Walimu wa Moi Girls wafanyiwa uchunguzi wa DNA Kenya katika kesi ya ubakaji wa mwanafunzi.
Walimu pamoja na wafanyakazi wengine
wakiume katika shule ya upili ya Moi Girls Nairobi wametakiwa
kufanyikwa uchunguzi wa DNA wakati maafisa wa upelelezi wanajaribu
kuchunguza tuhuma za kubakwa kwa mwanafunzi katika shule hiyo Ijumaa
usiku.
Polisi wamewaagiza walimu hao wa kiume, walinzi na jamaa wa
kiume wa walimu wanaoishi ndani ya Shule hiyo au wale wanaoaminika kuwa
walikuwa ndani ya shule hiyo mapema Jumamosi asubuhi.Uchunguzi huo wa DNA ni muhimu katika kubaini kesi za unyanyasaji wa kingono na hutumika kumithilisha mshukiwa dhidi ya maji maji yanayopatikana katika mwili wa muathiriwa na hivyo kuweza kuwana ushahidi mzito katika kesi.
Itasaidia pia kubaini iwapo washukiwa wataokaochunguzwa walikuwa katika eneo la tukio hilo la uhalifu au kuwaondoshea makosa yoyote.
Polisi wanajaribu kuchunguza matukio yaliojiri usiku huo wa mkasa na siku ya pili iliyofuata kujua ukweli upo wapi katika tuhuma hizo za kubakwa kwa wanafunzi wa Moi Girls ambazo zimezusha hasira kubwa nchini.
Maafisa wanachunguza pia tuhuma kwamba maafisa katika shule hiyo waliwaambia wanafunzi wajioshe na wanyamaze kuhusu kinachotuhumiwa kutokea.
Mambo muhimu ya kufanya kumsaidia muathiriwa wa ubakaji:
Kenya iliidhinisha sheria ya uhalifu wa kingono na muongozo wa kitaifa kuhusu namna ya kushugulikia visa vya unyanyasaji ili kutoa nafasi kwa watoto kupata huduma za afya.Hivyo basi katika kesi hii, sheria ya Kenya iko wazi kwamba mwanafunzi aliyebakwa ana haki ya kupata huduma ya baada ya kubakwa.
Jennifer Kaberi, mtaalamu wa malezi ya watoto Nairobi anasema hatua ya kwanza kuchukua wakati mtoto anaponyanyaswa ki ngono, ni :
- Mkimkimbize hospitali muathiriwa katika muda wa saa 72 baada ya ubakaji.
- Piga ripoti katika kituo cha polisi haraka iwezekanavyo.
- Usimuoshe au kusafisha sehemu yoyote ya mwili wa muathiriwa.
- Usizioshe au kuziharibu nguo alizovaa muathiriwa, badala yake ziweke kwenye mfuko wa kaki na sio mfuko wa plastiki.
- Madaktari watakagua kiwango cha majeraha na kumtibu mtoto.
- Watampa dawa pia ya kumkinga na virusi vya HIV au kupata uja uzito.
- Ripoti ya daktari itatumiwa katika uchunguzi wa polisi kwenye kesi.
Vyombo vya habari nchini vinaripoti kwamba ripoti ya daktari imethibitisha kwamba msichana wa shule hiyo alibakwa.
Mkasa huu umetokea hata wakati ambapo maandamano yamefanyika mjini Nairobi siku ya Jumatatu kulalamika kuhusu kilichotokea
Waandamanaji hao waliojumuisha wanafunzi wa zamani wa shule hiyo waliandamana nje ya shule hiyo wakiwa wamebeba mabango yaliokuwa na ujumbe wa kupinga ubakaji.
Waziri wa Elimu nchini Amina Mohammed leo anatarajiwa kuhotobia waandishi wa habari kutoa maelezo zaidi kuhusu mkasa huo katika shule ya Moi girls.
Amina alitoa agizo kwa maafisa katika wizara yake wafanye upya ukaguzi wa usalama katika shule zote kuepuka uwezekano wa wanafunzi kuingiliwa.
Gazeti la Daily Nation linaripoti kwamba tayari maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha uhalifu mkubwa na mwanakemia wa serikali hapo jana Jumatatu walichukuwa sampuli za wafanyakazi wanane wa shule hiyo miongoni mwao walimu 6 ili kufanyiwa ukaguzi wa maabara.
Kwa sasa shule hiyo imefungwa kwa wiki moja huku uchunguzi ukiendelea.
Walimu wa Moi Girls wafanyiwa uchunguzi wa DNA Kenya katika kesi ya ubakaji wa mwanafunzi.
Reviewed by RICH VOICE
on
Juni 05, 2018
Rating:
Hakuna maoni