Polisi waanza uchunguzi matapeli wa meseji za simu
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kitengo cha upelelezi
wa makosa ya mtandaoni, (Cybercrime investigation unit) kimesema kuwa
kinafanya uchunguzi kuwabaini wanaotuma ujumbe mfupi wa simu za mkononi
kwa nia ya kuwatapeli wananchi.
Taarifa
iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao makuu, Barnabas
Mwakalukwa, leo imesema yeyote aliyetapeliwa anatakiwa kutoa taarifa
katika kituo cha polisi alichokaribu nacho.
“Tunawataka
wananchi kuacha kutumia simu na mitandao ya kijamii vibaya na badala
yake itumike kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya mambo mbalimbali ya
maendeleo,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa
hiyo imesema, baadhi ya jumbe hizo ni zile zinazosema. ‘Ile hela tuma
kwa namba hii’ au ‘usipige kwa sasa, spika imeharibika, tuma ujumbe,’ au
‘Mjukuu wangu ile ndagu niliyokutumia imefanya kazi na sasa unapata
wateja wengi... sasa njoo uchukue ndagu nyingine ya mvuto na nyingine
kama hizo.’
Pamoja
na hayo Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kutumia mitandao
pamoja na simu katika kuelimisha na kuhabarisha na si vinginevyo ikiwa
ni pamoja na kuwataka wananchi kupuuzia jumbe hizo zenye lengo la
kitapeli.
BY RICH VOICE
Polisi waanza uchunguzi matapeli wa meseji za simu
Reviewed by RICH VOICE
on
Juni 07, 2018
Rating:
Hakuna maoni