Urusi yatia mguu mgogoro wa Korea Kaskazini, yaitahadharisha Marekani
Waziri
wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov amemwambia waziri wa
Ulinzi wa Marekani, Rex Tillerson kuwa kuiwekea vikwazo vingi Korea
Kaskazini hakutasaidia chochote kutatua mgogoro uliopo kuhusu mpango
wake wa nyuklia.
Katika
taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje nchini Urusi imesema kuwa
viongozi hao wamezungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio
yanayofanywa na Korea Kaskazini.
Lavrov
amesema kuwa diplomasia ndio njia pekee ya kumaliza wasiwasi katika
rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa
akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana.
Hata
hivyo, Waziri wa ulinzi wa Marekani amesema kuwa bado kuna fursa ya
kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini ili iweze kuachana na
mpango wake wa majaribio ya silaha za nyuklia huku Rais Trump akisema
mazungumzo sio suluhisho
Urusi yatia mguu mgogoro wa Korea Kaskazini, yaitahadharisha Marekani
Reviewed by RICH VOICE
on
Agosti 31, 2017
Rating:
Hakuna maoni