Thursday, September 8, 2016
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya Septemba 8
Thursday, September 8, 2016
Mahakimu 11 Wafukuzwa Kazi......Wengine 30 Kikaangoni
Watumishi 34 wa mahakama wakiwemo mahakimu 11, wamefukuzwa kazi kutokana na makosa mbalimbali ya kinidhamu.
Aidha, Tume ya Utumishi wa Mahakama inaendelea kujadili hatma ya mahakimu 30, waliokuwa wanatuhumiwa kuhusika na rushwa na kushinda zao mahakamani ili kuangalia kama walifanya makosa ya kinidhamu.
Jaji
Mkuu, Mohammed Chande Othman alisema hayo Dar es Salaam jana wakati
akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea taarifa za ukaguzi
wa mahakama pamoja na uendeshwaji wa mashauri.
Othman
alisema watumishi hao, wamefukuzwa kutokana na uamuzi wa kikao cha Tume
ya Mahakama, kilichofanyika Agosti 18, mwaka huu baada ya kushughulikia
masuala mbalimbali ya kinidhamu.
“Tumewafukuza
mahakimu wakazi wafawidhi, mahakimu wa mahakama za Mwanzo za Rombo,
Temeke, Bahi na Chamwino na watumishi wengine 23. Hii ni idadi ndogo
ambayo ni sawa na asilimia 0.005 ya wafanyakazi wote lakini kwa mahakama
ni doa kubwa,” alisema Jaji Mkuu.
Alisema
mahakimu hao wamefukuzwa kwa makosa mbalimbali ya kinidhamu, ikiwemo
kutumia muhuri wa mahakama kinyume cha taratibu, kuathiri utendaji wa
haki kwa kumsaidia mtu kufungua kesi moja katika mahakama mbili pamoja
na kufungua kesi ya mirathi bila kuwa na hati ya kifo.
Aliongeza
kuwa kuna makosa ya kisheria ambayo jaji au hakimu akikosea kutumia
kifungu cha sheria hawajibishwi, lakini kuna makosa ya kinidhamu ambayo
yanaondoa sifa ya kuwa hakimu au jaji.
Kuhusu
mahakimu walioshinda kesi za rushwa mahakamani, Jaji Chande alisema
mahakama inaweza isiwakute na hatia, lakini Tume itaangalia kama
walifanya vitendo vya ukosefu wa nidhamu na kuwawajibisha.
Aidha,
alisema mahakimu wengine 32 waliokuwa wanakabiliwa na kesi za jinai na
kushinda kesi mahakamani, wanafunguliwa mashitaka ya kinidhamu katika
Kamati ya Maadili ya Maofisa wa Mahakama kwa sababu inawezekana
hawajapatikana na hatia ya kosa la jinai, lakini kama kuna vitendo vya
ukosefu wa maadili watawawajibisha kimaadili.
Mahakama Maalumu ya Ufisadi
Katika hatua nyingine, Mahakama Maalumu ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi imeanza rasmi na wiki ijayo Kanuni za Uendeshaji wa mahakama hiyo, zinatarajiwa kuchapishwa.
Katika hatua nyingine, Mahakama Maalumu ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi imeanza rasmi na wiki ijayo Kanuni za Uendeshaji wa mahakama hiyo, zinatarajiwa kuchapishwa.
Jaji
Mkuu Othman alisema mahakama hiyo, imeanza rasmi Julai 18 mwaka huu
baada ya Rais John Magufuli kusaini sheria ya uanzishwaji wa mahakama
hiyo.
“Wiki
ijayo tutachapisha kanuni mbalimbali za uendeshwaji wa mahakama hiyo,
ikiwemo jinsi ya kulinda mashahidi pamoja na taratibu za ufunguaji wa
kesi,” alisema Othman.
Alisema
mahakama hiyo itakuwa na majaji wa kutosha ili kufanya kazi kwa
uadilifu na kumaliza kesi kwa wakati, pia haitakuwa ikiahirisha kesi
mara kwa mara.
Kuhusu
utendaji kazi wa mahakama, Jaji Mkuu alisema mahakama haiwezi kutoa
haki kama itakuwa inajificha au kuendeshwa kwa siri, ndiyo maana kwenye
maboresho ya mahakama, wameamua kuwapa fursa wananchi kutoa mapendekezo
au kero zao kupitia namba za simu pamoja na barua pepe.
Kesi za uchaguzi
Awali akiwasilisha taarifa za utendaji wa Mahakama Kuu, Mahakama za Hakimu Mkazi, Wilaya na za Mwanzo, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta alisema baada ya uchaguzi, walipokea kesi 247 za uchaguzi, 53 za kupinga matokeo ya ubunge na 194 za udiwani.
Awali akiwasilisha taarifa za utendaji wa Mahakama Kuu, Mahakama za Hakimu Mkazi, Wilaya na za Mwanzo, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta alisema baada ya uchaguzi, walipokea kesi 247 za uchaguzi, 53 za kupinga matokeo ya ubunge na 194 za udiwani.
Mugeta
alisema tayari wameshamaliza kesi 234, zimebaki 13, lakini hadi kufikia
Desemba mwaka huu kesi zote zitakuwa zimemalizika.
Aidha,
alisema tathmini waliyoifanya inaonesha kesi zilizopo zinawiana na
mahakimu, na kama watawezeshwa kwa vifaa vya kutendea kazi hadi Desemba
mwaka huu watamaliza kesi zote zilizofunguliwa mwaka huu.
Mahakama ya Rufaa
Kwa upande wake, Msajili wa Mahakama ya Rufaa, John Kahyoza alisema kiwango cha kumaliza mashauri katika Mahakama ya Rufaa kimeongezeka, pia wana lengo la kuhakikisha nakala za hukumu zinapatikana siku hukumu na ndani ya siku tatu zitapatikana kwenye tovuti ya Mahakama ya Tanzania.
Kwa upande wake, Msajili wa Mahakama ya Rufaa, John Kahyoza alisema kiwango cha kumaliza mashauri katika Mahakama ya Rufaa kimeongezeka, pia wana lengo la kuhakikisha nakala za hukumu zinapatikana siku hukumu na ndani ya siku tatu zitapatikana kwenye tovuti ya Mahakama ya Tanzania.
Aidha,
aliwaomba wananchi watoe ushirikiano ili rufaa zisikilizwe na kuisha
mapema, kwa sababu kuna watu wanashindwa kufika mahakamani bila sababu
za msingi au kutoa visingizio jambo linalosababisha rufaa zao kuchelewa.
Umuhimu wa mahakama
Katika hotuba yake kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria Februari 4, mwaka huu, Rais Magufuli alisema anaitegemea sana Mahakama na aliwaambia majaji na mahakimu nchini kuwa:
Katika hotuba yake kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria Februari 4, mwaka huu, Rais Magufuli alisema anaitegemea sana Mahakama na aliwaambia majaji na mahakimu nchini kuwa:
“Nawaomba
waheshimiwa majaji na waheshimiwa mahakimu, muitangulize Tanzania
kwanza. Mkiitanguliza Tanzania kwanza tutaweza kufika mbali na tutaweza
kuwasaidia watanzania wengi.
"Nimeamua
nchi iende, na itaenda. Anayefikiri ataikwamisha, atakwama yeye kwa
sababu Mungu yuko pamoja na mimi. Na watu ninaowategemea sana ni
Mahakama. Mahakama unafunga kila mmoja. Hata Rais nikitaka kufungwa na
Mahakama, nafungwa. Mbunge anafungwa, nani anafungwa, nyinyi ndio
wenyewe”.
Thursday, September 8, 2016
Marais EAC Kukutana kwa Dharura Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyeji wao Rais Magufuli
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano wa 17 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyika Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameitisha Mkutano wa
17 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi Wanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) utakaofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Septemba,
2016.
Mkutano
huo ambao ulitanguliwa na vikao vya maandalizi vya Makatibu Wakuu na
Mawaziri vilivyofanyika Jijini Arusha utajadili agenda kuu nne ambazo
ni:- Mahusiano ya kibiashara na uwekezaji kati ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) na Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Mkataba wa Ushirikiano wa
Kibiashara (EPA).
Agenda
zingine ni Kupokea Taarifa ya Mwezeshaji wa mazungumzo ya Amani nchini
Burundi, Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Tanzania; Kupata
taarifa ya hatua za kukamilisha uanachama wa Sudan Kusini kwenye EAC; na
Kuapishwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka
Rwanda.
Akizungumzia
mkutano huo kwa Waandishi wa Habari, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa
mkutano huu umeitishwa kwa dharura ili kuzungumzia agenda hizo muhimu
hususan ile ya nchi wanachama kukubaliana kwa pamoja kusaini au
kutosaini Mkataba wa EPA ifikapo tarehe 1 Oktoba, 2016.
Kuhusu
Mkataba wa EPA, Mhe. Waziri Mahiga alisema kuwa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ilianza mazungumzo na Jumuiya ya Ulaya ya kushirikiana
kibiashara kupitia EPA miaka 14 iliyopita na kuingia makubaliano ya
awali mwaka 2014.
Alieleza
kuwa kwa mujibu wa makubaliano hayo ya awali EU na EAC zilikubaliana
Mkataba huo usainiwe kwa pamoja na nchi zote za Jumuiya mwezi Julai 2016
kabla ya kuanza utekelezaji wake.
Hata
hivyo Tanzania ilitangaza kutosaini makubaliano hayo kwa sababu mkataba
huo unaweza kukwamisha juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya
Tanzania nchi ya Viwanda na Uchumi wa kati ifikapo 2025.
Aidha,
Tanzania inahitaji kujadiliana zaidi na nchi wanachama ili kujiridhisha
kuwa mkataba huo hautoathiri Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika
Mashariki hususan hatua ya mwanzo ya mkataba ambayo ni Umoja wa Forodha.
Kuhusu
nchi nyingine wanachama Mhe. Mahiga alieleza kwamba, tayari Kenya na
Rwanda zimesaini mkataba huo huku Uganda ikisubiri majadiliano ya nchi
wanachama kabla ya kusaini na Burundi ikijitoa kusaini mkataba huo kwa
vile tayari nchi za Ulaya zimeiwekea vikwazo vya kiuchumi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 07 Septemba 2016.
Thursday, September 8, 2016
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akagua makazi yake mapya Dodoma.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa makazi mapya
ya Waziri Mkuu katika eneo la Mlimwa na kuagiza umalizike kwa wakati ili
aweze kuhamia kama alivyoahidi.
Katika ziara hiyo aliyoifanya jana mchana (Jumatano, Septemba 7, 2016) Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na namna kazi ya ujenzi inavyofanyika.
“Nimekuja
kukagua makazi mapya na mahali pa kufanyia kazi. Kazi ya ujenzi
inaendelea vizuri, nimejionea mwenyewe na naamini katika kipindi kifupi
watakuwa wamekamilisha,” alisema.
Alisema
kutokamilika kwa ujenzi huo hauwezi kukwamisha azma yake ya kuhamia
Dodoma kwa sababu tayari inafahamika kuwa Makao Makuu ya Ofisi ya Waziri
Mkuu yako Dodoma.
Alisema
uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma hautokani na shinikizo la kisiasa
bali ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko
lake ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16
wa chama cha TANU.
“Tangu
wakati huo Serikali zote ziliendelea kufanya juhudi mbalimbali za
kuandaa miundombinu na hata awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa
uwekaji wa miundombinu hiyo,” alisema.
“Pia
tukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais aliyotoa kwenye hotuba yake ya Julai
23, 2016 alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, na akairudia tena
Julai 25, kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa na mimi siku hiyo
hiyo nikaweka msisitizo,” alisema.
Alisema
uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano wa kuhamia Dodoma unakuja baada ya
kuridhishwa na ujenzi wa miundombinu na maeneo ya kutolea huduma za
kijamii kwa wageni na wenyeji ikiwemo Hospitali ya Benjamini Mkapa
iliyopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yenye uwezo wa kutibu
magonjwa makubwa kama ya moyo na figo.
Waziri
Mkuu alisema tayari Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ina
mpango kamambe (master plan) na ina viwanja vya kutosha kujenga makazi
na ofisi mbalimbali.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
,,,,,,,
Thursday, September 8, 2016
Wazee wa CHADEMA Wamtuhumu Msajili wa Vyama Kwa Kuandaa Mitego Haramu ya Kukifuta Chama Hicho
Baraza
la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limetoa pongezi
kwa Kamati Kuu ya chama hicho kuahirisha maandamano na mikutano ya nchi
nzima iliyopewa jina la Ukuta.
Maandamano
hayo ambayo yalipangwa kufanyika kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu
yaliahirishwa na Kamati Kuu ya chama hicho kwa madai ya kuombwa na
viongozi wakuu wa madhehebu ya dini.
Akizungumza
katika Makao Makuu ya chama hicho jana, Katibu Mkuu wa Baraza hilo,
Roderick Lutembeka alisema, hatua ya kamati hiyo kuahirisha maandamano
hayo ni muhimu na inaonesha jinsi chama hicho kina viongozi wavumilivu.
“Kwa
kutambua moyo wa kiuongozi waliouonesha na dhamira ya dhati ya
kuwatumikia Watanzania wote, tunapenda kuwapongeza viongozi wetu wakuu
kwa uamuzi huu wa busara ambao umeuthibitishia umma kuwa chama kina
viongozi imara,” alisema Lutembeka
Katika
hatua nyingine, baraza hilo limesema limebaini kuwepo kwa njama
zinazopikwa dhidi ya chama hicho kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa na Baraza la Vyama vya Siasa nchini, kukifuta chama hicho.
“Taarifa
zinaonesha njama hizo zinalenga kukihujumu Chadema kwa kuandaa mitego
haramu ya kisiasa ili hatimaye yatolewe mapendekezo ya kukifuta katika
orodha ya vyama vya siasa,” alisema Lutembeka na kuongeza;
“Tarehe
15 Agosti mwaka huu Jaji Mtungi alitangaza kuwa, Baraza la Vyama vya
Siasa lilikuwa limeitisha kikao ambacho kingefanyika tarehe 29-30 Agosti
kujadili masuala ya hali ya kisiasa nchini. Siku mbili kabla ya kikao
Mwenyekiti wa baraza akatangaza kukiahirisha hadi tarehe 3-4 mwezi huu.
“Jambo
la kushangaza baada ya busara kutumika kupitia viongozi wa dini
kushawishi Chadema kuahirisha kwa kutoa mwanya wa mazungumzo hadi tarehe
1 mwezi ujao, Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa ikaibuka
tena na kutangaza kuahirisha kikao cha baraza hadi itakapotangazwa tena.
“Wakati
taarifa zote hizo zikitolewa na viongozi wa baraza, ofisini hapa
(Chadema) hakuna hata barua moja kutoka kwa msajili ya kutuita katika
kikao chochote kati ya hivyo. Kuanzia kile cha tarehe 29-30 Agosti,
tarehe 3-4 Septemba wala hiyo ya kuahirisha.
“Katika mazingira haya nani ambaye hatashawishika kuamini ofisi ya msajili inatii maagizo ya watawala,”
Thursday, September 8, 2016
Profesa Lipumba Aendelea Kupingwa Kila Kona.
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba
ameendelea kupingwa ndani ya chama hicho, na safari hii jumuiya ya
wanawake wa chama hicho ikiibuka na kumtaka ajiweke kando ili kuepusha
mpasuko zaidi.
Aidha,
wamewataka wanawake wafuasi wa chama hicho kote nchini, kuunga mkono
uongozi wa muda uliowekwa na Baraza Kuu la Uongozi wa CUF hivi karibuni,
ambao ulimtangaza Julius Mtatiro kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya
Uongozi ndani ya chama hicho kilichowahi kuwa kikuu cha upinzani
Tanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma jana, Makamu Mwenyekiti wa
Taifa wa Jumuiya ya Wanawake wa CUF, Savelina Mwijage ambaye pia ni
Mbunge wa Viti Maalumu, alisema kauli yao imelenga kuunga mkono hatua
iliyochukuliwa na Baraza la Uongozi dhidi ya wanaotajwa kukiuka Katiba.
Baraza
hilo lilikutana Agosti 28, mwaka huu mjini Zanzibar ikiwa ni hatua ya
kukabiliana na hali ya hewa iliyochafuka baada ya kundi la wanachama
kuvamia Mkutano Mkuu Maalumu wa uchaguzi Agosti 21, mwaka huu jijini Dar
es Salaam.
Mwijage
aliyefuatana na wabunge wengine wanne wa viti maalumu, amesema wanawake
ndani ya CUF wamefedheheshwa na wafuasi wa Profesa Lipumba kwa kufanya
vurugu, kudhalilisha wanawake wakati wa mkutano wa Dar es Salaam na pia
kukisababishia chama hasara ya Sh milioni 600 zilitozumika kugharamia
mkutano huo.
“Tunalaani
kwa nguvu zote vitendo vya baadhi ya watu wanaotaka kukivuruga chama,
lakini pia kuiingiza nchi katika migogoro ya udini, ukabili, ubara na
Uzanzibari. Mbinu hiyo imepitwa na wakati, tunawaomba Watanzania wote
wapuuze siasa hizo za uchochezi,” alisema.
Akizungumza
hatua ya kusimamishwa kwa baadhi ya viongozi 11 wa juu wa chama hicho,
wanaodaiwa kushiriki kukivuruga chama, alisema ni hatua sahihi na kwamba
hata Profesa Lipumba hapaswi kuwa nyuma ya vurugu hizo, kwani aliachia
madaraka kwa hiyari yake wakati chama kikielekea katika Uchaguzi Mkuu wa
mwaka jana.
Kauli
ya wanawake hao wa CUF ilikuja saa chache baada ya Mbunge wa Kaliua,
Magdalena Sakaya ambaye ni mbunge pekee wa kike mwenye jimbo kutoka
chama hicho, kuliambia Bunge kuwa hajatikiswa na uamuzi wa kumsimamisha
uanachama na kwamba anaendelea kutimiza majukumu yake ndani ya chama,
ambacho kabla ya mpasuko wa hivi karibuni, ndiye aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu Tanzania Bara.
Mbali
ya Lipumba na Sakaya, wengine waliositishiwa uanachama ni Abdul Kambaya
ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Ashura
Mustapha, Omar Mhina, Thomas Malima, Kapasha M. Kapasha, Mohamed Habib
Mnyaa, Haroub Shamis na Mussa Haji Kombo.
Ashura
ni mjumbe wa Baraza Kuu na aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari na
Mawasiliano ya Umma CUF wakati Mnyaa na Kombo, walikuwa wabunge kipindi
cha 2010-2015; Mnyaa akiwakilisha Jimbo la Mkanyageni na Kombo Jimbo la
Chake Chake, kisiwani Pemba.
Kutokana
na kusimamishwa kwa viongozi hao, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar,
Nassor Ahmed Mazrui alimtangaza Mtatiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu
Bara kuwa kiongozi wa kamati ya uongozi wa muda, inayowajumuisha pia
Ahmed Katani na Mwijage ambao ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la
Taifa.
Katani
ni Mbunge wa Tandahimba, Mtwara wakati Severina alikuwa mjumbe wa
kamati kama hiyo ilipoteuliwa Agosti mwaka jana baada ya Profesa Lipumba
kujiuzulu uenyekiti kwa barua ya Agosti 5, mwaka jana.
Baraza
hilo lilimteua pia Joram Bashange kukaimu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu
Bara na Mbaraka Maharagande kuwa Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari,
Uenezi na Mawasiliano kwa Umma hadi hapo nafasi hizo zitakapojazwa rasmi
kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Chama hicho.
Thursday, September 8, 2016
Afariki Kisimani Akimuokoa mbuzi
MKAZI
wa Kijiji cha Kazibizyo Kata ya Ng’anzo, Wilayani Bukombe, Sebastian
Lumbe (36), amefariki dunia kisimani alimoingia kumuokoa mbuzi kwa
ujira wa Sh 6,000.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Mtaa wa Misheni baada ya
mbuzi huyo kutumbukia kwenye kisima kinachodaiwa kuwa na urefu wa futi
30.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Misheni, Antony Kuya alithibitisha kutokea tukio hilo.
Alisema
baada ya mbuzi huyo kutumbukia kisimani, mmiliki wake, Marco Sylvester
alitangaza ujira wa Sh 6,000 kwa mtu ambaye angefanikiwa kumtoa na
ndipo Lumbe alipojitolea kuingia kisimani humo.
Alisema
kabla ya Lumbe kuingia kisimani humo na kukutwa na mauti, walijitokeza
watu wawili tofauti lakini kila walipoingia waligundua kisima hicho
kilikuwa kirefu.
Kwa sababu hiyo walighairi hadi alipofika yeye na kujitosa.
“Baada ya kuingia kisimani alianza kupiga kelele za kuomba msaada.
“Watu
waliokuwa karibu na kisima hicho walimtupia kamba lakini wakati
anajaribu kuivuta kupanda ilikatika na akaanguka kurudi kisimani.
“Baadaye
kijana mmoja, Leonard Mathayo aliingia kujaribu kumuokoa lakini wakati
akiwa humo ndani alisema baada ya kukaribia kufika mwisho wa shimo
alimkuta akitupa miguu.
“Alipoanza kumfunga kamba ili wamvute aliishiwa nguvu na kukosa hewa na hivyo ilimlazimu kuomba msaada kutoka nje,” alisema Kuya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo aliwaonya wananchi kuwa
waangalifu na visima virefu kama hivyo kwa sababu ni hatari.
Thursday, September 8, 2016
Profesa Lipumba Asema Hana mpango wa kuhama CUF wala kuanzisha chama Kingine ........Ataja Sababu Zilizomfanya Amkatae Lowassa
Aidha
amesema hana mpango wa kuanzisha chama chake kwa kuwa yeye bado ni
Mwenyekiti halali wa CUF kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho.
Akiongea
katika kipindi cha Powerbreakfast cha Clouds FM Alhamisi hii, Profesa
Lipumba amesema Katibu Mkuu wa CUF anataka kukiua chama cha CUF Tanzania
bara.
“Mimi nipo CUF bado, na ni Mwenyekiti halali kwa mujibu wa Katiba na sina mpango wa kuhamia chama kingine,”
“Katibu Mkuu wetu anataka chama hiki upande wa bara kife kabisa na ibaki CHADEMA pekee yake ndio maana anafukuza wabunge.,”
“Katibu Mkuu wetu anataka chama hiki upande wa bara kife kabisa na ibaki CHADEMA pekee yake ndio maana anafukuza wabunge.,”
Pia
Lipumba amesema Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif alikosea kumnyima mkono
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein kwa kuwa unapoenda kwenye msiba
jambo la msiba lilipaswa kutawala.
“Hata mimi nilipokutana na Maalim baada ya kunikatalia kurudi kwenye uenyekiti tulisalimiana.” Alisema Lipumba.
Katika hatua nyingine Lipumba alizungumzia sababu ya kutomkubali Mh. Edward Lowassa kuingia UKAWA.
“Sababu
za msingi za kutomkubali Mh. Edward Lowassa kuingia UKAWA, ni kwamba
ukiwa katika siasa unahitaji uongozwe na misingi na ‘principals’ na hoja
kwamba mnagombea kitu gani, na sisi tulianzisha UKAWA kwa kusema kwamba
tutafute nchi, serikali na dola inayowajibika ambayo inatengeneza mambo
vizuri, inatumia rasilimali vizuri itapambana na ufisadi na itajenga
demokrasia ya kweli katika nchi yetu, ukiwa na misingi hiyo kwamba
utataka kiongozi ambaye anaunga mkono misingi hiyo na tulikuwa wote
kwenye bunge la katiba na Mh. Edward Lowassa alikuwepo kwenye bunge hilo
hakuwa mmoja ya wabunge aliyeunga mkono rasimu ya Katiba,” alisema Lipumba.
Thursday, September 8, 2016
Ray C aonyesha muonekano wake mpya.........Mashabiki Wampa Ushauri Mzito
Msanii
wa muziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameonyesha picha yake ya kwanza toka
asaidiwe na jeshi la polisi miezi michache iliyopita baada ya kudaiwa
kuzidiwa na matumizi ya Madawa ya kulevya
Jumatano muimbaji huyo aliwaonyesha mashabiki wake muonekano wake mpya hali ambayo imewafanya mashabiki kumtaka kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya kwa kuwa amekuwa akisaidiwa mara kadhaa kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya lakini yeye amekuwa akirudia.
Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki wake.
Thursday, September 8, 2016
Majibu ya Waziri mkuu Majaliwa Leo Bungeni kuhusu wahusika wa mauaji ya askari na Swala la Uchumi wa Nchi
Serikali
ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaendelea kukutana na wadau tofauti
wanaohusika na masuala ya uchumi katika kuhakikisha uchumi wa nchi
unaendelea kukua.
Hayo
yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la
Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe mijini Dodoma aliyetaka kujua hali ya
uchumi ilivyo kwa sasa hapa nchini.
Waziri
Mkuu amesema kuwa lengo kuu la Serikali ya awamu ya tano ni
kuhakikisha uchumi wa nchi unaongezeka kupitia nyanja tofauti kwa
kushirikiana na taasisi za fedha zilizopo ili kufikia uchumi wa kati
kama ilivyoanishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza
kuhusu suala la midororo wa upokeaji wa mizigo katika bandari nchini,
Waziri Mkuu amesema kuwa mdororo huo umetokana na kupungua kwa kiasi cha
mizigo na kushuka kwa uchumi duniani.
Katika
suala ya mauaji yaliyotokea Tanga, Mwanza na Vikindu, Waziri Mkuu
amesema kuwa usalama wa wananchi utaendelea kuimarishwa huku serikali
ikiahidi kupambana vitendo vya mauaji kwa raia na askari katika maeneo
mbali mbali nchini.
“Serikali
imesikitika sana na jambo hili la mauaji hivyo itahakikisha wauaji hao
wanawekwa katika mikono ya Sheria na kuongeza ulinzi kwa maeneo yote
nchini kwa kuanzia ngazi ya vitongoji” alifafanua Waziri Mkuu.
Mbali na hayo Waziri Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kuthibiti matukio hayo.
Kuhusu
suala la uwepo wa tozo katika zao la korosho swali limeibuliwa na
Mbunge wa viti maalumu Mhe.Riziki Lulida (CUF), Waziri Mkuu Majaliwa
amesema kuwa Serikali imeshatoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya
kusimamia uondoaji wa Tozo zisizo na maana katika zao la korosho.
,,,,,,,,,,,,,,
Thursday, September 8, 2016
Waziri Mkuu: Serikali Haijashindwa Kuongoza Nchi
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo macho,
haijalala na haijashindwa kuongoza nchi bali imejipanga kuliongoza
Taifa kwa mafanikio makubwa.
"Serikali
haijashindwa kuongoza nchi. Nataka niwahakikishie waheshimiwa Wabunge
na wananchi wote kwamba tutaongoza nchi hii kwa mafanikio makubwa na
kazi hiyo imeanza kwa marekebisho makubwa kwa maeneo ambayo tunadhani
yatafanya Taifa hili liweze kupata mafanikio makubwa,” amesema.
Ametoa
kauli hiyo leo (Alhamisi, Septemba 8, 2016) Bungeni mjini Dodoma wakati
akijibu swali lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na
Mbunge wa Hai, Bw. Freeman Mbowe, ambaye alitaka kufahamu Serikali ina
mkakati gani wa kunusuru mdororo wa uchumi uliopo nchini.
Bw.
Mbowe alidai kwamba hali ya uchumi imeshuka na kwa mujibu wa taarifa za
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) uagizaji wa bidhaa kutoka nje umepungua,
uuzaji wa bidhaa nje ya nchi na sekta ya ujenzi imesimama hali
inayoashiria kudorora kwa uchumi.
Kuhusu
suala la kupungua kwa mizigo katika bandari na vituo vya forodha,
Waziri Mkuu amesema usafirishaji wa mizigo kwa njia ya bahari umeshuka
duniani kote kwa sababu ya kushuka kwa hali ya uchumi kutokana na
kuporomoka kwa bei ya mafuta na gesi.
Hata
hivyo Waziri Mkuu amesema tayari wafanyabiashara wa Rwanda na Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wameihakikishia Serikali kwamba mizigo yao
yote itakuwa inapitia Bandari ya Dar es Salaam hasa kwa mkakati wa
pamoja wa ujenzi wa reli ya standard gauge inayoanzia Dar es
Salaam-Tabora - Isaka.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inaendelea kuimarisha
amani na ulinzi kwenye maeneo yote nchini na kwamba vyombo vya dola
viko macho. “Watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu yakiwemo
mauaji watakamatwa popote walipo na kuchukuliwa hatua za kisheria,;
amesema.
Amesema
hatua hiyo inatokana na matukio ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni
ambapo raia wasiokuwa na hatia na askari waliuawa katika maeneo ya
Vikindu mkoani Pwani, Tanga na Mwanza. Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati
akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani
Katika
swali lake, Bw. Ngonyani alitaka kujua ya Serikali kuhusu kukomesha
mauaji hayo, yanayotokea kwa watu wasio na hatia pamoja na askari,
ambapo Waziri Mkuu, alitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wananchi na
familia, ambazo ndugu zao walipoteza maisha katika mauaji hayo.
Pia
ametoa wito kwa Watanzania wote kuhakikisha wanawafichua watu ambao
wanawatilia shaka na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili waweze
kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua
Habari na Ofisi ya Waziri Mkuu
Thursday, September 8, 2016
Jeshi La Polisi Latolea Ufafanuzi Taarifa Inayosambazwa Kwenye Mitandao Juu Ya Kukamatwa Watu Wanaokuwa Kwenye Nyumba Za Wageni Mchana
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam anatoa rai kwa wakazi wa Jiji la
Dar Es salaam na wageni wanaoingia jijini wakitokea mikoani kupuuza
taarifa za sauti zinazozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Polisi
wanawakamata ovyo watu wanaolala kwenye nyumba za kulala wageni.
Taarifa
hizo za uvumi zinazoendelea kuzagaa kwenye mitandao ya Kijamii kama
WHATSAPP, TELEGRAM na pia zimechapishwa kwenye baadhi ya magazeti kwamba
Askari Polisi wanawakamata watu ovyo mchana wakiwa kwenye nyumba za
kulala wageni kwa madai ya kukamata kwa makosa ya uzembe na uzururaji
na pia kutimiza kauli ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ‘HAPA
NI KAZI TU’.
Kimsingi
niwatoe hofu raia wema kuwa tunaendelea na oparesheni za kuwasaka
watuhumiwa wa makosa mbalimbali yakiwemo wanaofanya biashara ya nyumba
za kulala wageni kinyume cha sheria (guest bubu), majambazi na wahalifu
wengine wa makosa mbalimbali.
Aidha
taarifa za kuaminika zimebaini kuwa baadhi ya nyumba za kulala wageni
zimekuwa zikitumika kuhifadhi magenge ya wahalifu, dada poa na kaka poa,
hivyo Jeshi la Polisi tunawajibika kufuatilia na kuwakamata wahalifu.
Niwajibu
wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala
wageni, Hoteli, migahawa, Vilabu vya vileo, kumbi za starehe
zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria, hatua kali
za kisheria dhidi yao zitachukuliwa.
Sheria
ya Mwenendo ya makosa ya jinai kifungu cha 60(1) (sura ya 77
iliyofanyiwa marekebisho 2002) kinampa nguvu askari kufanya ukaguzi wa
maeneo yote yaliyotajwa hapo juu na kumkamata mtu yeyote anayetiliwa
shaka akienda kinyume na utaratibu wa biashara hizo.
Sambamba
na hayo nawatahadharisha wafanyabiashara wote wa nyumba za kulala
wageni wafuate taratibu za kupokea wageni kwa kuandika kwenye vitabu,
kuandika namba za vitambulisho vyao na sehemu wanayotoka, na pale
watakapomtilia mashaka mteja yeyote watoe taarifa kituo chochote cha
polisi.
Pia
wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi wanawajibika
kuwatambua wageni wote wanaoingia kwenye himaya zao na kuwachukulia
hatua stahiki ili kuimarisha usalama katika jiji letu la Dar Es salaam.
DAR ES SALAAM BILA UHALIFU INAWEZEKANA, TUSHIRIKIANE KUISAFISHA JIJI LETU
S.N.SIRRO - CP
KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
Thursday, September 8, 2016
Makamu wa Rais: Viongozi Na Watumishi Wa Umma Kuchukuliwa Hatua Kali Iwapo Watabainika Kukiuka Taratibu Za Kazi
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
ameiagiza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nchi kuchunguza na
kuwachukulia hatua kisheria na za kinidhamu viongozi na watumishi wa
umma ambao wanakiuka taratibu za kazi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 8-Sep-2016 mjini Mtwara
wakati anafungua jengo la sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma
Kanda ya Kusini ambalo ujenzi wake umegharimu takribani shilingi bilioni
MBILI.
Makamu
wa Rais amesema iwapo kama hatua hizo zitachukuliwa haraka zitakomesha
na kupunguza kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa viongozi na watumishi wa
umma hali ambayo itaongeza uwajibikaji katika utendaji wa kazi miongoni
watendaji hao.
Amesisitiza
kuwa serikali itaendelea kuiimarisha sekretarieti ya maadili ya
viongozi wa umma nchini kwa kuijengea uwezo wa rasilimali watu na fedha
kwa kadri hali ya uchumi itakavyo ruhusu ili waweze kutekeleza majukumu
yao kwa ufanisi.
Makamu
wa Rais amewahimiza viongozi na watumishi wa umma kuthamini na
wahakikishe walinda maslahi ya umma wakati wote wa utendaji wao wa kazi
ili kuondoa malalamiko kwa wananchi.
Makamu
wa Rais amesema ni jambo la muhimu kwa sekretarieti hiyo kufutilia
mienendo ya viongozi wa umma na kuwabaini wale wanaokwenda kinyume na
misingi ya uadilifu na wachukuliwe hatua ipasavyo kabla hawaleta madhara
kwa serikali na jamii kwa ujumla.
Makamu
wa Rais pia ametoa rai maalum kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kuitumia
ofisi hiyo mpya ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya
Kusini kwa kutoa taarifa kuhusu mienendo ya viongozi wanaokiuka maadili
ya umma katika utendaji wao wa kazi ili waweze kuchukuliwa hatua.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala bora Angela Kairuki amesisitiza kuwa kazi ya kuhakiki
mali na madeni ya viongozi wa umma itaendelea kwa kasi nchini na mwaka
huu sekretarieti hiyo itahakiki mali za viongozi wapatao 500 kote
nchini.
Naye
Jaji Mstaafu na Kamishna wa Maadili Nchini Salome Kaganda akitoa
taarifa kuhusu ujenzi wa jengo hilo ameiomba serikali itenge fedha za
kutosha kwa ajili ya kufanikisha zoezi la uhakiki wa mali na madeni ya
viongozi kwa nchi nzima.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Mtwara.
8-Sep-2016.
LA LIGA: RONALDO KUREJEA REAL JUMAMOSI BERNABEU NA OSASUNA!
- Details
- Created: Tuesday, 06 September 2016 20:18
Msimu huu mpya Ronaldo, ambae ndie Mchezaji Bora Barani Ulaya, hajacheza hata Mechi moja ya Klabu yake Real Madrid na alirejea Mazoezini baada ya Real kutwaa UEFA SUPER CUP walipoibwaga Sevilla mapema Agosti na pia kuzikosa Mechi mbili za La Liga ambazo zote Real walishinda.
Mechi inayofuata kwa Real ni Jumamosi Uwanjani kwao Santiago Bernabeu kwenye La Liga watakapocheza na Osasuna lakini Kocha wa Real Zinedine Zidane huenda akapanga Kikosi mchanganyiko huku akiwa na jicho moja kwenye Mechi inayofuata ya UEFA CHAMPIONZ LIGI watakapocheza Jumatano Septemba 14 tena wakiwa Nyumbani Santiago Bernabeu na Sporting Lisbon ikiwa ni Mechi yao ya kwanza kabisa ya Kundi lao ya Mashindano hayo makubwa kabisa kwa Klabu Barani Ulaya ambayo wao ndio Mabingwa Watetezi.
Huenda Zidane akampa muda Ronaldo Uwanjani ili kumjenga polepole baada ya hivi karibuni kuzidisha kasi ya Mazoezi baada ya kupona Goti lake.
Kwenye La Liga, Real, Barca na Las Palmas ndizo Timu pekee zenye Pointi 6 baada ya kushinda Mechi zao zote 2 za kwanza za Msimu mpya na Ligi hiyo kusimama kwa Wiki 2 kupisha Mechi za Kimataifa.
LA LIGA
Ratiba:
**Saa za Bongo
Ijumaa Septemba 9
2145 Real Sociedad v RCD Espanyol
Jumamosi Septemba 10
1400 Celta de Vigo v Atletico de Madrid
1700 Real Madrid CF v Osasuna
1915 Malaga CF v Villarreal CF
1915 Sevilla FC v Las Palmas
2130 FC Barcelona v Deportivo Alaves
Jumapili Septemba 11
1300 Sporting Gijon v CD Leganes
1700 Valencia C.F v Real Betis
1915 Granada CF v SD Eibar
2130 Deportivo La Coruna v Athletic de Bilbao
ULAYA U-21: MARCUS RASHFORD AICHEZEA ENGLAND U-21 KWA MARA YA KWANZA, AFUMUA HETITRIKI!
- Details
- Created: Tuesday, 06 September 2016 21:41
England, wakiwa chini ya Meneja Gareth Southgate, Leo walimtumia Marcus Rashford, Kijana wa Man United mwenye Miaka 18, kwa mara ya kwanza kwenye Kikosi hicho baada ya Meneja wa England Sam Allardyce kuridhia aende huko badala ya Kikosi cha Kwanza.
Leo hii Rashford alijibu hilo kwa kupiga Bao 3 moja likiwa la Penati walipoishindilia Norway 6-1 licha ya wapinzani hao kuwa na Kijana Staa wa Real Madrid Martin Odegaard.
++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-MARCUS RASHFORD:
-HUPIGA BAO KILA MECHI YAKE YA KWANZA AKICHEZEA TIMU KWA MARA YA KWANZA!
-Mechi zake za kwanza kwa Man United kwenye Ligi Kuu England na EUROPA LIGI alifunga.
-Mechi yake ya kwanza kwa Kikosi cha Kwanza cha England alifunga.
-Hii Mechi yake ya kwanza kwa England U-21 amefunga.
++++++++++++++++++++
Bao nyingine za England zilifungwa na Lewis Baker, Ruben Loftus-Cheek na Nathaniel Chalobah.
Bao pekee la Norway lilifungwa na Ghayas Zahid.
Sasa England wamebakisha Mechi 2 kwenye Kundi la 9 na wanahitaji Pointi 3 tu kutinga Fainali Mwakani huko Poland.
VIKOSI VILIVYOANZA:
England: Gunn, Iorfa, Targett, Chalobah, Chambers, Hause, Baker, Ward-Prowse, Rashford, Loftus-Cheek, Redmond.
Akiba: Wildsmith, Holding, Hayden, Galloway, Gray, Watmore, Akpom.
Norway: Rossbach, Haraldseid, Jenssen, Grogaard, Fossum, Sorloth, Odegaard, Berge, Daehli, El Younoussi, Selnaes.
Akiba: Dyngeland, Trondsen, Zahid, Rosted, Thorsby, Meling, Espejord.
KOMBE LA DUNIA 2018: ARGENTINA BILA MESSI YANASA, NEYMAR AIPAISHA BRAZIL, CAVANI, SUAREZ WAIRUSHA URUGUAY!
- Details
- Created: Wednesday, 07 September 2016 06:34
Kombe la Dunia – Russia 2018
Mechi za Makundi
Matokeo:
Jumatano Septemba 7
Uruguay 4 Paraguay 0
Venezuela 2 Argentina 2
Chile 0 Bolivia 0
Brazil 2 Colombia 2
Peru 2 Ecuador 1
++++++++++++++++++++++++
Mechi 5 za Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini chini ya Mwamvuli wa Shirikisho lao CONMEBOL kusaka Nchi 4 zitakazotinga moja kwa moja huko Russia Mwaka 2018 kwenye Fainali za Kombe la Dunia zimepigwa Alfajiri ya Leo.
Brazil, wakicheza kwao huko Arena Amazonia, Manaus, waliichapa Colombia 2-1 kwa Bao za Miranda, Dakika ya Pili, na Neymar, Dakika ya 74, huku Bao la Colombia likifungwa na Marquinhos aliejifiunga mwenyewe Dakika ya 36.
Argentina, wakicheza Ugenini na bila ya Kepteni wao Lionel Messi, walitoka Sare 2-2 na Venezuela ambao waliongoza 2-0 kwa Bao za Dakika za 35 na 53 za Anor na Martinez na Argentina kusawazisha Dakika za 58 na 83 kupitia Prattor na Otamendi.
Uruguay, wakiwa kwao, waliishindilia Paraguay 4-0 huku Wafungaji wao wakiwa Edinson Cavani, Bao 2, Rodriguez na Luis Suarez.
++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-CONMEBOL itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.
-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye Kundi lao itashinda Mechi ya Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Solomon Islands na Tahiti.
++++++++++++++++++++++++
Hii ni Raundi ya 8 ya Mechi za Kanda hii na sasa Uruguay wapo kileleni wakifuatia Brazil, Argentina na Ecuador.
MSIMAMO:
CONMEBOL
Kombe la Dunia – Russia 2018
Mechi za Makundi
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Alhamisi Septemba 1
Bolivia 2 Peru 0
Ijumaa Septemba 2
Colombia 2 Venezuela 0
Ecuador 0 Brazil 3
Argentina 1 Uruguay 0
Paraguay 2 Chile 1
BAADA VAKESHENI, LIGI KUU ENGLAND DIMBANI JUMAMOSI, YA KWANZA DABI YA MANCHESTER, MAN UNITED-MAN CITY!
- Details
- Created: Wednesday, 07 September 2016 10:43
BAADA
kupumzika kwa Wiki 2 kupisha Mechi za Kimataifa, LIGI KUU ENGLAND, EPL,
itarejea tena kilingeni Jumamosi Septemba 10 na Mechi ya kwanza kabisa
ni Dabi ya Manchester kati ya Mahasimu Manchester United na Manchester
City.
Mechi hii itachezwa Uwanjani Old Trafford na kuzikutanisha Timu
ambazo, pamoja na Chelsea, ndizo pekee zilizocheza Mechi zao 3 na
kushinda zote na hivyo kuwa kileleni.
Mechi hii, ambayo itachezwa Saa 8 na Nusu Mchana na kusimamiwa na
Refa Mark Clattenburg, inawakutanisha Mameneja wapya kwa Klabu zao ambao
ni Mahasimu tangu huko Spain walipozioongoza Real Madrid na Barcelona.
++++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Safari hii Ligi hii ya England haina tena Jina la Mdhamini na
itajulikana rasmi kama Ligi Kuu tofauti na Msimu uliopita ilipoitwa
Barclays Premier League kutokana na udhamini wa Barclays.
+++++++++++++++++++++++++++
Hivi sasa Jose Mourinho, aliekuwa Real Madrid, ni Meneja wa Man
United na Pep Guardiola, aliekuwa Barcelona ni Meneja wa Man City.
Mara baada ya mtanange huo wa Dabi, Saa 11 Jioni, zipo Mechi
nyingine 6 za EPL ikiwemo ile ya Arsenal kucheza Nyumbani na Southampton
na Tottenham kuwa Ugenini kucheza na Stoke City.
Jumamosi itafungwa na Mechi ya Saa 1 na Nusu Usiku huko Anfield ambako Liverpool watacheza na Mabingwa Watetezi Leicester City.
Jumapili ipo Mechi 1 kati ya Swansea City na Chelsea na Jumatatu
Usiku pia ipo Mechi moja huko Stadium of Light kati ya Sunderland na
Everton.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 10
1430 Man United v Man City
1700 Arsenal v Southampton
1700 Bournemouth v West Brom
1700 Burnley v Hull
1700 Middlesbrough v Crystal Palace
1700 Stoke v Tottenham
1700 West Ham v Watford
1930 Liverpool v Leicester
Jumapili Septemba 11
1800 Swansea v Chelsea
Jumatatu Septemba 12
2200 Sunderland v Everton
KUELEKEA DABI YA MANCHESTER: IBRA AMTIA MCHECHETO BRAVO!
- Details
- Created: Thursday, 08 September 2016 08:50
Zlatan
Ibrahimovic amechochea moto wa Dabi ya Manchester itakayochezwa
Jumamosi Uwanjani Old Trafford kwa kumpelekea onyo Kipa mpya wa
Manchester City Claudio Bravo kupitia Mtandao wa Jamii wa Facebook.
Bravo, mwenye Miaka 33 na ambae ni Nahodha wa Nchi yake Chile,
alijiunga na Man City hivi karibuni kutoka Barcelona na Jumamosi
anatarajiwa kukaa Golini kwa mara ya kwanza wakati City ikitua Old
Trafford kuwavaa Mahasimu wao Manchester United.
Ibrahimovic, aliejiunga na Man United Msimu huu akitokea PSG na
ambae ndie Mfungaji Bora wa Man United kwa sasa, aliposti Video kwenye
Facebook ikiwa na kauli ya 'kumtisha' Bravo huku akionekana akifungasha
Boksi lenye vifaa vya Mazoezi ili alitume kama Paseli liende Uwanja wa
Etihad kwa Bravo.
Bango la Video hiyo lilikuwa na maneno: "Karibu Manchester! Hivi ni vifaa vya Mazoezi, utavihitaji. Ntakuona Jumamosi."
Shirika la Marekani Liberty Media kununua Formula 1
- Saa 3 zilizopita
Shirika la habari
la Liberty limesema litanunua biashara ya mashindano ya magari ya
langalanga ya Formula 1, katika mkataba wa thamani ya dola bilioni nne
unusu za kimarekani.
Liberty, ambayo inamilikiwa na bilionea John
Malone, katika hatua za kwanza itanunua hisa chache katika kampuni hiyo
kutoka kwa muungano wa wawekezaji wanaouza hisa.Baadaye, itachukua udhibiti kamili iwapo maafisa wasimamizi wa mashindano wataidhinisha ununuzi.
Liberty imesema Bernie Ecclestone, ambaye amedhibiti mashindano hayo kwa muda mrefu, ataendelea kuwa afisa mkuu mtendaji wa Formula One.
Chase Carey, naibu mwenyekiti wa 21st Century Fox, atakuwa mwenyekiti mpya.
Mathieu Flamini: Crystal Palace wamchukua kiungo wa zamani Arsenal
- Saa moja iliyopita
Crystal Palace
wamemchukua kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mathieu Flamini, ambaye
alikuwa amesalia kuwa ajenti huru baada ya kuruhusiwa kuondoka na klabu
ya Arsenal majira ya joto.
Flamini, 32, amepewa mkataba wa hadi mwisho wa msimu.Mchezaji huyo aliondoka kwa Gunners baada ya kucheza mechi 246 vipindi viwili na kushinda vikombe vya FA mara tatu.
Mfaransa huyo pia alishinda Serie A mwaka 2011 miaka mitano aliyokaa AC Milan.
Ndiye mchezaji wa tano kununuliwa na Palace kwa mkataba wa kudumu majira ya sasa.
Flamini alihamia Italia baada ya kukaa miaka minne Arsenal kisha akarejea Emirates mwaka 2013.
Palace wamewanunua pia Andros Townsend, Steve Mandanda, James Tomkins, na Christian Benteke.
Wamempokea pia Loic Remy kwa mkopo kutoka Chelsea.
SHUKRANI ZANGU NI KWA BBC SWAHILI ,MPEKUZI PAMOJA NA SOKA IN BONGO
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 08, 2016
Rating:
Hakuna maoni