Mkuu wa Wilaya Aingilia Kati Ugomvi wa FFU na Wananchi wa Ukonga Dar




Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewapiga marufuku askari wa kikosi cha FFU na kusema hataki kuwaona wakisumbua wananchi katika eneo la Ukonga Dar es Salaam na kutaka waliohusika wachukuliwe hatua kwa kitendo walichofanya kuwapiga wananchi.

Sophia Mjema amesema hayo alipowatembelea wananchi hao ambao wamelalamika kufanyiwa fujo na kupigwa na askari hao kwa siku mbili kutokana na askari mmoja kuuwawa na watu wasiojulikana.

 Mkuu wa Wilaya anasema kuwa askari hao walipaswa kufanya uchunguzi kujua ni watu gani walihusika kufanya mauaji ya askari huyo na si kwenda kufanya fujo na kuwapiga wananchi pasipokuwa na sababu.

"Kama kuna askari alipatikana ameshafariki utaratibu ulikuwa uchunguzi ufanyike ili waweze kujiridhisha baada ya hapo wale ambao wangetambulika ndiyo wangechukuliwa hatua lakini kwa hili halikubaliki, kwa hiyo nasema hivi askari wote waliohusika kufanya fujo na vurugu wachukuliwe hatua za kinidhamu na huku barabarani sitaki kuona FFU yoyote anasumbua wananchi" alisema Mjema

Aidha Mkuu wa Wilaya huyo ametaka wananchi ambao wameumizwa na askari hao kwa vipigo kwa siku mbili mfululizo waweze kujiorodhesha kwa majina ili wapatiwe matibabu na kusema wale ambao wamepoteza mali zao utaratibu utafanyika kuona nini kifanyike
Mkuu wa Wilaya Aingilia Kati Ugomvi wa FFU na Wananchi wa Ukonga Dar Mkuu wa Wilaya Aingilia Kati Ugomvi wa FFU na Wananchi wa Ukonga Dar Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 24, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...