Saturday, September 17, 2016
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya Septemba 17
Friday, September 16, 2016
Kutoka Mahakamani: Zombe Aachiwa Huru, Mwenzake Ahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa
Mahakama
ya Rufani imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa upelelezi
wilaya ya Kinondoni (OC-CID), Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni,
baada ya kumtia hatiani kwa kosa ka mauaji ya wafanyabiashara watatu wa
madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro.
Wakati
Bageni akihukumiwa kitanzi, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Dar
(RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na maafisa
wengine wawili wa Polisi, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari wameachiwa
huru, baada ya mahakama kuwaona kuwa hawana hatia.
Bageni amehukumiwa adhabu hiyo leo baada ya mahakama ya Rufani kukubaliana na rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu kuwaachia huru katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara hao.
Wafanyabiashara
hao, Savings Chigumbi, Ephraim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva
teksi wa Manzese, Juma Ndugu, waliuawa Januari 14,2006, kwa kupigwa
risasi Mbezi Luis, Dar.
Saturday, September 17, 2016
Lipumba, Sakaya, Kambaya watuhumiwa kupanga njama za utekaji viongozi wa CUF
Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha ambaye pia ni Kaimu Naibu Mkuu CUF, Bara Joran Bashange
Chama
cha Wananchi (CUF) kinawatuhumu waliokuwa viongozi wa chama hicho,
Profesa Ibrahim Lipumba, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho na
Magdalena Sakaya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Bara kufanya jaribio la
kumteka Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha ambaye pia ni Kaimu Naibu Mkuu
CUF, Bara Joran Bashange.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari, Uenezi na
Mahusiano ya Umma CUF inadai kuwa jana majira ya 2:30 asubuhi vijana
wanaosadikiwa kuwa wa Prof Lipumba wamefanya jaribio la kutaka kumteka
Bashange wakati akitoka nyumbani kwake eneo la Buguruni.
Na
kwamba watekeji hao wakiwa na gari aina ya Noah yenye namba ya Usajili T
760 CEX baada ya jaribio la kumteka, walifanikiwa kumuingiza katika
gari hiyo ya NOAH iliyokuwa na vioo vyeusi (tinted).
Taarifa
hiyo ilieleza kuwa Bashange alipambana na kuomba msaada kwa kuita watu
waliojirani kwa yowee la kuita “Majambazi” ndipo wananchi wakalizingira
gari hilo na kuweka mawe na magogo na kuita Polisi.
Baada ya Polisi kufika waliwakagua vijana hao na kuwakuta na pingu, silaha kadhaa na kitambulisho feki cha polisi.
Baada ya ukaguzi kufanyika vijana watatu walikamatwa na mmoja alifanikiwa kukimbia.
Taarifa
hiyo ilifafanua kuwa mmoja kati ya vijana waliokamatwa ni mlinzi wa
karibu wa Prof. Lipumba aitwaye HAJI “Mrangi” ambaye ni maarufu na
anadaiwa kujulikana kwa ushiriki wake wa vitendo vya kihuni na kiharamia
kama hivyo.
Hata
hivyo, katika mahojiano ya awali mmoja wa vijana hao alitoa ushirikiano
na kueleza kuwa wametumwa na Abdul Kambaya na kwamba anayeongoza
oparesheni yao hiyo ni mtu aitwaye Athumani (Mganga wa Kienyeji na
Mwalimu wa mafunzo ya Kareti) aishiye Ilala akisaidiwa na watu wengine
wanaojulikana Abubakar Fambo, Mohamed Ibrahim na Hassan Kingwele (
Mlinzi wa Magdalena Sakaya (MB).
Vijana
hao waliokamatwa wanakiri kuwa mipango yote hiyo Prof. Lipumba anaijua
kama vile walivyoongoza mpango wa kuhujumu Mkutano Mkuu Maalumu wa CUF
ulioahirishwa pale Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza.
Joran
Bashange ameumizwa maeneo kadhaa ya mwili na anaendelea na matibabu na
taarifa za ndani zinaonesha kuwa wahusika walielekezwa kumshambulia
vibaya na kumuua ikiwa wangelifanikiwa kuondoka naye.
Vijana waliohusika na utekaji huo na gari lao wanashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Polisi Buguruni.
Chama cha CUF kimelaani kitendo hicho na kimesema kinachukua hatua stahiki.
Pia
Chama hicho kimesema kinaamini kuwa kwa sasa Prof. Lipumba na watu wake
wamekusudia kuendesha hujuma za wazi na kuvuka mipaka ya ushindani wa
kisiasa za ndani ya Chama na kujivika joho la ‘Uintarahamwe na Umungiki’
wa wazi dhidi ya Chama na kuhatarisha na kutishia usalama wa maisha ya
viongozi wa Chama.
Saturday, September 17, 2016
Wanaowapigia simu polisi bila sababu Kuchukuliwa Hatua za Kisheria
JESHI
la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limeahidi kuwachukulia hatua kali
wananchi wanaotumia vibaya simu za dharura, zenye namba 111 na 112.
Simon
Sirro, Kamishina wa Jeshi la Polisi amesema kuwa watu wamekuwa wakipiga
simu hizo na kutoa taarifa za uongo au kupiga simu na kisha kuwapa
watoto wadogo waongee.
“Polisi
tutawafuatilia wote kupitia mitandao yetu General Packet Radio Service
(GPRS),inayoonyesha maeneo walipo na simu wanazotumia ili kuwakamata na
kuwachukulia hatua kali za kisheria. Haiwezekani mtu apige simu halafu
baada ya simu kopokelewa anaweka muziki,” amesema.
Kamanda
Sirro amesema ni vyema wananchi wakaacha mzaha na matumizi ya namba
hiyo ya Jeshi la Polisi kwani kwa kufanya hivyo inapunguza morali ya
askari wa jeshi hilo kufanya kazi kwa kujituma.
“Wananchi
wote watumie simu zetu kutoa taarifa zenye ukweli na zitafanyiwa kazi
kwa wakati, wawasiliane na sisi pale wanapoona viashiria vya uhalifu ama
tukio lolote linaloleta uvunjifu wa amani na siyo kupiga simu na
kufanya mzaha,” amesema Sirro.
Saturday, September 17, 2016
UKUTA Waiponza Redio ya Lowassa....Yafungwa Kwa Miezi 3 na Faini ya Milioni 5
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia Kamati yake ya Maudhui
imekifungia kituo cha Redio 5 Arusha kwa kipindi cha miezi mitatu pamoja
na kukitoza faini ya sh. Milioni 5 kwa kosa la kukiuka baadhi ya Kanuni
za Huduma za Utangazaji (maudhui) kupitia kipindi chake cha Matukio
kilichorushwa Agosti 25, 2016.
Kwa
mujibu wa taarifa ya kamati hiyo, katika kipindi hicho Mbunge wa Jimbo
la Arusha Mjini Mh. Godbless Lema alitamka maneno ya kashfa yaliyolenga
kumdhslilisha Rais John Magufuli na serikali kwa ujumla.
Wakati
akisoma maamuzi ya kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui
Joseph Mapunda, aliongeza kuwa kituo hicho pia kilirusha maneno yaliyo
tamkwa na Lema ambayo yalikuwa yakihamasisha wananchi kushiriki katika
maandamano ya Ukuta yaliyopigwa marufuku na Jeshi la Polisi.
“Maneno
ya Lema yalilenga kuhamasisha wananchi kupambana na jeshi la polisi na
hivyo kusababisha uvunjifu wa amani na kuhatarisha usalama wa Taifa,” alisema.
Mapunda
alisema uamuzi huo umetolewa na kamati hiyo baada ya kamati hiyo
kusikiliza maelezo ya utetezi yaliyotolewa na wa Uongozi wa Redio 5
Arusha.
“Baada
ya kusikiliza maelezo ya utetezi kamati imeridhia kuwa kipindi cha
matukio kilikiuka baadhi ya kanuni za maudhui namba 5(a,b,c,d,f,h) 6(2)
(b, c) na 18 (1) (b),” alisema.
Aliongeza kuwa ”
kituo hicho kinatozwa faini ya sh. Milioni 5 ambazo zitatakiwa kulipwa
ndani ya siku 30 kuanzia leo, kinafungiwa kwa miezi 3 na kuwekwa chini
ya uangalizi maalumu kwa muda wa Mwaka 1 baada ya kipindi cha kufungiwa
kumalizika, “
Hata hivyo, Mapunda alisema haki ya wahusika kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo iko wazi ndani ya siku 30 kuanzia leo.
Kwa
upande wa kituo cha redio cha Magic Fm ambacho nacho pia kwa mujibu wa
kamati hiyo kinadaiwa kukiuka kanuni za maudhui kupitia kipindi chake
cha Morning Magic kipengele cha Paka Rangi ambapo kilirusha maneno
yanayodaiwa kumkejeli rais na wananchi, kimepewa onyo kali pamoja na
kutakiwa kuomba radhi kwa muda wa siku tatu mfululizo.
“Baada
ya kusikiliza na kutafakari kwa kina maelezo ya utetezi yaliyotolewa na
Uongozi wa Magic Fm Redio, Kamati ya Maudhui imeridhika kuwa kipindi
cha Morning Magic kilikiuka baadhi ya kanuni za huduma za utangazaji
2005. Kamati ya maudhui inaamua kutoa onyo kali kwa Magic Radio, ” alisema na kuongeza.
“Pia
inatakiwa kumuomba radhi Rais John Magufuli, wasikilizaji na wananchi
kwa ujumla. Tangazo la kuomba radhi litolewe kwa siku tatu mfululizo
katika taarifa za habari za saa 10.00 alasriri, na 3.00 usiku kuanzia
tarehe 17,9,2016.”
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 17, 2016
Rating:
Hakuna maoni