Rais Magufuli: Mwekezaji Ambaye Hataki Atupishe na Kutuachia Madini Yetu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameitaka Tume iliyofanya mazungumzo na kampuni ya uchimbaji ya madini Barrick Gold Mining, kuandaa mazungumzo maalumu ya  aina hiyo hiyo kwenye madini ya Tanzanite na Almasi ili nchi ipate faida na kama wamiliki hao wakikataa basi waondoke moja kwa moja.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati alipokuwa akipokea taarifa maalum ya mazungumzo kati ya timu ya wataalamu aliyoiunda na timu ya wataalamu kutoka kampuni ya Barrick Gold Mining kuhusu madini ya dhahabu.

 "Baada ya tume hii ya dhahabu nataka mfanye 'negotiation' ya namna hii kwenye almasi lakini pia mfanye negotiation kama hii kwenye Tanzanite, Mpangee mapema, muanze haraka. Hakuna kulala. Zege hailali. Lazima tufanye kwa spidi  ili Almasi nayo muingie kwenye majadiliano yake tuweze kupata faida. Atakaye kataa kuja kufanya majadiliano atupishe atuache moja kwa moja na madini yetu. Kamati hii imeonyesha njia.... Atakayekataa atupishe. Tutafanya hivyo kwenye madini yote na nyinyi mmeshaonyesha njia," Rais Magufuli .

Pamoja na hayo  Rais Magufuli amesema amekubaliana na  mapendekezo yaliyotolewa na Waziri Prof. Kabudi kuwa iendelee kufuatilia madai yote kwa ajili ya pande zote mbili.

Kwa upande mwingine Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Barick nchini imekubali kulipa fidia ya dola milioni 300 ambazo sawa na bilioni 700 za Tanzania, pamoja na kuweka mgao sawa wa faida wa 50/50 na serikali, kufuatia mazungumzo ya ripoti ya makinikia yaliyofanyika kwa zaidi ya miezi mitatu,
Rais Magufuli: Mwekezaji Ambaye Hataki Atupishe na Kutuachia Madini Yetu Rais Magufuli: Mwekezaji Ambaye Hataki Atupishe na Kutuachia Madini Yetu Reviewed by RICH VOICE on Oktoba 19, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...