TECNO Pouvoir 2 Uhakika Wa Chaji Ndani Ya Masaa 96.
Pamoja
ya kuwa kampuni inayosifika katika uzalishaji wa simu zinazotunza
chaji, kampuni ya simu ya TECNO imeendelea kudhihirisha ubora wake kwa
mara nyengine tena kupitia TECNO pouvoir 2 (TECNO LA7) ikiwa ni
muendelezo wa ‘TECNO L series’ yenye betri 5000mAh na mtandao wa 4G.
Na
pamoja ya kuwa na betri kubwa aina ya Li-Polymer, 5V2A yenye kujaa
chaji kwa haraka na kudumu nayo zaidi ya siku tatu lakini bado kampuni
ya simu ya TECNO hakusita kuhakikisha TECNO pouvoir 2 inakuwa na
muonekano mzuri kwa kupitia umbo lake jembamba la ‘metallic’ lenye
kutawaliwa na wigo mpana wa kioo chenye uwiano wa 18:9.
TECNO
pouvoir imebeba kamera mbili nyuma ikiwa na megapixel 13 na flashi
mbili za LED na mbele ikiwa na megapixel 8 na LED flashi pamoja na mix
flashi zenye kupiga picha nzuri na zenye wang’avu kutokana na aina ya
kioo cha TECNO pouvoir 2 kuwa na upana wa nchi 6.0 HD+ (1440*720) 450nit
IPS. Mix flashi inafanya kazi kama ilivyo kwa flashi za kawaida
isipokua yenyewe inapatikana ndani ya kioo cha simu na inafanya kazi
wakati wa kupiga ‘selfie’ tu.
Na
ikiwa simu ya kwanza kwa toleo la ‘TECNO L series’ kuwa na kasi ya
mtandao wa 4G lakini pia TECNO pouvoir 2 inaufanisi mzuri zaidi kutokana
na processor ya MT6739WA 1.3 ghz Quard-core pamoja na Android 8.1 Oreo
na HiOS ya 3.3.
TECNO
pouvoir 2 inatumia aina tofauti tofauti za ‘security’ ikiwamo
fingerprint inayopatikana nyuma ya simu na face id yenye kunlock simu
kupitia paji la uso na ndio simu ya kwanza ya toleo la ‘TECNO L series’
kutumia face id.
Simu
hii pia imekuja na memory ya ndani ya GB 16 na GB 2 za ram
vinavyoiwezesha simu kuhifadhi mafile mengi na kufanya kazi zaidi ya
moja kwa wakati mmoja pasipo kuathiri uwezo wa simu lakini pia TECNO
pouvoir inaweza kubeba hadi GB 64 memory ya ziada.
TECNO pouvoir 2 inapatikana katika rangi tatu tofauti nyeusi, gold na city blue.
Kwa bahari zaidi tembelea http://www.tecno-mobile.com/tz/index.php?id=740#/
TECNO Pouvoir 2 Uhakika Wa Chaji Ndani Ya Masaa 96.
Reviewed by RICH VOICE
on
Juni 12, 2018
Rating:
Hakuna maoni