Korea Kusini yaitaka Marekani kusitisha mazoezi ya kijeshi nchini humo
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In ameitaka Marekani kuacha kwa muda mazoezi yake ya kijeshi nchini humo mpaka kumalizika kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika mapema mwakani.
Anasema hii itasaidia pia kuifanya Korea Kaskazini kutotilia shaka uwepo wa wanamichezo wake kwenye michuano hiyo.
Korea Kusini itakua mwenyeji wa michezo hiyo itakayofanyika katika mji wa Pyeongchang mwezi Februari ikiwa ni kilomita 80 kutoka mpaka wake na Korea Kaskazini.
Mapema Canada na Marekani ziliapa kuendeleza mazoezi hayo ili kuisukuma Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa Nyuklia.
Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa katika mgogoro wa muda mrefu kufuatia mpango wa matumizi ya mabomu ya Nyuklia unaofanywa na Korea Kaskazini.
Michuano ya Olimpiki ya majira ya bariki inatarajiwa kuhusisha pia wanamichezo kutoka Korea Kaskazini jambo ambalo Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In anaeleza kuwa ni la kuimarisha uhusiano zaidi.
Korea Kusini yaitaka Marekani kusitisha mazoezi ya kijeshi nchini humo
Reviewed by RICH VOICE
on
Desemba 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni