Waziri Ataka Watoto Walioungana Kagera Wafikishwe Muhimbili Haraka
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Ummy Mwalimu
amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, kuhakikisha watoto waliozaliwa
wakiwa wameungana wanafikishwa Muhimbili.
Waziri
Ummy ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo ambaye alihoji je serikali ina
taarifa kuwa kuna watoto wamezaliwa Kagera wakiwa wameungana.
Akijibu swali hilo, Ummy amesema: “Wanaozaliwa wakiwa na maumbile ya ajabu wapelekwe hospitali.
“Na
kuhusu watoto waliozaliwa wakiwa wameungana huko Kagera, namwagiza
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera ahakikishe watoto hao wanafikishwa
Muhimbili,”.
Waziri Ataka Watoto Walioungana Kagera Wafikishwe Muhimbili Haraka
Reviewed by RICH VOICE
on
Juni 05, 2018
Rating:
Hakuna maoni