Burundi kuitambulisha katiba mpya siku ya Alhamis
Hata hivyo wapinzani na baadhi ya
nchi za kigeni wamekosoa mchakato huo mzima kwamba haukuzingatia sheria
na katiba mpya inanuwia kumbakiza madarakani Rais Pierre Nkurunziza
hadi mwaka 2034.
Taarifa ya Ikulu ya Burundi imethibitisha kuwa
sherehe za utiaji sahihi kwenye katiba mpya na kuitambulisha kwa
raia zitafanyika alhamisi saba katika mkoa wa kati wa Gitega eneo la
Bugendana ambako huko ndiko kulikozinduliwa rasmi mchakato wa
katiba, lakini pia kampeni ya chama madarakani CN DD/FDD ya kuipiga
debe katiba hiyo. Aidhaa taarifa hiyo ya Ikulu imetoa mwaliko kwa magavana wote na Wakuu wa tarafa za Burundi kushiriki kwenye sherehe hizo. Wamealikwa pia wawakilishi wa vyama vya kisiasa , asasi za kiraia pamoja na Viongozi wa kidini .
Itakuwa mara ya kwanza katika historia ya Burundi kuwa na sherehe za kuipokea katiba mpya. Wadadisi wa siasa za Burundi wanahisi utaratibu huo mpya ni ujumbe wa Rais Nkurunziza wa azama yake ya kukamilisha shughuli ya katiba ambayo yeye ameipigia debe kwamba inakuja kuipa Burundi hadhi na Uhuru wake kamili wa kujitawala .
Lakini pia ni ujumbe ambao kiongozi huyo anaupeleka kwa Jumuiya ya kimataifa hususan, mataifa ambayo yalitilia shaka na kukosoa mpango mzima wa marekebisho ya katiba wakitaja kwamba uliandaliwa kinyume cha sheria .
Ni hivi majuzi tu Umoja wa mataifa, na baadhi ya nchi za magharibi washirika wa zamani wa Burundi kama Ufaransa na Ubelgiji walikemea vikali mchakato mzima wa katiba kwamba uligubiikwa na dosari nyingi na kwamba katiba hiyo mpya inatishia hata maridhiano ya kitaifa na uwakilishi wa makabila kwa Mujibu wa Mkataba wa Aman iwa Arusha. Madai ambayo yamepingwa vikali na Wakuu wa Burundi.
Burundi kuitambulisha katiba mpya siku ya Alhamis
Reviewed by RICH VOICE
on
Juni 05, 2018
Rating:
Hakuna maoni