Wananchi wa Catalonia wanapiga kura kuchagua viongozi wapya

Na 

mediaRaia wa eneo la Catalonia wakiwa kwenye moja ya kampeni kabla ya kura siku ya Alhamisi.REUTERS/Yves Herman
Raia wa Catalanua hii Alhamisi hii wanapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria ambao huenda ukatoa mustakabali wa eneo hilo linalotaka kujitenga na utawala wa Madrid, kura inayofanyika miezi miwili baada ya jaribio la kujitangazia uhuru kushindikana.
Kura hii inawashindanisha viongozi matajiri wa eneo hilo la kaskazini dhidi ya vyama vingine ambavyo vinataka kusalia sehemu ya Hispania, na kura za maoni zinaonesha wagombea kutoka pande zote wanakaribiana.
Lakini swali bado linabaki, je wananchi kuwapa mamlaka viongozi wa vuguvugu linalotaka kujitenga na Hispania? Mmoja wa wagombea yuko gerezani na mweingine yuko uhamishoni nchini Ubelgiji.
Au je watapoteza viti 72 walivyokuwa navyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 hatua ambayo itakuwa imevunja rasmi ndoto yao ya kutaka kijitenga na Hispania?
Jimbo la Catalunia ambalo ni kitovu cha uwekezaji na utalii nchini humo limeshuhudia makampuni zaidi ya elfu 3 yakihamisha makao yao makuu baada ya viongozi wa eneo hilo kufanya maandamano yaliyopigwa marufuku na Serikali.
Wakati eneo hili likisalia kugwanyika, polisi walitumiwa kudhibiti waandamanaji waliokuwa wanashinikiza kujitenga ambapo watu kadhaa walijeruhiwa na wengine wanaendelea kushikiliwa.
Baada ya mvutano wa muda mrefu Octoba 27 mwaka huu viongozi wa Catalunia kupitia bunge walifanya kura ya maoni kuidhinisha kujitenga, lakini furaha yao ilidumu kwa saa chache baada ya utawala wa Madrid kuwafuta kazi viongozi wote wa eneo hilo na kushika hatamu ya uongozi.
Wananchi wa Catalonia wanapiga kura kuchagua viongozi wapya Wananchi wa Catalonia wanapiga kura kuchagua viongozi wapya Reviewed by RICH VOICE on Desemba 21, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...