DCI azungumzia tukio la Tundu Lissu ,Ben Sanane na mwandishi wa habari Azory Gwanda

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), amefunguka na kusema wao wanaendelea na upelelezi juu ya taarifa ya kutekwa kwa Ben Saanane na kudai hawawezi kusema kila hatua wanayochukua pia amedai polisi wanachukulia 'serious' shambulio la Lissu

DCI Boaz amesema hayo jan Disemba 20, 2017 wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa amepata taarifa juu ya kupotea kwa mwandishi wa habari Azory Gwanda, Ben Saanane na kudai hawawezi kuwa wanatoa taarifa kwa kila hatua ambayo wamefikia.

"Tumepata taarifa za huyo mwandishi kupotea na kwa taratibu zetu tunachukua kila hatua inayostahili kuchukuliwa wakati wa utafutaji wa mtu aliyepotea.

"Zipo taratibu ambazo tunapaswa kuzichukua sisi kama polisi, suala la Ben Sanane tumeshalisema sana sisi kama upepelezi hatuwezi kusema kila hatua tunayochukua, hairuhusiwa kisheria na katika kanuni zetu za upelelezi lakini niwathibitishie kwamba kila hatua inayostahili kufanywa ili kutrace mtu imeshafanyika" alisema DCI Boaz na kuongeza;

”Pengine nitoe rai kwa wananchi na waandishi wa habari taarifa kwetu ni muhimu sana na huwa tunazifuatilia. Tunaendelea kuwaomba kama mna taarifa ambazo ni za uhakika watuletee tutazifanyia kazi.”

Akizungumzia tukio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana, Boaz alisema jambo hilo limezungumzwa sana na viongozi, hivyo asingependa kulizungumzia na kwamba Jeshi la Polisi linachukulia tukio hilo kwa umakini na hawawezi kujibishana na watu katika magazeti.

“Tunachukua hatua zote ambazo zinatuwezesha kutambua ni nani katenda tukio hilo,” alisema Boaz.
DCI azungumzia tukio la Tundu Lissu ,Ben Sanane na mwandishi wa habari Azory Gwanda DCI azungumzia tukio la Tundu Lissu ,Ben Sanane na mwandishi wa habari Azory Gwanda Reviewed by RICH VOICE on Desemba 21, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...