Puskas: Bao la Olivier Giroud ndilo bora zaidi 2017

Olivier Giroud alifunga dhidi ya Crystal Palace

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Bao alilolifunga mchezaji wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Olivier Giroud dhidi ya Crystal Palace limeshinda tuzo ya Bao Bora la Fifa mwaka 2017, maarufu kama Tuzo ya Puskas.
Alifunga bao hilo siku ya Mwaka Mpya katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kwenye bao hilo maarufu kama 'scorpion kick', Giroud aliufikia mpira kutoka kwa mshambuliaji Alexis Sanchez kutoka nyuma yake akaupiga kwa mguu wake wa kushoto na kuupitishia juu ya bega kisha ukaugonga mwamba wa goli kabla ya kutulia kimiani.
Bao hilo la Giroud lilipata kura 36.1% kati ya jumla ya kura 792,062 zilizopigwa.
Giroud alikuwa anashindania tuzo hiyo na Deyna Castellanos wa Venezuela na kipa wa Afrika Kusini Oscarine Masuluke.

Kipa bora zaidi

Mshindi wa Kombe la Dunia na mshindi wa Serie A mara 10 Gianluigi Buffon ndiye mshindi wa tuzo ya mlindalango bora duniani mwaka huu.
Aliwasaidia Juventus kushinda taji la ligi mara ya sita mtawalia msimu uliopita.
Aidha, alicheza dakika 600 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya bila kufungwa.
Buffon, 39, amewashinda kipa Keylor Navas, wa Real Madrid na Manuel Neuer wa Bayern Munich.
"Ni heshima kubwa sana kwangu kupokea tuzo hii katika umri wangu huu," alisema Buffon.


Puskas: Bao la Olivier Giroud ndilo bora zaidi 2017 Puskas: Bao la Olivier Giroud ndilo bora zaidi 2017 Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 24, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...