Sunday, September 18, 2016
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Septemba 18
Sunday, September 18, 2016
Aliyebaka na kulawiti kwenye kaburi afungwa miaka 30 jela
Mahakama
ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu Ally Rashid maarufu kwa
jina la Ally Mwizi kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na
hatia ya kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka 25, makaburini.
Hukumu
hiyo iliyovuta hisia za watu wengi wa Manispaa ya Mpanda ilitolewa jana
na Hakimu wa mahakama hiyo, Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na
ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka pasipo kutia shaka,
ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi, Jamila Mziray.
Awali
Mwendesha Mashtaka Mziray alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo
alitenda kosa hilo Juni 17, mwaka huu, saa 2:00 usiku katika makaburi ya
Kashaulili yaliyoko katika Mtaa wa Kotazi, Manispaa ya Mpanda.
Ilidaiwa
kuwa mshtakiwa kabla ya kutenda kosa hilo alimfuata msichana huyo
ambaye alikuwa ameibiwa vitu vyake vya ndani ya nyumba ambapo
alimdanganya kuwa ana uwezo wa kumsaidia kuvipata vitu vyote
alivyoibiwa.
Mziray
alidai kuwa baada ya msichana huyo kuahidiwa na mshtakiwa kuwa vitu
vyake alivyoibiwa vitapatikana alimlipa mshtakiwa Sh 30,000 ili
akamwoneshe vitu vyake alivyoibiwa.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa siku hiyo ya tukio mshtakiwa alimpigia simu
msichana huyo saa 2:00 usiku akimtaka waonane ili akamwonesha vitu vyake
vilivyoibiwa.
Mziray
alieleza mshtakiwa alikwenda nyumbani kwa msichana huyo na wakaongozana
hadi kwenye makaburi ya Kashaulili ambako alidai ndiko vilipo vitu
vilivyoibwa lakini ghafla mshtakiwa alimpiga ngwala msichana huyo na
kumbaka na kumlawiti huku akimtishia maisha iwapo akijaribu kupiga
kelele.
“Baada
ya kumtendea unyama msichana huyo, mshtakiwa alimwomba dada huyo waende
kwenye nyumba ya kulala wageni inayoitwa Kingi Paris ili wakaendelee
kufanya mapenzi zaidi kwa kile alichodai kuwa nyumba hiyo ya wageni
inafaa zaidi kufanyia tendo la ndoa kuliko juu ya kaburi,” alidai.
Sunday, September 18, 2016
Mwenyekiti UVCCM mbaroni kwa kughushi kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa.
Siku
tatu baada ya kutuliza vurugu baina ya viongozi na wanachama wa Jumuiya
ya Vijana ya CCM (UVCCM), polisi inamshikilia mwenyekiti wa umoja huo,
Lengai Ole Sabaya kwa tuhuma za kughushi kitambulisho cha Idara ya
Usalama wa Taifa.
Viongozi
hao walipambana Alhamisi wiki hii wakati wakigombea ofisi ya umoja huo
ya mkoa, vurugu zinazodaiwa kusababishwa na mgogoro wa chini kwa chini
uliodumu kwa miezi miwili kati ya makundi mawili yanayokinzana.
Wakati hali hiyo haijatulia, juzi saa 6.00 usiku, Sabaya alikamatwa katika baa ya Mile Stone akiwa na wenzake.
Habari
zilizopatikana jijini Arusha zinasema kitambulisho hicho kilipelekwa
kituo kikuu cha polisi ambako kulifunguliwa jadala la kesi ya madai
namba RB 5055/2016. Ilifunguliwa na hoteli ya Sky Way aliyokwenda kulala
na kuondoka bila kulipa gharama za malazi.
Awali,
ilidaiwa kwamba mwenyekiti huyo aliweka rehani kitambulisho hicho na
simu yake ili kupewa muda wa kulipa deni la hoteli hiyo.
Meneja wa hoteli hiyo, Filipo John alisema kiongozi huyo alikuwa akidaiwa Sh309,400 za siku sita alizolala hotelini hapo.
Pia,
John alikiri kupokea kitambulisho hicho na simu ambavyo alisema baada
ya kiongozi huyo kuondoka bila kulipa, alipeleka malalamiko kwa uongozi
wa mtaa na baadaye alipeleka kesi hiyo polisi.
“Nilipeleka
kesi kwa balozi na mwenyekiti wa mtaa, lakini walishauri vitu vyake
vipelekwe polisi. Baada ya kunilipa nilifuta kesi,” alisema meneja huyo.
Kamanda
wa polisi wa Mkoa, Charles Mkumbo alisema wanaendelea kumshikilia Ole
Sabaya kwa ajili ya upelelezi na atafikishwa mahakamani kesho.
Sunday, September 18, 2016
Lowassa Kumwanika Profesa Lipumba
Aliyekuwa
mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, anajiandaa kuweka wazi
ushiriki wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba katika
mchakato wake wa kuhamia Chadema mpaka kuwa mgombea urais.
Akizungumza
kwa simu na mwandishi wa habari hii akiwa Nairobi nchini Kenya jana,
Lowassa ambaye pia alikuwa Waziri Mkuu, wakati wa Serikali ya Awamu ya
Nne ya Rais Jakaya Kikwete, alisema akirudi kutoka safari hiyo,
atafafanua mbele ya vyombo vya habari, tuhuma dhidi yake zilizotolewa na
Profesa Lipumba.
“Kwa
sasa naomba uniache kwanza maana nipo safarini Nairobi, nikija Dar es
Salaam nitazungumzia suala hilo kwa undani kupitia vyombo vya habari,
hivyo subirini nirudi,” alisema Lowassa.
Madai ya Lipumba
Hivi
karibuni Profesa Lipumba alitupa lawama moja kwa moja kwa Lowassa,
kwamba ujio wake ndani ya Ukawa, unaoundwa na Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi
na NLD, ndiyo ulisababisha matatizo katika vyama hivyo kwa kiasi
kikubwa.
Kwa
mujibu wa Profesa Lipumba, kabla ya kujiunga kwa Lowassa Ukawa, vyama
hivyo walikaa kikao ambacho aliwashauri viongozi wenzake wa Ukawa
kutazama mtu anayeweza kuendana na mahitaji yao awe ndani au nje ya
umoja huo.
Alisema
ni kweli aliona wangeweza kupata ushindi kupitia Lowassa, lakini hata
ushindi huo ungepatikana, wangeenda kusimamia mambo gani? Maana suala ni
kusimamia katika eneo fulani.
Alifafanua
kuwa suala lililopo katika siasa ni baada ya kuchaguliwa, uunde
serikali ili usimamie misingi fulani ambayo itakidhi mahitaji ya
wananchi.
“Sisi
tulisema tunahitaji serikali inayowajibika, itakayopambana na rushwa,
itakayotumia rasilimali za nchi vizuri, na itakayohakikisha mali ya
asili ya Tanzania inawasaidia Watanzania wote,” alisema na kuongeza kuwa hayo Lowassa asingeweza.
Baada
ya kikao hicho cha kumjadili Lowassa, Profesa Lipumba alisema walifanya
kingine wakiwa na Mbowe (Freeman, Mwenyekiti wa Chadema); Mbatia
(James, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi) na Lowassa kujadili suala hilo kwa
mara ya pili kuwa ni vyema CUF, wakaribishwe kwanza ambapo walikuwa
hatua za mwisho.
Alisema
baada ya mchakato huo kwisha, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif
Hamad, alianza vikao vingine visivyomshirikisha yeye Lipumba, kwa
kumwalika Mbowe ili wafanye mazungumzo.
Lipumba
alidai kuwa Mbowe alipoitwa na Maalim Seif kwenda Zanzibar, alimfuata
na kumweleza kuwa ameitwa na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar.
“Mbowe
alinipigia simu akaniambia kuwa ameitwa kwenye kikao na kwamba ndio
kulikuwa na hoja ya Lowassa kuingia Ukawa, wakati Chadema walikuwa na
msimamo kuwa kwenye Ukawa asikaribishwe mtu wa nje,”alifafanua.
Alisema
Mbowe aliendelea kumweleza kuwa, baada ya kikao kile ndipo Chadema
waligundua kuwa kuna sintofahamu ndani ya CUF, jambo lililowafanya wao
Chadema watoe hoja ya kuwa na mgombea wao, kwakuwa watakuwa na wabunge
wengi basi hata Waziri Mkuu atatoka huko na CUF itatoa mgombea mwenza.
Lipumba
alisema baada ya hali hiyo kutokea; ya Maalim Seif kufanya vikao
vingine bila kumshirikisha, alikuwa katika wakati mgumu maana hata
mazungumzo yale hakushirikishwa, ilihali yeye ndio Mwenyekiti wa CUF na
yalikuwa yanafanywa na Katibu kimnya kimnya.
Sunday, September 18, 2016
Sheria zote Nchini kuwa kwa Kiswahili
Katibu
Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome amesema kuanzia
sasa sheria zote zitakazotungwa nchini zitakuwa katika lugha ya
Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wengi ambao ndio walengwa wa sheria
hizo, kuzielewa.
Uamuzi
huo unakwenda sambamba na kuzitafsiri sheria zote zinazotumika nchini
ambazo ziko katika lugha ya Kiingereza ili kutimiza lengo hilo la
kuwafanya wananchi wengi wazielewe.
“Kwa
sasa serikali imeamua kuwa sheria zote nchini zitakuwa katika lugha ya
Kiswahili na zile ambazo ziko katika lugha ya Kiingereza zitatafsiriwa
ili kuwawezesha Watanzania wengi ambao ndio walengwa wa sheria hizo
kuzielewa,” alisema.
Pia
alisema serikali itazifanyia marekebisho sheria zote ambazo zimekuwa
zikilalamikiwa na wadau mbalimbali kuwa hazikidhi mahitaji au haja,
haziendani na wakati uliopo sasa ili kutekeleza azma yake ya kuwahudumia
wananchi wake kwa ukamilifu.
Profesa
Mchome ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana baada ya kupokea
mapendekezo yaliyowasilishwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na
Maendeleo Afrika (WILDAF), ambayo yanataka kufutwa kwa sheria mbalimbali
za kimila zinazosimamia masuala ya mirathi ambazo zinalalamikiwa
kuwakandamiza wanawake nchini.
Profesa
Mchome amewashukuru WILDAF kwa kazi waliyoifanya na kuwaahidi kuwa
wataalamu wake wizarani watayafanyia kazi mapendekezo yao ili
kuhakikisha gurudumu la sheria nchini linasonga mbele na kuwasaidia
wananchi wengi.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa WILDAF, Judith Odunga alisema
mapendekezo hayo yanataka kufutwa kwa sheria za kimila ambazo kwa kiasi
kikubwa zimekuwa zikiwakandamiza wanawake, kuwanyima haki ya kumiliki
mali na kufanyiwa vitendo vya kidhalilishaji pale wanapofiwa na waume
zao.
Alisema
katika mapendekezo hayo WILDAF inaiomba serikali itunge sheria moja
ambayo pamoja na zile za kidini itashughulikia masuala ya mirathi na
kuweka usawa wa kisheria katika urithi wa mali kati ya mwanamke na
mwanamume, ikiwa ni pamoja na watoto wa kiume na wa kike kuwa na usawa
katika kurithi mali inapotokea mzazi wa kiume amefariki dunia.
Sunday, September 18, 2016
Manispaa ya Kinondoni Yavunjwa Rasmi....Meya Boniface Kapoteza Nafasi Yake
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli amevunja
Baraza la Madiwani rasmi baada ya serikali kuigawa manispaa hiyo kuwa
mbili. Kagurumjuli alilivunja juzi saa 11:00 baada ya kumalizika kwa
Baraza la Madiwani la kawaida.
Alipokuwa
akitangaza kulivunja baraza hilo, Kagurumjuli alisema amevunja baraza
hilo kwa kuwa serikali imegawanya manispaa hiyo kuwa wilaya mbili, ya
Kinondoni na Ubungo hivyo kwa kuwa wilaya zote tayari zina wakurugenzi,
wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya imempasa kufanya hivyo.
“Baraza la madiwani limevunjwa, kuvunjwa kwa baraza hili ni ukomo wa meya pia,” alisema.
Aliongeza kuwa wiki ijayo kutakuwa na uchaguzi wa meya katika manispaa hizo.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni alikuwepo kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo ni
Boniface Yakob ambaye amebaki nafasi yake ya udiwani.
Kuvunjwa kwa baraza hilo kulikuwa kunatarajiwa baada ya serikali kugawanya manispaa ya Kinondoni kuwa mbili.
Sunday, September 18, 2016
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete avutiwa na wimbo ‘Matatizo’ wa Harmonize
Wimbo ‘Matatizo’ wa msanii wa muziki Harmonize, ni moja kati ya nyimbo ambazo zinapendwa na Rais Mtaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.
Wiki
moja iliyopita Mh.Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwaalika viongozi wa
WCB pamoja na wasanii wake nyumbani kwake na kula nao chakula cha
mchana.
“Unajua
wakati Mh Jakaya Kikwete anatoka madarakani Diamond Platnumz bado
alikuwa hajasaini wasanii wengine chini la WCB Wasafi, hivyo tulikwenda
kuwatambulisha kina Harmonize, Raymond pamoja na Rich Mavoko pia na
kukabidhi kazi zao, lakini uzuri wakati tunakabidhi kazi Mh Jakaya
Kikwete alikuwa amevutiwa na wimbo wa Harmonize wa matatizo, akawa
anasema alikuwa kwenye gari aliisikiliza kazi hiyo na kusema kuwa kijana
ameimba sana,” Sallam alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV.
Sallam alisema hatua ya kukutana na JK wanaimani itawasaidia kuwapa connection katika muziki wao.
KATIKA HABARI ZA KIMATAIFAAAAAAAAAA
Marekani yashambulia majeshi ya serikali Syria
Marekani imekiri mashambulizi ya anga yanayoongozwa na nchi hiyo kuwaua wanajeshi kadhaa wa Syria mnamo wakati hatua ya usitishwaji mapigano ikiendelea nchini humo. Kufuatia mashambulizi hayo Urusi imetaka ipate maelezo ya kina kutoka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Kundi la waangalizi wa haki za binadamu lenye makao yake nchini Uingereza limesema kiasi ya wanajeshi 80 wa Syria wameuawa katika mashambulizi hayo. Taarifa ya jeshi la serikali nchini humo imelaani mashambulizi hayo ambayo yamesababisha kundi la itikadi kali la Dola la Kiisilamu kuingia kirahisi katika maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa na jeshi hilo. Hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Syria SANA. Kwa upande mwingine serikali ya Marekani imeelezea kusikitishwa kwake na mashambulizi hayo ambayo imedai yalilenga kimakosa maeneo yanayodhibitiwa na vikosi vya serikali ya Syria. Wakati huo huo, balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin alitoka nje ya kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichokuwa kimeitishwa kwa ajili ya kujadili mashambulizi hayo ya Marekani, akipinga kauli iliyotolewa na Balozi wa Marekani kwenye Umoja huo, Samantha Power, aliyekosoa kile alichokiita "unafiki wa Urusi" na kukifananisha sawa na mazingaombwe.Polisi wawili wauawa Saudi Arabia
Watu ambao bado hawajatambulika wamewaua kwa kuwapiga risasi maafisa wawili wa polisi katika jimbo la mashariki linalozalisha mafuta nchini Saudi Arabia. Kwa mujibu wa kituo cha matangazo ya televisheni cha Al-Arabiya kinachomilikiwa na serikali ya nchi hiyo, polisi hao walipigwa risasi wakati wakiwa katika doria ya kawaida. Jimbo la mashariki ni eneo la makaazi kwa Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia katika taifa hilo la kifalme linaloongozwa na wahafidhina wa madhehebu ya Sunni. Kumekuwa na matukio kadhaa ya kuvishambulia vikosi vya usalama jimboni humo katika siku za hivi karibuni, yanayodaiwa kufanywa na wanamgambo wa Kishia kutokana na kile wanachosema ni kukandamizwa kwa jamii yao.Ulinzi waimarishwa wakati wa tamasha la Oktoberfest
Mamlaka ya mji wa Munich nchini Ujerumani imechukua hatua ya kuimarisha ulinzi wakati wa tamasha la mwaka huu la unywaji pombe lijulikanalo kama Oktoberfest . Hatua hizo ni pamoja na kamera zilizowekwa katika maeneo mbalimbali kuzunguka eneo la tamasha hilo na pia kuzuia mabegi makubwa ya mgongoni kuwekwa katika mahema kwenye maeneo linakofanyika tamasha hilo. Meya wa mji wa Munich, Dieter Reiter, alikuwa wa kwanza kuanza kunywa fundo la bia hapo jana mchana, ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasimi wa moja ya matamasha makubwa duniani ya unywaji pombe. Kiasi cha maafisa wa polisi 600 wanatarajiwa kuwepo katika tamasha la mwaka huu, ikiwa wameongezwa polisi 100 zaidi kuliko idadi ya mwaka jana, huku mamlaka ya mji huo ikitumia kiasi cha euro milioni 3.6 kwa ajili ya kuongeza walinzi wengine wa usalama 450, katika tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufikia tamati Oktoba 3, mwaka huu.Wanamgambo 38 wa Boko Haram wauawa
Wanajeshi wa Niger na Chad wanasema wamewaua wapiganaji 38 wa kundi la itikadi kali la Boko Haram katika operesheni iliyofanywa na wanajeshi hao kufuatia uvamizi wa kundi hilo katika miji miwili ya mpakani kusini mashariki mwa Niger mapema wiki hii. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hapo jana na kamanda mkuu wa vikosi vya Niger, wanajeshi wawili kutoka katika vikosi vya nchi hizo mbili walipata majeraha kidogo wakati wa operesheni hiyo, ambayo imefanyika baada ya kutokea mapigano katika kijiji cha Toumour kilichoko jirani na Ziwa Chad na pia jirani na mpaka wa Nigeria.Makaazi mengine ya wakimbizi yachomwa moto Ujerumani
Polisi nchini Ujerumani inachunguza tukio la kuchomwa moto makaazi ya wakimbizi kwenye mji wa kusini magharibi wa Erbach, ambapo wakazi watano wa mji huo wamelazimika kupelekwa hospitali baada ya kuvuta hewa iliyochanganyika na moshi. Maafisa wa polisi katika mji huo wamesema makaazi hayo ya wahamiaji yalichomwa moto kwa makusudi, wakati watu 26 walipokuwa ndani yake. Meya wa mji huo wa Erbach amesema hakutarajia mkasa kama huo kutokea, kwani hakujawa na tukio lolote kubwa la maandamano ya kupinga wahamiaji walioko katika mji huo. Kwa mujibu wa Serikali Kuu ya Shirikisho, visa zaidi ya 700 vya mashambulizi dhidi ya makaazi ya wahamiaji vimeripotiwa kufanyika nchini Ujerumani katika kipindi cha mwaka huu.Maelfu waandamana Ujerumani kupinga kusainiwa mkataba wa TTIP
Maelfu ya watu wameandamana katika miji kadhaa nchini Ujerumani kupinga juhudi zinazofanywa na Umoja wa Ulaya za kutaka kusaini mikataba ya ushirikiano wa biashara huru kati ya Umoja huo na mataifa ya Marekani na Canada ijulikanayo kama TTIP na CETA. Waratibu wa maadamano hayo wamesema takribani watu 320,000 walijitokeza kushiriki maandamano yaliyofanyika katika miji ya Berlin, Frankfurt, Cologne, Stuttgart, Hamburg, Leipzig na Munich hapo jana. Maafisa wa polisi wamethibitisha idadi ya watu 70,000 walioshiriki maandamano hayo katika mji wa Berlin iliyotolewa na waandaaji wa maandamano hayo, huku wakitoa makadirio ya watu 40,000 katika mji wa Cologne na 30,000 katika mji wa Hamburg. Wakiwa wamebeba mabango yanayopinga mikataba hiyo, waandamanaji wamezitaka serikali za mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya kutokuingia kwenye makubaliano hayo. Iwapo mkataba wa TTIP utasainiwa, itakuwa ni hatua mojawapo ya kuwepo kwa ukanda mkubwa duniani wa biashara huru ulio na wateja kiasi ya milioni 800.KATIKA MICHEZOOOOOOOOOOOO
VPL: SIMBA YAING’OA AZAM FC KILELENI, MABINGWA YANGA WAMZIBA MDOMO JULIO, PRISONS, MBEYA CITY NGOMA NGUMU SOKOINE!
LIGI KUU VODACOM
Jumamosi Septemba 17
Mwadui FC 0 Yanga 2
Azam FC 0 Simba 1
Mbeya City 0 Tanzania Prisons 0
Mtibwa Sugar 2 Kagera Sugar 0
Majimaji FC 1 Ndanda FC 2
Ruvu Shooting 1 Mbao FC 4
++++++++++++++++++++++
SIMBA imeiwasha Azam FC Bao 1-0 Uwanjani Uhuru Jijini Dar es Salaam na kukwea kilele cha VPL, Ligi Kuu Vodacom, wakati Mabingwa Yanga wakiichapa Mwadui FC 2-0 huko Shinyanga na kumyamazisha ‘Kada’ wa Simba Jamhuri Kiwelu, Al-maarufu kama Julio, ambae ni Kocha wa wa Timu hiyo alietamba Yanga ni wa ‘kawaida tu’.
Jijini Dar es Salaam, Bao la Dakika ya 67 la Shiza Kichuya limewapa Simba ushindi wa 1-0 walipocheza na Simba.
Huko Shinyanga, Bao za Yanga zilifungwa na amissi Tambwe, Dakika ya 5, na Donald Ngoma, Dakika ya 90.
LIGI KUU VODACOM
Jumapili Septemba 18
Stand United v Ruvu JKT
Jumanne Septemba 20
African Lyon v Toto Africans
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
Simba |
5 |
4 |
1 |
0 |
8 |
2 |
6 |
13 |
2 |
Yanga |
4 |
3 |
1 |
0 |
8 |
0 |
8 |
10 |
3 |
Azam FC |
5 |
3 |
1 |
1 |
7 |
3 |
4 |
10 |
9 |
Mtibwa Sugar |
5 |
3 |
0 |
2 |
6 |
6 |
0 |
9 |
4 |
Mbeya City |
5 |
2 |
2 |
1 |
6 |
3 |
3 |
8 |
5 |
Tanzania Prisons |
5 |
2 |
2 |
1 |
3 |
2 |
1 |
8 |
6 |
Ruvu Shooting |
5 |
2 |
1 |
5 |
4 |
7 |
-3 |
7 |
7 |
Stand United |
4 |
1 |
3 |
0 |
3 |
2 |
1 |
6 |
8 |
Kagera Sugar |
5 |
1 |
3 |
1 |
1 |
2 |
-1 |
6 |
9 |
African Lyon |
4 |
1 |
2 |
1 |
4 |
5 |
-1 |
5 |
10 |
Ndanda |
5 |
1 |
2 |
2 |
4 |
6 |
-2 |
5 |
11 |
Mbao FC |
5 |
1 |
1 |
3 |
6 |
9 |
-3 |
4 |
12 |
Mwadui FC |
5 |
1 |
1 |
3 |
3 |
6 |
-3 |
4 |
14 |
Toto Africans |
4 |
1 |
0 |
3 |
1 |
3 |
-2 |
3 |
15 |
JKT Ruvu |
3 |
0 |
2 |
1 |
0 |
1 |
-1 |
2 |
16 |
Majimaji |
5 |
0 |
0 |
5 |
2 |
11 |
-9 |
0 |
RONALDO, BALE KUIKOSA TRIPU YA JIJINI BARCELONA JUMAPILI!
Real Madrid watawakosa Mastaa wao wakubwa Cristiano Ronaldo na Gareth Bale kwenye Tripu yao kwenda huko Estadi Power 8 Jijini Barcelona kuwavaa RCD Espanyol katika Mechi ya La Liga.
Kukosekana kwa Mastaa hao kumethibitishwa na Kocha wa Real Zinedine Zidane.
Bale aliumia Paja na kutolewa nje kwenye Mechi yao ya La Liga ya Jumatano iliyopita walipotoka nyuma na kuifunga Sporting Lisbon 2-1 kwenye Mechi ya Kundi lao la UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Ronaldo kwa sababu ni Mgonjwa.
Akiongea hii Leo, Zidane ameeleza kuwa Wawili hawamo kwenye Kikosi chao kwa ajili ya Mechi na Espanyol.
Uamuzi huo umechukuliwa hasa kwa vile Real wakabiliwa na Mechi 5 katika Wiki 2 zijazo.
Real wanasaka ushindi wao wa 15 mfululizo kwenye Mechi za La Liga ili kuweka Rekodi mpya.
Kukosekana kwa Wawili hao ni nafasi murua kwa James Rodriguez kuanza Mechi yake ya kwanza Msimu huu kwa Real baada ya mara kadhaa kuingia akitokea Benchi.
LA LIGA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Ijumaa Septemba 16
Real Betis 2 Granada 2
Jumamosi Septemba 17
1400 CD Leganes v FC Barcelona
1715 Atletico de Madrid v Sporting Gijon
1930 SD Eibar v Sevilla FC
2145 Las Palmas v Malaga CF
Jumapili Septemba 18
1300 Osasuna v Celta de Vigo
1715 Athletic de Bilbao v Valencia C.F
1930 Villarreal CF v Real Sociedad
RCD Espanyol v Real Madrid CF
Jumatatu Septemba 19
2145 Deportivo Alaves v Deportivo La Coruna
Jumanne Septemba 20
2100 Malaga CF v SD Eibar
2300 Sevilla v Real Betis
Jumatano Septemba 21
2100 Celta de Vigo v Sporting Gijon
2100 Real Madrid CF v Villarreal CF
2300 FC Barcelona v Atletico de Madrid
2300 Real Sociedad v Las Palmas
2300 Granada CF v Athletic de Bilbao
Alhamisi Septemba 22
2100 Deportivo La Coruna v CD Leganes
2100 Osasuna v RCD Espanyol
2300 Valencia C.F v Deportivo Alaves
Ijumaa Septemba 23
2145 Real Betis v Malaga CF
Jumamosi Septemba 24
1400 SD Eibar v Real Sociedad
1715 Sporting Gijon v FC Barcelona
1930 Athletic de Bilbao v Sevilla FC
2145 Las Palmas v Real Madrid CF
RIPOTI SPESHO
TOKA TFF: OFA YA WAZIRI NAPE KUIONA SERENGETI LEO, WACHEZAJI WAJAZWA MINOTI!
KUONA SERENGETI NA CONGO –BRAZZAVILLE BURE, VIJANA WAJAZWA NOTI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape
Nnauye ametoa ofa kwa wananchi kujumuika pamoja leo Septemba 18, 2016
katika mchezo wa mpira wa miguu utakaozikutanisha timu za vijana taifa
za Tanzania na Congo-Brazzaville kwenye Uwanja wa Taifa, ulioko
Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.
Timu hizo zitakutana kweye mchezo wa kwanza kuwania nafasi ya
kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa
chini ya miaka. Zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo
Brazzaville na timu itafayopata ushindi wa jumla katika michezo miwili
itafuzu kwa fainali hizo.
Nape alitoa ofa hiyo tangu jana Septemba 17, 2016 na leo asubuhi
Septemba alipata kifungua kinywa na wachezaji wa Serengeti Boys ambako
alitoa Sh 200,000 kwa kila mchezaji zilizotokana na kundi linalosapoti
Serengeti Boys ambao walichangia Sh 2,600,000 wakati nyingine zilitoka
kwa wadau wengine.
Nape ameahidi pia kununua bao moja kwa Sh 500,000 na atalipa fedha
hizo kadiri ya idadi ya mabao hata kama yatafika 10 hivyo gharama yake
itakuwa Sh 5,000,000. “Kuna wabunge na viongozi wengine wameahidi kutoa
fedha zaidi, kwa hiyo Serengeti Boys kazi kwenu kutafuta ushindi leo
mbele ya Watanzania watakaoingia uwanjani bure.”
Kuingia bure kesho ni ofa iliyotolewa na Nape ambako Rais Jamal
Malinzi amemshukuru Nnauye ambaye ni Mbunge wa Mtama kwa ofa hiyo ambayo
imelenga kutoa hamasa kwa Watanzania kwenda kushangilia timu yao.
Katika mchezo huo ambao Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, amesema
kwamba amemaliza kila kitu na kwamba anasubiri Watanzania kuja uwanjani
leo kuishangilia timu yao, utachezwa na waamuzi kutoka Shelisheli ambako
mpiga kipenga atakuwa Nelson Fred akisaidiwa na Hensley Petrousse na
Stive Marie wakati mwamuzi wa akiba akiwa Allister Barra. Kamishna wa
mchezo atakuwa Gladmore Muzambi kutoka Zimbawe.
IMETOLEWA NA TFF
PEP 'AWAPIGA MISUMARI WAPINZANI ENGLAND': BOURNEMOUTH NDIO TIMU BORA, DE BRUYNE NDIE MCHEZAJI BORA BAADA MESSI!
Meneja
wa Manchester City Pep Guardiola amesema Bournemouth ndio Timu Bora
waliyokutana nayo kwenye EPL, Ligi Kuu England Msimu huu.
Jana, City ikiwa kwao Etihad, iliitwanga Bournemouth 4-0 kwenye
Mechi ya EPL ambayo imeendeleza wimbi lao la ushindi na kuwakita
kileleni mwa Ligi hiyo.
Licha ya Wikiendi iliyopita kutolewa jasho na Mahasimu wao Man
United wakipata ushindi wa mbinde wa 2-1 huku Man United 'wakiminywa'
Penati 2 za wazi, Guardiola amediriki kutamba Bournemouth ndio Timu
Bora.
Guardiola ameeleza: "Kitu muhimu tumeshinda Gemu hii Siku chache
baada Mechi ngumu ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI. Bournemouth ndio Timu
Bora hadi sasa na walitupa taabu sana walipomiliki Mpira. Timu nyingine
zinacheza Mipira mirefu!"
Wakati huo huo, Bosi huyo wa Man City anamtathmini Mchezaji wake
kutoka Belgium Kevin de Bruyne kuwa ni Mchezaji Bora kupita wote
ukimwondoa Lionel Messi.
De Bruyne ndie aliefunga Bao la Kwanza wakati City inaichapa Bournemouth 4-0 hapo Jana.
Hadi sasa De Bruyne ameifungia City Bao 18 na kutoa Msaada wa Magoli mara 16.
Guardiola amedai: "Messi yupo kwenye Ligi ya pekee.Hamna Mtu anaefikia huko. Lakini Kevin anaweza kuwa huko!"
MAN CITY - Mechi zao zifuatazo:
Jumatano Septemba 21
EFL CUP - Raundi ya 3
2145 Swansea v Man City
Jumamosi Septemba 24
EPM
1700 Swansea v Man City
Jumatano Septemba 28
UEFA CHAMPIONZ LIGI - Kundi C
2145 Celtic v Man City
LIGI KUU ENGLAND: EVERTON YAIPIGA BORO 3, IPO NAFASI YA 2!
LIGI KUU ENGLAND
Matokeo:
Jumamosi Septemba 17
Hull City 1 Arsenal 4
Leicester City 3 Burnley 0
Man City 4 Bournemouth 0
West Bromwich Albion 4 West Ham 2
Everton 3 Middlesbrough 1
++++++++++++++++++++++++++
Everton walitoka nyuma kwa Bao la utata na kuitandika Middlesbrough 3-1 katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, iliyochezwa huko Goodison Park Jijini Liverpool.
Middlesbrough walitangulia kwa Bao la Dakika ya 21 kwa madai ya Negredo kupiga kichwa wakati alimgonga Kipa Stekelenburg mkononi na mpira kutinga wavuni.
Everton walisawazisha, nao kwa Bao la utata Dakika ya 24 kwa Bao la Gareth Barry lakini Kipa wa Boro Valdes alistahili kulindwa kutokana na Faulo ya Williams.
Bao nyingine za Everton zilipachikwa Seamus Coleman na Romelu Lukaku na Everton kuongoza 3-1 hadi Mapumziko na Bao hizo kudumu hadi mwishoni.
Ushindi huu umeitwika Everton Nafasi ya Pili kwenye EPL baada ya Mechi 4 ukiwa ni mwanzo mzuri katika Miaka 38 ya Klabu hiyo.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Everton: Stekelenburg; Coleman, Williams, Jagielka, Baines; Gueye, Barry; Mirallas, Barkley, Bolasie; Lukaku
Akiba: Joel, Deulofeu, Lennon, Cleverley, Valencia, Funes Mori, Holgate.
Middlesbrough: Valdes; Barragan, Ayala, Gibson, Friend; De Roon, Forshaw; Nsue, Ramirez, Downing; Negredo.
Akiba: Guzan, Espinosa, Clayton, Fischer, Chambers, Nugent, Traore
REFA: LEE MASON
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumapili Septemba 18
1400 Watford v Man United
1615 Crystal Palace v Stoke
1615 Southampton v Swansea
1830 Tottenham v Sunderland
LIGI KUU ENGLAND: CITY, ARSENAL, WBA WAJIPIGIA 4, MABINGWA LEICESTER WAPIGA 3!
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 17
Hull City 1 Arsenal 4
Leicester City 3 Burnley 0
Man City 4 Bournemouth 0
West Bromwich Albion 4 West Ham 2
1930 Everton v Middlesbrough
++++++++++++++++++++++++++
EPL, Ligi Kuu England, imeendelea Leo kwa ushindi mnono kwa Mabingwa Watetezi Leicester City, Man City, Arsenal na West Bromwich Albion.
Wakiwa kwao King Power Stadium waliitandika Burnley 3-0 kwa Bao za Islam Slimani, Bao 2, na Mee kujifunga mwenyewe.
Huko Etihad, Man City iliiwasha Bournemouth 4-0 kwa Magoli ya Kevin De Bruyne, Kelechi Iheanacho, Raheem Sterling na Gundogan katika Mechi ambayo Dakika ya 86 City walibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Nolito kumtwanga Kichwa Adam Smith.
Nao Arsenal, wakicheza Ugenini, waliichapa Mtu 10 Hull City Bao 4-1 kwa Bao za Alexis Sanchez, Bao 2, Theo Walcott na Xhaka wakati Bao la Hull lilifungwa kwa Penati ya Snodgrass.
Hull walibaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 40 baada ya Livermore kupewa Kadi Nyekundu.
WBA, wakiwa kwao The Hawthorns, waliitwanga West Ham 4-2 wakiongoza 3-0 hadi Haftaimu kwa Magoli ya Chadli, Bao 2, Rondon na McClean wakati Bao za West Ham zikipachikwa na Antonio na Lanzini.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumapili Septemba 18
1400 Watford v Man United
1615 Crystal Palace v Stoke
1615 Southampton v Swansea
1830 Tottenham v Sunderland
Reviewed by RICH VOICE
on
Septemba 18, 2016
Rating:
Hakuna maoni