Wabunge CCM Wammwagia Sifa Rais Magufuli Bungeni
Wabunge
wa CCM wamempongeza Rais John Magufuli anavyoshughulikia sekta ya
madini ikiwamo kuzuia usafirishaji wa mchanga wa madini ya dhahabu
‘makinikia’ nje ya nchi.
Wabunge
hao Goodluck Mlinga (Ulanga) na Sixtus Mapunda (Mbinga Mjini) wamesema
hayo leo Juni 1, 2018 bungeni wakati wakichangia bajeti ya madini ya
mwaka 2018/19.
“Nampongeza
Rais (Magufuli) kwa kuzuia makinikia kupeleka nje ya nchi, Tanzania ni
nchi ya nne kwa uzalishaji wa dhahabu kwa nchi za Afrika na duniani.
Katika nchi matajiri wa uzalishaji wa mali tupo lakini mafanikio ya
wananchi na Serikali tuko chini,” amesema Mlinga.
Amesema anampongeza Rais kwa kujenga ukuta katika mgodi wa Mirerani kwani ni madini adhimu.
“Tanzania ni nchi ya nne kwa uzalishaji wa gesi katika bara la Afrika. Lakini katika nchi masikini tupo,” amesema.
Akiendelea
kuchangia, Mlinga amesema, Rais anapaswa kufanya mabadiliko katika
wizara ya madini kwani watendaji wake wamesababisha haya.
Naye Mapunda amesema alichokifanya Rais ni jambo kubwa kwani tuna madini mengi lakini yalikuwa hayatunufaishi.
“Tuko
katika mpito kutengeneza mfumo bora wa kutunufaisha na yote yanahitaji
ushirikiano na kupeana moyo. Biashara ya dhababu ni ya familia kubwa na
jinsi ya kuiingia inahitaji kutumia ubongo mkubwa sana,” amesema Mapunda
na kuongeza:
“Ili
kuingia kupambana nao inahitaji kuwa na mfumo mzuri na Serikali
inapoanza kutengeneza sheria, hawa hawawezi kukubali, lazima
watatuhujumu.”
Wabunge CCM Wammwagia Sifa Rais Magufuli Bungeni
Reviewed by RICH VOICE
on
Juni 01, 2018
Rating:
Hakuna maoni