Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Makongoro Mahanga Akamatwa kwa Amri ya Mahakama Kuu
Mbunge
wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na
Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani.
Mahakama
iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kushindwa
kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba Msemakweli Sh14
milioni.
Fedha
hizo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada ya kushinda kesi
ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja kwenye
kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”.
Katika kitabu hicho anamtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye shahada za udaktari wa kughushi.
Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6 milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.
Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Makongoro Mahanga Akamatwa kwa Amri ya Mahakama Kuu
Reviewed by RICH VOICE
on
Agosti 31, 2017
Rating:
Hakuna maoni