FRIDAY 09/09/2016
LEO TUNAANZA NA MICHEZO
STRAIKA WA CHELSEA ARUDISHWA SIKU 9 TU TOKA UHAMISHONI!
Loic
Remy amerejeshwa Klabuni kwake Chelsea Siku 9 tu baada ya kuwa kwa
Mkopo huko Crystal Palace bila kucheza hata Mechi moja baada ya kuumia.
Reny, Raia wa Ufaransa mwenye Miaka 29, aliumia Pajani Mazoezini
Majuzi Jumatatu na sasa amerejeshwa Klabuni kwake Chelsea kupata
matibabu zaidi.
Palace imethibitisha tukio hili na kusema atakuwa nje kwa Wiki kadhaa.
Meneja wa Palace, Alan Pardew, amesema: “Kwa bahati mbaya Remy
aliumia Mazoezini Jumatatu. Si vibaya sana lakini Wikiendi hii hawezi
kucheza na sijui atakuwa nje kwa muda gani hadi vipimo vikamilike.”
Remy alijiunga na Chelsea Mwaka 2014 na kufunga Bao 8 katika Mechi 32.
Hadi sasa Palace wamecheza Mechi 3 za Ligi Kuu England na kuambua Pointi 1 tu na Jumamosi wapo Ugenini kucheza na Middlesbrough.
Mapema Leo Palace walimsaini Kiungo wa zamani wa Arsenal Mathieu
Flamini ambae ni Mchezaji Huru na kufikisha idadi ya Wachezaji wao wapya
kwa Msimu huu kuwa Watano na wengine ni Andros Townsend, Steve Mandanda, James Tomkins, Christian Benteke na huyu Loic Remy.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 10
1430 Man United v Man City
1700 Arsenal v Southampton
1700 Bournemouth v West Brom
1700 Burnley v Hull
1700 Middlesbrough v Crystal Palace
1700 Stoke v Tottenham
1700 West Ham v Watford
1930 Liverpool v Leicester
Jumapili Septemba 11
1800 Swansea v Chelsea
Jumatatu Septemba 12
2200 Sunderland v Everton
ANFIELD ‘MPYA - JUMAMOSI LIVERPOOL KUIFUNGUA NA MABINGWA LEICESTER!
LIVERPOOL
watacheza Uwanja wa Nyumbani kwao Anfield Jumamosi kwa mara ya kwanza
Msimu huu baada kucheza Mechi 3 za Ligi Kuu England, EPL, Ugenini
wakipisha upanuzi wa Jukwaa Kuu la Uwanja wao.
Jumamosi Liverpool watawakaribisha Mabingwa Watetezi wa England
Leicester City kwenye Mechi ya EPL ambayo itatanguliwa na Ufunguzi rasmi
wa Jukwaa Kuu jipya ambao Mmiliki Mkuu wa Klabu hiyo kutoka Kampuni ya
Kimarekani Fenway Group, John W Henry, Mwenyekiti Tom Werner na Rais
Mike Gordon watahudhuria.
+++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Kupanuliwa kwa Jukwaa Kuu la Anfield kutaiongezea Mapato
Liverpool kwa Siku za Mechi kwa kiwango cha Pauni Milioni 20 hadi 30
kwa Msimu.
-Kabla, Liverpool walikuwa wakivuna Pauni Milioni 59 tu.
-Manchester United ndio wanaovuna kiwango cha juu kabisa cha zaidi ya Pauni Milioni 100.
+++++++++++++++++++++++
Jukwaa hilo limepanuliwa na kuongezwa Ngazi 3 juu za kukalia
Washabiki, kupanua Ukumbi wa Wachezaji kuingia na kutoka Uwanjani kutoka
Vyumba vya Kubadili Jezi, Mabenchi ya Wachezaji wa Akiba na Jopo lao la
Ufundi kutengenezwa upya, sehemu maalum kwa Walemavu na kuboreshwa kwa
miundo mbinu ya Watazamaji.
Jukwaa Kuu la Anfield litaongeza Viti 8,500 na kuufanya Uwanja huo sasa upakie Watazamaji 54,000.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 10
1430 Man United v Man City
1700 Arsenal v Southampton
1700 Bournemouth v West Brom
1700 Burnley v Hull
1700 Middlesbrough v Crystal Palace
1700 Stoke v Tottenham
1700 West Ham v Watford
1930 Liverpool v Leicester
Jumapili Septemba 11
1800 Swansea v Chelsea
Jumatatu Septemba 12
2200 Sunderland v Everton
KUELEKEA DABI YA MANCHESTER: MOURINHO ANENA UPINZANI WAKE NA GUARDIOLA!
>>”LIGI KUU ENGLAND SI LA LIGA YENYE SAMAKI MKUBWA MMOJA TU, HUKU KUNA PAPA KILA KONA!”
WAKATI
Dunia ya Soka ikisubiri kwa hamu Dabi ya Manchester itakayochezwa
Jumamosi hii Uwanjani Old Trafford kati ya Mahasimu Manchester United na
Manchester United huku kukiwa na shauku ya ziada ya kuwaona Mameneja
wapya wa Klabu hizo, Jose Mourinho na Pep Guardiola, wakikwaana kwa mara
nyingine, Mourinho ametoa tahadhari kubwa.
Mourinho, ambae sasa ni Meneja wa Man United, ameonya hatatumbukizwa
tena kwenye uhasama wa kupindukia na Guardiola ambae ni Meneja wa Man
City.
Wawili hao walikuwa na upinzani uliojaa vituko na bashasha kubwa huko
Spain walipoongoza Timu pinzani wakati Mourinho akiwa Real na Guardiola
akiwa Barcelona.
Lakini, kabla ya wote kuwa Makocha Viongozi, Wawili hao walikuwa Timu
moja Barcelona, Mourinho akiwa mmoja wa Jopo la Makocha na Guardiola
akiwa Mchezaji na kisha kuanza Ukocha.
Wanahabari na Wachambuzi huko Uingereza, na Duniani kote, wamekuwa
wakingoja kwa shauku Wawili hao wakikutana uso kwa uso kwa mara ya
kwanza huko England.
Lakini Mourinho amesema kwenye La Liga wasiwasi wake mkubwa ulikuwa
kwa Samaki mmoja mkubwa tu lakini England kuna Papa kila kona.
Ameeleza: “Uzoefu wangu hauniruhusu niwe mpumbavu. Kwa Miaka Miwili
mimi na Pep tulikuwa kwenye Ligi ambayo Bingwa nakuwa mimi au yeye, Real
Madrid au Barcelona!”
“Kwa hali kama hiyo, kukwaruzana kibinafsi kunaeleweka kwani huweza kubadilisha mambo!”
“Lakini kwenye Ligi Kuu, nikimtilia mkazo yeye na Manchester City, na
yeye atie mkazo kwangu na Manchester United, Mtu mwingine atakuwa
Bingwa!”
ZA KIMATAIFAAAA
Matumizi ya Koili ni bora kuliko tembe katika kuzuia ujauzito
Wanawake wanapaswa
kushauriwa kwamba njia ya kuzuia ujauzito ya matumizi ya koili ni bora
zaidi kuliko njia ya dharura ya kumeza vidonge vinavyomezwa baada ya
tendo la ngono (morning-after pill), kwa mujibu wa ushauri mpya
uliotolewa Uingereza
Limekuwa likishauriwa ni "jambo jema " kuwapatia wanawake coili kwa kipindi cha muongo.
Lakini Taasisi ya Kitaifa ya Uingereza ya afya na ubora wa Kliniki (NICE) inasema ushauri kuhusu suala hili unapaswa kuboreshwa.
Kati
ya mwaka 2014 na 2015, 95% ya wanawale waliopewa vidonge vya dharura
na huduma za afya na masuala ya ngono kwa ujumla walipewa vidonge vya
kuzuia mimba vya... morning-after pill.
Coil, ambayo pia
hutambuliwa kwa lugha ya kitaalam kama...intrauterine device au IUD, ni
njia inayofaa ikiwa itaingizwa katika siku tano baada ya kufanya ngono
bila kinga na Coil lazima zipachikwe vizuri hasa na daktari ama muunuzi
aliyepewa mafunzo, katika kliniki ya afya ya uzazi ama kwenye kituo cha
upasuaji.
Kama itakuwa vigumu kumpata daktari katika muda wa siku
tano , mwanamke anaweza kushauriwa kumeza tembe za morning-after pill
kabla ya coili haijafungwa.
'Kufahamu muda ni muhimu'
Sue
Burchill, mkuu wa wauguzi katika hospitali ya Brook, ambayo hutoa
huduma za afya ya ngono kwa vijana 25,000 walio chini ya umri wa mika
25 kila mwaka anasema, said: "runaamini vijana wote wanapaswa kuwa na
taarifa sahihi kuhusu njia tofauti za dharura za kuzuia mimba zilizopo
ili wawe na uelewa kuhusu uamuzi juu ya njia iliyo bora kwa mahitaji ya
binafsi, na tunatolea witro mamlaka za ndani husika nchini kutopuuza
hili kwa kupunguza udhamini kwa ajili ya huduma za afya ya ngono
"tunafahamu
kwamba matumizi ya coili ndio njia iliyo inayofaa ya uziaji mimba wa
dharura iliyopo, kwa hivyo tunapaswa kuendelea kuhakikisha tunawezesha
watu kutumia injia hii na kuimarisha utaoaji wa huduma hizi miongoni
mwa wale wanaozitoa."
Profesa Gillian Leng, naibu mkurugenzi
mkuu wa NICE, anasema : "kwa kweli ni muhimu kwamba huduma zote za
kuziwia mimba zitolewe kwa wanawake zikiambatana na ushauri mzuri
kuhusu njia za kuzuia mimba.
" Pia tunataka kuhakikisha wanawake
wanaelezwa kwamba coili ni njia bora zaidi ya kuzuwia mimba kuliko tembe
katika wakati wa dharura."
DK Jan Wake, wa GP na mjumbe wa
shirika linalotoa maagizo kuhusu njia za kupanga uzazi, anasema :
"kuelewa muda wa tendo la ngono, hata hivyo, ni muhimu na wanawake
wanaoamua kutumia coili wanapaswa kutembelea kliniki walizoshauriwa
kwenda mapema iwezekanavyo.
Watalii 45 wakwama mlimani Ufaransa
Juhudi za uokoaji
za kuwanasua watalii 45 ambao wamekwama kwenye magari ya kutumia kamba
katika mlima wa Mont Blanc, Ufaransa zimeanza tena.
Watalii hao
walilala usiku wa Alhamisi kwenye kibaridi kikali wakiwa wamekwama juu
ya barafu takriban 3,800m (futi 12,468) juu mlimani.
Walikuwa miongoni mwa watu 110 waliokwama baada ya magari hayo kupatwa na hitilafu Alhamisi alasiri.
Inaaminika magari hayo yalikwama baada ya kamba kushikana kutokana na upepo mkali.
Watu
65 waliokolwa kwa kutuia helikopta baadaye Alhamisi lakini juhudi
zikasitishwa giza lilipoingia na kukawa na mawingu hivyo kuifanya vigumu
kuona.
"Tulilazimika kusitisha juhudi za uokoaji kwa sababu za
kiusalama," alisema Georges Francois Leclerc, mkuu wa idara ya uokoaji
ya Haute-Savoie.
"Tunatumai tutawapata wote salama Ijumaa asubuhi," alisema ni kuongeza kwamba ni operesheni ngumu sana.
Watalii waliokwama walipewa vyakula, blanketi na maji.
Maji ya mto yageuka 'rangi ya damu' Urusi
Wachunguzi wa
masuala ya mazingira nchini Urusi wanajaribu kubaini chanzo cha maji ya
mto ulio karibu na kiwanda cha nikeli cha kampuni ya Norilsk Nickel
yamebadilika rangi na kwua na rangi nyekundu.
Picha za maji ya mto Daldykan ambayo yamebadilika rangi zimesambazwa sana katika vyombo vya habari Urusi.
Gazeti
la serikali la Rossiiskaya Gazeta linasema kuvuja kwa bomba la
kusafirisha taka za mchanganyiko wa shaba nyekundu na nikeli huenda
likawa kiini cha maji hayo kubadilika rangi.
Norilsk Nickel ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa nikeli na palladium duniani.
Kampuni hiyo ina vinu na tanuri nyingi rasi ya
Taimyr eneo la Krasnoyarsk katika jimbo la Siberia. Ujenzi wa vinu hivyo
vikubwa ulifanyika enzi za muungano wa Usovieti.
Kampuni hiyo ina
kiwanda kwa jina Nadezhda karibu na mto Daldykan lakini maafisa wake
wanasema hawajapata dalili zozote za uchafuzi kutoka kwa kiwanda hicho.
Rais wa kampuni hiyo ni bilionea Vladimir Potanin.
Korea Kaskazini yalipua bomu ‘sawa na la Hiroshima’
Shirika la habari
la serikali ya Korea Kaskazini limesema taifa hilo limefanya majaribio
ya bomu kupima uwezo wa bomu lake la nyuklia la kurushwa kwa kombora.
Mlipuko wa bomu hilo umesababisha tetemeko la ardhi katika eneo lililofanyiwa majaribio.
Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 5.3 kwenye vipimo vya Richter.
Maafisa
wa jeshi la Korea Kusini wanakadiria kwamba mlipuko huo ulikuwa sawa na
wa kilo tani kumi za TNT, ukubwa sawa na wa bomu lililoangushwa
Hiroshima na Marekani wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia. Baadhi
wanasema huenda bomu hilo la Korea Kaskazini likawa lilikuwa na nguvu ya
kilo tani 20.
Bomu lililoangushwa Hiroshima mwaka 1945 lilikuwa na nguvu ya kilo tani 15 (tani 15,000).
Bomu
lenye nguvu zaidi la nyuklia lililowahi kulipuliwa lilikuwa lile
lililopewa jina Tsar-bomba, ambalo lililipuliwa na Urusi mwaka 1961.
Lilikuwa na nguvu ya mega tani 50, sawa na nguvu ya tani milioni 50 za TNT (50,000,000).
Wataalamu
bado wanaendelea kudadisi iwapo lilikuwa bomu la haidrojeni, jambo
ambalo linaweza kulipa nguvu zaidi kushinda mlipuko wa bomu la kawaida
la nyuklia.
Hilo likithibitishwa, basi itakuwa ni mara ya tano kwa Pyongyang kutekeleza jaribio la silaha za kinyuklia.
Jaribio la leo limetekelezwa siku ambayo serikali inaadhimisha kuanzishwa kwa taifa la sasa la Korea Kaskazini mwaka 1948.
Jamii ya kimataifa imeghadhabishwa na hatua hiyo ya Korea Kaskazini.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye ametaja jaribio
hilo kuwa "jaribio la kujiangamiza" ambalo linaonyesha "kutomakinika"
kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Bi Park, ambaye
amesitisha ghafla ziara yake ng'ambo, amesema baada ya kutekeleza
jaribio hilo la tano la nyuklia "serikali ya Kim Jong-un itakaribisha
vikwazo zaidi na kutengwa zaidi na jamii ya kimataifa."
"Uchokozi kama huu utaongeza kazi safari yake ya kuelekea kwenye maangamizi."
Bi Park alifanya pia amzungumzo ya dharura na Rais wa Marekani Barack Obama kwa njia ya simu.
Kuvumiliwa
China,
mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kidiplomasia, pia imeshutumu hatua
hiyo na kuihimiza Pyongyang kukoma kuchukua hatua ambazo zinaweza
kuzidisha hali.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema majaribio kama hayo ya Korea Kaskazini hayawezi kuvumiliwa.
Friday, September 9, 2016
Viongozi wa Afrika Mashariki Waigomea Ulaya....Wajipa Miezi Mitatu Kuutafakari Mkataba wa EPA
JUMUIYA
ya Afrika Mashariki (EAC), imeiomba Jumuiya ya Ulaya (EU), iipe muda wa
miezi mitatu kujua hatima ya wao kusaini Mkataba wa Kiuchumi na Jumuia
hiyo (EPA).
Uamuzi
huo ulifikiwa jana Ikulu Dar es Salaam na viongozi wa Jumuiya hiyo
baada ya kikao cha 17 kilichodumu kwa takribani saa sita.
Akizungumza
baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa EAC, Rais John Magufuli alisema
kikao hicho kilikuwa na ajenda nne, ila ya EPA ilikuwa ngumu kulingana
na uzito wake.
Alitaja
ajenda hizo kuwa ni ripoti ya mgogoro wa Burundi, kuingizwa rasmi kwa
Sudan Kusini kwene Jumuiya, kupitishwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa EAC na
EPA.
Rais
Magufuli alisema viongozi wote kwa pamoja walikubaliana kupewa muda wa
miezi mitatu ili Sekretarieti ya EAC iangalie na kupitia masharti ya EPA
kabla ya kusaini ili kila mmoja afaidike.
Hata hivyo nchi ambazo zilishasaini makubaliano hayo kutoka Jumuiya hiyo ni Kenya.
Alisema
katika kikao hicho, walibaini mambo 10 ambayo yanapaswa kuangaliwa
kabla ya kufikia uamuzi kwa maslahi ya nchi na wananchi.
Mwenyekiti
alitaja mambo ya kuangaliwa kuwa ni kwa namna gani nchi za EAC
zitafaidika, njia gani itatumika kuzuia bidhaa za kilimo na kulinda
wakulima.
Maeneo
mengine ni usawa, makusanyo yatokanayo na bidhaa zitakazoingizwa,
Burundi itasainije huku ikiwa imewekewa vikwazo na EU, kujitoa kwa
Uingereza EU na athari zake, kukosekana kipengele cha kuruhusu nchi
zingine kujihusisha na nchi za EAC kibiashara, kukosekana ushuru wa
forodha na kipengele cha nchi kujitoa pale inapoona haijaridhika na
mkataba.
Rais Magufuli alisema mkataba huo ukisainiwa kwa wakati huu, nchi wanachama zinaweza kuingia kwenye mtego mbaya.
“Tumejadiliana
kwa muda mrefu ila mjadala mkubwa ulikuwa suala la EPA ambapo
tumekubaliana tupewe miezi mitatu ili tukutane Januari na kutoa uamuzi
wa pamoja,” alisema Magufuli.
Alisema Tanzania iko kwenye mkakati wa kujenga viwanda, hivyo ni lazima iwe makini katika kusaini mkataba huo.
Aidha, aliiomba EU kutoiadhibu Kenya kutokana na uamuzi huo kwani nia yao ni nzuri hivyo wapewe nafasi.
Mwenyekiti
huyo alisema viongozi wote walikubaliana kuiidhinisha Sudani Kusini
kuwa mwanachama wa EAC na Christopher Bazivamo kutoka Rwanda kuwa Naibu
Katibu Mkuu Mpya na mapendekezo ya kutatua mgogoro wa Burundi.
Friday, September 9, 2016
Makamu Wa Rais Atembelea Kituo Cha Kuchakata Gesi .....awataka wafanyakazi kufanya kazi kwa uzalendo
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyakazi wa kiwanda
cha kuchakata gesi asilia kilichopo Madimba mkoani Mtwara wawe
wazalendo na wafanye kazi kwa bidii katika kulinda na kuutunza uwekezaji
huo mkubwa ambao serikali inautegemea katika uzalishaji wa nishati ya
umeme wakati taifa linaelekea kwenye nchi ya viwanda.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyakazi na watendaji wa kiwanda hicho baada ya kutembelea kiwanda kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mtwara.
Amesema
kiwanda cha kuchakata gesi asilia ni hazina kubwa kwa Taifa hivyo ni
kikalindwa na kutunzwa ipasavyo kutokana na umuhimu wake katika
uzalishaji wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya nchi.
Makamu
wa Rais pia amewashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wa kiwanda hicho
cha kuchakata gesi asilia cha Madimba na amewahakikishia kuwa serikali
itaendelea kuwajali na kuwathamini katika utendaji wao wa kazi na kwamba
serikali itahakikisha wafanyakazi wa kiwanda hicho wanapewa motisha ya
kutosha ili waongeze maradufu utendaji wao wa kazi ili malengo ya
serikali ya kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia viwanda inatimia kwa
sababu taifa litakuwa na nishati ya umeme ya uhakika.
Makamu
wa Rais amewataka watendaji wa Shirika la Maendeleo la Petroli (TPDC)
ambalo linasimamia mradi huo kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya
kusaidia huduma za jamii katika vijiji vinavyozunguka mradi huo kila
mwaka ili wananchi waweze kuwa walinzi wa mitambo hiyo.
Akitoa
maelezo mafupi ya mradi huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini Prof. James Mdoe amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata
gesi ya futi za ujazo milioni 210 kwa siku.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha kuchakata gesi cha
Madimba Mhandisi Leonce namna gesi inavyopokelewa na kuchakatwa na
kusafirishwa kwa watumiaji.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
akiangalia mfumo wa uendeshaji na usalama wa kiwanda cha kuchakata gesi
cha Madimba mkoani Mtwara.
Friday, September 9, 2016
Profesa Semboja adai Ukubwa wa deni la taifa hauwezi kuyumbisha uchumi
Na: Frank Shija, MAELEZO
Ukubwa
wa deni la taifa siyo jambo linaloweza kusababisha kuyumba kwa uchumi
wa nchi, kinachooneka ni kuendela kuaminiwa kwa Tanzania ndani na nje ya
nchi jambo linalopelekea tuna pata fursa ya kukopesheka kwa ajili ya
miradi ya maendeleo.
Hayo
yamebainishwa na Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi, Profesa Haji Semboja
alipofanya mahojiano maalum na mwandishi kutoka Idara ya Habari,
MAELEZO kuhusu hali ya uchumi ilivyo kutokana na ongezeko la deni la
Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
“Ukubwa wa deni la taifa siyo mzigo mbaya, ni mzigo wa kimaendeleo. Unnecessary devil” Alisema Profesa Semboja.
Aliongeza
kuwa kutokana kwa imani waliyo nayo wahisani ndani na nje ya nchi ndiyo
maana washirika wetu wanatukopesha fedha kwa ajili ya miradi ya
maendeleo kama ambavyo tumeshuhudia ujenzi wa Daraja la Kigamboni, hivi
karibuni tutanufaika na usafiri wa ndege”. Alisema Profesa Semboja.
Aidha
amempongeza Rais wa Awamu ya Tano Mhe. Dkt. Jonh Pombe Joseph Magufuli
kwa hatua alizochukua za kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma kwa
kuondoa safari za nje zisizo za rasmi pamoja na kupiga vita vitendo vya
rushwa.
Semboja
aliendelea kusema kuwa kinachofanyika hivi sasa ni Serikali ya awamu ya
Tano kulipa madeni ya watangulizi wake huku ikitekeleza miradi ya
maendeleo jambo linaloongeza imani miongoni mwa wahisani.
Hata
hivyo alionya juu ya matumizi mabaya ya rasilimali fedha kuwa
zinasababisha kushindwa kutekeleza wajibu wa kulipa deni kwa wakati na
kupelekea kulimbikiza madeni jambo ambalo si sahihi.
Alitajaa
baadhi ya matumizi mabaya ya fedha kuwa ni pamoja na safari za nje na
ndani ya nchi zisizokuwa na tija, ulevi, kupelekea fedha katika miradi
isiyopangwa na mengine.
Wananchi
wametakiwa kutoyumbishwa na waelewi kuwa kupitia fedha zinazokopwa
wanufaika wakuu ni wananchi wenyewe, mfano fedha zitakazo tumika kujenga
Nyumba za Magomeni ambazo Mhe. Rais amehaidi waliokuwa wakazi wake
kuishi bila kulipia kwa kipindi cha miaka mitano zikitokana na mikopo
hiyo wananufaika.
Friday, September 9, 2016
Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.
Msafara
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu
Hassan ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo
ya Rais ,mkoani Mtwara, umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao
wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.
Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara .Majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa Makamu wa Rais.
Awali
kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Makamu wa Rais kuacha njia
na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel
ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.
Barabara
ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na
kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha
njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
Friday, September 9, 2016
Mahakama Yaizuia NHC Kupiga Mnada Mali za Freeman Mbowe
Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Ardhi imeliamuru Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC) kutouza au kupiga mnada mali za Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mpaka kesi ya msingi
itakapomalizika.
Shirika
hilo lilizichukua mali mbalimbali za kampuni za Mbowe ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Hai, wiki iliyopita kupitia mawakala wa kampuni ya
Fosters Auctioneers katika jengo lililopo makutano ya mitaa ya Mkwepu na
Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam.
Hatua
hiyo ya NHC ilitokana na mgogoro wa muda mrefu, wakimtuhumu Mbowe
kushindwa kulipa deni la zaidi ya Sh. 1.3 bilioni, ikiwa jumla ya fedha
za kodi ya kupangishwa kwenye jengo hilo.
Kutokana
na mvutano huo, Mbowe alifungua kesi katika Mahakama Kuu, Kitengo cha
Ardhi, kupinga hatua ya NHC kumuondoa katika jengo hilo, pamoja na
kuchukua mali zake huku wakitangaza kuzipiga mnada baada ya siku 14
tangu kuzichukua.
Jana, Jaji Siyovelwa Mwangasi alitoa
zuio na kuiamuru NHC kutouza wala kupiga mnada mali hizo za Mbowe mpaka
mahakama hiyo itakapotolea uamuzi katika kesi ya msingi.
Katika kesi hiyo namba 722 ya mwaka 2016, Mbowe anawakilishwa na Mawakili Peter Kibatala na Omary Msemo.
Jaji
Mwangasi amesema kuwa, anakubaliana na maombi ya mlalamikaji na kutaka
mali hizo zisiuzwe hadi hapo mahakama itakapofanyia uamuzi kesi ya
msingi.
Hatua
hiyo inakuja baada ya upande wa NHC kupitia mawakili wake Aloyce Sekule
na Miriam Mungula kushindwa kuwasilisha hoja za msingi kueleza, ni
kwanini zuio hilo lisitolewe hadi hapo kesi ya msingi itakapoanza
kusikilizwa.
Awali,
mawakili wa NHC, walidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza
maombi ya Mbowe kwa kuwa hakuna kesi ya msingi ambayo imefunguliwa,
hivyo maombi hayo yatupiliwe mbali.
Wakili Kibatala alijibu hoja hiyo kwa kusema, hatua ya kuwasilisha maombi hayo inalenga kubaini kama kweli Mbowe anadaiwa kodi ama la.
Kibatala alidai
kuwa mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, hivyo inaweza
ikatoa uamuzi wowote, na ndiyo maana wamewasilisha maombi hayo ili
itolewe amri ya muda ya kuzuia mchakato huo.
Miongoni
mwa hoja za Mbowe alizoziwalisha mahakamani hapo, ni pamoja na hoja
kuwa, yeye (Mbowe) na shirika hilo walikubaliana kwamba atalikarabati na
kulipanua jengo hilo kwa asilimia 100. Makubaliano ambayo yaliingiwa
mwaka 1997.
Amedai
kuwa katika makubaliano hayo yeye na NHC walikubaliana watamiliki jengo
hilo kwa pamoja kwa muda wa miaka 99, huku Mbowe katika mgawanyo wa
mapato akitakiwa kupata asilimia 75 na NHC ikitakiwa kupata asilimia 25.
Pia alieleza
kuwa katika makubaliano hayo, licha ya mwenendo wa kibiashara kutokuwa
mzuri, muda wote alikuwa akilipa asilimia hiyo 25, kwa mujibu wa
makubaliano yao.
Hivyo
kutokana na hatua ya NHC kuvunja mkataba huo kwa kumtoa kwenye jengo na
kuchukua mali zake, anaiomba mahakama iliamuru shirika hilo limlipe
fidia.
Mbowe aliondolewa kwenye jengo husika mnamo Septemba mosi kwa madai ya kushindwa kulipa deni la zaidi ya Sh. bilioni 1.3.
Mawakala
wa NHC walifika katika jengo hilo saa 12:30 asubuhi na wafanyakazi
zaidi ya 50 na kwenda moja kwa moja katika kampuni ya Free media pamoja
na ukumbi wa Bilcanas na kuchukua vifaa mbalimbali ikiwemo, meza, viti
na kompyuta.
Siku
chache baada ya kuondolewa kwa Mbowe katika jengo hilo, Rais John
Magufuli alilisifu shirika hilo kwa hatua hiyo na kulitaka lichukue
hatua kama hizo kwa wadaiwa wengine zikiwemo taasisi za umma
Friday, September 9, 2016
Polisi Wamhoji Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob
Maofisa
wa Polisi wamemhoji Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob kabla
ya hajakutana na waandishi wa habari kwa madai kuwa wamepata taarifa
mkutano wake huo ulilenga kumkashifu Rais John Magufuli.
Maofisa
hao waliovalia kiraia walionana na Jacob ofisini kwake na walimruhusu
kuendelea na mkutano huo baada ya meya huyo kuwahakikishia kwamba hana
nia hiyo bali alitaka kutoa ufafanuzi wa baadhi ya masuala baada ya ujio
wa Rais, Kinondoni Jumanne iliyopita.
“Kwa
mara ya kwanza meya anahojiwa, lakini niliwaambia wana usalama lengo
langu ni nini na sipo kwa ajili ya kumkashifu Rais, ila nafahamu vita
iliyopo kati yetu na baadhi ya viongozi,” alisema Jacob.
Pamoja
na ufafanuzi huo, Jacob aliwataka baadhi yao (askari) kushiriki kwenye
mkutano huo wa wanahabari kufuatilia alichotaka kuwaeleza wanahabari na
polisi mmoja alibaki kusikiliza bila kutambulishwa.
Kamanda
wa Polisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda alisema hakukuwa na tatizo lolote
polisi kuwapo eneo hilo, kwani wanafanya shughuli zao za ulinzi na
usalama wa raia na hasa ikizingatiwa kuwa kuna Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Katika
mkutano huo, meya Jacob alitoa ufafanuzi wa yaliyojiri Jumanne
iliyopita wakati Rais Magufuli alipofanya ziara katika manispaa hiyo na
kubatilisha umiliki wa eneo la Magomeni Kota lililokuwa mali ya
halmashauri kuwa ya Serikali Kuu.
Meya
Jacob aliwaambia wanahabari kuwa uamuzi wa Serikali kuchukua eneo hilo
umeisababishia halmashauri yake hasara ya zaidi Sh4.5 bilioni kutokana
na gharama walizoingia.
Katika
eneo hilo, nyumba 644 zilivunjwa mwaka 2011 kwa miadi ya kwamba
zikijengwa upya, wananchi waliokuwa wakiishi hapo wakiwa wapangaji
wangerejeshwa, lakini mradi huo ulichelewa kuanza.
Akiwa
ameambatana na baadhi ya madiwani, Jacob alisema hasara hiyo imetokana
na halmashauri kutumia Sh2 bilioni kumlipa mkandarasi kwa ajili ya
michoro ya eneo litakavyokuwa.
Alisema
pia manispaa hiyo imetoa Sh1 bilioni kwa mkandarasi Gulf kwa ajili ya
kuchora ramani ya ofisi mpya za halmashauri na kusimamia ujenzi wa mradi
huo na kutumia Sh700 milioni kuwalipia kodi wapangaji hao baada ya
kuwahamisha.
“Faida
tuliyoipata ni kwamba wananchi tuliopanga kuwahudumia tayari Rais
amewahudumia. Hatupingi maamuzi ya Serikali, lakini wananchi watambue
kwamba manispaa haina chochote itakachokipata, bali kila kitu kitakuwa
kinafanywa na Serikali Kuu,” alisema Jacob.
Meya
alisisitiza kuwa madiwani wa Ukawa hawapingi uamuzi huo ila baadhi ya
viongozi wanaomzunguka Rais hawamwambii ukweli wa mambo kuhusu mradi wa
Magomeni Kota na kwamba baadhi ya watumishi wa Serikali ndiyo
waliosababisha kufikia hatua hiyo.
“Siku
ile ningepata nafasi hata dakika tatu, ningemweleza Rais Magufuli
ukweli wa mambo wa mradi huu. Lakini kuna baadhi ya viongozi
waliomzunguka waliamua kuninyima nafasi hiyo. "
Hata
hivyo, Jacob alimwomba Rais Magufuli kukutana naye ili amweleze kwa
undani jambo linalomuumiza kuhusiana na masuala ya ardhi yanayoikumbuka
Kinondoni.
Alifafanua
kwamba, Serikali iliyopita na manispaa hiyo ilishaingia mkataba na
kampuni ya Blue Marine ya Romania kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa
Magomeni Kota ambao ulifikia katika hatua nzuri lakini baadhi ya
watumishi wa Serikali waliamua kuweka ‘kauzibe’ na kuipa sifa mbaya
Kinondoni.
“Tulikuwa
tunasubiri utiaji wa saini kutoka Serikali Kuu, lakini baada ya kuona
Kinondoni inaongozwa na Ukawa wameamua kuleta ‘figisufigisu’ za
kuukwamisha,” alisema Jacob.
Katika
ziara hiyo, Rais Magufuli alielezea kusikitishwa kwake na namna tatizo
la wakazi hao lilivyoshughulikiwa na kuwaahidi kuwa Serikali yake
itahakikisha hawasumbuliwi.
Friday, September 9, 2016
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 9
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 09, 2016
Rating:
Hakuna maoni