Marekani: Tutaendelea na mazungumzo na Korea Kaskazini
Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis amesema kuwa Marekani itaendelea na mazungumzo ya kidiplomasia na Korea Kaskazini.
Matamshi
hayo yanajiri baada ya rais Donald Trump kusema katika mtandao wake wa
Twitter kwamba mazungumzo sio suluhu kwa mipango ya kijeshi ya Korea
Kaskazini.
Urusi pia imeionya Marekani dhidi ya kuchukua hatua za kijeshi akisema madhara yake yatakuwa makubwa.
Korea Kaskazini ilizua wasiwasi baada ya kurusha kombora kupitia anga ya Japan siku ya Jumanne.
Kombora
hilo ambalo Japan limelitaja kuwa tishio lisilo la kawaida , lilivuka
katika anga ya kaskazini ya kisiwa cha Japana cha Hokkaido mapema siku
ya Jumanne, na kusababisha raia kujificha kabla ya kombora hilo kuanguka
baharini yapata kilomita 1,180 .
Korea
Kaskzini baadaye ilisema kuwa ni hatua mojawapo ya operesheni zake za
kijeshi katika eneo la pacific na kurejelea tishio lake la kushambulia
kisiwa cha pacific cha Guam.
Siku
chache zilizopita, bwana Trump alikuwa amenukuliwa akisema anaamini
kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un alikuwa ameanza kuiogopa
Marekani.
Lakini
katika chapisho lake la siku ya Jumatano , alisema: Marekani imekuwa
ikizungumza na Korea Kaskazini na kuwalipa fedha kwa miaka 25.
''Kuzungumza
nao sio suluhisho''.lakini alipoulizwa iwapo ni kweli kwamba Marekani
imepoteza matumaini ya kidiplomasia , bwana Mattis alitofautiana wazi na
rais Trump akisema: Hapana. Sisi hatujapoteza matumaini kupitia kutatua
maswala kidiplomasia .
Alikuwa akizungumza alipokutana na mwenzake wa Korea Kusini Song, Young-moo katika Pentagon.
''Tunaendelea kufanya kazi pamoja na waziri na mimi tunagawana majukumu ili kulinda mataifa yetu, idadi yetu na maslahi yetu''
Marekani: Tutaendelea na mazungumzo na Korea Kaskazini
Reviewed by RICH VOICE
on
Agosti 31, 2017
Rating:
Hakuna maoni