Rais Dkt. Magufuli Amuapisha Balozi Dk. Dau Pamoja Na Makatibu Tawala Wa Mikoa Mitatu Ikulu Jijini Dar Es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
14 Septemba, 2016 amemuapisha Dkt. Ramadhani Kitwana Dau kuwa Balozi wa
Tanzania nchini Malaysia.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi, Dkt. Ramadhan Kitwana Dau alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Mhe.
Balozi Dkt. Ramadhani Kitwana Dau anajaza nafasi iliyoachwa wazi na
aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima
ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki.
Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa mitatu aliowateua
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Walioapishwa ni kwanza, Bw. Eliya
Mtinangi Ntandu anayekuwa Katibu Tawala wa kwanza wa Mkoa wa Songwe
ulioanzishwa rasmi Mwezi Februari 2016.
Pili, Bw. Adoh Stephen Mapunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.
Bw. Adoh Stephen Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.
Tatu, Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu.
Baada
ya kuapishwa, Mhe. Balozi Ramadhani Kitwana Dau na Makatibu Tawala wote
watatu wamekula Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma
kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na
kushuhudiwa na Rais Magufuli.
Matukio yote yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
14 Septemba, 2016

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Bw. Tixon Nzunda kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Bw. Eliya Ntandu kuwa Katibu Tawala mkoa wa Songwe, Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau mara
baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Majambazi Yavamia Magari ya Mnadani na Kumuua Dereva Mmoja kwa Risasi
Majambazi
wapatao 10 juzi usiku walivamia magari mawili yaliyobeba
wafanyabiashara waliokuwa wakitokea mnadani na kumuua kwa risasi, dereva
aliyegoma kuwapa fedha na simu.
Dereva huyo, Chrispin Inyangwe (40) alipigwa risasi ya mgongoni alipojaribu kupambana nao.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana eneo la katikati ya vijiji vya
Miula na Kalundi vilivyopo Kata ya Kipande wilayani Nkasi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema wafanyabiashara hao
walikuwa wakitokea mnadani na walipofika eneo hilo walikuta mawe
yamepangwa barabarani kuzuia magari.
Alisema
baada ya kuona mawe hayo, magari hayo yalilazimika kusimama na ndipo
majambazi hao waliokuwa na silaha za moto, mapanga na marungu
walipoibuka na kufyatua risasi hewani na baadaye kutaka wafanyabiashara
hao wasalimishe fedha na simu zao za mkononi.
Kamanda huyo alisema baadhi ya wafanyabiashara walisalimisha fedha na simu zao, na waliokataa walishambuliwa.
Inasemekana
kwamba Inyangwe ambaye alikuwa dereva wa gari aina ya Mitsubishi Canter
alikaidi kutoa fedha na kutaka kupambana nao, ndipo watu hao waliokuwa
na bunduki aina ya SMG walipomfyatulia risasi iliyompata mgongoni na
kufariki dunia papo hapo.
Kitendo
hicho kiliwafanya wafanyabiashara wengine waliokuwa wakikataa kutoa
fedha, kuzisalimisha sambamba na simu zao, ndipo majambazi hao
walipowaachia na kukimbia.
Watu
19 waliojeruhiwa walipelekwa Hospitali ya Mkoa mjini Sumbawanga.
Kamanda Kyando alisema majeruhi 12 waliruhusiwa kurejea nyumbani na
wengine saba wanaendelea na matibabu na kwamba polisi wanaeendelea na
msako wa watu hao.
Wakurugenzi Wapya 13 Waapishwa.....Watakiwa kufuatilia maagizo ya viongozi
Wakurugenzi wapya 13 wa halmashauri wameapa
kulinda maadili na kukabidhiwa majukumu ya kufuatilia maagizo ya Rais,
Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, kwenye maeneo yao na kutoa mrejesho wa
hatua za utekelezaji wake.
Kiapo hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angela Kairuki
aliyewataka kutilia mkazo ufuatiliaji wa maagizo na kupambana na tatizo
la watumishi hewa ambao idadi yao imefikia 17,102 waliogundulika katika
kipindi cha kuanzia Machi mpaka sasa.
Wakurugenzi hao walioteuliwa hivi
karibuni na Rais, John Magufuli waliapishwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George
Simbachawene katika ukumbi wa Tamisemi mjini Dodoma.
Akizungumza mara
baada ya kiapo hicho, waziri Kairuki aliwataka wakurugenzi hao
kutekeleza matamko yote yanayotolewa na viongozi wa ngazi za juu
serikalini, kwa kutoa mrejesho wa utekelezaji wake.
Kairuki aliwataka
kufanya kazi kwa bidii ili wawatumikie wananchi wanaowaongoza.
Alisema
katika ziara nyingi alizozifanya, amekuta wakurugenzi hawafuatilii
matamko yanayotolewa na viongozi wa ngazi za juu serikalini katika
maeneo yao.
“Hata kwa wale ambao wanayafuatilia huwa hawatoi mrejesho wa
hatua zilizofikiwa katika kutekeleza matamko hayo, hivyo ninawaomba
mkayatekeleze maagizo na kurudisha mrejesho kwa kiwango kinachotakiwa,”
alisema Kairuki.
Pia, aliwataka wakurugenzi hao kwenda kusimamia fedha
za miradi ya maendeleo zinazotolewa na Serikali hadi senti ya mwisho,
ili kuhakikisha inatekelezwa kwa asilimia 100.
Alisema kuna baadhi ya
miradi ya maendeleo, inatekelezwa kwa fedha za Serikali na wakati huo
huo inatumia fedha za wafadhili.
Waziri Kairuki aliwataka wakurugenzi
hao kuhakikisha kuwa miradi yote inayotumia fedha za Serikali
inasimamiwa ipasavyo.
“Utakuta mradi mmoja unafadhiliwa na pia
unatumia fedha za Serikali, kwa hiyo wafadhili wakija kukagua
wanaonyeshwa jengo likiwa limekamilika na Serikali nayo ikija kukagua
inaonyeshwa jengo hilohilo. Nataka mkasimamie fedha zote za Serikali
kwenye mamlaka zenu,” alisema Kairuki.
Alisema kuna baadhi ya maeneo ambako fedha
za Tasaf (mpango wa kunusuru kaya maskini), zimetumika kujengea maabara
na kununulia madawati kinyume na malengo yaliyokusudiwa.
Pia, aliwataka
kuhakikisha kuwa hatua kali za kinidhamu zinachukuliwa kwa wakati kwa
watumishi waliosimamishwa kazi katika kipindi cha miezi sita na si zaidi
ya hapo.
Alisema mtumishi aliyechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo
kufukuzwa au kusimamishwa kazi, mchakato wake wote ufanyike ndani ya
miezi sita.
Aliwataka pia wakurugenzi hao kufuata maadili ya viongozi wa
umma, kwani wakikiuka watafikishwa kwenye baraza la maadili ya viongozi
wa umma ambalo kwa sasa limeongezewa meno.
Waziri Kairuki aliwataka
wakurugenzi hao kusimamia suala la rasilimali watu, kwani utafiti
ulionyesha kuwa asilimia 80 hadi 90 ya watumishi wa umma ni watoro.
Alisema katika baadhi ya maeneo kuna wakaguzi na waratibu wa elimu wa
kata, lakini hawatembelei shule zao kuona kama walimu wanahudhuria
shuleni au la.
Kadhalika, aliwataka wakurugenzi hao kuachana na tabia
ya kuwatumia viongozi wa Serikali walioko chini yao, kama vile watendaji
wa kata, vijiji na wenyeviti wa vijiji kuwalimia mashamba yao.
Alisema
watakaobainika kufanya vitendo hivyo, watachukuliwa hatua kali za
kinidhamu.
Waziri Simbachawene aliwataka wakurugenzi hao kwenda kuchapa
kazi bila kumwonea yeyote. Aliwaambia kuwa kukusanya mapato kiwe ni
kipaumbele chao cha kwanza, kwani kipimo cha mamlaka yoyote kujitegemea
ni uwezo wake wa kukusanya mapato.
Aliwataka wakurugenzi hao kuhakikisha
kuwa wanawatembelea watumishi wao wote ili kujua penye upungufu, idadi
yao na hata ikiwezekana kuwajua kwa majina yao.
Wakurugenzi walioapishwa
jana ni Godwin Kunambi (Dodoma) Elias Ntiruhungwa (Tarime), Mwantumu
Dau (Bukoba) na Frank Bahati (Ukerewe) Wengine ni Hudson Kamonga
(Mbulu), Mwailwa Pangani (Nsimbo), Godfrey Sanga (Mkalama), Yusufu
Semuguruka (Ulanga), Bakari Mohamed (Nachingwea), Juma Mnweke (Kibondo),
Butamo Ndalahwa (Moshi), Waziri Mourice (Karatu) na Fatma Latu
(Bagamoyo).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki
akiongea Wakurugenzi wapya mara baada ya kuapishwa jana mjini Dodoma.
Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene. Kushoto kwa Simbachawene
ni Mkurugenzi mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilimanjaro Bi. Butamo
Nuru Ndalahwa
Wanafunzi Wacharaza Viboko Walimu Wao ........Mmoja Ang'olewa Meno Matano, Mwingine Ngeu Kichwani
Waziri wa Elimu, Prof Joyce Ndalichako
Wawanafunzi
wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Usevya wilayani Mlele Mkoa wa
Katavi, wanadaiwa kuwashambulia kwa kuwacharaza viboko walimu wao wawili
miongoni mwao akiwemo Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Makonda Ng’oka
“Membele'‘ (34) ambaye ameng’olewa meno matano kwa kipigo hicho.
Walimu
hao wawili wamedai kuwa hawako tayari kuendelea kufundisha katika shule
hiyo huku wakisisitiza kuwa ni fedheha kwao kucharazwa viboko na
wanafunzi wao wenyewe ambapo Mwalimu Gabriel Kambona aliachwa na ngeu
kichwani.
Mei
mwaka huu, Ng’oka “Membele” alifikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa
Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake akidaiwa kutenda kosa
hilo kati ya Novemba 2015 na Aprili mwaka huu.
Ilisemekana
kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule hiyo
kulifuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano sasa wako Kidato
cha Sita katika shule hiyo kumkataa na kutishia kuandamana kupinga
vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi wake.
Wanafunzi
hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi yao ikiwa ni
adhabu mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo.
Hata
hivyo, baada ya kutopatikana ushahidi wa kumtia hatiani Ng’oka, Julai
27, mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda ilimwachia
huru.
Mwalimu
Ng’oka aliripoti kwenye kituo chake cha kazi shuleni Usevya Agosti Mosi
mwaka huu ambako kurejea kwake shuleni hapo kunadaiwa kuamsha hasira
kwa baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wakidai hawapo tayari kumwona
mwalimu huyo na familia yake shuleni hapo.
Akizungumza
na wanahabari jana mjini hapa, Ng’oka alidai kuwa hayuko tayari
kuendelea kufundisha kwenye shule hiyo akihofia usalama wake na kutokana
na kipigo alichokipata cha kushambuliwa na baadhi ya wanafunzi wake wa
kidato cha tano na cha sita wakati akiwa nyumbani kwake na familia yake.
Akisimulia
mkasa huo, alisema Agosti 12, mwaka huu usiku alikuwa nyumbani kwake
shuleni hapo pamoja na familia yake pamoja na mwalimu mwenzake, Gabriel
Kambona aliyekuwa amemtembelea.
“Ghafla,
saa mbili usiku nikiwa maliwatoni nikioga lilitokea kundi la wanafunzi
wa kidato cha tano na sita wakiwa na silaha za jadi kama vile fimbo,
marungu, mawe na matofali na kuanza kuishambulia familia yangu pamoja na
mwalimu Kambona,” alieleza na kuongeza kuwa alilazimika ‘kuchomoka’
bafuni baada ya kusikia mayowe yaliyokuwa yakipigwa na familia yake
wakiomba msaada. Alipofika sebuleni alishuhudia wanafunzi hao
wakiishambulia familia yake kwa kuwacharaza viboko.
“Ndipo
walinigeukia na kuanza kunishambulia kwa kunipiga kwa marungu na fimbo
hadi nikapoteza fahamu nilizinduka nikiwa nimelazwa kwenye Kituo cha
Afya Usevya na kubaini kuwa nimepoteza meno yangu matano huku nikiwa
nimejeruhiwa vibaya kichwani. Baadaye nilihamishiwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Mpanda ambako nililazwa wiki moja na nusu kwa matibabu na sasa
nimepewa rufaa niende Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar kwa
matibabu zaidi,” alieleza.
Alidai
kuwa uhasama baina yake na wanafunzi hao umedumu kwa muda mrefu, lakini
anashangaa uongozi wa Halmashauri ya Mpimbwe na Wilaya ya Mlele
umeshindwa kumpangia kituo kingine cha kazi na kuchukua hatua yoyote kwa
wanafunzi hao licha ya kupeleka majina yao kwa kuwa anawafahamu wote
waliohusika.
Mwalimu
Kambona alidai kuwa hayuko tayari kuendelea kufundisha kwenye shule
hiyo kwamba kitendo cha kupigwa na wanafunzi wake kimemfedhehesha.
Kwa
mujibu wa mwalimu huyo, walimu wa shule hiyo waliketi baada ya kutokea
kwa tukio hilo, na walifikia maamuzi kuwa wanafunzi wote waliobainika
kushiriki kuwashambulia walimu wao wasimamishwe shule akidai kuwa
uongozi wa Halmashauri ya Mpimbwe na Wilaya ya Mlele ulipinga.
“Nimeandika
barua ya kuomba uhamisho kwani nia aibu kwangu kuendelea kufundisha
wanafunzi ambao wamenishambulia na kunitoa ngeo kichwani ….. siku hiyo
ya tukio niliibiwa simu mbili za kiganjani lakini jana nimefanikiwa
kuikamata simu moja kwa mwanafunzi wa kidato cha tano anayeitwa , Alex
Maiko Makona na tayari amemfikisha katika Kituo cha Polisi cha Usevya,” alidai.
Mwenyekiti
wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Katavi, Gregori Mshota alisema tayari
chama chake kimeanza kuwasiliana na uongozi wa Halmashauri ya Mpimbwe
na uongozi wa Wilaya ya Mlele ili kuhakikisha mwalimu huyo anakuwa
salama.
Ofisa
Elimu wa Mkoa wa Katavi, Ernest Hinju alidai kuwa suala hilo lipo
ofisini kwake na wameanza kulitafutia ufumbuzi. “Jambo hili linahitaji
ushirikishwaji wa vyombo mbalimbali ikiwemo Bodi ya Shule ya Sekondari
ya Usevya,” alieleza.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa katika ziara mkoani Katavi mwezi
uliopita, mke wa mwalimu Ng’oka alitinga kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kijijini Maji Moto akiwa na bango lenye malalamiko ya
kutishiwa usalama wa maisha wa familia yake, na Waziri Mkuu alimwagiza
Kamanda wa Polisi wa Mkoa kushughulikia malalamiko hayo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Apokea Zaidi Ya Sh. Bil. 1.4 Kwa Ajili Ya Maafa Ya Tetemeko La Kagera
agera imefungua akaunti maalumu katika benki ya CRDB
kwa ajili ya kupokea michango kutoka kwa watu mbalimbali. Namba za
akaunti hiyo ya Kamati ya Maafa ya Kagera ni CRDB 0152225617300.
Pia
Waziri Mkuu aliwapongeza na kuwashukuru waheshimiwa Wabunge kwa kuamua
kutoa posho zao za kikao cha jana kwa ajili ya kuchangia wahanga wa
tetemeko hilo na kuwaomba wananchi wengine kujitokeza na kutoa michango
yao.
Wakati
huo huo viongozi wa makampuni ya mafuta ya GBP, Oil Com na Moil
wameahidi kujenga shule mbili za Nyakato na Ihungo ambazo sehemu kubwa
ya miundombinu yake imeharibika vibaya. Shule hizo zitajengwa katika
kipindi cha siku 30.
Hafla
hiyo iliyoongozwa na Waziri Mkuu ilihudhuriwa na Waziri wa Viwanda na
Biashara, Charles Mwijage, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Balozi, Dk. Aziz Mlima.
Namba ya akaunti ya kuwachangia walioathiriwa na tetemeko la ardhi Kagera
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Septemba 14
katika habari za kimataifaaa
Habari | 14.09.2016 | 10:10
Mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Juncker,
amehimiza mshikamano katika Umoja wa Ulaya baada ya kujiondoa kwa
Uingereza, akisema ingawa Ulaya haikabiliwi na kitisho cha kugawanyika,
inapaswa kufanya kazi pamoja. Katika hotuba yake mbele ya Bunge la
Ulaya, ambayo imezigusia sera kadhaa ya kisiasa na za kiuchumi,
Juncker
amezitaka nchi za Ulaya kushirikiana kupambana na wimbi la siasa kali za
kizalendo zinazoshika kasi.
Hotuba yake imetolewa siku mbili kabla ya
mkutano wa kilele wa nchi za Umoja wa Ulaya ambao utafanyiuka katika mji
mkuu wa Slovakia, Bratislava, wa kwanza bila wawakilishi wa Uingereza.
Mkutano huo unatarajiwa kuchora ramani ya mwelekeo wa Umoja wa Ulaya,
baada ya kujiondoa kwa Uingereza. Jean-Claude Juncker ameitumia hotuba
hiyo kuitaka Uingereza kuanzisha rasmi mchakato wa kujiondoa katika
Umoja wa Ulaya, haraka iwezekanavyo.
Mpango wa kusitisha mapigano nchini Syria unaoenekana
kuendelea kuheshimiwa, masaa zaidi ya 36 baada ya kuanza kutekelezwa,
limesema shirika la kuchunguza haki za binadamu nchini Syria lenye makao
nchini Uingereza, na kuongeza hata hivyo kuwa watu wenye mahitaji
makubwa bado hawajafikiwa na msaada.
Mpango huo uliofikiwa katika
makubaliano baina ya Marekani na Urusi, unavihusu vikosi vya serikali na
vya waasi, lakini unalitenga kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS, na
mengine yenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida.
Kwa mujibu
wa Umoja wa Mataifa, watu wapatao 275,000, mashariki mwa mji wa Aleppo
wamekuwa katika mzingiro tangu mwezi Julai bila uwezekano wa kufikishiwa
msaada.
Afisa wa Umoja wa huo amesema bado wanasubiri ruhusa ya
serikali ili kuwapelekea msaada wa kibinadamu watu hao.
Serikali mjini
Damascus imeeleza bayana kuwa haitaruhu kupelekwa kwa msaada kutoka
Uturuki, ambayo ni hasimu wake na mshirika mkubwa wa waasi.
Ripoti ya bunge la Uingereza iliyochapishwa leo imesema
uingiliaji kati nchini Libya ulioidhinishwa na aliyekuwa waziri mkuu wa
nchi hiyo, David Cameron, ulitokana na taarifa potofu za kijasusi, na
uliharakisha kusambaratika kwa taifa hilo lililo kaskazini mwa Afrika,
kisiasa na kiuchumi.
Mwanzoni mwa mwaka 2011, Uingereza na Ufaransa
ziliongoza kampeni ya kimataifa kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa
Libya, Muammar Gaddafi, wakitumia ndege za kivita kuyarudisha nyuma
majeshi yake, na kuwaruhusu waasi kuuangusha utawala wake wa miaka zaidi
ya 40.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge la Uingereza iliyoiandika ripoti
hiyo, Crispin Blant, amesema David Cameron alikuwa na mchango katika
maamuzi ya kuingilia kati nchini Libya, na anapaswa kubeba lawama za
mchango wa Uingereza katika mzozo wa Libya.
Rais wa zamani wa Israel, Shimon Peres, ambaye alipelekwa
hospitali jana akiwa na ugonjwa wa kiharusi, leo hii amelezewa kuwa
katika hali mahtuti, lakini iliyotulia.
Rafi Walden, daktari wa kiongozi
huyo amesema Peres mwenye umri wa miaka 93 hakabiliwi tena na kitisho
kwa maisha yake, akiongeza kuwa alikuwa akiweza kufahamu yanayozungumzwa
kumhusu. Aidha, daktari huyo amesema Shimon Peres ambaye pia ni mshindi
wa tuzo ya Nobel ya Amani kwa wakati huu amepewa dawa za kumtuliza ili
ubongo wake ulioathiriwa vibaya na kiharusi uweze kupata nafuu haraka.
Peres alikimbizwa hospitalini mjini Tel Aviv jana baada ya kupata
maumivu makali ya kichwa kufuatia hotuba ya saa nzima aliyokuwa ameitoa.
Kiongozi huyo mkongwe vile vile aliwahi kuwa waziri mkuu wa Israel kati
ya mwaka 1984 na 1986.
Mkutano wa kilele wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za
Pembe ya Afrika, IGAD, ulimalizika jana katika mji mkuu wa Somalia -
Mogadishu, kwa kutoa maazimio ya kutaka kuimarishwa kwa vikosi vya Umoja
wa Afrika na vya serikali ya Somalia, ili kuweza kukabiliano na kitisho
cha ugaidi, na kuyakomboa maeneo yanayosalia mikononi mwa wanamgambo wa
al-Shabaab.
Huo ulikuwa mkutano wa kwanza wa aina hiyo kufanyika mjini
Mogadishu tangu mwaka 1991, wakati taifa hilo lilipotumbukia katika
mzozo wa kivita.
Viongozi katika mkutano huo pia walizungumzia uchaguzi
mkuu ujao nchini Somalia, mgogoro ulioibuka upya nchini Sudan Kusini, na
kuhimiza wakimbizi wa Somalia kurejea nyumbani kwa hiari yao.
Nchi
wanachama wa jumuiya ya IGAD ni pamoja na Kenya, Ethiopia, Uganda,
Djibouti, Sudan na Somalia.
katika habari za kimichezo na burudani
STRAIKA wa Arsenal Olivier Giroud amemlaumu Kiungo wa Paris Saint-Germain Marco Verratti
baada ya wote kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kuvaana kwenye
Mechi ya Kundi A la UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI Jana Usiku huko Parc des Princes, Paris iliyomalizika 1-1.
Wawili
hao walilambwa Kadi za Njano za Pili katika Dakika za Majeruhi na Refa
Viktor Kassai wa Hungary na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Tukio hilo lilitokea baada ya Giroud kumwangusha Verratti na kisha Marquinhos wa PSG kumsukumiza mwenzake Verrati kwa Giroud na kusababisha Refa Kassai kuwapa Kadi wote Wawili.
Baadae
Giroud akalamika: “Nikiwa kwenye Kadi ya Njano, sikutaka kuleta rabsha.
Nilimzuia Verratti nay eye akajirusha chini, sikuelewa hilo. Marquinhos
alinisukuma toka nyuma na sijui kwanini Verratti ajiangushe mara ya
pili. Hilo lilikuza tukio. Inasikitisha na hasa sijui kama Refa aliona
vizuri tukio lenyewe!”
Kwenye Mechi hiyo, Edinson Cavani aliipa PSG Bao baada ya Sekunde 42 na Alexis Sanchez kuisawazishia Arsenal kwenye Dakika ya 78.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Matokeo:
Jumanne 13 Septemba 2016
KUNDI A
Basel 1 Ludo Razgrad 1
Paris St Germain 1 Arsenal 1
KUNDI B
Benfica 1 Besiktas 1
Dynamo Kiev 1 Napoli 2
KUNDI C
Barcelona 7 Celtic 0
Man City v Borussia Monchengladbach [ILIAHIRISHWA, KUCHEZWA LEO]
KUNDI D
Bayern Munich 5 FC Rostov 0
PSV Eindhoven 0 Atletico Madrid 1
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Jumatano 14 Septemba 2016
*Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu
KUNDI E
Bayer Leverkusen v CSKA
Tottenham v Monaco
KUNDI F
Legia Warsaw v Borussia Dortmund
Real Madrid v Sporting Lisbon
KUNDI G
Club Brugge v Leicester City
FC Porto v FC Copenhagen
KUNDI H
Juventus v Sevilla
Lyon v Dinamo Zagreb
KUNDI C
Man City v Borussia Monchengladbach [ILIAHIRISHWA JANA]
++++++++++++++++++++++++++++++
Mechi za Kwanza za Makundi E hadi H ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, pamoja na ile iliyoahirishwa Jana kutokana na Mvua ya Kundi C kati ya Man City na Borussia Monchengladbach zitachezwa Leo Usiku,
Timu
mbili za England, Mabingwa Leicester City na Tottenham, Leo wapo
dimbani kwa Tottenham kucheza Uwanja wa Wembley badala ya ule wa kwao
White Hart Lane, Jijini London kwa kuwavaa AS Monaco ya France kwenye
Mechi ya Kundi E na Leicester City, wakicheza UCL kwa mara ya kwanza
kabisa katika Historia yao, wako Ugenini huko Belgium kuivaa Club Brugge
kwenye Mechi ya Kundi G.
Mechi
kali hii Lo ni ya Kundi H huko Jijini Turin Nchini Italy kati ya
Juventus na Mabingwa wa UEFA EUROPA LIGI Sevilla ya Spain.
Nao
Mabingwa Watetezi Real Madrid, ambao wapo Kundi F, wapo kwao Santiago
Bernabeu, kucheza na Sporting Lisbon ya Ureno ambayo ndiyo Timu Staa wa
Real Cristiano Ronaldo alikoanzia Soka la Kulipwa.
Mechi nyingine ya Kundi F ni kati ya Legia Warsaw na Borussia Dortmund.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Matokeo:
Jumanne 13 Septemba 2016
KUNDI A
Basel 1 Ludo Razgrad 1
Paris St Germain 1 Arsenal 1
KUNDI B
Benfica 1 Besiktas 1
Dynamo Kiev 1 Napoli 2
KUNDI C
Barcelona 7 Celtic 0
Man City v Borussia Monchengladbach [ILIAHIRISHWA, KUCHEZWA LEO]
KUNDI D
Bayern Munich 5 FC Rostov 0
PSV Eindhoven 0 Atletico Madrid 1
Ratiba:
Jumanne 27 Septemba 2016
KUNDI E
CSKA v Tottenham
Monaco v Bayer Leverkusen
KUNDI F
Borussia Dortmund v Real Madrid
Sporting v Legia Warsaw
KUNDI G
FC Copenhagen v Club Brugge
Leicester City v FC Porto
KUNDI H
Dinamo Zagreb v Juventus
Sevilla v Lyon
Jumatano 28 Septemba 2016
KUNDI A
Arsenal v Basel
Ludo Razgrad v Paris St Germaine
KUNDI B
Besiktas v Dynamo Kiev
Napoli v Benfica
KUNDI C
Borussia Monchengladbach v Barcelona
Celtic v Man City
KUNDI D
Atletico Madrid v Bayern Munich
FC Rostov v PSV Eindhoven
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MAKUNDI:
Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba
Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba
Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba
Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba
Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba
Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba
MECHI ZA MTOANO:
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Jumanne 13 Septemba 2016
KUNDI A
Basel 1 Ludo Razgrad 1
Paris St Germain 1 Arsenal 1
KUNDI B
Benfica 1 Besiktas 1
Dynamo Kiev 1 Napoli 2
KUNDI C
Barcelona 7 Celtic 0
Man City v Borussia Monchengladbach [ILIAHIRISHWA, KUCHEZWA LEO]
KUNDI D
Bayern Munich 5 FC Rostov 0
PSV Eindhoven 0 Atletico Madrid 1
++++++++++++++++++++++++++++++
Mechi za Kwanza za Makundi A hadi D za UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI zilichezwa Jana lakini ile ya Kundi C Uwanjani Etihad Jijini Manchester kati ya Manchester City na Borussia Monchengladbach ya Germany iliahirishwa kutokana na Mvua kubwa.
Huko
Nou Camp, Jijini Barcelona Nchini Spain katika Mechi nyingine ya Kundi
C, na Barcelona iliitwanga Celtic ya Scotland 7-0 na huko Paris, France,
kwenye Mechi ya Kundi A, Paris St Germain na Arsenal zilitoka 1-1.
Huko Munich, Germany, Mechi ya Kundi D, iliisha kwa Wenyeji Bayern Munich kuwaadhibu FC Rostov 5-0.
Barcelona 7 Celtic 0
Lionel
Messi alipiga Bao 3, Luis Suarez 2 na Neymar na Iniesta kufunga 1 kila
mmoja wakati Barcelona ikiitwanga Celtic 7-0 kwenye Mechi ya Kundi C
huko Nou Camp.
VIKOSI:
Barcelona: Ter Stegen, Pique, Umtiti, Alba, Gomes, Rakitic, Busquets, Roberto, Messi, Suarez, Neymar
Akiba: Cillessen, Arda, Iniesta, Rafinha, Mascherano, Alcacer, Digne
Celtic: De Vries, Gamboa, Lustig, Sviatchenko, Toure, Tierney, Roberts, Brown, Bitton, Sinclair, Dembele
Akiba: Gordon, Izaguirre, Armstrong, Rogic, O’Connell, McGregor, Forrest
REFA: Ovidiu Hategan (Romania)
Paris St Germain 1 Arsenal 1
Huko
Parc des Princes, Paris, Nchini France, Edinson Cavani aliipa Bao PSG
baada ya Sekunde 42 tu toka Gemu ianze lakini Alexi Sanchez alisawazisha
na kuipa Arsenal Sare ya 1-1 katika Mechi ya Kundi A.
Mechi
hii iliisha kwa kila Timu kubaki Mtu baada ya Olivier Giroud na
Verratti kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya wote kupewa Kadi za
Njano za Pili baada ya kuvaana Dakika za mwishoni.
VIKOSI:
PSG: Areola; Aurier, Marquinhos, Thiago Silva, Maxwell; Verratti, Krychowiak, Rabiot; Di Maria, Cavani, Matuidi
Akiba: Trapp, Kimpembe, Moura, Motta, Pastore, Meunier, Jesé
Arsenal: Ospina; Bellerin, Mustafi, Koscileny, Monreal; Cazrola, Coquelin; Iwobi, Ozil, Ozil-Chamberlain; Sanchez
Akiba: Cech, Holdig, Gibbs, Xhaka, Elneny, Lucas, Giroud
REFA: Viktor Kassai (Hungary)
Bayern Munich 5 FC Rostov 0
Huko Munich, Germany, Mechi ya Kundi D, iliisha kwa Wenyeji Bayern Munich kuwaadhibu FC Rostov 5-0.
Bao za Bayern zilipachikwa na Robert Lewandowski, Penati, Kimmich, Bao 2, Tomas Muller na Bernat.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
*Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu
Jumatano 14 Septemba 2016
KUNDI E
Bayer Leverkusen v CSKA
Tottenham v Monaco
KUNDI F
Legia Warsaw v Borussia Dortmund
Real Madrid v Sporting Lisbon
KUNDI G
Club Brugge v Leicester City
FC Porto v FC Copenhagen
KUNDI H
Juventus v Sevilla
Lyon v Dinamo Zagreb
Jumanne 27 Septemba 2016
KUNDI E
CSKA v Tottenham
Monaco v Bayer Leverkusen
KUNDI F
Borussia Dortmund v Real Madrid
Sporting v Legia Warsaw
KUNDI G
FC Copenhagen v Club Brugge
Leicester City v FC Porto
KUNDI H
Dinamo Zagreb v Juventus
Sevilla v Lyon
Jumatano 28 Septemba 2016
KUNDI A
Arsenal v Basel
Ludo Razgrad v Paris St Germaine
KUNDI B
Besiktas v Dynamo Kiev
Napoli v Benfica
KUNDI C
Borussia Monchengladbach v Barcelona
Celtic v Man City
KUNDI D
Atletico Madrid v Bayern Munich
FC Rostov v PSV Eindhoven
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MAKUNDI:
Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba
Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba
Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba
Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba
Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba
Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba
MECHI ZA MTOANO:
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)
MANCHESTER
UNITED wanaanza kampeni yao ya Mechi za Makundi ya UEFA EUROPA LIGI
Alhamisi Usiku Ugenini huko Uwanjani De Kuip, Stadion Feijenoord Jijini
Rotterdam Nchini Netherlands kupambana na Feyenoord kwenye Mechi ya
Kundi A.
Mechi nyingine ya Kundi A ni kati ya Zorya Luhansk ya Ukraine wakicheza na Fenerbahçe ya Uturuki.
Timu
nyingine ya England ambayo ipo kwenye Mashindano haya ni Southampton
ambao wapo Kundi K na wapo Nyumbani kucheza na Sparta Praha ya Czech
Republic.
TATHMINI – Feyenoord v Man United
Man
United ndio kwanza wanatoka kufungwa na Man City 2-1 kwenye Mechi ya
EPL, Ligi Kuu England, na Meneja wao Jose Mourinho amedokeza ataibadili
Timu.
Wachezaji
ambao wanatarajiwa kuanza Mechi hii ni Chipukizi Marcus Rashford na
Ander Herrera ambao kwenye Mechi na City waliingizwa Kipindi cha Pili na
kuleta uhai mkubwa.
Man
United imeshacheza na Feyenoord mara 2, kwenye Kundi lao la UEFA
CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 1997/98, na Man United kushinda Mechi zote mbili
ikiwemo 3-1 huko Uwanjani De Kuip ambako Andy Cole alipiga Hetitriki.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MAN UNITED – Mechi zao za Kundi A:
**Saa za Bongo
MD 1 – Alhamisi Sep 15 2000 – Feyenoord v Man United
MD 2 – Alhamisi Sep 29 22:05 – Man United v Zorya Luhansk
MD 3 – Alhamisi Okt 20 22:05 – Man United v Fenerbahce SK
MD 4 – Alhamisi Okt 27 2000 – Fenerbahce SK v Man United
MD 5 – Alhamisi Nov 24 2305 – Man United v Feyenoord
MD 6 – Alhamisi Des 8 2100 – Zorya Luhansk v Man United
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Hivi
sasa Feyernoord ipo chini ya Kocha Giovanni van Bronckhorst ambae ni
Mchezaji wa zamani ewa Arsenal na baadae kuhamia Barecelona na kisha
kurudi kwao kuichezea Feyernoord.
Kikosi
cha Feyernoord kina Wachezaji kadhaa waliowahi kuzichezea Klabu za Ligi
Kuu England na hao ni Dirk Kuyt, aliekuwa Liverpool, Kipa Brad Jones,
ambae nae alikuwa Liverpool na Eljero Elia aliewahi kuichezea
Southampton kwa Mkopo Mwaka 2015.
Nayo
Timu ya Straika wa Tanzania Mbwana Samatta, Genk ya Belgium itaanza
Ugenini na Rapid Wien ya Austria katika Kundi F ambapo pia wapo Sassuolo
ya Italy, watakaokuwa Nyumbani, kucheza na Athletic Bilbao ya Spain.
UEFA EUROPA LIGI
Mechi za Ufunguzi
Alhamisi Septemba 15
KUNDI A: Feyenoord v Manchester United, Zorya Luhansk v Fenerbahçe
KUNDI B: Young Boys v Olympiacos, APOEL v Astana
KUNDI C: Mainz v St-Étienne, Anderlecht v Qäbälä
KUNDI D: AZ Alkmaar v Dundalk, Maccabi Tel-Aviv v Zenit
KUNDI E: Viktoria Plzeň v Roma, Astra Giurgiu v Austria Wien
KUNDI F: Rapid Wien v Genk, Sassuolo v Athletic Club
KUNDI G: Standard Liège v Celta Vigo, Panathinaikos v Ajax
KUNDI H: Konyaspor v Shakhtar Donetsk, Braga v Gent
KUNDI I: Salzburg v Krasnodar, Nice v Schalke
KUNDI J: QarabaÄŸ v Slovan Liberec, PAOK v Fiorentina
KUNDI K: Inter Milan v Hapoel Beer-Sheva, Southampton v Sparta Praha
KUNDI L: Osmanlıspor v Steaua Bucureşti, Villarreal v Zürich
TAREHE MUHIMU
Droo
26/08/16: Makundi
12/12/16: Raundi ya Mtoano ya Timu 32
24/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16
17/03/17: Robo Fainali
Makundi
15/09/16: Mechidei 1
29/09/16: Mechidei 2
20/10/16: Mechidei 3
03/11/16: Mechidei 4
24/11/16: Mechidei 5
08/12/16: Mechidei 6
16/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Mechi za Kwanza
23/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Marudiano
09/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi za Kwanza
16/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Marudiano
13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza
20/04/17: Robo Fainali, Marudiano
04/05/17: Nusu Fainali, Mechi za Kwanza
11/05/17: Nusu Fainali, Marudiano
24/05/17: Fainali (Friends Arena, Solna, Stockholm, Sweden)
shukrani zasngu kwa soka in bongo na mpekuzi
Hakuna maoni