Catalonia kufanya uchaguzi wake mkuu leo


Serikali ya Madrid inasema hali sasa ni shwari
Image captionSerikali ya Madrid inasema hali sasa ni shwari
Raia wa Catalonia leo hii watachagua viongozi wao wapya, katika uchaguzi ambao serikali kuu ya Uhispania inaamini utamaliza msuguano wa kisiasa unaoendelea.
Serikali kuu ya Madrid iliuvunja utawala uliokuwepo awali, baada ya kuandaa kura ya maoni iliyotajwa kuwa haikufuata kanuni, iliyotaka uhuru wa eneo hilo.
Watu wengi wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huu
Image captionWatu wengi wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huu
Rais wa Catalonia aliyeondolewa madarakani, Carles Puigdemont, amekuwa akiendeleza kampeni zake za kujitenga na Madrid akiwa uhamishoni chini Ubelgiji kwa kupitia mitandao ya kijamii.
Mwezi Oktoba yalifanyika maandamano makubwa ya Catalonia kutaka kujitenga na Hispania
Image captionMwezi Oktoba yalifanyika maandamano makubwa ya Catalonia kutaka kujitenga na Hispania
Takwimu zinaonyesha kuwa vyama vinavyotaka kujitenga na vile vinavyotaka kusalia kwenye serikali ya Madrid vinalingana katika kura za maoni.
Mwandishi wa BBC wa eneo hilo anasema kuna kila dalili uchaguzi huu ukaibua tena hisia za kutaka kujitenga kuliko kutatua matatizo.
Catalonia kufanya uchaguzi wake mkuu leo Catalonia kufanya uchaguzi wake mkuu leo Reviewed by RICH VOICE on Desemba 21, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...