Wednesday, October 5, 2016
Tundu Lissu akosekana Tena Mahakamani Kisutu, aibukia Mwanza
Tundu
Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, jana alishindwa kufika katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kujibu mashitaka ya uchochezi huku
mdhamini wake akiieleza mahakama kuwa, yupo jijini Mwanza akisimamia
kesi ya Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda katika Mahakama Kuu ya Mwanza.
Lissu
ambaye pia ni wakili wa Mahakama Kuu na mwansheria mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo anashitakiwa kwa uchochezi pamoja na washitakiwa
wengine ambao ni ni Jabir Idrissa, mwandishi mwandamizi wa Gazeti la
MAWIO, Simon Mkina, mhariri wa Gazeti hilo na Ismail Mehboob, meneja wa
kampuni ya uchapishaji magazeti ya Flint.
Mdhamini
wa Lissu, Ibrahim Hemed, alitoa taarifa ya kutofika kwa mdhamana wake
mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Ibrahim
alidai kwamba Lissu amempatia taarifa kuwa ameshindwa kufika kwa sababu
yupo kwenye kesi ya uchaguzi huku Peter Kibatala wakili wa utetezi
akiiomba mahakama ipokee taarifa za Lissu na ikubali kuhairisha kesi
hiyo.
“Lissu ni wakili pekee wa mlalamikiwa Esther Bulaya katika kesi ya uchaguzi,” alisema Kibatala.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 31 mwaka huu.
Katika
kesi hiyo Lissu anaunganishwa kama mshitakiwa kufuatia kunukuliwa
akitoa maoni yake katika habari iliyochapishwa na gazeti la MAWIO ikiwa
na kichwa cha habari “Machafuko yaja Zanzibar.”
Wednesday, October 5, 2016
Sinema ya CUF Yazidi Kunoga.......Bodi ya Wadhamini Nayo Yagawanyika Viipandevipande
Bodi
ya wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF), imegawanyika vipande viwili
kutokana na mgogoro wa uongozi unaoendelea ndani ya chama hicho.
Kugawanyika
kwa bodi hiyo kumekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wake, Abdallah
Katau kutangaza kutomtambua Profesa Lipumba, huku baadhi ya wajumbe
wakipinga tamko hilo wakiliita ni batili kwa mujibu wa katiba ya CUF.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wajumbe
wenzake, mjumbe wa bodi ya chama hicho, Peter Malebo, alisema hawatambui
tamko lililotolewa na mwenyekiti wao kwani bodi hiyo inajiandaa
kuwakutanisha mwenyeki wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu
Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad ili kuweza kutafuta suluhu ya
mgogoro huo.
Alisema
kutokana na hali hiyo, watakaa na wajumbe wenzao na kujadili suala hilo
kabla ya kuwaita viongozi hao ikiwa ni pamoja na kujadili ushauri wa
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.
“Tutakaa
na wajumbe wenzetu ili tuweze kujadiliana mgogoro wa viongozi wetu
pamoja na kupitia maazimio ya Msajili wa Vyama Vya Siasa ili tuweze
kupata hoja ya kuwahoji kwenye kikao hicho.
“Lengo
letu ni kuhakikisha kuwa chama chetu kinarudi kwenye hadhi yake kama
ilivyokua awali kuliko hivi sasa ambapo kimegubikwa na mgogoro wa
uongozi wa kitaifa,” alisema Malebo.
Alisema
ikiwa watashindwa kupata mwafaka wataitisha Mkutano Mkuu wa dharura
ili waweze kuwaeleza wajumbe wa mkutano huo hali ya chama na hatua za
kuchukua.
“Kama
mwafaka hautapatikana katika kikao hicho, tutalazimika kuitisha Mkutano
Mkuu Maalumu ambao pamoja na mambo mengine, tutawaeleza mgogoro wa
viongozi wetu ili wajumbe waweze kutoa uamuzi,” alisema.
Alisema Bodi ya Wadhamini wa CUF inaundwa na wajumbe wanane ambapo kutoka upande wa bara ni watano na Zanzibar watatu.
Aliwataja
wajumbe hao kuwa ni pamoja na Abdalah Katau, Peter Malebo, Ally
Mbarouk, Amin Mrisha, Zacharia Kwangu, Yohana Mbelwa na Dk. Juma Muchi.
Alisema
mpaka sasa bodi hiyo imegawanyika ambapo wajumbe kutoka Zanzibar
wanamwunga mkono Maalim Seif huku wale wa bara wakimwunga mkono Profesa
Lipumba hali inayozidi kupandisha joto ndani ya chama hicho.
“Kinachotutafuna
ndani ya CUF ni ubaguzi unaoonyeshwa waziwazi kutoka kwa viongozi wa
Zanzibar jambo ambalo limechangia kila mtu kuwa upande wake, lakini
tutaitana na kujadiliana suala hili ili tuweze kupata mwafaka,” alisema.
Alisema
bodi hiyo inafanya kazi ndani ya kipindi cha miaka mitano ambapo
iliteuliwa mwaka 2011 na itamaliza muda wake, Desemba mwaka huu.
Atoa onyo Chadema
Katika
hatua nyingine, Malebo aliwataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kutoingilia mgogoro huo kwa madai hauwahusu.
Alisema,
kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kujitokeza hadharani
na kudai hamtambui Profesa Lipumba inaonyesha wazi kuwa ameshiriki
kuongeza mgogoro ndani ya chama hicho.
“Mbowe
haumhusu mgogoro wa viongozi wa CUF, huu ni mgogoro wa ndani ya chama,
tunamshangaa kujitokeza hadharani na kudai hamtambui Lipumba, yeye ni
nani ndani ya chama?, tunamuonya asirudie,” alisema.
Alisema,
chama hicho kimejipanga kupambana na watu wanaoingilia mgogoro wao
wakati si wanachama wa chama hicho, jambo ambalo limechangia kuendelea
kuchochea vurugu hizo.
Wednesday, October 5, 2016
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi atoa ONYO kwa wanaotumia jina la cheo chake vibaya
Wednesday, October 5, 2016
Saed Kubenea kizimbani tena kwa kupotosha
Mbunge
wa Ubungo, Saed Kubenea amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kuandika
makala ya kupotosha na kusababisha hofu kwa jamii.
Kubenea,
ambaye ni mbunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka na
Wakili wa Serikali, Dereck Mukabatunzi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Wilbard Mashauri.
Wakili
Mukabatunzi alidai kuwa Julai 25, mwaka huu katika Mtaa wa Kasaba,
Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Kubenea alichapisha habari
ya uongo inayoweza kusababisha hofu na taharuki kwa jamii au kuondoa
amani.
Inadaiwa
Kubenea alichapisha makala hiyo kwenye gazeti la Mwanahalisi la Julai
25 hadi 31, mwaka huu, lenye namba 349 ISSN: 1832-5432 ikiwa na kichwa
cha habari “Yuko wapi atakayeiokoa Zanzibar”.
Baada
ya kusomewa mashitaka, Kubenea alikana kutenda kosa hilo na upande wa
Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe
nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali.
Wednesday, October 5, 2016
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Octobar 5
habari za kimataifaa.
Mzozo kati ya Urusi na Marekani kuhusu Syria wapamba moto
Rais wa Colombia kukutana na mpinzani wake kujadili makubaliano ya amani
Upinzani Congo watishia maandamano kuhusu chaguzi
Mashitaka ya uhalifu dhidi ya shairi tata la Boehmermann yaondolewa
EU yaidhinisha makubaliano ya mazingira ya Paris
Kimbunga Mathew chaikumba Haiti
katika michezoooo
RASHFORD ATAKUWA SUPASTAA!
KEPTENI
wa Manchester United na England Wayne Rooney ameeleza kuwa Chipukizi
Marcus Rashford atapanda chati na kuwa Supastaa mwenye Jina kubwa kwenye
Soka.
Rashford, mwenye Miaka 18, ameibuka na kupanda juu haraka mno baada
ya Meneja aliepita wa Man United Louis van Gaal kumpa nafasi kucheza
kwa mara ya kwanza Timu ya Kwanza kwenye UEFA EUROPA LIGI dhidi ya
Midtjylland Mwezi Februari.
Kwenye Gemu hiyo Kijana huyo akapiga Bao 2 na Siku 3 baadae, kwenye
Mechi yake ya kwanza ya EPL, Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal akapiga
tena Bao 2.
Tangu wakati huo Rashford amekuwa ni moto kwenye Mechi zote anazochezeshwa.
Ingawa Rooney amekiri bado Staa huyo hajakomaa lakini amebainisha uwezo na kipaji chake kitamfikisha mbali.
Rooney ameeleza: "Marcus anafanya vizuri. Ni Kijana mdogo mwenye
mvuto mkubwa Duniani hivi sasa. Nina hakika akiendelea kufanya bidii na
kukua basi atakuwa Supastaa Miaka ijayo!"
Radhford alikuwemo kwenye Kikosi cha England kilichokuwa Fainali za
EURO 2016 huko France Juni na Julai chini ya Kocha Roy Hodgson lakini
alipokuja Sam Allardyce na kuisimamia England Mechi 1 tu hakuitwa.
Badala yake Rashford akachukuliwa England U-21, chini ya Gareth
Southgate, na yeye kupiga Hetitriki kwenye ushindi dhidi ya Norway.
Radhford sasa amerejeshwa tena England ambayo sasa ipo chini ya
Meneja wa muda Gareth Southgate na Jumamosi itacheza na Malta kwenye
Mechi ya Kundi lao la Nchi za Ulaya zinazosaka kwenda Russia Mwaks 2018
kucheza Fainali za Kombe la Dunia huku Rashford akitabiriwa sana kuanza
Mechi hiyo.
Hivi sasa Rashford pia yumo Kikosi cha Kwanza cha Man United chini ya Meneja Jose Mourinho na kumfanya Rooney asugue Benchi.
Rooney amenena: "Ni muhimu Wachezaji chipukizi wanaofurahisha wazawadiwe wakistahili na nadhani anastahili!KOMBE LA DUNIA 2018: BONUCCI AWANIA KUIBONDA TENA SPAIN KAMA WALIVYOITENDA KWENYE EURO 2016!
ALHAMISI
Italy watapambana na Spain kwenye Mechi ya Pili ya Kundi G la Nchi za
Ulaya kuwania nafasi za kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018
huko Russia na Leonardo Bonucci anataka Italy waibonde tena Spain kama
ilivyokuwa Mwezi Julai kwenye EURO 2026.
Bonucci, Sentahafu anaechezea Juventus, amesema wao wanataka
waifunge Spain kama walivyoitoa kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16
walipoichapa 2-0.
Wakati huo Spain walikuwa ndio Mabingwa Watetezi wa Ulaya.
++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia
-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia
-Washindi wa Pili 8 wa Makundi watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia
++++++++++++++++++++++++
Akiongea na Wanahabari kuelekea Mechi hii itakayochezwa Alhamisi
huko Juventus Stadium Mjini Turin Nchini Italy, Bonucci amesema:
"Nkifikiria Paris, nafurahia sana. Kumbukumbu hiyo inatupa morali kwani
tuliwabwaga Vigogo Duniani ingawa wakati huo hawakuwa imara sana!"
Hata hivyo, Bonucci amekiri Mechi hii ya sasa ni tofauti kwani kila Timu sasa ina Kocha Mpya.
Italy sasa wapo chini ya Giampiero Ventura baada kuondoka Antonio
Conte na Spain wako chini ya Julen Lepetegui baada ya kung'oka Vicente
del Bosque.
Kwenye Mechi zao za kwanza za Kundi G Spain, ikiwa Nyumbani,
iliibomoa Liechtenstein 8-0 na Italy, wakiwa Ugenini waliipiga Israel
3-1.
ULAYA – KOMBE LA DUNIA 2018
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa
Alhamisi Oktoba 6
KUNDI D
Austria v Wales
Moldova v Serbia
Republic of Ireland v Georgia
KUNDI G
2145 Italy v Spain
Liechtenstein v Albania
Macedonia v Israel
KUNDI I
Iceland v Finland
Kosovo v Croatia
Turkey v Ukraine
Ijumaa Oktoba 7
KUNDI A
France v Bulgaria
Luxembourg v Sweden
Netherlands v Belarus
KUNDI B
Hungary v Switzerland
Latvia v Faroe Islands
Portugal v Andorra
KUNDI H
Belgium v Bosnia-Herzegovina
Estonia v Gibraltar
Greece v Cyprus
Jumamosi Oktoba 8
KUNDI C
1900 Azerbaijan v Norway
Germany v Czech Republic
Northern Ireland v San Marino
KUNDI E
1900 Armenia v Romania
1900 Montenegro v Kazakhstan
Poland v Denmark
KUNDI F
1900 England v Malta
Scotland v Lithuania
Slovenia v Slovakia
Jumapili Oktoba 9
KUNDI D
1900 Wales v Georgia
Moldova v Republic of Ireland
Serbia v Austria
KUNDI G
1900 Israel v Liechtenstein
Albania v Spain
Macedonia v Italy
KUNDI I
1900 Finland v Croatia
1900 Ukraine v Kosovo
Iceland v Turkey
Jumatatu Oktoba 10
KUNDI A
Belarus v Luxembourg
Netherlands v France
Sweden v Bulgaria
KUNDI B
Andorra v Switzerland
Faroe Islands v Portugal
Latvia v Hungary
KUNDI H
Bosnia-Herzegovina v Cyprus
Estonia v Greece
Gibraltar v Belgium
Jumanne Oktoba 11
KUNDI C
Czech Republic v Azerbaijan
Germany v Northern Ireland
Norway v San Marino
KUNDI E
1900 Kazakhstan v Romania
Denmark v Montenegro
Poland v Armenia
KUNDI F
Lithuania v Malta
Slovakia v Scotland
Slovenia v England
MASHABIKI KUNG'OA VITI TAIFA, SIMBA YAPIGWA FAINI YA SH MILIONI TANO, YAPEWA ONYO KALI AU MECHI ZAKE ZITACHEZWA BILA MASHABIKI
Simba imepigwa faini ya Sh milioni 5 kutokana na mashabiki wake kung’oa viti vya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.
Mashabiki
wa Simba waling’oa viti wakati timu yao ikicheza na Yanga ikiwa ni
baada ya mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe kufunga, lakini kabla
alikuwa ameshika mpira.
Kamati ya Bodi ya Ligi ya uendeshaji na Usimamizi wa Ligi iliyokaa jana, imefikia uamuzi wa kuipa Simba adhabu hiyo.
Kama hiyo haitoshi, kamati hiyo imeionya Simba kwa kusisitiza ni onyo kali na kama itatokea tena itatoa adhabu kali.
Moja ya adhabu ambazo zimetajwa ni pamoja na Simba kucheza bila ya mashabiki.
Msisitizo wa kamati hiyo, umesema adhabu hiyo imetolewa kutoka kwa mujibu wa kanuni ya 42(3) na 24(7) za Ligi Kuu Bara.
STAND UNITED, MBEYA CITY KILA MMOJA ANAJIAMINI KUMMALIZA MWENZAKE
STAND UNITED |
Vikosi
vya Mbeya City na Stand United vimechimbana mkwara mzito kila upande
ukitamba kuibuka na ushindi katika mchezo unaotarajiwa kupigwa Jumamosi
hii huko mkoani Mbeya.
Timu
hizo zinakutana zikiwa na jeuri ya kuibuka na ushindi katika michezo
yao ya mwisho ya ligi msimu huu, ambapo City iliifunga Mwadui kwa bao
1-0 na kukamata nafasi ya saba ikiwa na pointi 11, Stand ikaitungua
Majimaji mabao 2-0 na kufikisha pointi 15, ikiwa nafasi ya pili, nyuma
ya kinara Simba mwenye 17.
Ofisa
Habari wa Stand, Deo Makomba, ameeleza kuwa hawana wasiwasi na mwendo
walionao sasa, wamepania kumfunga kila watakayekutana naye ingawa
wanajua Mbeya City ni timu ngumu lakini wataichapa hukohuko kwao.
“Cha
msingi waamuzi wawe ‘fair’ tu na watende haki lakini kuhusu kikosi
chetu tunakiamini na benchi la ufundi lipo vizuri, mchezo hautakuwa
mwepesi lakini tumepanga kushinda katika kila mchezo ulio mbele yetu,
maana nia yetu ni kuhakikisha tunamaliza katika nafasi tatu za juu msimu
huu,” alisema Makomba.
Kwa
upande wa Ofisa Habari wa City, Dismas Ten, alisema: “Tunachokitaka
siku zote ni ushindi na ukizingatia tupo nyumbani, kwa hiyo tumejizatiti
ingawa mpira ni dakika 90, hizo zitaamua nani mshindi baada ya mchezo.
Timu itaanza maandalizi (jana) leo jioni tayari kwa ajili ya mchezo
huo.”
TFF ‘YAJIBARAGUZA’ ETI HAIJAMFUNGIA SAANYA, INAMCHUNGUZA TU…LAKINI YAKUBALI KUFUTA KADI YA MKUDE
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limekerwa na kuvuja kwa taarifa ya Kamati ya Saa 72 kilichoketi jana na kuwafungia waamuzi wawili wa mechi ya watani, Simba na Yanga. Na katika kile kinachoonekana ‘kujibaraguza’, Kamati hiyo imetoa taarifa eti haiwajafungia Martin Saanya na Samuel Mpenzu, badala yake inawachunguza. Lakini taarifa za uhakika kutoka kwenye kikao cha Kamati jana usiku zilisema, Saanya na Mpenzu kila mmoja amefungiwa miaka miwili. Taarifa rasmi ya Kamati iliyotolewa leo imesema kwamba waamuzi hao pamoja na Ferdinand Chacha sasa wanachunguzwa kwa uchezeshaji wao, lakini Simba SC imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 na kutakiwa kufidia gharama za uharibu waliofanya Jumamosi. Mashabiki wa Simba walifanya vurugu Uwanja wa Taifa Jumamosi baada ya Yanga kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Tambwe alifunga bao hilo dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban. Bao hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga. Na katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele. Kwa hali hiyo, mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani. Polisi walitumia milipuko ya gesi za kutoa machozi kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea hadi Simba SC wakasawazisha dakika ya 87 kwa bao la Shizza Kichuya. Na Mpenzu naye anadaiwa kukataa bao safi la Simba lililofungwa na Ibrahim Hajib mapema kipindi cha kwanza akidai aliotea. Taarifa pia imesema Kamati hiyo imefuta adhabu ya kadi nyekundu ya Mkude, baada ya kubaini hakuwa na hatia, wakati Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Manara ametozwa faini ya Sh. 200, 000 kwa kuingia uwanjani baada ya mechi. Katika hatua nyingine, klabu ya Azam FC imetozwa faini ya Sh. 3,000,000 kwa kosa la kuvaa nembo ya mdhamini (Vodacom) upande mmoja badala ya pande zote mbili.
Tuesday, October 4, 2016
Waziri Mkuu Alaani Mauaji Ya Watafiti Chamwino, Dodoma
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amelaani kitendo cha wanakijiji kuwaua watumishi
wa Serikali waliokuwa wakifanya utafiti wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Oktoba 3, 2016) wakati akizungumza
na waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu
wake wa kukutana na makundi mbalimbali.
Mauaji
ya watafiti hao, Teddy Nguma, Jafari Mafuru na dereva wao Bw. Nicas
Magazine yalitokea Oktoba Mosi, 2016 baada ya kushambuliwa na wakazi wa
kijiji cha Makang’wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Amesema
Serikali imesikitishwa na mauaji ya watu watatu wakiwemo watafiti
wawili kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Seliani (SARI) kilichopo
mkoani Arusha ambao walikuwa kazini kuchunguza sampuli za udongo ili
kubaini kama matetemeko yataendelea kutokea.
“Kutokana
na tetemeko lilitokea mkoani Kagera, Serikali iliamua kushirikisha
watalaamu mbalimbali kufanya uchunguzi kuona kama tetemeko hilo ni
endelevu au la katika maeneo mengine. Kitendo cha watu kujichukulia
hatua mkononi na kukatisha uhai wa watumishi ambao walikuwa kazini
hakikubaliki,” amesema
.
Amesema watalaamu hao walifika katika Wilaya ya Chamwino na kufanya
kazi kwa siku tano na siku ya sita ndipo walipoenda eneo la kijiji cha
Iringa Mvumi kuendelea na kazi ambapo waliuawa wakiwa kazini.
“Serikali
kupitia kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa inaendelea na uchunguzi wa
kuwabaini watu waliofanya kitendo hicho’’ amesema. Hata hivyo, Waziri
Mkuu amewatoa wasiwasi watumishi wanaohamia Dodoma kuwa Dodoma ni salama
na kila anayekuja yupo salama. “Dodoma ipo salama na tunatarajia kila
anayehamia hapa atakuwa salama na hata wakazi wa hapa wataendelea kuwa
salama,’’ amesema.
Akizungumzia
kuhusu migogoro ya ardhi inayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini,
Waziri Mkuu amesema hali hiyo inajitokeza hivi sasa baada ya wananchi
wengi kutambua thamani ya ardhi.
Amesema
miaka ya nyuma watu wachache walitambua thamani ardhi hivyo kuchukua
maeneo makubwa na kuyamiliki. Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa
migogoro hiyo inamalizika kwa kuweka kuweka msisitizo kuwe mipango ya
matumizi bora ya ardhi ikiwa ni pamoja na kupima ardhi yote na kutoa
hati kwa wananchi.
“Tunataka
ardhi yote ipimwe na kila mtu anayepewa ardhi apewe hati ya kumiliki na
si vinginevyo’’ amesema. Wakati huohuo, Waziri Mkuu aliwaasa waandishi
wa habari wawe makini na kazi yao na wajiepushe na upotoshaji kwenye
taarifa wanazozitoa kwa wananchi. Amesema vyombo vya habari ni kiungo
muhimu baina ya Serikali na wananchi, hivyo aliwataka viongozi wote wa
umma washirikiane na vyombo vya habari kwa kutoa habari za utekelezaji
wa kazi za Serikali.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amepokea msaada wa sh. milioni 11.42 kutoka
kwa taasisi na wadau mbalimbali mkoani Dodoma zikiwa ni kwa ajili ya
kusaidia waathirika wa tetemeko lililotokea mkoani Kagera Septemba 10,
2016 na kusababisha vifo vya watu 17.
Michango
aliyopokea leo imetolewa na Mzee Thakar Singh na familia yake sh.
milioni 5; NSSF Dodoma (sh. milioni 1.2); Shirika la Bima ya Taifa tawi
la Dodoma (sh. milioni moja); Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (sh.
milioni moja) na Ofisi Rais TAMISEMI (sh. milioni 2). Wengine ni
TRA-Dodoma (sh. milioni moja); Dodoma FM (sh. 200,000) na Mwalimu
Mstaafu, Mama Amina Mafuru aliyetoa sh. 20,000/-.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
S. L. P. 980,
DODOMA. JUMANNE, OKTOBA 04, 2016
Tuesday, October 4, 2016
Taarifa Kwa Wataalamu Wa Afya Wanaotarajia Kuanza Mafunzo Kwa Vintendo (Internship).
Reviewed by RICH VOICE
on
Oktoba 05, 2016
Rating:
Hakuna maoni