Majambazi Yateka Basi na Kupora Abiria
Majambazi
sita wameteka basi la Kampuni ya Safi na likitokea Kijiji cha Mamba
wilayani Chunya kwenda jijini Mbeya na kisha kuwapora abiria jana.
Miongoni
mwa waliotekwa ni pamoja na baadhi ya madiwani waliokuwa wakielekea
mjini Chunya kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani
Maalumu kwa ajili ya kupitia na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika jana.
Akizungumzia
tukio hilo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya,
Ramadhani Shumbi aliyekuwa mmoja wa waathirika wa uvamizi huo, alisema
tukio hilo lilitokea saa moja kasorobo asubuhi katika eneo la Loge.
Shumbi
ambaye ni Diwani wa Kata ya Mamba, alisema walipofika eneo hilo lililo
na msitu mkubwa, walikuta kuna gogo kubwa lililolazwa na kufunga
barabara na kisha walijitokeza watu sita mmoja akiwa amebeba bunduki na
wengine mapanga na fimbo.
Alisema
watu hao walipiga risasi tatu hewani na kuanza kupiga vioo vya basi
wakiwaamuru abiria washuke, lakini iliwachukua abiria takribani dakika
10 wakigoma kushuka kabla ya baadhi walioonekana kutishika zaidi kuanza
kushuka kwa kuruka kupitia madirishani.
Alisema
baadaye iliwalazimu abiria wote kushuka na ndipo jambazi wakaanza
kuwasachi na kunyang’anya fedha taslimu na simu za mikononi huku
walioonekana kubisha, wakipigwa.
“Baada
ya kushuka tulilazwa chini na kuanza kukaguliwa ambapo walichukua fedha
na simu na mimi mwenyewe ni mwathrika wa simu na fedha kidogo
nilizokuwa nazo. Ushauri wangu ni kuwa mabasi kama haya yaanze safari
saa moja asubuhi badala ya saa kumi na moja ama kumi na mbili,” alieleza diwani huyo.
Majambazi Yateka Basi na Kupora Abiria
Reviewed by RICH VOICE
on
Agosti 30, 2017
Rating:
Hakuna maoni