Kwa Picha: Miili ya wanajeshi waliouawa DRC yarejeshwa Tanzania
Miili ya wanajeshi 14 wa Tanzania waliouawa wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewasili jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Miili hiyo imesafirishwa kwa ndege za Umoja wa Mataifa kutoka nchini DR Congo.
Waliuawa wakati wa shambulio lililotekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Wanajeshi wengine zaidi ya 50 walijeruhiwa.
Umoja wa Mataifa ulisema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo.
Waasi wa ADF ndio wanaotuhumiwa kutekeleza shambulio hilo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alishutumu vikali shambulio hilo na kusema ni sawa na uhalifu wa kivita.

Aliitaka DR Congo kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo na kusema kwamba waliohusika wanafaa kuwajibishwa.
Wanajeshi zaidi walitumwa eneo hilo na kamanda wa kikosi cha kulinda amani anaelekeza shughuli ya kuwaondoa majeruhi.
Bw Guterres alisema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni.





Kwa Picha: Miili ya wanajeshi waliouawa DRC yarejeshwa Tanzania
Reviewed by RICH VOICE
on
Desemba 12, 2017
Rating:
Hakuna maoni