Wapigadebe 150 kufikishwa mahakamani
Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza kukamata watu
wapatao 150 kuanzia Agosti 14 hadi 17 mwaka huu, kwa makosa ya
kuwabughuzi abiria katika maeneo mbalimbali ya jiji katika vituo vya
mabasi.
Wakati
akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Lucas Mkondya, alisema
watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia misako na operesheni kali
iliyofanywa na polisi, na kwamba watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka
yanayowakabili.
“Stendi
ya mabasi ya Ubungo walikamatwa 39, Posta 12, Ferry 7, Tegeta 12,
Tandika 16, Mnazimmoja 6, Stesheni 5, Manzese 12, Bunju 8 na Stereo 7,” amesema.
Katika
hatua nyingine, Kamanda Mkondya alisema Jeshi la Polisi katika nyakati
tofauti ilikamata watuhumiwa 167 kwa makossa mbalimbali ya kihalifu
ikiwemo kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, unyang’anyi wa
kutumia sialaha na utapeli, kucheza kamali na kuuza pombe haramu ya
gongo.
“Katika
operesheni hii kali ambayo ni endelevu, jumla ya kete 96 za dawa ya
kulevya, misokoto ya bangi 107, gongo lita 60 zilikamatwa. Tunaomba raia
wema kuendelea kutoa taarifa za wahalifu ili tuwakamate na hatua kali
za kisheria zifuatwe dhidi yao,” alisema.
Alisema
watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa kulingana na makossa yao na kwamba
upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria
zaidi.
Wapigadebe 150 kufikishwa mahakamani
Reviewed by RICH VOICE
on
Agosti 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni