Uchaguzi Kenya: Mahakama yashindwa kusikiliza kesi

HABARI ZA HIVI PUNDE

Mahakama ya Juu Kenya yashindwa kusikiliza kesi ya kuahirishwa kwa uchaguzi kutokana na ukosefu wa majaji wa kutosha mahakamani.
Jaji Mkuu David Maraga amesema baadhi ya majaji wamo nje ya nchi na wengine hawangeweza kufika mahakamani kwa sababu mbalimbali.
Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa na wapiga kura watatu wakisema Tume ya Uchaguzi haiko tayari kuandaa uchaguzi huru na wa haki kesho.
Jaji Mkuu amekuwa mahakamani na Jaji Isaac Lenaola pekee.
Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu hakuweza kufika kortini baada ya kupigwa risasi kwa dereva wake jana jioni.
Jaji Ibrahim, ambaye amekuwa akiugua, yuko nje ya nchi.
Majaji Smokin Wanjala na jacktone Ojwang hawakuweza kufika kortini pia.
Jaji Njoki Ndung'u alikuwa amesafiri nje ya jiji la Nairobi na hakuweza kupata usafiri wa kumuwezesha kufika mahakamani kwa wakati.
"Sisi wawili hatuwezi kufikisha idadi inayohitajika ya majaji mahakamani kwa mujibu wa kifungu 162 (2) cha Katiba. Kesi imeahirishwa hadi wakati mwingine," ametangaza Jaji Maraga.
Uchaguzi Kenya: Mahakama yashindwa kusikiliza kesi Uchaguzi Kenya: Mahakama yashindwa kusikiliza kesi Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 25, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...