Picha ya faru aliyeuawa yashinda tuzo ya picha bora
Picha ya kutisha ya uhalifu wa mazingira imetangazwa kuwa mshindi katika tuzo za shindano la wapiga picha la mwaka huu.
Picha hiyo iliopigwa na mpiga picha wa Afrika Kusini Brent Stirton inaoyesha hali ya faru mweusi katika mbuga ya wanyama pori ya Hluhluwe Imfolozi.
Wawindaji haramu walimuua mnyama huyo usiku kabla ya kumtoa pembe zake.
Stirton alipiga picha hiyo ikiwa miongoni mwa uchunguzi kuhusu biashara haramu ya bidhaa za faru.
Mpiga picha huyo alizuru zaidi ya maeneo 30 uliofanyika uhalifu huo wakati wa uchunguzi wake ambao aliutaja kuwa wa kuogofya.
Mwanangu wa kwanza atazaliwa mnamo mwezi Februari ; nina umri wa miaka 48. Unaweza kupoteza utu mara nyengine.
Stirton, ambaye alipokea tuzo hiyo katika tamasha la chakula cha jioni lililofanyika katika jumba la kumbukumbu mjini London , anaamini kwamba unyama huo aliofanyiwa faru huyo ulitekelezwa na wakaazi wa eneo hilo.
Lengo kubwa la uwindaji huo ni kuuza pembe mbili za faru huyo kwa wafanyibiashara.
Wafanyibiashara hao baadaye huzipeleka pembe hizo hadi Afrika Kusini kupitia Msumbiji hadi China ama hata Vietnam.
Katika mataifa hayo ya bara Asia, pembe za faru zina thamani ya juu ikilinganishwa na dhahabu ama dawa ya kulevya ya Cocaine.
Biashara hiyo hupata msukumo wa imani kwamba sawa na kucha za vidole vya mguuni, zinaweza kutibu ugonjwa wowote kutoka saratani hadi mawe ya figo.
Brent Stirton aliambia BBC : Kwa mimi kushinda tuzo hii, kwa majaii kuweza kutambua kazi yangu ni wazi kwamba tunaishi katika muda tofauti na kwamba hili ni swala nyeti.
''Swala la kuangamia kwa baadhi ya wanyama ni la kweli na faru ni mojawapo ya aina ya wanyama wanaoendelea kuangamia kwa kiwango kikubwa na ninashukuru kwamba majaji waliweza kutambua picha yangu kwa kuwa inaliangazia swala hili kwa hatua nyengine''.
Lewis Blackwell, mwenyekiti wa jopo la majaji hao wa WPY, alisema kuwa picha hiyo ya faru ilikuwa na athari kubwa katika jopo lake.
''Watu wanaweza kusinywa ama kushtushwa lakini ukweli ni kwamba picha hiyo inakuvutia na kukufanya kuhisi kana kwamba unataka kujifunza mengi.Unataka kujua habari kuihusu. Na huwezi kuitoroka kwa sababu inakuangazia yale yanayoendelea duniani''.
Picha ya faru aliyeuawa yashinda tuzo ya picha bora
Reviewed by RICH VOICE
on
Oktoba 19, 2017
Rating:
Hakuna maoni