba 23:
1. SALA NA UTAMBULISHO WA WAGENI WAALIKWA:
1.1. Sala ya Wakristo ya Kubariki Kikao.
1.2. Sala ya Waislamu ya Kubariki Kikao.
1.3.
Utambulisho wa wageni waalikwa waliohudhuria, pia wenye udhuru – Waziri
wa Michezo na Sanaa; Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT), Mwenyekiti
wa Chama Cha Mpira wa Miguu Dar-Es-Salaam (DRFA) na Rais wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
2. KUFUNGUA KIKAO
3. KUPITIA DONDOO ZA KIKAO KILICHOPITA CHA MKUTANO WA WANACHAMA NA KUIDHINISHA.
4. KUTHIBITISHA WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI NA KUMPUMZISHA MJUMBE MMOJA NA
kuongeza mjumbe mwingine kwenye baraza la wadhamini. mwenyekiti kuomba
ridhaa ya kumteua mjumbe mmoja bila ya kuitisha mkutano mkuu kupunguza
gharama kwaklabu.
5. KUPITIA NA KUJADILL MUHTASARI YA MAKUBALIANO YA BODI YA WADHAMINI
kulingana na maagizo ya wanachamakukodisha timu ya Yanga na nembo ya
Yanga kwa kipindi cha miaka kumi na kupata maamuzi kupitia kura za
wanachama.
6. KUJADILI MWEYEKITI ABAKI KAMA MWENYEKITI AU
kulingana na maslahi yake kwenye kampuni, kama italeta mgongano katika
kampuni yake inayokodisha timu ya Yanga na nembo ya Yanga kwa kipindi
cha miaka kumi ili kupata maamuzi kupitia kura za wanachama.
7. KURUDIA KUPITIA MAREKEBISHO YA KATIBA ILIYOAGIZWA NA WANACHAMA KUPITIA VIKAO VYAO MBALIMBALI
na baadhi kukataliwa na TFF, baadhi hazijasajiliwa kazi na BMT na
baadhi RITA wamezikalia bila kuzifanyia kazi kwa sababu zisizojulikana
kupata msimamo wa Wanachama kwa kuzingatia katiba ya Yanga inayosema
mikutano ya wanachama ndio yenye mamlaka ya mwisho ilimradi tu maamuzi
hayo yaangukie ndani ya sheria za nchi na si sahihi vyombo hivyo
kuingiliaa maamuzi halali ya wanachama.
8.
KUPITIA UTENDAJI WA KAMATI YA MASHINDANO, RATIBA YA LIGI KUU BARA,
ADHABU YA YANGA KUTOKA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
AMBAYO ILISABABISHWA NA FUJO ZA MASHABIKI WA SIMBA.
9.
KUPATA MAAMUZI JUU YA WANACHAMA AMBAO HAWAFIKI KATIKA MIKUTANO BADALA
YAKE WANAKUWA WASEMAJI WA YANGA BILA KUWA NA MAMLAKA HAYO na kuleta uchonganishi wa wazi ndani ya klabu, kupotsoha jamii nakuchafua majina ya viongozi wa klabu.
10. TAREHE YA UCHAGUZI MDOGO KUJAZIA NAFASI ZILIZO WAZI
na kupata mwongozo wakutumia katiba ipi kati ya 2010 au 2014.pamojana
masahihisho baada ya 2014, au bila ya masahihisho ya 2014 yaliyoamuliwa
na wanachama.
11. HOTUBA YA MWENYEKITI –maoni
na msimamo wake juu ya maazimio ya wanachama kwenye kikao; kusema
anayoyajua ya siri kuhusu yanga na adui wa Yanga na kufafanua wanaoleta
vurugu Yanga, baadhi ni mamluki wa wafanyabiashara wenzake walioshindwa
kumshinda kwa njia halali na sasa wanaitumia yanga kama sehemu pekee
iliyobaki kumuumiza kupitia mbinu zinazotumika hasa kwa kuleta vurugu
ndani ya yanga ili kumchafua yeye binafsi, kufanya kwao hivyo ni
kushusha hadhi ya klabu na maoni yake kwa maslahi ya yanga, kipi
kifanyike.
12. MENGINEYO.
13. SALA.
13.1. Sala ya waislamu ya kubariki maamuzi ya mkutano.
13.2. Sala ya wakristo kubariki maamuzi ya mkutano.
14. Kufunga mkutano.
VPL: LIGI KUU VODACOM
Ratiba:
**Mechi zote kuanza Saa 10 Jioni isipokuwa inapotajwa
Jumamosi Oktoba 22
African Lyon v Mbeya City [Saa 8 Mchana]
Ndanda FC v Mwadui FC
Mtibwa Sugar v Stand United
Kagera Sugar v Yanga
Azam FC v JKT Ruvu [Saa 1 Usiku]
Maji Maji FC v Ruvu Shooting
+++++++++++++++++++++++
LEO
zipo Mechi 6 za VPL, Ligi Kuu Vodacom, na moja ni ile ya Mabingwa
Watetezi Yanga ambao wapo Ugenini huko Uwanja wa Kaitaba, Bukoba kucheza
na Kagera Sugar.
Mechi
nyingine 5 za Leo ni mbili zitakazochezwa Jijini Dar es Salaam wakati
Azam FC wakicheza na JKT Ruvu juko Azam Complex, kwenye Viunga vya Jiji
la Dar es Salaam kuanzia Saa 1 Usiku na ya pili ni ile ya Uwanja wa
Uhuru kati ya African Lyon na Mbeya City.
Mechi
nyingine ni huko Manungu, Morogoro kati ya Wenyeji Mtibwa Sugar na
Stand United na huko Songea kati ya Maji Maji FC na Ruvu Shooting.
Hadi
sasa Simba ndio wapo kileleni mwa VPL sasa wakiwa na Pointi 26 kwa Mechi
10 baada ya kushinda Mechi 8, Sare 2 na Kutofungwa.
Timu ya Pili ni Stand United wenye Pointi 20 kwa Mechi 11 na wa 3 ni Yanga wenye Pointi 18 kwa Mechi 9.
Jumapili
Oktoba 23 zipo Mechi 2 wakati Simba watakapocheza na Toto Africans ya
Mwanza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na huko Sokoine, Mbeya ni kati ya
Tanzania Prisons na Mbao FC.
++++++++++++++++++++++++
VPL
YANGA - Mechi zao:
Okt 22 Kagera Sugar v Yanga
Okt 26 Yanga v JKT Ruvu
Okt 29 Yanga v Mbao FC
SIMBA - Mechi zao:
Okt 23 Simba v Toto African
Okt 29 Mwadui v Simba
Nov 2 Stand United v Simba
++++++++++++++++++++++++
VPL: LIGI KUU VODACOM
Ratiba:
Jumapili Oktoba 23
Simba v Toto Africans
Tanzania Prisons v Mbao FC
Hakuna maoni