Wafuasi wa Odinga wachoma matairi Kisumu
Katika maeneo mengi Kisumu, mji ambao ni ngome ya Raila Odinga, wakazi wamefunga barabara na kuchoma matairi.
Mwandiswa BBC Alistair Leithead anasema hajashuhudia kituo chochote ambapo upigaji kura unaendelea.
Ametutumia picha hii:
Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee amepiga kura yake katika eneo la Mutomo, Gatundu katika kaundi ya Kiambu.
Wakazi katika mtaa wa Bangladesh eneo la Jomvu mjini Mombasa wamefunga barabara za kuelekea kwenye vituo vya kupigia kura.
Wamekabiliana na polisi waliokuwa wakijaribu kuwatawanya.
Rais Kenyatta anatimiza miaka 56 hivi leo. Alizaliwa siku sawa na ya leo mwaka 1961.
Watoto hawa wamekuwa kwenye kituo cha kupigia kura cha Mutomo, ambacho ndicho Bw Kenyatta, wakiwa na fulana zenye ujumbe wa kumtakia heri siku ya kuzaliwa kwake.
Mama yao Joan Wamaitha amemwambia mwandishi wa BBC Anthony Irungu kuwa: "Walitazama video ya heri ya siku ya kuzaliwa ya rais na wakasisitiza wapate fulana hizi na wamsalimie Rais Kenyatta."
Familia hii imefika katika kituo cha kupigia kura cha Mutomo, Gatundu katika jimbo la Kiambu na mavazi ya kipekee - mavazi ya rangi za bendera ya Kenya.
Rais Kenyatta amejiandikisha kupigia kura katika kituo hicho na anatarajiwa kupiga kura baadaye leo.
Naibu Rais William Ruto, ambaye ni mgombea mwenza wa Rais Uhuru Kenyatta, amepiga kura yake katika kituo cha shule ya msingi ya Kosachei eneo la Turbo mjini Eldoret magharibi mwa Kenya.
Wapiga kura katika kituo cha shule ya msingi ya Kimbo katika eneo la Githurai 45, Kiambu wamevumilia mvua na baridi kali kwenye foleni kusubiri fursa ya kupiga kura.
Mvua imenyesha katika maeneo mengi Kenya usiku wa kuamkia leo.
Leo ni siku ya marudio ya uchaguzi na pia ni siku sawa na aliyozaliwa Rais Uhuru Kenyatta mwaka 1961.
Baadhi ya idara za serikali zimechukua fursa hii kumtumia salamu za heri.
Katika baadhi ya maeneo Kisumu, ngome ya Raila Odinga, baadhi ya wafanyakazi wa tume ya uchaguzi waliofaa kuendesha uchaguzi wa leo hawajafika vituoni bado.
Msimamizi wa uchaguzi kituo cha shule ya sekondari ya Lions High ameambia BBC kwamba kati ya wafanyakazi 399 eneo hilo, ni watatu pekee waliojitokeza.
Masanduku ya kupigia kura pamoja na vifaa vingine vya uchaguzi vinaendelea kuandalwia.
Tume ya taifa ya uchaguzi IEBC imesema vituo vingi vilifunguliwa kwa wakati, saa kumi na mbili asubuhi.
Vituo ambavyo vilichelewa kufunguliwa, muda utaongezwa baadaye jioni.
Lango la kuingia kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Olympic katika mtaa wa Kibera, Nairobi lilikuwa imefungwa kwa minyororo.
Lakini maafisa wa polisi wamefanikiwa kuvunja minyororo hiyo na sasa kituo hicho kimefunguliwa.
Katika kituo cha Shule ya upili ya Lions, kufikia saa moja na robo vifaa vya kupigia kura vilikuwa vinawasilishwa kituoni wakati huo.
Hakukuwa na mpiga kura hata mmoja kituoni.
Mwandishi wa BBC David Wafula amekuwa katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Moi Avenue, katikati mwa jiji la Nairobi.
Tazama video hii kuhusu hali ilivyo:
Mwandishi wetu Robert Kiptoo yupo mjini Nakuru ambapo shughuli ya upigaji kura inaendelea ambapo sawa na kwingine, idadi ya waliojitokeza si sawa na ya waliojitokeza uchaguzi wa tarehe 8 Agosti.
Wafuasi wa Odinga wachoma matairi Kisumu
Reviewed by RICH VOICE
on
Oktoba 26, 2017
Rating:
Hakuna maoni