Waziri wa Ujenzi atoa miezi sita kumaliza upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa mkandarasi Nyanza Road Construction inayojenga barabara ya
Furahisha hadi Pasiansi KM 2.8 wakati alipokagua ujenzi wa barabara
hiyo, jijini Mwanza.
*****
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka
Mkandarasi wa kampuni ya Beijing Construction Engineering Group
anayejenga uwanja wa ndege wa Mwanza kumaliza kazi ya upanuzi wa uwanja
huo ifikapo mwezi Februari Mwakani.
Profesa
Mbarawa ametoa kauli hiyo alipokuwa akikagua kazi ya ujenzi na upanuzi
wa uwanja wa ndege wa Mwanza pamoja na daraja la watembea kwa miguu
lililopo maeneo ya furahisha, jijini Mwanza.
Profesa
Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi na upanuzi wa uwanja huo
kutaimarisha hali ya usafiri wa anga kwa wakazi wa Mwanza na mikoa
mingine na hivyo kukuza shughuli za kibiashara nchini.
“Hakikisheni
upanuzi wa uwanja wa ndege huu unakamilika haraka ili kurahisisha na
kuboresha huduma za usafirishaji kiwanjani hapa”, alisema Waziri Mbarawa.
Aidha,
Profesa Mbarawa amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Nyanza Road
Construction kumaliza kwa wakati upanuzi wa barabara ya ‘Mwanza-Airport’
eneo linaloanzia Ghana Quarters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza KM 9.15
pamoja na daraja la watembea kwa miguu la furahisha ili kukuza uchumi na
kupunguza kero ya msongamano wa magari katika jiji la Mwanza.
Katika
hatua nyingine Prof. Mbarawa amewataka wananchi wa Mwanza kutoharibu
miundombinu ya barabara na madaraja ambayo Serikali inatumia gharama
kubwa katika utengenezaji wake.
“Naomba muitunze na kuithamini miundombinu hii kwani Serikali inatumia gharama kubwa katika kutengeneza na kukarabati”, alisisitiza Prof. Mbarawa.
Ujenzi
wa uwanja wa ndege wa Mwanza ni mkakati wa Serikali kuhakikisha ujenzi
wa uwanja huo unaboreshwa kuwa wa kisasa na wa kimataifa ili kuwezesha
ndege kubwa kutua kwa wingi na kuwa kiungo muhimu kwa mikoa 10 ya kanda
ya Ziwa na Kati.
Mkandarasi
wa kampuni ya Nyanza Road Construction inayojenga barabara ya Furahisha
hadi Pasiansi akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua ujenzi wa barabara
hiyo jijini Mwanza.
Thursday, September 15, 2016
Serikali yatoa majibu ya hatua iliyofikia kuhusu viwanda ilivyovibinafsisha
Serikali
inatekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli la kuhakikisha viwanda vilivyobinafsishwa vinafanya kazi
linatekelezwa tangu mwezi Novemba mwaka 2015.
Hayo yalibanishwa
jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Manyoni Mhe. Yahaya Massare
lililohusu utekelezaji wa ahadi ya Rais kuvirudisha viwanda vyote
vilivyobinafsishwa lakini havifanyi kazi.
Waziri Mwijage alisema
kuwa Serikali kupuitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
inaendelea na zoezi la kuchambua mikataba ya mauzo kwa viwanda
vilivyobinafsishwa ambavyo ama havifanyi vizuri au vimesimamisha
uzalishaji kabisa.
Waziri alibainisha
kuwa timu ya wataalamu toka Wizara ya Viwanda na Ofisi ya Usajili wa
Hazina walifuatilia na kufanya tathimini kwa kutembelea kiwanda baada ya
kiwanda hatua ambayo inasaidia kutafuta ufumbuzi wa matatizo
yaliyopelekea kiwanda kutofanya kazi.
Aidha, Waziri Mwijage alisema
kuwa uchambuzi wa mikataba ya viwanda hivyo unafanyika kwa ushirikiano
na Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na Wizara za kisekta ikiwemo Wizara
ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Nishati na Madini, pamoja na Wizara
ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Hata hivyo, Waziri Mwijage alisema
kuwa katika kutekeleza ahadi hiyo ya Rais, Serikali imetwaa Kiwanda cha
Chai Mponde kilichopo wilaya ya Lushoto mkoani Tanga ambacho mwekezaji
amekiuka makubaliano ya mkataba.
Mbali
na hayo, akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Emmanuel
Mwakasaka lililohusu mpango wa Serikali kujenga maabara ya kupima ubora
na kiwango cha asali inayozalishwa hapa nchini.
Waziri Mwijage alisema
kuwa Serikali inaendelea kuhimiza ujenzi wa viwanda nchini ikiwemo
viwanda vya asali na kuhakikisha vinakuwa na maabara zinazoweza kupima
viwango vya msingi.
Waziri Mwijage aliongeza
kuwa kuhusu ujenzi wa maabara mkoani Tabora, Wizara itahakikisha
wawekezaji wanaofuatilia ujenzi wa viwanda vya asali wanakuwa na maabara
za kupima viwango vya msingi vya msingi na kuiachia TBS kuweka viwango
vya kitaifa na kudhibiti viwango hivyo.
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO, Dodoma
Thursday, September 15, 2016
Kompyuta zenye majibu ya waliopima ukimwi zaibwa
Kompyuta mpakato zenye majibu ya watu waliopima ukimwi pamoja na majina yao zimeibwa mkoani Tabora.
Kompyuta
hizo zipatazo 30 zenye thamani ya Sh70 milioni, zimeibwa kwenye ofisi
ya shirika lisilo la kiserikali la Jhpiego linaloshughulika na masuala
ya Ukimwi na tohara.
Kompyuta
hizo zimeibwa mwishoni mwa wiki kwenye ofisi hiyo iliyo jirani na ofisi
za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa amesema tayari taarifa za tukio
hilo zimewafikia na wanaendelea na uchunguzi wa kina kufahamu
kilichotokea.
Inadaiwa kuwa kompyuta hizo, zina majina ya watu waliopima VVU na majibu yao.
“Kinachotatiza
ni kwamba kama majina ya watu wenye virusi yakijulikana itakuwa ni
utata mkubwa kwani ofisi hiyo itakuwa imewaweka katika wakati mgumu
pasipo wao kupenda,” kilisema chanzo chetu cha habari.
Mkurugenzi wa Jhipego, Dk Albert Komba amethibitisha kutokea kwa wizi huo.
Thursday, September 15, 2016
JK Atoa Ya Moyoni Kuhusu Rais Magufuli Kutokwenda Zambia
Rais
mstaafu, Jakaya Kikwete ameunga mkono uamuzi wa Rais John Magufuli
kuahirisha safari kwenda nje ya nchi ili kushiriki katika maafa ya
tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Kikwete amesema uamuzi huo ni wa busara kwa kuwa Serikali inatakiwa kufanya juhudi za makusudi kushughulikia tatizo hilo.
Kikwete
aliyemtumia salamu za pole Dk Magufuli na waathirika wa tukio hilo,
amesema misaada ya haraka na dharura inahitajika ili waathirika
waendelee kupata huduma zote muhimu hasa za kibinadamu.
Kiongozi
huyo mstaafu ameyasema hayo katika hafla ya makabidhiano ya nyumba 22
za watumishi wa afya, 10 zikiwa Chalinze, mbili Bagamoyo na nyingine 10
Mafia zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa mkoani Pwani.
“Ndugu
zangu pamoja na leo hii tunakabidhiana nyumba 22 za watumishi wa afya
mkoani kwetu, naomba tusimame tuwakumbuke wenzetu waliopoteza maisha
katika tetemeko la ardhi huko Bukoba na pia natumia fursa hii kutoa pole
kwa waathirika wote na Rais Dk Magufuli,” amesema.
Ameongeza kuwa: “kiukweli amefanya uamuzi wa busara kuahirisha safari yake ili kushiriki katika maafa haya.”
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika Kituo cha Afya Msoga, Chalinze.
Thursday, September 15, 2016
Serikali Yabariki Wenye Jinsia Mbili Kuchunguzwa
Mamlaka
ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali itakuwa na uwezo na mamlaka ya
kuchunguza watu waliozaliwa na jinsi mbili na kubaini jinsi tawala yenye
nguvu zaidi.
Muswada
wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka
2016, uliopitishwa juzi usiku saa nne bungeni unampa Mkemia Mkuu mamlaka
ya kuchunguza na kubaini jinsi ya mtu na kutatua utata kwa mtu
atakayekuwa amezaliwa na jinsi mbili.
“Waheshimiwa
wabunge naona wengi wenu mnadhani mkemia mkuu kazi yake ni kuchunguza
vinasaba kubaini uhalali wa mzazi na mtoto, maana naona wabunge wengi
wamelishabikia hilo, lakini katika teknolojia ya vinasaba yanahusu pia
utambuzi wa jinsi, watu unakuta wanawake au wanaume wanazaliwa jinsi ya
kike na kiume, kwa hiyo tunaangalia jinsi tawala ni ipi ina nguvu,” alisema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Ummy
alikuwa akijibu michango ya wabunge waliochangia wakati wa kujadili
Muswada wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu 2016 kabla ya kuupitisha
juzi usiku, waliotaka mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu kutoa elimu kwa
wananchi juu ya shughuli zake.
Alisema
kwa sheria hiyo, sasa mkemia mkuu kupitia maabara yake anaweza kusema
jinsi ya kike au ya kiume ndio yenye nguvu, lakini pia kuna suala la
kuhakikisha utambuzi wa mwanadamu hasa wakati yanapotokea majanga pamoja
na watu wanaosafiri kwa makundi.
Alikubaliana
na wabunge kuwa iko haja ya kuwaelimisha wananchi juu ya kazi za
maabara ya mkemia mkuu ambao wengi wao wanadhani inafanya kazi hiyo tu
ya kubaini vinasaba vya mzazi na mtoto, lakini sasa wafahamu hata
waliozaliwa na jinsi mbili wanaweza kutegua utata huo kwa kubaini jinsi
tawala au jinsi yenye nguvu zaidi kama ni ya kiume au ya kike.
Alisema
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekuwepo kihistoria tangu mwaka
1890 na imekuwa chombo cha kiserikali cha uchunguzi cha kikemia wa
kimaabara kwa bidhaa mbalimbali na kuongeza kuwa imekuwa ikifanya
uchunguzi wa kikemia wa vyakula, dawa na vipodozi hasa pale inapotokea
utata au kuhusisha masuala ya kesi za jinai.
Akifafanua
zaidi, alisema kwa upande wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wao
wanafanya udhibiti wa ubora wa chakula, dawa na vipodozi na maabara hii
inafanya uchunguzi wa kikemia.
“Maabara
ya Mkemia Mkuu kazi yake ni kufanya uchunguzi wa kikemia, vinasaba,
kesi za jinai na sayansi jinai. Chombo hiki hakipimi kudhibiti ila
kufanya uchunguzi kwa ajili ya vitu vyenye maslahi ya taifa au masuala
yenye utatanishi na ushindanishi,” alisema waziri huyo.
Akitoa
mfano wa mahindi, alisema kulikuwa na tatizo la sumu kuvu, kwa hiyo
mkemia mkuu anafanya uchunguzi wa kimaabara na kusema wamekuta mahindi
yana sumu au la, au anaweza mfanyabiashara kuleta maziwa ya mtoto TFDA
ikapata mashaka, mkemia mkuu atayafanya uchunguzi wa maabara atasema
kama kuna sumu ama kuna kemikali isiyo salama kwa matumizi wa binadamu.
“Baada
ya uchunguzi wa kimaabara mwenye jukumu la kusema mahindi haya yasiuzwe
au maziwa haya yasiuzwe ni TFDA na sio maabara ya mkemia mkuu. Vile
mfanyabiashara anaweza kuleta bidhaa, TFDA ikaitilia mashaka, kwa hiyo
huyu mwenye bidhaa anaweza kukata rufaa kwa mkemia mkuu ili apimiwe
bidhaa yake kuithibitishia TFDA kuwa bidhaa yake ni salama,” alisema.
Waziri
Ummy alikuwa akijibu hoja za wabunge, ambao walikuwa wana hofu kuwa
Maabara ya Mkemia Mkuu inaweza kuingilia kazi za taasisi kama TFDA na
Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Alizungumzia
pia kuhusu kuipa mamlaka ya mwisho maabara hiyo, akisema katika nchi
zote duniani zenye maabara hizo, lazima serikali iwe na msemaji wa
mwisho wa uchunguzi wa masuala ya kimaabara na kikemia, vinasaba,
sayansi jinai na kesi za jinai, lakini pia haifuti sheria wala maabara
zingine za uchunguzi zilizoanzishwa kwa mujibu wa sheria mbalimbali.
Kuhusu
kutenga bajeti ya kutosha, Ummy alisema serikali imepokea maoni ya
wabunge na kuwa baada ya kupitisha muswada huo maabara hiyo imepewa
hadhi ya mamlaka na sasa imepewa hadhi na hivyo fungu lake lazima liwe
zuri kwa ajili kuendesha shughuli za maabara lakini pia kuajiri
watumishi 400 kwani waliopo sasa 192 hawatoshi.
Waziri
Ummy alisema wamepokea ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, kufanya
uchunguzi wa matumizi ya shisha na kuongeza kuwa tayari mkemia mkuu
alifanya uchunguzi na kubaini watumiaji wa shisha wanachanganya bangi,
heroine na kokeni na ndio maana serikali ilipiga marufuku kuitumia.
Hata
hivyo, alisema sasa itajikita zaidi kuchunguza ili kubaini viambata
kiasi gani vilivyopo katika shisha na kwa nini serikali iendelee kupiga
marufuku matumizi ya shisha nchini.
Thursday, September 15, 2016
Gavana BOT afichua siri ya kilio cha fedha kupotea mtaani
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi
hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha
fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema
kuwa kwakuwa taasisi hiyo ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki
na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa hakuna fedha iliyopotea bali fedha
zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa njia ya udanganyifu kwakuwa
sasa Serikali imebana mianya hiyo.
“Hakuna
fedha iliyopotea, Serikali imebana shughuli za watu na ‘mission town’
sasa shughuli zote zinafanywa na Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea,
lakini kwetu hazijapotea,” alisema Profesa Ndulu.
Hata
hivyo, Profesa Ndulu alikiri kupungua kwa fedha katika mabenki nchini
hali iliyopelekea kupunguza kasi ya utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema
hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za mashirika ya umma na taasisi
kutoka benki za biashara kwenda BoT.
“Fedha
hizo zitarudi katika benki hizo wakati zitakapopelekwa kwenye
Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali,” Profesa Ndulu
aliahidi.
Katika
hatua nyingine, Gavana huyo wa Benki Kuu alisema kuwa uchumi
unatarajiwa kukuwa kwa asilimia 7.2 mwaka huu, huku akibainisha kuwa
moja kati ya sababu zinazopelekea ukuaji huo ni ongezeko la uzalishaji
wa umeme na saraju.
Akizungumzia
hali ya deni la taifa, alisema kuwa deni la taifa la ndani limeongezeka
kutoka shilingi trilioni 8.6 Mwezi Desemba mwaka jana hadi shilingi
trilioni 10 mwezi Juni mwaka huu.
Profesa
Ndulu alibainisha kuwa wakati deni linalotokana na kukopa ndani
likipaa, deni linatokana na ukopaji wa limepungua baada ya Serikali
kupunguza ukopaji nje ya nchi.
Thursday, September 15, 2016
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Beno Ndulu Atoa Taarifa Kuhusu Hali Halisi ya Uchumi wa Tanzania
1.0 Hali ya Uchumi wa tanzani
1.1 Ukuaji
wa Uchumi
Kwa
mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, hali ya ukuaji wa uchumi wa
Tanzania imeendelea kuwa ya kuridhisha. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016,
ukuaji wa Pato la Taifa unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 5.5 ikilinganishwa
na ongezeko la asilimia 5.7 kipindi kama hicho mwaka 2015 (Kielelezo Na. 1).
Kielelezo Na. 1:
Mwenendo wa Ukuaji wa Uchumi Robo ya Kwanza ya Mwaka (Asilimia)
Chanzo: NBS, Ukokotoaji - Benki Kuu
Shughuli zilizochangia ukuaji huu wa uchumi kwa kiasi kikubwa ni pamoja na kilimo
(asilimia 11.7), biashara (asilimia 10.6), uchukuzi (asilimia 10.1), sekta ya
fedha (asilimia 10.1) na mawasiliano (asilimia 10.0).Shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi ya juu zaidi katika
robo ya kwanza ya mwaka 2016 ni sekta ya fedha (asilimia 13.5), mawasiliano
(asilimia 13.4), na utawala wa umma (asilimia 10.2) (Kielelezo Na. 2).
Kielelezo Na. 2a:
Ukuaji wa Shughuli Mbalimbali za Uchumi Robo ya Kwanza ya Mwaka (Asilimia)
Kielelezo Na. 2b: Mchango wa Shughuli
Mbalimbali za Uchumi katika Ukuaji wa Uchumi Robo ya Kwanza ya Mwaka (Asilimia)
1.2 Matazamio
ya Ukuaji wa Uchumi Mwaka 2016
Kwa kuangalia viashiria mbalimbali inaonekana kuwa hali ya uchumi wetu itaendelea
kuimarika katika mwaka 2016. Kwa mfano:
Uzalishaji wa umeme nchini katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 umeongezeka kwa
asilimia 14.5 kufikia kWh milioni 3,454.2 ikilinganishwa na kWh milioni 3,016.7
katika kipindi kama hicho mwaka 2015. Ongezeko hili limetokana kwa kiasi
kikubwa na jitihada za serikali katika kutumia nishati ya gesi kwenye
uzalishaji umeme kufuatia kukamilika kwa bomba la gesi kutoka Mtwara na Lindi hadi
Dar es Salaam pamoja na mtambo wa Kinyerezi I. Umeme unaozalishwa kwa kutumia
nishati ya gesi umeongezeka kwa asilimia 52.2 (Kielelezo
Na. 3). Hali hii itasaidia kuongezeka kwa
uzalishaji viwandani pamoja na sekta nyingine zinazotegemea nishati ya umeme, na
hivyo kuchangia katika kuongeza kwa pato la Taifa. Gharama ya umeme itashuka pia.
Kielelezo Na. 3:
Mwenendo wa Uzalishaji Umeme Nchini
Januari - Juni
Uzalishaji wa saruji katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 umeongezeka kwa
asilimia 7 kufikia tani elfu 725.4 ikilinganishwa na tani elfu 680.1 zilizozalishwa
katika robo ya kwanza ya mwaka 2015. Hali hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na
ongezeko la uzalishaji wa kampuni ya Dangote ambayo ina uwezo wa kuzalisha tani
milioni tatu kwa mwaka (Kielelezo Na. 4). Ni matarajio yetu kwamba
uzalishaji katika kiwanda cha Dangote chenye uwezo wa tani milioni 3 na katika viwanda
vingine vya saruji nchini utaongezeka katika kipindi kilichobaki cha mwaka 2016
kwani mahitaji ya nchi bado ni makubwa kuliko uzalishaji ulivyo hivi sasa. Aidha kuna miradi mikubwa mingi ya hapo
baadaye itakayokuwa na mahitaji makubwa ya saruji kama vile mradi wa reli ya
kati.
Kielelezo Na. 4:
Mwenendo wa Uzalishaji Sarujii
Januari – Machi
Uagizaji wa malighafi
za viwandani kutoka nje umeongezeka kwa
asilimia 19.4 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 kufikia Dola za Marekani
milioni 520.2 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2015 (Kielelezo
Na. 5). Hali hii imechangiwa na kuendelea
kukua kwa shughuli za uzalishaji viwandani. Ukuaji huu utaendelea kuchangia
pato la Taifa kiujumla katika mwaka 2016.
Kielelezo Na. 5:
Mwenendo wa Uagizaji Malighafi za Viwandani
Januari – Juni
Mauzo ya bidhaa za
viwanda nje ya nchi yameendelea kukua kwa kasi
ya kuridhisha. Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 mauzo ya bidhaa nje ya nchi
yalifikia kiasi cha Dola za Marekani milioni 728.5, sawa na ongezeko la
asilimia 15.6 ikilinganishwa na kiasi kilichouzwa kipindi kama hicho mwaka 2015
(Kielelezo Na. 6).
Kielelezo Na. 6:
Mwenendo wa Uuzaji wa Bidhaa za Viwandani Nje ya Nchi
Januari – Juni
Makusanyo ya kodi katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 yameendelea kuwa
bora zaidi ikilinganishwa na nusu ya kwanza ya mwaka 2015, ikiashiria kuimarika
kwa usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuendelea kuimarika kwa
hali ya
uchumi wa nchi.
Mikopo itolewayo na mabenki
ya biashara kwenye sekta binafsi,
imeendelea kuongezeka kwa kasi ya kuridhisha katika nusu ya kwanza ya mwaka
2016 kwa Shilingi bilioni 1,167.2, japo ni pungufu ikilinganishwa na ongezeko
la Shilingi bilioni 1,577.5 la mwaka 2015. Ongezeko hili linaendana na malengo
ya sera ya mwaka 2015/16 ambayo yanajumuisha utulivu wa mfumuko wa bei (Kielelezo
Na. 7).
Kielelezo Na. 7:
Mwenendo wa Ongezeko la Mikopo kwa Sekta Binafsi
Januari - Juni
Chanzo: Benki kuu
Miradi mikubwa ya
viwanda na miundombinu inayoendelea na inayotarijiwa kuanza kazi siku za usoni
itachangia katika kuimarisha uchumi. Hii ni pamoja na:
Ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge)
Ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda ambalo
litahusu vile vile upanuzi wa bandari ya
Tanga
Ujenzi wa Export Processing Zone ya Kurasini
– itakayokuwa mhimili wa biashara kati ya China na Ukanda huu wa Afrika
Mradi wa kuzalisha megawati 240 za umeme wa
Kinyerezi II unaoendelea kujengwa.
Miradi ya kupanua viwanja vya ndege nchini
kwa mfano- Dodoma, na mingine inayoendelea -katika viwanja vya Dar es Salaam,
Mwanza, Mbeya n.k.
Ujenzi wa maghala ya taifa ya kuhifadhi
chakula yenye uwezo wa kuhifadhi tani 350 yatakayojengwa kwa msaada wa Serikali
ya Hungary katika sehemu mbalimbali nchini hususan katika mikoa inayozalisha
mazao ya nafaka kwa wingi.
Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote
kilichopo Mtwara ambacho kipo mbioni kuzalisha kulingana na uwezo wake (full
capacity);
Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha
Mkuranga, Pwani ambacho ujenzi wake unaendelea
Kiwanda cha kuzalisha mbolea mkoani Lindi -
kinajengwa
Kiwanda cha bidhaa za chuma – mkoani Pwani
ambacho kiko mbioni kukamilika.
Kwa kuzingatia mwenendo wa viashiria mbalimbali vya shughuli za uchumi, ni
dhahiri kwamba hali ya uchumi wa Tanzania ni nzuri na inatoa matumaini makubwa
kwamba shughuli halali za kiuchumi zinaendelea kutekelezwa kama ilivyotarajiwa hapo
awali hivyo lengo la ukuaji wa pato la Taifa la asilimia 7.2 kwa mwaka 2016
litafanikiwa. Hii inachangiwa pia na ukweli kwamba serikali ya awamu ya tano imejipanga
katika kuimarisha uchumi endelevu usiokuwa na mianya ya rushwa; usimamizi
thabiti wa rasilimali za umma; na ujenzi wa miundombinu bora kwa lengo la
kujenga uchumi wa viwanda chini ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
Wastani wa mfumuko wa bei katika
miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016 umeendelea kuwa mzuri ukiendelea kushuka
hadi kufikia asilimia 5.5 mwezi Juni 2016 na asilimia 4.9 mwezi Agosti 2016
kutoka asilimia 6.8 mwezi Desemba 2015 (Kielelezo
Na. 8). Kushuka huku kwa wastani wa mfumuko wa bei kulichangiwa zaidi na
bei zisizojumuisha bei za vyakula na nishati (core inflation) zikifuatiwa na zile za nishati na mafuta. Wastani
wa mfumuko wa bei usiojumuisha bei za vyakula na nishati (core inflation), ambao ni kiashiria sahihi zaidi cha utekelezaji wa
sera ya fedha, umeendelea kubaki katika viwango vya chini (wastani wa asilimia
2.8 katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2016) kutokana na hatua mbalimbali thabiti
za sera ya fedha na bajeti katika kudhibiti ujazi wa fedha na ukwasi katika
uchumi.
Mfumuko wa bei unatarajiwa kuendelea
kubakia katika viwango vya tarakimu moja katika siku zijazo na kufikia lengo la
muda wa kati la asilimia 5. Hii ni kutokana na matarajio ya hali nzuri ya hewa itakayochangia
kupungua kwa kasi ya kuongezeka kwa bei za vyakula, pamoja na ongezeko dogo la
bei ya mafuta nchini inayotokana na mwenendo wa bei ya mafuta katika soko la
dunia, na utulivu wa thamani ya Shilingi. Pia, mwendelezo wa sera thabiti ya
fedha, usimamizi mzuri wa matumizi na mapato ya Serikali, na upatikanaji wa
umeme utokanao na gesi ambao utasaidia kupunguza gharama za uzalishaji
viwandani vitaendelea kuimarisha utulivu wa mfumuko wa bei. Hata hivyo ni
muhimu kuzingatia kuwa upungufu wa mavuno ya mazao ya chakula uliojitokeza kwa
baadhi ya nchi za ukanda wa kusini mwa Afrika unaweza kusababisha shinikizo la
mfumuko wa bei katika siku za usoni.
Kielelezo Na. 8:
Mwenendo wa Mfumuko wa Bei (Badiliko la Miezi 12)
Chanzo: Benki kuu
1.4 Utekelezaji wa Sera ya Fedha
Ili kufikia malengo ya serikali ya
kuimarisha uchumi na kudumisha utulivu wa mfumuko wa bei, Benki Kuu imeendelea
kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti ukwasi ili uendane na mahitaji
halisi ya uchumi. Ongezeko la fedha taslimu (reserve money) ambacho ni kipimo cha ukwasi kwenye uchumi
limeendelea kubakia ndani ya malengo katika kipindi chote cha miezi sita ya
kwanza ya mwaka 2016. Katika kipindi hicho ujazi wa fedha taslimu ulikua kwa
wastani wa asilimia 11.6; wakati ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3)
ulikua kwa wastani wa asilimia 14.4, ikiwa ni ndani ya makadirio ya ukuaji
usiozidi asilimia 16.0 kwa mwaka 2015/16.
Wakati huohuo sekta ya fedha imeendelea kuchangia ukuaji wa
shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kasi nzuri ya kutoa mikopo kwa wakati na
kwa kiwango cha kutosha. Mikopo kwa sekta binafsi ilikua kwa wastani wa asilimia
21.3 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016, sawa na kiwango kilichopatikana
katika kipindi kama hicho mwaka 2015. Mikopo mingi kwa sekta binafsi
ilielekezwa kwenye shughuli za biashara kwa wastani wa asilimia 19.3 ya jumla
ya mikopo yote, shughuli za watu binafsi wastani wa asilimia 19.0, uzalishaji
viwandani wastani wa asilimia 10.6, uchukuzi na mawasiliano wastani wa asilimia
7.9, na shughuli za kilimo asilimia 7.8.
Benki Kuu inaendelea kutekeleza sera madhubuti ya fedha kwa kutumia
zana mbalimbali za sera ili kuhakikisha kwamba mahitaji ya ukwasi kwa ajili ya
shughuli mbalimbali za kiuchumi yanafikiwa bila ya kuchochea mfumuko wa bei.
1.5
Mwenendo wa Thamani ya Shilingi ya Tanzania
Thamani ya Shilingi imeendelea
kuwa tulivu katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, kufuatia hatua mbalimbali za
sera ya fedha zilizochukuliwa na Benki Kuu katika kusimamia hali ya ukwasi
kwenye uchumi pamoja na mwenendo wa uchumi ndani na nje ya nchi. Kuimarika kwa
sekta ya nje kulikotokana na ongezeko la mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi
na kupungua kwa thamani ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje kumechangia katika
utulivu wa thamani ya shilingi. Kupungua kwa thamani ya bidhaa kutoka nje kumechangiwa
zaidi na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. Katika kipindi cha
miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2016 Shilingi imekuwa ikibadilishwa kwa kati
shilingi 2,180 hadi 2,190 kwa dola moja ya Marekani (Kielelezo Na. 9).
Kielelezo Na. 9: Mwenendo wa Thamani ya Shilingi
Chanzo:Benki kuu
Hali hii ya
utulivu wa thamani ya Shilingi kwenye soko huru la fedha inadhihirisha kuwa sera
thabiti za uchumi pamoja na mwenendo mzuri wa urari wa mapato ya fedha za
kigeni, ndio jawabu la kulinda thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni na
sio kudhibiti matumizi ya dola kama ambayo imekuwa ikidaiwa mara kwa mara. Nchi
zenye udhibiti mkubwa wa fedha za kigeni mfano Afrika Kusini imeshuhudia
kuyumba sana kwa thamani ya fedha yake tofauti na shilingi ya Tanzania.
Hivyo nguvu
kubwa inapaswa ielekezwe katika kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta
mbalimbali hususan zile zinazoboresha urari wa malipo ya nje kama vile utalii,
viwanda, uchimbaji madini, kilimo n.k. Ikumbukwe kuwa uhuru wa kumiliki na
kutumia fedha za kigeni nchini Tanzania uliwekwa kama hatua ya kukabiliana na
hali iliyokuwepo miaka ya 1980 ya kuadimika sana kwa fedha za kigeni na mchango
wa uhuru huo tumeuona katika kuwepo kwa fedha za kigeni za kutosha. Nchi
zilizojaribu kuondoa uhuru huo, mfano Zambia, zimeshuhudia kutoweka kwa fedha
za kigeni kwenda nje. Hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuhimiza na kuweka
mazingira mazuri ya uzalishaji na kuondokana na fikra za kuingilia soko huru kama
jawabu la kulinda thamani ya shilingi.
1.6 Mwenendo wa Sekta ya Kibenki
Katika
miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016, sekta ya kibenki imeendelea kukua
ikichangiwa na uanzishwaji wa taasisi mpya za kifedha ikiwemo Benki ya Waalimu
Tanzania (Mwalimu Commercial Bank Plc) na Canara Bank (Tanzania) Limited.
Takwimu za awali za tathmini ya hali ya mabenki yetu zinaonesha kuwa mabenki
yetu ni imara na salama, yakiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha. Kufikia mwezi
Juni 2016, kulikuwa na jumla ya benki na taasisi za fedha zinazosimamiwa na
Benki Kuu zipatazo 65 zenye matawi 739 nchini kote.
Kiwango cha mitaji kikilinganishwa na mali iliyowekezwa (total
capital to total risk weighted assets and off-balance sheet exposures)
kilikuwa asilimia 17.17 kikilinganishwa na kiwango cha chini kinachotakiwa
kisheria cha asilimia 12.0. Hali ya ukwasi ambayo hupimwa kwa kuangalia uwiano
kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu na amana zinazoweza
kuhitajika katika muda mfupi (liquid assets to demand liabilities) ulikuwa
asilimia 37.03 ukilinganishwa na uwiano wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia
20 (Jedwali Na. 1).
Amana za wateja katika mabenki zilipungua kutoka shilingi
trilioni 20.52 mwezi Desemba 2015 kufikia shilingi trilioni 20.24 mwezi June
2016. Miongoni mwa sababu zilizochangia kupungua kwa amana kwenye mabenki ni
pamoja na uamuzi wa Serikali kuhamisha sehemu ya fedha za taasisi na mashirika
ya umma kutoka mabenki ya biashara kwenda Benki Kuu ya Tanzania. Aidha mikopo (loans and overdafts) iliongezeka kutoka
shilingi trilioni 15.28 mwezi Desemba 2015 hadi kufikia shilingi trilioni 15.67
mwezi Juni 2016.
Upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wasiofikiwa
na mabenki umeendelea kuongezeka kutokana na ubunifu wa mipango ya utoaji wa
huduma za malipo ya rejareja kupitia simu za mikononi, pamoja na huduma za
uwakala wa mabenki (agent banking services).
Kiujumla kwa
kuangalia viashiria vyote vya msingi hali ya ukwasi wa benki imeendelea kuwa ya
kuridhisha. Benki Kuu katika kusimamia majukumu yake ya kisera, imeendelea
kutoa mikopo ya muda mfupi kupitia “reverse
repos” pamoja na kununua fedha za kigeni zinazotokana na mauzo ya bidhaa
nje ya nchi kutoka kwenye benki. Kwa viashiria hivi ni dhahiri kwamba uamuzi wa
serikali wa kuagiza fedha zake zote kuwekwa kwenye akaunti maalum Benki Kuu
hakujasababisha sekta ya kibenki kutokuwa na ukwasi wa kutosha na kuacha
kukopesha kwa sekta binafsi kama inavyofikiriwa na baadhi yetu.
Ni vyema jamii ya
Watanzania ikafahamu kwamba akaunti ambazo fedha za mashirika zimehamishiwa
Benki Kuu ni akaunti za kukusanya mapato tu. Akaunti za matumizi bado ziko
katika benki za biashara ili kuyawezesha mashirika kufanya malipo kupitia
akaunti hizo. Hivyo, bado benki za biashara ni kiungo muhimu kati ya mashirika
ya umma na watoa huduma kwa mashirika hayo. Pia hali ya utoaji mikopo kama
tulivyoona awali ni nzuri na watanzania wanaendelea kuhudumiwa na benki zetu
kama inavyotarajiwa.
Jedwali Na. 1: Viashiria vya Uimara wa Sekta ya Fedha
1.7 Sekta
ya Nje na Akiba ya Fedha za Kigeni
Katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016, nakisi ya urari wa biashara ya
bidhaa, huduma na uhamisho mali nchi za nje (current account deficit) ilipungua kwa asilimia 61.7 na kufikia
nakisi ya dola za Kimarekani milioni 970.4, kutoka nakisi ya dola za Kimarekani
milioni 2,532.5 mwaka 2015. Kupungua huko kulitokana zaidi na ongezeko la
thamani ya bidhaa za viwandani, mapato yatokanayo na utalii na huduma za
usafirishaji nje ya nchi, pamoja na kupungua kwa thamani ya bidhaa zilizoagizwa
kutoka nje ya nchi hususan bidhaa za mitaji, na bidhaa za matumizi ya kawaida. Katika
kipindi cha miezi sita iliyoishia Juni 2016, kikilinganishwa na kipindi kama
hicho mwaka uliotangulia, thamani ya bidhaa na huduma zilizouzwa nje ya nchi
ziliongezeka kwa asilimia 14.2 na kufikia dola za Kimarekani milioni 4,473.2
wakati thamani ya bidhaa na huduma toka nje zilipungua kwa asilimia 18.3 na
kufikia dola za Kimarekani milioni 5,360.7
Hazina ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha na kuendelea
kukidhi mahitaji ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza bidhaa na huduma nje
ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuongeza imani kwa wawekezaji katika uchumi wetu;
japo kumekuwepo na ucheleweshwaji wa fedha za wahisani na mikopo ya kibiashara
kutoka nje ya nchi. Hadi mwezi June 2016, akiba ya fedha za kigeni ilifikia
dola za Kimarekani milioni 3,870.3 ambazo zinatosheleza kuagiza bidhaa na
huduma kutoka nje ya nchi kwa takriban miezi 4. Wakati huo huo, rasilimali za
fedha za kigeni za mabenki (gross foreign
assets) zilikuwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 835.0
1.8 Deni
la Taifa
Deni la Taifa limeendelea kuongezeka na kufikia dola za Kimarekani milioni
20,851 mwishoni mwa mwezi Juni 2016, kutoka dola za Kimarekani milioni 19,861
mwezi Desemba 2015. Deni la nje liliongezeka kwa asilimia 2.6 na kufikia dola
za Kimarekani milioni 16,281 mwezi Juni 2016 (sawa na asilimia 77.8 ya deni la
taifa), kutoka dola za Kimarekani milioni 15,864 mwezi Desemba 2015. Hii
ilitokana na kuongezeka kwa mikopo mipya pamoja na malimbikizo ya malipo ya
madeni. Katika deni hilo la nje, asilimia 83.4 ni deni la Serikali na taasisi
za umma. Pamoja na ongezeko hilo, takwimu zinaonyesha kuwa deni letu bado ni
stahimilivu. Kwa mfano, deni la nje kwa thamani ya sasa (Net Present Value) ni karibu ya asilimia 20 ya Pato la Taifa,
ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 50 ya Pato la Taifa (Sept-15 DSA). Hii
inaonyesha kuwa bado kuna nafasi kubwa ya kukopa bila kuhatarisha ustahimilivu wa
deni letu.
Deni la ndani liliongezeka kufikia shilingi bilioni 10,038.4 mwishoni mwa
mwezi Juni 2016 kutoka shilingi bilioni 8,597.0 mwezi Desemba 2015. Ongezeko
hilo lilitokana na Serikali kukopa kupitia dhamana na hati fungani ajili ya
kugharamia bajeti ya Serikali kwa mwaka 2015/16, ikichangiwa pia na kupungua
kwa misaada na mikopo kutoka nje.
Jedwali Na 2 linaonyesha
vyanzo vya fedha za Serikali na matumizi yake katika kipindi cha miezi 6
kuanzia Januari hadi Juni 2016. Kama inavyoonekana jumla ya mapato ya ndani
ilikuwa shilingi bilioni 7,267 wakati matumizi ya kawaida (ukiondoa riba)
yalikuwa shilingi bilioni 6,488, hivyo mapato yalitosha kulipia matumizi ya
kawaida ya Serikali. Hii ni kuonyesha kwamba madeni ya nje na ndani yalitumika
kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na kurejesha madeni yaliyopita.
Jedwali Na. 2: Vyanzo vya Fedha vya
Serikali na Matumizi Yake (Shilingi bilioni)
Thursday, September 15, 2016
Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli
VIJANA
watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Dk.
John Magufuli na Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi
wanne waliouawa na majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es
Salaam hivi karibuni.
Washtakiwa
hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
Salaam mbele ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na Wakili
wa Serikali, Salum Mohammed.
Walisomewa
mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, Huruma Shahidi,
Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage.
Akisomewa
mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24, mwaka huu eneo la
Ubungo External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka maoni katika group
linaloitwa Dsm 11 4u Movement, akisema ‘JPM sijui anawaza nini
kichwani… hata samahani hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa
kwa sababu ya mtu mmoja aliyeamua kujilipua ufahamu wake’, ‘sijaona
tatizo kwa hilo, ila kwa huyu bwana misimamo ambaye amesema msinijaribu
na ilhali kajaribiwa na ubwabwa wa jubilee kusema yote’.
‘Siasa
si chuki wala upinzani si uadui, ajifunze kushindana kwa hoja sio
mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo na kichwa wala miguu ya polisi’.
Mshtakiwa Suleiman Saidi anadaiwa Agosti 25, mwaka huu maeneo ya Kigogo, kwa kutumia mtandao wa Facebook, aliandika ‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.
Katika
kesi nyingine, mshtakiwa Juma Mtatuu akiwa eneo la Ocean Road, Agosti
24, mwaka huu anadaiwa kuwa alituma ujumbe katika Facebook akisema ‘Huyu
hata akifa ataenda peponi, na kufanya mazoezi kote kule wamekufa
Mbagala, mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama, tarehe moja
naelekea Kahama kwa Ukuta, mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya
Ukuta, kifo kipo tuu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha’
KATIKA HABARI ZA KIMATAIFAA
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Mapambano yarindima upya mashariki mwa Ukraine
Waasi wanaotaka kujitenga nchini Ukraine na vikosi vya
serikali wanalaumina juu ya ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha vita
yaliyotakiwa kuanza usiku wa kuamkia leo huko mashariki mwa nchi
hiyo.Siku ya Jumanne waasi walitangaza hatua ya upande mmoja ya
kusitisha vita ambapo waziri wa amambo ya nje wa Ujerumani
aliyeitembelea nchi hiyo alisema siku iliyofuatia kwamba serikali pia
imekubali kusitisha mapigano.Hii leo Televisheni ya Urusi imenukuu
maafisa wa waasi wakisema kwamba vikosi vyao vilishambuliwa kwa
makombora mapema asubuhi.Msemaji wa jeshi la Ukraine Ivan Arefyev
amesema mapigano yalizuka usiku wa manane lakini waasi walitumia silaha
ndogo ndogo na mabomu ya kurusha kwa mkono majira ya asubuhi.Mawaziri wa
mambo ya nje wa Ufaransa na Ujerumani ambao ndio wasuluhishi wakuu
katika mgogoro huo wa Ukraine walikutana jana na rais wa nchi hiyo na
wanatarajiwa kuelekea upande wa mashariki hii leo.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Msaada wa kiutu bado haujawafikia wasyria wanaokabiliwa na dhiki
Hatua ya kusitisha mapigano nchini Syria imeendelea
kuheshimiwa hii leo licha ya kuripotiwa mara kadhaa kutokea ukiukaji.
Hata hivyo msaada wa kibinadamu haujaweza kufika katika nchi hiyo na
umezuiwa katika eneo la mpakani na Uturuki. Shirika linalofuatilia haki
za binadamu nchini Syria limesema kwamba tangu kuanza kwa usitishaji huo
wa mapigano Jumatatu usiku hakujakua na dalili za malori ya msaada
kuingia ndani ya Syria.Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
amesema kiasi malori 20 ya msaada yameegesha katika eneo la mpaka na
Uturuki yakisubiri kuingia Syria.Mamia kwa maelfu ya wasyria bado
wanakabiliwa na hali ya kuzingirwa au kuwepo katika maeneo yasioyoweza
kufikika nchini humo.Serikali ya Syria inapinga hatua ya kuingizwa
msaada nchini humo bila ridhaa yake wakati waasi wanataka msaada huo
usiingizwe kupitia maeneo kadhaa yaliyoko chini ya vikosi vya rais
Bashar al Assad.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Oxfam yatoa ripoti muhimu juu ya hali ya wakimbizi duniani
Kiasi wakimbizi milioni 3.8 na wanaoomba hifadhi ya uhamiaji
walizikimbia nchi zenye mizozo na kuingia katika nchi nyingine zenye
mizozo. Hayo yamesemwa na shirika la msaada la Oxfam katika ripoti yake
iliyochapishwa hii leo.Shirika hilo limetowa mfano wa Yemen nchi
inayokumbwa na vita na iliyo masikini katika Mashariki ya kati kwamba
kuna kiasi watu milioni 2 wanaoishi kama wakimbizi wa ndani lakini nchi
hiyo vile vile inawahifadhi wakimbizi kutoka nchi nyingine zenye mizozo
kama Eritrea,Ethiopia na hata Syria.Ripoti ya Oxfam imetolewa wiki moja
kabla ya rais Barack Obama kuongoza mkutano wa kwanza wa kilele wa
Umoja wa Mataifa juu ya wakimbizi mjini New-York.Obama anatarajiwa
kuwatolea mwito viongozi wa dunia kuchukua hatua zaidi kuwasaidia
wakimbizi katika nchi kama Lebanon,Uturuki,Kenya na Jordan.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Mradi tata wa nyuklia wa Hinkley kutathminiwa
Serikali ya Uingereza imesema leo kwamba imetoa ruhsa ya
kuendelea kwa mradi wenye utata wa nyuklia wa Hinkley baada ya Waziri
Mkuu Theresa May kutoa maagizo ya kufanyika tathmini juu ya mradi
huo.Katika taarifa waziri wa biashara Greg Clark ameeleza kwamba baada
ya mapendekezo ya mradi huo wa Hinkley kufanyiwa mapitio
kitakachofuatia ni kuanzishwa msururu wa hatua za kuhakikisha usalama na
kuhakikisha kwamba mradi huo haufanyiwi mabadiliko bila ya ridhaa ya
serikali.Awali bodi ya kampuni ya umeme inayomilikiwa na serikali ya
Ufaransa EDF iliidhinisha hatua ya kushiriki kwake katika mradi huo wa
kusini magharibi mwa England na baadae serikali mpya ya Uingereza
ikiongozwa na Theresa May ilitangaza kwamba inataka kuutathmini upya
mradi huo.China inahodhi robo ya hisa za mjradi huo,na wachambuzi
walionya kwamba Uingereza ingehatarisha uhusiano wake na nchi hiyo
endapo ingeufutilia mbali mradi huo wa nyuklia.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Benki ya dunia yasikitishwa na kiwango cha ufadhili wa Gaza
Benki ya Dunia imesema kwamba fedha zilizotolewa na wafadhili
kwa ajili ya ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza ni chini ya nusu ya kiwango
kilichoahidiwa kutolewa na wafadhili hao baada ya vita kati ya kundi la
Hamas na Israel mwaka 2014. Upungufu huo ni miongoni mwa sababu kadhaa
zinazochangia kuulemaza uchumi wa Palestina ambako kiwango cha wasiokuwa
na ajira katika Ukanda huo wa Gaza kimefikia asilimia 42 na asilimia 18
upande wa Ukingo wa Magharibi.Benki hiyo ya dunia pia imesema kwamba
vizuizi vya Israel vinachangia kuurudisha nyuma uwezo wa Palestina
kushindana kiuchumi na kuwafukuza wawekezaji wa kibinafasi.Taasisi hiyo
ya fedha ya dunia imeshauri kwamba Israel iruhusu ujenzi zaidi wa
majengo katika ukingo wa Magharibi na kupunguza vizuizi vyake
Gaza.Ripoti hiyo iliyotolewa leo itawasilishwa kwa kamati maalum ya nchi
wafadhili kwa ajili ya Palestina huko New-York wiki ijayo.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Angela Merkel alivalia njuga suala la ajira kwa wakimbizi
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema Ujerumani inahitaji
mpango unaotekelezeka wa kuwajumuisha wakimbizi katika mfumo wa nguvu
kazi haraka iwezekanavyo. Hayo Bi Merkel ameyasema leo katima mkutano na
makambuni muhimu ya Ujerumani, ambayo yamewaajiri wakimbizi 100
miongoni mwa zaidi ya milioni moja waliowasili nchini Ujerumani mwaka
uliopita. Kansela Angela Merkel ambaye umaarufu wake umeshuka kutokana
na sera yake ya kuwafungulia mlango wakimbizi, hapo jana alikutana mjini
Berlin na wakurugenzi wa makampuni muhimu, akitaka kujua kwa nini
hawachukui hatua, na kujadiliana nao juu ya namna ya kurekebisha hali
hiyo. Makampuni mengi yanasema vikwazo vikubwa vya kuwaajili wakimbizi
ni ufahamu haba wa lugha ya kijerumani, na kushindwa kwa wakimbizi hao
kuthibitisha uhalali wao wa kuishi nchini Ujerumani kwa muda mrefu.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Clinton arudi kwenye kampeini yake
Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic nchini
Marekani Hillary Clinton amerudi tena katika kampeini ya uchaguzi baada
ya kutibiwa maradhi ya homa ya mapafu yaliyomzuia kuonekana kwenye
kampeini hizo kwa siku tatu na kusababisha kuibuka maswali juu ya kwa
kiasi gani wagombea wa vyama vyote viwili Democratic na Republican
wanavyoweza kuzungumzia juu ya afya zao.Kambi ya kampeini ya Clinton
imejibu kwa kutangaza barua mpya ya daktari wake inayosema mgombea huyo
ana afya ya kuweza kuongoza taifa.Kwa upande mwingine mgombea wa
Republican Donuld Trump amesema hata yeye anapanga kutangaza hali yake
ya kiafya ingawa haifahamiki lini atatoa maelezo hayo na kwa kiwango
gani.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Maandamano yaitikisa upya miji ya Ufaransa
Waandamanaji wameingia mitaano kote nchini Ufaransa hii leo
katika hatua mpya ya maandamano ya kupinga mageuzi ya sheria ya kazi
yanayopendekezwa na serikali ya kisosholisti ingawa wapinzani wa mageuzi
hayo wanaonekana kuishiwa nguvu.
Kadhalika waandamanaji wameingia mitaani katika mji wa mashariki wa
Belfort ambako serikali imejikuta iko katika mvutano na kampuni kubwa ya
ujenzi wa Treni la Alstom kuhusiana na hatma ya kiwanda hicho
kinachokabiliwa na kitisho.Katika miezi ya nyuma maandamano mengi nchini
humo yalikabiliwa na vurugu zilizozuka kati ya waandamanaji na polisi
wa kupambana na ghasia ambapo kiasi watu 40 walijeruhiwa na wengine
kukamatwa.Hata hivyo vyama vya wafanyakazi leo vimeitisha maandamano
hayo mapya ingawa mwitikio wa waliojitokeza umeonekana kuwa
mdogo.Makampuni kadhaa ya ndege kama Rynair yametangaza kufuta safari
zake kadhaa za ndege za kutoka au kuingia Ufaransa kufuatia mgomo huo
Wakati
pambano la timu ya Mwadui dhidi ya Yanga likizidi kupamba moto, Kocha
Mkuu wa Mwadui ya mkoani Shinyanga, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema
atahakikisha anashinda mchezo wake dhidi ya wapinzani wake hao
keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani humo.
Kocha
Julio amesema kuwa kutokana na yeye kutangaza kustaafu soka mara baada
ya msimu huu kumalizika atahakikisha kuwa anaifunga Yanga ili astaafu
soka kwa heshima, kitu ambacho kinaweza kuwapa hasira zaidi Yanga
kuelekea mchezo huo.
“Nimejipanga
kuhakikisha kuwa Yanga wanapata kipigo na nitahakikisha kuwa tunawapa
kipigo kikali ili watambue kuwa makocha wazawa ni wazuri kuliko Wazungu.
“Ifahamike
tangu timu yangu ipande daraja Yanga haijawahi kunifunga kwenye uwanja
wa nyumbani hivyo sitaruhusu historia ivunjwe bali nitahakikisha kuwa
Yanga haondoki na pointi katika mchezo huo.
“Mimi sitishwi na
ubora wa wachezaji wa Yanga bali nitahakikisha malengo niliyojiwekea
yanatimia kwani kila mchezaji wangu nimempa majukumu maalumu ya
kuhakikisha kuwa wachezaji wa Yanga hawaleti madhara kwenye lango letu
hivyo lazima walifahamu hilo,” alisema Julio.
Katika
kile kinachoonekana presha kuwa kubwa kuelekea mechi dhidi ya Simba,
wikiendi hii, benchi la ufundi la Azam FC ambalo linaongozwa na makocha
kutoka Hispania limekataa mazoezi yao kushuhudiwa na waandishi wa
habari.
Leo asubuhi ikiwa ni siku mbili kabla ya mchezo huo
ripota wa SALEHJEMBE alifika kwenye Uwanja wa Azam Complex kwa ajili ya
kushuhudia kilichokuwa kikiendelea lakini akakutana na ukuta wa chuma.
Baada ya kufika uwanjani hapo aripota huyo aliambiwa hataruhusiwa
kuingia ndani kushuhudia mazoezi hayo kwa kuwa tayari kocha ameanza
mazoezi maalum kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa
Uhuru.
Imeelezwa kuwa kocha huyo aliwakubalia watu wa habari wa
klabu hiyo pekee lakini wengine wote kutoka nje ya Azam FC
hawakuruhusiwa kushuhudia kilichokuwa kikiendelea.
Mchezo huo ni
mmoja wa mchezo mkubwa kwa kuwa Azam imekuwa ikitoa ushindani mkali
katika miaka ya hivi karibuni tofauti na zamani ambapo ilionekana mechi
kubwa ni za Yanga na Simba pekee.
Kikosi
cha Yanga kimeondoka alfajiri ya leo jijini Dar es Salaam kuelekea
Mwanza kisha Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
dhidi ya Mwadui FC.
Yanga
na Mwadui zanatarajiwa kukutana Jumamosi ya keshokutwa kwenye Uwanja wa
Kambarage mkoani Shinyanga, mchezo ambao unatarajiwa kuwa mgumu
kutokana na upinzani wa timu hizo licha ya kuwa Yanga ndiyo ambayo
inaonekana kuwa vizuri zaidi uwanjani kutokana na matokeo yake ya hivi
karibuni.
Yanga iliondoka Dar es Salaam kwa ndege ya Fast Jet na
tayari imetua Mwanza ambapo asubuhi hii ilikuwa ikifanya mchakato wa
kuelekea Shinyanga.
Mwadui inanolewa na Kocha Jamhuri Kihwelo
‘Julio’ ambaye tayari amesikika akijinadi kuwa lazima ataifanyia Yanga
kwa kuifunga na kuwataka wale wanaodhani kuwa mabingwa hao watetezi wa
Ligi kuu Bara watapata pointi tatu kirahisi mkoani humo, wanajidanganya.
Mwadui
ipo katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 4
katika michezo minne wakati Yanga ina pinti saba katika michezo mitatu.
YANGA SC WAWASILI SHINYANGA, ILIBIDI WAPANDE HADI DALA DALA ILI KUWAHI
KIKOSI
cha Yanga SC kimewasili salama Shinyanga baada ya safari ya tangu
asubuhi kutoka Dar es Salaam kuanzia angani hadi barabarani.Yanga
walipanda ndege kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ambako walipanda basi
hadi Shinyanga, tayari kwa mchezo wao wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara.Hata
hivyo, baada ya kufika Mwanza, Yanga walilazimika kukodi Hiece mbili
daladala za Uwanja wa Ndege, kwenda Mwanza mjini kupanda basi walilokodi
kuwapeleka Shinyanga.
Basi la Yanga baada ya kuwasili hotelini mjini Shinyanga
Wachezaji wa Yanga wakiwa ndani ya ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza
Kipa Deo Munishi 'Dida' nje ya basi leo wakati wa safari ya Shinyanga
Hapa
wachezaji wa Yanga wanapanda daladala kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza
kulifuata basi katikati ya mji kwa safari ya Shinyanga
Katibu
Mkuu wa Yanga; Baraka Deusdedit amesema; “Nachoweza kusema basi
lilichelewa kufika Uwanja wa Ndege kuchukua wachezaji, na hatukuona
sababu ya kupoteza muda mwingi kulisubiri,”. “Tukaona tuchukue usafiri
wowote wa haraka tulifikie kuliko kuwaacha wachezaji wanazagaa ovyo
Uwanja wa Ndege, ndiyo tukakodi dala dala,”amesema Deusdedit akizungumza
na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo. Yanga
SC watakuwa wenyeji wa Mwadui FC Jumamosi Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.Kwa
ujumla Ligi Kuu inaendelea wikiendi hii, mbali ya Yanga na kuwa wageni
wa Mwadui Shinyanga – Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Azam FC
watamenyana na Simba SC na Mbeya City na Prisons Uwanja wa Sokoine mjini
Mbeya.Mtibwa
Sugar na Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Ruvu
Shooting na Mbao FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Maji
Majina Ndanda FC Uwanja wa Majimaji mjini Songea.Jumapili kutakuwa na michezo miwili, Stand United wakiikaribisha JKT Ruvu Stars Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na African Lyonwakimenyana na Toto Africans Uwanja wa Uhuru.
STARS YAPOROMOKA VIWANGO VYA
Shirikisho la soka Duniani, FIFA limetoa orodha ya viwango vya ubora kwa mataifa mbalimbali duniani kwa mwezi Septemba.
Orodha inaonesha kwamba, Tanzania imeporomoka kwa nafasi nne kutoka 124 hadi kushika nafasi ya 132.
Kufungwa dhidi ya Nigeria katika mchezo uliokuwa wa kusaka tiketi ya
kufuzu Afcon mwaka 2017 pengine ndiyo sababu kubwa ya Tanzania
kuporomoka.
Uganda bado wameendelea kuwa bora Afrika Mashariki na ukanda wote wa
CECAFA kwa ujumla wakishika nafasi ya 65 duniani na 15 barani Afrika.
Rwanda wanafuata kwa karibu baada ya kupanda mpaka nafasi ya 107 kutoka nafasi ya 121.
Barani Afrika, Ivory Coast wameendelea kuwa kileleni, huku wakishika
nafasi ya 34 duniani, wakifuatiwa na Waarabu wa Algeria, Senegal na
Ghana.
Kinara wa ulimwengu wanabaki kuwa Argentina wakfuatiwa kwa karibu na Ubelgiji, Ujerumani, Colombia na Brazil.
KEPTENI
wa Manchester United Wayne Rooney hayumo kwenye Kikosi cha Timu hiyo
kilichoruka kwenda Rotterdam kucheza na Klabu ya Netherlands Feyenoord
katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.
Wengine ambao hawamo kwenye Kikosi hicho cha Wachezaji 20 ni Luke Shaw, Antonio Valencia na Jesse Lingard.
Maneja Jose Mourinho amesema Rooney amecheza Mechi zote za England
na Man United na hivyo amepumzishwa ile awe freshi kwa ajili ya tripu
yao ya Ugenini hapo Jumapili wakicheza kwenye EPL, Ligi Kuu England na
Watford.
Kuhusu ushiriki wao kwenye Mashindano haya, Morinho amekiri Klabu
haikutaka kuwemo lakini maadamu wamo basi watawania kutwaa Ubingwa.
Ameeleza: "Si ndoto ya kila Mchezaji mkubwa lakini hatumo CHAMPIONZ
LIGI. Lazima tuyatizame Mashindano haya kwa heshima. Tunataka tufanye
vyema!"
Mbali ya Marcus Rashford kuanza Mechi hii kama Mourinho
alivyodokeza, wengine wanaotarajiwa kucheza ni Marcos Rojo atakaechukua
nafasi ya Luke Shaw pamoja na Michael Carrick, Matteo Darmian, Timothy
Fosu-Mensah na Memphis Depay.
=============
JE WAJUA?
Man United imeshacheza na Feyenoord mara 2, kwenye Kundi lao la
UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 1997/98, na Man United kushinda Mechi zote
mbili ikiwemo 3-1 huko Uwanjani De Kuip ambako Andy Cole alipiga
Hetitriki.
==============
Wakati huo huo, Feyenoord wamelazimika kupunguza uwezo wa Uwanja De
Kuip na kuwa na Watazamaji 30,000 tu ili kukwepa Adhabu zaidi toka UEFA
kwani kwa sasa wapo kwenye Angalizo baada ya fujo za Mashabiki wao
Msimu uliopita na kupunguzwa huko kutasaidia udhibiti wa fujo za
Mashabiki.
Manchester United - Kikosi cha Wachezaji 20: De Gea, Romero,
Johnstone, Darmian, Bailly, Blind, Fosu-Mensah, Rojo, Smalling, Carrick,
Fellaini, Herrera, Mata, Memphis, Pogba, Schneiderlin, Young,
Ibrahimovic, Martial, Rashford.
UEFA EUROPA LIGI
Mechi za Ufunguzi
Alhamisi Septemba 15
KUNDI A: Feyenoord v Manchester United, Zorya Luhansk v Fenerbahçe
KUNDI B: Young Boys v Olympiacos, APOEL v Astana
KUNDI C: Mainz v St-Étienne, Anderlecht v Qäbälä
KUNDI D: AZ Alkmaar v Dundalk, Maccabi Tel-Aviv v Zenit
KUNDI E: Viktoria Plzeň v Roma, Astra Giurgiu v Austria Wien
KUNDI F: Rapid Wien v Genk, Sassuolo v Athletic Club
KUNDI G: Standard Liège v Celta Vigo, Panathinaikos v Ajax
KUNDI H: Konyaspor v Shakhtar Donetsk, Braga v Gent
KUNDI I: Salzburg v Krasnodar, Nice v Schalke
KUNDI J: QarabaÄŸ v Slovan Liberec, PAOK v Fiorentina
KUNDI K: Inter Milan v Hapoel Beer-Sheva, Southampton v Sparta Praha
KUNDI L: Osmanlıspor v Steaua Bucureşti, Villarreal v Zürich
Mechi
za kwanza za Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI ziliendelea Jana na
Mabingwa Watetezi Real Madrid kuponyoka kipigo toka Timu ya zamani ya
Staa wao Cristiano Ronaldo Sporting Lisbon ya Ureno kwenye Mechi ya
Kundi F.
Real walitanguliwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 48 la Bruno Cesar
lakini Ronaldo akawasawazishia Dakika ya 89 na Alvaro Morata kuwapa
ushindi wa 2-1 kwa Bao la Dakika ya 94.
Nayo ile Mechi ya Kundi C iliyoahirishwa Juzi kutokana na Mvua
kubwa Uwanjani Etihad Jijini Manchester ilichezwa Jana na Man City
kuitwanga Borussia Monchengladbach 4-0.
Bao za City zilipigwa na Sergio Aguero, Bao 3 moja likiwa la Penati, na Kelechi Iheanacho.
Nayo Tottenham, ikiwa Kundi E na ikicheza 'kwao' Wembley Stadium
badala ya White Hart Lane unaofanyiwa ukarabati, ilichapwa 2-1 na AS
Monaco.
Monaco walitangulia 2-0 kwa Bao za Dakika za 16 na 31 za Bernardo
Silva na Thomas Lemar na Spurs kupata Bao lao Dakika ya 45 kupitia Toby
Alderweireld.
Nao Mabingwa wa England Leicester City wameanza Ulaya kwa kushinda Ugenini walipoichapa Club Brigge ya Belgium 3-0.
Bao za Leicester zilufungwa dakika za 5, 29 na 61 ambazo zilifungwa
na Marc Albrighton na 2 za Riyad Mahrez moja likiwa la Penati.
Ule mtanange wa Kundi H uliochezwa huko Turin, Italy kati ya Juventus na Sevilla uliisha 0-0.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Matokeo:
Jumanne 13 Septemba 2016
KUNDI A
Basel 1 Ludo Razgrad 1
Paris St Germain 1 Arsenal 1
KUNDI B
Benfica 1 Besiktas 1
Dynamo Kiev 1 Napoli 2
KUNDI C
Barcelona 7 Celtic 0
Man City v Borussia Monchengladbach [ILIAHIRISHWA]
KUNDI D
Bayern Munich 5 FC Rostov 0
PSV Eindhoven 0 Atletico Madrid 1
Ratiba:
Jumanne 27 Septemba 2016
KUNDI E
CSKA v Tottenham
Monaco v Bayer Leverkusen
KUNDI F
Borussia Dortmund v Real Madrid
Sporting v Legia Warsaw
KUNDI G
FC Copenhagen v Club Brugge
Leicester City v FC Porto
KUNDI H
Dinamo Zagreb v Juventus
Sevilla v Lyon
Jumatano 28 Septemba 2016
KUNDI A
Arsenal v Basel
Ludo Razgrad v Paris St Germaine
KUNDI B
Besiktas v Dynamo Kiev
Napoli v Benfica
KUNDI C
Borussia Monchengladbach v Barcelona
Celtic v Man City
KUNDI D
Atletico Madrid v Bayern Munich
FC Rostov v PSV Eindhoven
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MAKUNDI:
Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba
Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba
Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba
Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba
Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba
Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba
MECHI ZA MTOANO:
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)
Wadukuzi wa Urusi wafichua faili zaidi za Wada
Wadukuzi
wanaoaminika kutoka Urusi wametoa faili zaidi ya wanariadha zilizoibwa
kutoka kwa mamlaka kuu duniani ya kudhibiti utumiaji wa dawa za
kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha (Wada).
Wanariadha hao
wanajumuisha muendeshaji baiskeli wa Uingereza Sir Bradley Wiggins,
mwanariadha wa Olimpiki mwenye hadhi kubwa zaidi nchini humo, na bingwa
mara nne wa mashindano ya Tour de France Chris Froome.
Hakuna dalili zozote zinazowahusisha wanariadha hao na uhalifu.
Wada
inasema kuwa udukuzi wa kimitandao ni jaribio la kudhoofisha mfumo
mzima wa dunia wa kukabiliana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli
miongoni mwa wanariadha.
Mkurugenzi mkuu wa Wada Olivier Niggli,
anakosoa ufujaji wa taaarifa hizo na kusema kwamba "hakuna shaka"
udukuzi huo ulikuwa tendo la kulipiza kisasi dhidi ya ripoti ya Wada kwa
wanariadha wa Urusi kwamba taifa hilo iliwasaidia wanariadha wake
kudanganya huku akiomba utawala nchini Urusi kuzima udukuzi huo.
Rekodi
hiyo ilitolewa na kundi moja linalojiita "Fancy Bears" mara nyingi
ikishinikiza kile kinachojulikana kama "Therapeutic Use Exemptions"
(TUEs) na kukubalia dawa zilizopigwa marufuku kutumika na "wanariadha"
ili kuthibitishwa mahitaji ya matibabu.
Kundi hilo linasema kuwa TUEs "imeidhinishwa kutumika" na kwamba Wada "ni fisadi na inaeneza udanganyifu".
Taarifa
hiyo inahusisha Wamarekani 10, Waingereza 5 na Wajerumani 5 kwa pamoja
na mwanaridha mmoja mmoja kutoka Denmark, Urusi, Poland, Romania na
Jamhuri ya Czech.
Miongoni mwa majina hayo kutoka Jamhuri ya Czech ni
bingwa mara mbili wa mchezo wa Tennis wa Wimbledon Petra Kvitova na
mshindi wa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya olimpiki ya London
mwaka 2012, Robert Harting, raia wa Ujerumani.
Orodha hiyo pia
inajumuisha majina 11 washindi wa medali mbali mbali katika mashindano
ya mbio zilizomalizika hivi majuzi mjini Rio De Jeneiro, likiwemo jina
la mmarekani Bethanie Mattek-Sands, ambaye alishinda dhahabu katika
mashindano ya tennis inayojumuisha wachezaji wawili.
Ufujaji huu
mpya unafuatia mwingine uliotokea hapo awali ambapo taarifa inayohusiana
na wanariadha wa Marekani ilitolewa akiwemo mshindi wa dhahahu wa
mazoezi ya viungo Simone Biles.
SHUKRANI ZANGU KWA BBC SWAHILI ,MPEKUZI,MAMBOMOTOMOTO YA SOKA ,SHAFF DAUDA,SALEHE JEMBE NA BIN ZUBERY AMBAO NDIO CHANZO CHA HABARI HIZI ZOTE ZA KIMICHEZO HABARI ZA KIJAMII LAKINI PIA NA DW HABARI ZA ULIMWENGU ,
USISAHAU KUTEMBELEA BLOG HII ILI UWEZE KUHABARIKA ,
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 15, 2016
Rating: 5
Hakuna maoni