Serikali Yamjibu Tundu Lissu Sakata la Ndege Kushikilia Canada kisa Madeni
Serikali
kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa
imejibu hoja zilizotolewa na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu
kuhusu kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania aina ya Bombadier Q-400 Dash 8
nchini Canada.
Zamaradi
Kawawa amekiri kuwa ni kweli ununuzi wa ndege hizo umeingiliwa na
mgogoro na kukiri kuwa ndege hiyo Q-400 Dash 8 inashikiliwa nchini
Canada kwa madai ya kuwa ndege hiyo imeshikiliwa kwa mgogoro wa
kutengeneza na wanasiasa wa Tanzania wasioitakia mema nchi ya Tanzania.
"Ununuzi
wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na
wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania, Wanasiasa waliotengeneza
mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia" alisema Zamaradi Kawawa
Aidha
Zamaradi Kawawa amesema kuwa ndege ya tatu ambayo ilikuwa inatarajiwa
kuingia nchini mwezi Julai amedai kuwa itaingia muda si mrefu na
kuwataka Watanzania waiamini serikali ya Tanzania iliyopo chini ya Rais
John Pombe Magufuli
"Ndege
ya 3 ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini Serikali yao
ila serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu
kuhujumu maendeleo ya nchi, Watanzania tuwe wazalendo kulinda, kutetea
na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi,
tuunge mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuleta maendeleo bila
kujali itikadi ya chama, kabila au dini" alisisitiza Zamaradi Kawawa
Mbali na hilo Kawawa amesema kuwa serikali imeanza kuchukua hatua kadhaa kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hizo
"Kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili" alisema Zamaradi Kawawa
Serikali Yamjibu Tundu Lissu Sakata la Ndege Kushikilia Canada kisa Madeni
Reviewed by RICH VOICE
on
Agosti 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni