Tuesday, September 27, 2016

'Panya Road' Waibuka Upya Na Kutesa Wananchi Moshi Baa Jijini Dar Es Salaam

SeeBait

Na Dotto Mwaibale

KUNDI la uhalifu la watoto wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 25 maarufu kama panya road linatishia usalama wa wananchi na mali zao maeneo ya Moshi Baa na vitongoji vingine katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kufuatia kukithiri kwa vitendo hivyo katika kipindi kisichopungua wiki mbili tayari watoto watatu walikuwa wakidaiwa kuhusika na kundi hilo wameuawa na wananchi wenye hasira kali.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Dar es Salaa jana   mkazi wa eneo la Moshi Baa Relini aliyejitambulisha kwa jina la Mwarami Abubakar alisema hali sio shwari katika eneo kufuatia matukio ya kila siku ya kuvamiwa wananchi kujeruhiwa na kuporwa mali zao na kundi hilo.

"Tayari vijana wawili wiki iliyopita wamechomwa moto na wananchi wenye hasira huku mwingine akipigwa juzi hadi kutolewa utumbo na kufariki papo hapo," alisema Abubakar.

Mkazi mwingine wa eneo la Kwa Mkolemba Khamisi Fadhil alisema kundi hilo limekuwa likifanya vitendo hivyo mchana kweupe na wanatembea kuanzia vijana nane hadi 10 wakiwa na silaha za jadi kama nondo, visu na mapanga na mtu yeyote wanayekutana naye ni lazima wampige na kumpora.

Wenye maduka wanalazimika kufunga kuanzia saa moja jioni kuhofia kundi hilo ambalo huvunja milango ya nyumba na kufanya uporaji" alisema Fadhil.

Fadhil alisema maeneo ambayo vijana hao wameshamiri ni Moshi Baa Relini, Kwa Mkolemba, Diwani na Bomba mbili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Kamishna Msaidizi (ACP), Salum Hamdan alisema polisi imejipanga vilivyokukabiliana na vitendo hivyo katika mkoa wake.

"Kwanza napenda kukuambia kwamba hakuna kundi linalojiita panya road wote tunawahesabu ni wahalifu kama walivyo wahalifu wengine na hivi ninavyongea na wewe tupo katika siku ya sita ya operesheni ya kukakamta watu wanaojihusisha na uhalifu wa ujambazi wakiwemo wanaouza pombe haramu ya gongo," alisema Kamanda Hamdan.

Aliongeza kuwa katika mkoa wake hivi karibuni utakuwa shwari baada ya askari wake kusambaratisha watu hao wanaofanya vitendo hivyo.

Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062

 

 

Tuesday, September 27, 2016

Watoto 2,570 waripotiwa kulawitiwa kwa kipindi cha miezi saba

SeeBait
Vitendo vya ukatilitili wa kijinsia kwa watoto vimeendelea kuongezeka kwa kasi nchini katika kipindi cha mwezi Januari hadi Julai mwaka huu ambapo zaidi ya watoto 2,570 wa kike na kiume wamelawitiwa na kubakwa.

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka 21 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) yaliyofanyika jana katika Makao makuu ya watoto yaliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Helen Kijo-Bisimba alisema idadi hiyo ni kubwa ukilinganisha na ya mwaka jana.

Hata hivyo, Mama Bisimba alisema kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi, takwimu hizo zinaweza kuwa ndogo kutokana na kesi nyingi za ubakaji na ulawiti kwa watoto kutoripotiwa polisi kwa sababu ya mila na desturi za maeneo mengi nchini.

“Ripoti ya Jeshi la Polisi kupitia dawati la jinsia kati ya Januari na Machi 2016 inaonyesha matukio ya watoto kubakwa na kulawitiwa yakiendelea kuongezeka kutoka 180 hadi 1765 hayo ni matukio yaliyotolewa taarifa katika vituo mbalimbali vya polisi nchi nzima ukilinganisha na matukio 1585 mwaka 2015. Hata hivyo waliohusika na matukio hayo wameonekana wakirandaranda bila kuchukuliwa hatua za kisheria, ” alisema.

Alisema ripoti hiyo inaonyesha kuwa kesi 1,203 zipo katika hatua ya upelelezi, 822 zipo mahakamani na watuhumiwa 234 wamekwisha hukumiwa.

“Pia utafiti uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto kwa kushirikiana na Tanzania kitengo cha ustawi wa jamii unaonyesha kati ya watoto 10 wa kike 4 wamebakwa, na kati ya watoto 10 wa kiume 3 wamelawitiwa zaidi ya mara tatu. Utafiti huo unaonyesha kwa ujumla kuwa watoto wa kike na wa kiume 6 walifanyiwa ukatili huo na watu ndani ya familia,” alisema.

Bisimba alisema asilimia 49 ya ukatili hufanyika nyumbani, 23 hufanyika njiani wakati wa kwenda shule au kurudi, na asilimia 15 hufanyika shuleni. Pia ripoti hiyo ya UNICEF inaonyeaha kuwepo kwa matukio ya watoto kulawitiana na kubakana wenyewe kwa wenyewe kutokana na kuvizoea vitendo hivyo.

LHRC imeitaka serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria kuifanyia marekebisho sheria ya mtoto na kutilia mkazo malezi bora kwa watoto ikiwemo kuweka kipengele kitakachotoa adhabu kali kwa familia itakayoshindwa kutoa malezi bora kwa mtoto.

LHRC inayoshughulika na utetezi wa sheria na haki za binadamu ilianzishwa Septemba 26, 1995.

 

 

 

Tuesday, September 27, 2016

Waziri Mkuu Majaliwa atoa wiki moja kwa Afisa Elimu kutafuta walimu wa kidato cha tano na sita

SeeBait
WAZIRI MKUUkuu  Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Yussuph Kipengele kupeleka walimu wa kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za Mkongo na Utete wilayani Rufiji. 
 
Ametoa agizo hilo  Jumatatu, Septemba 26, 2016  wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani Rufiji.  baada ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed Mchengelwa kumwambia kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kidato cha tano na sita licha ya kuwa na shule. 
 
"Hatuwezi kuwa na shule ambazo hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha ni Mkuu wa shule na mwalimu mmoja tu, wakati kule Kibaha kuna walimu walmerundikana ,sasa fanya realocation tarehe 4,Oktoba uniletee taarifa walimu wamefika Rufiji.",alisema Waziri Mkuu. 
 
Akizungumzia suala la upungufu wa watumishi wa umma kwenye sekta mbalimbali, Waziri Mkuu alisema baada ya kazi ya uhakiki watumishi hewa itakapokamilika, serikali itaangalia kwenye maeneo yenye upungufu na hivyo kutangaza ajira. 
 
 "Hivi sasa serikali inakamilisha masuala ya uhakiki wa watumishi, tukimakamilisha na kujua idadi ya watumishi na maeneo yenye upungufu tutaanza tena kuajiri, tulisitisha kupisha kwanza kazi hii,alisema Waziri Majaliwa. 
 
Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji Waziri, Mkuu alisema watendaji wa halmashauri na vijiji wanapaswa kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima na kutaka mifugo isiongezwe kwenye maeneo ambayo hayajaruhusiwa. 
 
 Alisema wenyeviti wa vijiji wanapaswa kusimamia utekelezaji wake katika mpango wa matumizi bora ya ardhi na kwamba atakayeruhusu idadi kubwa ya mifugo kuingia kijijini zaidi ya ile iliyokubalika atawajibishwa ikiwemo kufukuzwa kazi na hatua nyingine za kisheria. 
 
 "Hatuwezi kuendelea kuwa na watumishi wasio na nidhamu, wale wote watakaoingia mifugo zaidi ya uwezo wa kijiji wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua, lakini pia wafugaji ni marufuko kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima"alisema Waziri Mkuu. 
 
 Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kwenda makao makuu ya wilaya ya Rufiji, Utete, Waziri Mkuu aliahidi kuchukua ombi hilo na kusema bajeti ijayo litatengewa fedha kuwa ajili ya kufanya maandalizi ya upembuzi kuona gharama yake kabla ya kutangaza zabuni ya ujenzi. 
 
 Kuhusu utengenezaji wa madawati, Waziri Mkuu alisema ifikapo Oktoba 30, mwaka huu kila wilaya nchini inapaswa iwe imekamilisha utengenezaji wa madawati hayo kwenye shule nchini. 
 
 Aidha, alisema ipo miradi mingi inayoendeshwa kwa maslahi binafsi ukiwemo mradi wa Bonde la Rufiji(RUBADA), ambao wamebaini kuna ubabaishaji mkubwa, hivyo wamepeleka timu ya wataalamu kuhakiki ili wale wabadhirifu wachukuliwe hatua. 
IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATATU, SEPTEMBA 26, 2016

 

 

 

Tuesday, September 27, 2016

Matukio Zaidi Ya Picha Wakati Rais Dkt. Magufuli Alipotembelea Bandari Ya Dar Es Salaam Jana

SeeBait
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam   Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi  Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wafanyakazi waliokuwa wakimshangilia wakati akitembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitembelea bandari ya Dar es salaam Septemba 26, 2016 akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi i Dkt Leonard Chamriho na uongozi wa Bandari
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa  Meneja wa Kitengo cha Kontena wa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa  Meneja wa Kitengo cha Kontena wa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa mapendekezo  kwa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa  Meneja wa Kitengo cha Kontena wa  Kampuni ya Ushushaji Shehena ya makasha  Bandarini ya Tanzania International Container Terminal (TICTS)  Bw. Donald Talawa  alipotembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mary Mhayaya kuhusu  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu zoezi la  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu zoezi la  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
tpa18
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo  kuangalia sehemu ya kupimia kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongozwa na Mhandisi Mary Mhayaya kuhusu akikagua mtambo wa  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mary Mhayaya kuhusu  chumba cha mitambo ya  uthibiti wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini  kutoka kwenye meli (Oil Flow Meter) katika bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo ya chumba cha ukaguzi wa mizigo (scanner) inayoingia nchini  katika bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo ya chumba cha ukaguzi wa mizigo (scanner) inayoingia nchini  katika bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Wafanyakazi wa bandari ya Dar es salaam wakimlaki kwa furaha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipofika kuongea nao baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Bandarini Bw.  Mashaka Karume akieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipotembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Wafanyakazi wa bandari ya Dar es salaam wakimsikiliza   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipofika kuongea nao baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuongea na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga  wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia mkono kuwaaga  na wafanyakazi wa bandari baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam  Septemba 26, 2016

 

 

Tuesday, September 27, 2016

Waziri Mhagama atoa siku saba kwa wadaiwa wa NSSF

SeeBait
Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ametoa siku saba kwa taasisi za serikali, wizara, kampuni na watu binafsi kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Waziri Mhagama pia ameziagiza bodi za wadhamini za mifuko mingine ya hifadhi ya jamii, kuhakikisha zinawashinikiza wadeni wao kulipa madeni yote wanayodaiwa ili kuiwezesha mifuko hiyo kujiendesha kwa ufanisi zaidi.

Ametoa tamko hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Amemtaka Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Erick Shitindi kuhakikisha uongozi wa mifuko unampatia ripoti ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika wote walioshindwa kulipa madeni yao kwa mifuko yao.

“Ninafahamu fika kuna mikataba ambayo ilisainiwa na pande zote mbili kabla ya kutolewa kwa hiyo mikopo na makubaliano mengine hivyo naomba basi mikataba hiyo itumike kufanikisha agizo hili,’’ alisema.

Pia alimuagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF, Profesa Samwel Wangwe kuhakikisha anampatia ripoti muafaka ya utekelezaji wa agizo hilo.

“Kwa niaba ya serikali, ninataka kuona kwamba wadaiwa wote wa mifuko hii bila kujali nafasi zao kiuchumi au kisiasa wanalipa madeni wanayodaiwa…hii lazima ijumuishe kampuni, wawekezaji na taasisi za serikali,’’ alisisitiza.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema licha ya mfuko wake kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo majengo, bado wateja wake wengi hawajalipa madeni wanayodaiwa na mfuko huo ikiwemo watu binafsi, taasisi za serikali na binafsi wakiwemo pia wale walionunua nyumba za shirika hilo.

Alisema shirika hilo, bado linadai Sh bilioni 20 kutoka kwa wapangaji wake, deni linalohusisha pia dola za Marekani milioni 1.2.

Alifafanua kuwa kiasi kingine cha Sh bilioni 86, kinadaiwa kama adhabu kutoka kwa waajiri walioshindwa kukamilisha makato ya wafanyakazi wao.

Madeni mengine ni pamoja na deni la Sh milioni 42 na dola za Marekani milioni 35.9 zilizotolewa kama mikopo kwa sekta binafsi mbalimbali huku mkopo mwingine wa Sh bilioni 38 ulitolewa kupitia Saccs na bado hazijarejeshwa.

“Hata hivyo, tumeanza kuchukua hatua mahsusi kulingana na matakwa ya sheria kuhakikisha kwamba madeni yote yanalipwa,’’ alibainisha Profesa Kahyarara.
Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Mhe. Jenister Mhagama akiwa ameambatana na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe. (kushoto) akizungumza mbele ya Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Mhe. Jenister Mhagama wakati waziri huyo alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia).
Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia) akizungumza mbele ya Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu Mhe.  Jenister Mhagama wakati waziri huyo alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe (kushoto).

 

 

 

Tuesday, September 27, 2016

Picha za Rais Magufuli Akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wa Ofisi Ya Tamisemi Dkt. Zainabu Chaula.

SeeBait
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Zainabu Chaula kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Zainabu Chaula mara baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

 

 

 

Tuesday, September 27, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Septemba 27

SeeBait


 

Tuesday, September 27, 2016

Prof. Lipumba Augomea mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi CUF

SeeBait

Mgogoro  ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) bado unafukuta ambapo jana Prof. Ibrahim Lipumba, aligomea mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho ulioitishwa leo visiwani Zanzibar

Alisema, taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari kuhusu kufanyika kwa mkutano huo hazitambui kwa kuwa, mamlaka zinazohusika kuitisha kikao hicho hazijakidhi matakwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam kupitia taarifa iliyoandaliwa na Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara aliyesimamishwa na chama hicho alisema, matakwa ya katiba hayakuzingatiwa.

“Wajibu wa Kamati ya Utendaji ya Taifa utakuwa kuandaa.. agenda za Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na kutayarisha na kuhifadhi mihtusari ya vikao vyote vya Mkutano Mkuu wa Taifa, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na vya kamati ya utendaji ya taifa yenyewe na kuwasilisha taarifa ya yatokanayo kutokana na utekelezaji wa maamuzi ya kikao kilichohusika kilichopita,” Prof. Lipumba amenukuu katiba ya chama hicho ibara ya 85(5).

Prof. Lipumba alisema, Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa chama hicho yupo nje ya nchi na kwamba, kutokana na Katiba ya CUF,Naibu Katibu Mkuu atakayemfuata Katibu Mkuu kwa madaraka ni yule aliyetoka upande tofauti wa Jamhuri ya Muungano na upande anaotoka Katibu Mkuu
Kwa upande wake Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara aliyesimamishwa alisema;

"Mimi sijaitisha wala sina taarifa ya kikao cha kamati  ya utendaji kilichofanyika Zanzibar, kwa taarifa nilizonazo hakuna wajumbe wa kamati ya utendaji kutoka Bara waliokua Zanzibar wakati wa kikao hicho. Nachukua nafasi kuwajulisha wajumbe wote wa baraza kuu kuwa hakuna kikao chochote cha baraza kuu kilichoandaliwa na kamati ya utendaji ya Taifa ambayo kikatiba mimi ndiye mwenyekiti wake wakati katibu mkuu hayupo.

“Mimi ndiye mwenye mamlaka ya Katibu Mkuu kwa sababu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara kikatiba ndiye msimamizi namba moja wa Katibu Mkuu” .

Alisema, Katiba ya CUF ya mwaka 1992 Toleo la 2014 kifungu cha 95 (3) kinaeleza “Naibu Katibu Mkuu atakayemfuata Katibu Mkuu kwa madaraka ni yule aliyetoka upande tofauti wa Jamhuri ya Muungano na upande anaotoka Katibu Mkuu,” na kwamba, Katibu Mkuu anatoka Zanzibar na yeye anatoka Bara.

Hata hivyo Prof. alisisitiza kuwa, Sakaya hana taarifa ya kikao hicho cha kamati tendaji kilichofanyika Zanzibar.

Pamoja na kuwepo kwa sintofahamu kutokana na uamuzi wa Jaji Mutungi kumtambua Prof. Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho, (Lipumba) amepongeza kurejeshwa kwake.

Prof. Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho aliyesimamishwa na CUF mwezi uliopita, alirejea kwenye nafasi hiyo kwa kauli ya Jaji Mutungu, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. 
Prof. Lipumba alieleza kushangazwa na hatua ya Jaji Mutungi kukosolewa na baadhi ya wanasheria na majaji mashuhuri kuwa, hakuna sheria inayompa furasa jaji huyo kuchukua hatua aliyoichukua.
 
 

Tuesday, September 27, 2016

Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam Degree-2016/2017

SeeBait

The following applicants have been selected to join various undergraduate degree programmes for the 2016/2017 academic year. 
The selected applicants should report at the Mwl. J.K. Nyerere Mlimani Campus on Saturday 8th October 2016 for the orientation week which will start on Monday 10th October 2016. 
Applicants selected for admission into Dar es Salaam University College of Education (DUCE) and Mkwawa University College of Education (MUCE) should report directly to the college's campuses in Chang'ombe and Iringa respectively on the same dates. 
Joining instructions and admission letters should be collected at the University campuses where one is admitted. Joining instructions and other important information can also be downloaded from the University website.

 
 

Tuesday, September 27, 2016

Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Chuo Kikuu Tumaini Makumira University 2016/2017

SeeBait

List Of Students Admitted By Tcu To Join Tuma For Academic Year 2016/2017 (1st Selection)
Kupata Majina  << BOFYA  HAPA>> 
 
 

Tuesday, September 27, 2016

Masauni Azindua Wiki Ya Nenda Kwa Usalama Barabarani, Kitaifa Mjini Geita....Aagiza Matuta barabara kuu Yaondolewe

SeeBait

Serikali imeagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kuondoa matuta kwenye barabara kuu, ambayo yametajwa kuwa chanzo cha ajali.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, ametoa agizo hilo jana wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Usalama Barabarani katika Viwanja vya Kalangalala mkoani Geita.

Alisema matuta yaliyoko kwenye barabara kuu, yamekuwa moja ya vyanzo vya ajali nyingi nchini na kusisitiza kuwa hali ya ajali iliyopo ni vyema suala la usalama barabarani kuwa ajenda ya kitaifa.

Pia alivitaka vvyombo vya usalama, kuwachukulia hatua kali na stahiki wale wote wanavunja sheria za Usalama Barabarani bila kumuogopa au kumuonea mtu yeyote.

Alisema ajali za barabarani zimekuwa ni tatizo kubwa na kuwa takwimu za miaka mitatu kuanzia Januari 2013 hadi Desemba 2015, zinaonesha kuwa ajali zilizotolewa taarifa ni 46,536 ambazo zimeua watu 11,230.

Masauni alisema kuwa kundi linaloongoza kwa kuathirika na ajali hizo ni abiria ambapo watu 3,444 wamekufa, wakifuatiwa na watembea kwa miguu 3,328.

Alisema wapanda baiskeli wanashika nafasi ya tatu kwa watu 2,493 kupoteza maisha, huku madereva waliokufa ni 813 na wasukuma mikokoteni zaidi ya 400 wamepoteza maisha.

“Takwimu za miezi sita tangu Januari mpaka Agosti mwaka huu, ajali 6,971 zimetokea na kusababisha vifo 2,217 na kati ya hivyo 1,809 ni vile vilivyotokana na pikipiki. Hali ya ajali sio nzuri na ni vyema suala la usalama barabarani likawa ajenda ya kitaifa,” alisema.

Alisisitiza kutolewa elimu ya watumiaji wote kuhusu matumizi sahihi ya barabara, wamiliki na madereva kuacha kuendesha vyombo chakavu na kufanyika kwa ukaguzi wa mara kwa mara.

“Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pia linatakiwa kuendelea kufanya ukaguzi wa matairi, bodi na vipuri vya mabasi,” alisema.

Aidha, Masauni aliwataka watumiaji wote wa barabara, kufuata sheria na kanuni za barabarani, kuacha kushabikia mwendo kasi, kuvuka kwenye vivuko vya watembea kwa miguu na waendesha baiskeli na mikokoteni kuacha kuendesha barabarani na watoto kuvuka barabara wakiwa chini ya uangalizi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Edwin Ngonyani, alisema kutokana na kukithiri kwa ajali, Baraza lilikuja na mikakati ya miezi sita ya kupunguza ajali hususan zinazotokana na makosa ya kibinadamu.

Alisema makosa ya kibinadamu yamekuwa yakichangia ajali kwa asilimia 80 na kufuatiwa na mwendokasi ambao unachangia kwa asilimia 12, mazingira ya barabara yanachangia kwa asilimia 6 na asilimia 2 zinatokana na sababu nyingine.

“Tumekuja na mikakati ambayo inatekelezwa kwa miezi sita, lengo kuu ni kuondoa makosa ya kibinadamu yanayochangia ajali, na Februari mwakani tutatathmini mafanikio ya mikakati hiyo,” alisema.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani katika Jeshi la Polisi, Mohammed Mpinga, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, alisema katika Wiki ya maadhimisho hayo watoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara, na kutoa elimu kwa waendesha pikipiki 300 na walimu 100, na pia watakagua vyombo vya moto na kupima afya za madereva kwa kutumia zahanati mwendo.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayofanyika Kitaifa katika Viwabya vya CCM Kalangalala mjini Geita. Maadhimisho hayo yalizinduliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia).
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka Makao Makuu, Koplo Faustina Ndunguru wakati alipokuwa anatoa maelezo jinsi magari mbalimbali yanavyovunja sheria za barabarani. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa zawadi ya Kombe la Ushindi wa kwanza Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam, Veronica Innocent, ambaye alishinda nafasi ya kwanza katika uchorani wa picha zinazoonyesha usalama barabarani ambayo zilipambanishwa katika shule za Mkoa wa Dar es Salaam na Geita.
Washiriki wa maonesho (waendesha bodaboda) wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita jana. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki ajali tunataka kuishi salama”. 
 
 
habari za kimataifaaa
 


Habari | 27.09.2016 | 17:11

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema ana mashaka iwapo pendekezo la kuwekwa eneo lisiloruhusiwa kuruka ndege nchini Syria linaweza kutekelezwa kwa kuzingatia hali ya sasa nchini humo. Merkel ameyasema hayo mara baada ya kukutana na waziri mkuu wa Malaysia Nijab Razak. Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank- Walter Steinmeier alitoa wito wa kutekelezwa kwa hatua hiyo kwa ndege za kijeshi nchini Syria angalau kwa siku saba kufuatia mashambulizi yalioulenga msafara wa malori ya misaada ya kibinadamu karibu na Aleppo. Merkel amesema ni juu ya utawala wa rais Bashar al-Assad na Urusi kuchukuwa hatua za kuboresha fursa za usitishaji mapigano na msaada wa kibinadamu. Wakati huo vikosi vya jeshi la Syria vimefanikiwa kudhibiti wilaya ya kati iliyokuwa mikononi mwa waasi mjini Aleppo hii leo ambako jeshi linapambana kuchukua tena ngome za upinzani. Mapambano hayo ni mwendelezo wa operesheni ya jeshi la Syria inayojumuisha mashambulizi ya angani na yale ya ardhini.

 

Reviewed by RICH VOICE on Septemba 27, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...