Friday, September 23, 2016


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 23



SeeBait

























 

Friday, September 23, 2016


Rais Magufuli ateua viongozi wa juu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL)



SeeBait

 kimataifaaaaaaa

 

Kundi la kiraia la kushughulikia dharura nchini Syria katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi la White Helmets limetunukiwa tuzo ya haki ya kuishi - maarufu kama tuzo mbadala ya Nobel. Kundi hilo linalojulikana kama White Helmets, limetambuliwa na baraza la tuzo ya haki za binadamu la nchini Swden kwa ujushaa, huruma na ushiriki wake katika kuwaokoa raia kutokana na uharibifu wa vita nchini Syria. Mapema mwezi huu White Helmet walikuwa miongoni mwa makundi 73 ya misaada yaliyosimamisha mahusiano na Umoja wa Mataifa yakiyatuhumu mashirika ya misaada ya kibinadamu ya umoja huo pamoja na washirika wake kwa kulaghaiwa na serikali ya Syria. Mwanaharakati wa Urusi Svetlana Gannushkina ambaye amepigania haki za wakimbizi kwa miongo kadhaa, Mozn Hassan wa Misri na vuguvugu lake la wanawake la Nazra pamoja na gazeti huru la Cumhuriyet la nchini Uturuki pia wametunukiwa tuzo hiyo pamoja na White Helmets. Washindi wa tuzo hiyo iliyozinduliwa mwaka 1980 na Jakob Uexkull kwa lengo la kutambua na kuthamini michango ya watu na vikundi ambavyo vinajitolea kuokoa maisha ya watu watagawana kiasi cha euro milioni 315,000.

 

Rais wa Syria Bashar al Assad amesema mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vikosi vya jeshi lake mashariki mwa nchi hiyo yalikuwa ya kukusudia na yalidumu kwa saa moja ambapo ameitupia lawama Marekani kwa kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoandaliwa baina yake na Urusi. Katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press Assad amesema vita nchini mwake ambayo imeingia mwaka wa sita ina uwezekano wa kuendelea kwa kile alichookita ni uungwaji mkono wa wapinzani kutoka nje. Assad amesema Marekani haina dhamira ya kweli kuungana na Urusi katika mapambano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS.


Polisi nchini Morocco imewakamata watu wanne wanaoshukiwa kuwa wanajihadi wakihusishwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS ambao walikuwa wanapanga mashambulizi nchini humo. Wapelelezi walimkamata mtu mmoja kaskazini mwa mji wa Mekenes ambaye alikuwa akipanga shambulio la kigaidi nchini Morocco, kwa mujibu wa taarifa za wizara ya mambo ya ndani. Taarifa hiyo imesema mshukiwa huyo ana uzoefu katika utengenezaji wa mabomu na alikaribia kununua malighafi nyingine za kutengeneza bomu. Wiki iliyopita washukiwa wenye itikadi kali walikamatwa maeneo ya Tangiers kaskazini mwa Morocco wakiwa katika mchakato wa kufanya mashambulizi hatari. Serikali mjini Rabat imesema zaidi ya makundi 150 ya kigaidi yamegundulika tangu mwaka 2002, yakiwemo dazeni kadhaa katika miaka mitatu iliyopita yaliyokuwa na mafungamano na wanajihadi kutoka Iraq na Syria.


Roketi lililorushwa kutokea upande unaoshikiliwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS nchini Syria limeshambulia katika mpaka wa Uturuki hii leo na kuwajeruhi watu kadhaa. Roketi hilo limepiga maeneo ya soko katikati mwa mji ulioko mpakani wa Kilis na kuvunja madirisha huku ripoti ya televisheni ya NTV ikisema watu kadhaa wamejeruhiwa. Shambulio hilo linakuja mwezi mmoja baada ya mashambulizi ya kiwango cha juu ya kijeshi yaliyoanzishwa na vikosi vya Uturuki nchini Syria yakilenga kuwafurusha wanajihadi nje ya eneo lake la mpakani. Mji wa Kilis umekumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya maroketi kutoka upande wa Syria katika miezi ya hivi karibuni ambapo hadi sasa watu 22 wamepoteza maisha ambao nusu yao ni wakimbizi wa Syria.  

Maafisa wa Afghanistan wamesema kwamba wamekamilisha mkataba wa amani na kiongozi wa kivita mwenye utata Gulbuddin Hakmatyar ambaye analiongoza kundi la wanamgambo la Hezb-i-Islami. Serikali ina matumaini kwamba mpango huo utachochea wapiganaji wengine kufuata nyayo hizo. Mshauri wa usalama wa ndani wa Afghanistan ametangaza katika ukurasa wake wa Twitter muda mchache baada ya kutiwa saini kwa mkataba huo leo Alhamis. Mamia ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Afghanistan kupinga hatua hiyo na kusema mkataba huo ni uhalifu. Wanasema makubaliano yoyote na kiongozi huyo ni uhaini wakiongeza kwamba amani haiwezi kupatikana kwa kuitoa sadaka haki. Chini ya mkataba huo Hekmatyar atapatiwa msamaha wa makosa ya zamani pamoja na kuachiliwa kwa wanachama wa kundi la Hezb-i-Islami. Kabul pia itafanya kampeni ya kuondolewa vikwazo vya kimataifa kwa kiongozi huyo wa kikabila.


Jeshi la Iraq limesema vikosi vyake vimechukua udhibiti kamili wa mji wa kaskazini wa Shirqat kutoka mikononi mwa wapiganaji wa kunDola la KIislamu IS karibu na ngome yake mjini Mosul. Maafisa wamesema IS wamepata hasara kubwa ingawa hapakuwa na maelezo ya kina.  Majeshi ya serikali yakiungwa mkono na Marekani yalianzisha mashambulizi makali siku ya Jumanne kuukamata tena mji huo ambao upo kilometa 100 kusini mwa Mosul. IS iliudhibiti mji wa Shirqat mwaka 2014 baada ya kufanya shambulio kaskazini mwa Iraq. Wakati huo waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen (Uzula fon deya leyan) amesema mapambano dhidi ya IS nchini Iraq yamekuwa ya mafanikio. Ujerumani imekuwa ikiyapatia majeshi ya ndani vifaa na silaha  pamoja na mafunzo, ambapo kwa mujibu wa waziri Leyen huo ulikuwa ni mkakati sahihi. 


Watu saba wameuawa katika shambulio la usiku huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo kundi la waasi wa Uganda la ADF limeshutumiwa kwa kutekeleza mauaji hayo. Msemaji wa jeshi Mark Hazakuy ameiambia AFP kwamba mauaji hayo yametokea katika mkoa wa Beni eneo la Kasinga ambapo pia nyumba zilichomwa moto wakati mapigano baina ya askari na waasi yakiendelea. Mamlaka za mji huo zimesema jumla ya nyumba 15 zilichomwa moto na kwamba watu watano hawajulikani walipo. ADF kundi la waasi, ambalo kwa sehemu linafuata itikadi kali za Kiislamu kutoka nchini Uganda, limekuwa likilaumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na kujihusisha na utekaji na biashara ya magendo. Eneo la Beni linakabiliwa na vikundi mbalimbali vya waasi vinavyochochea vurugu vikigombania haki ya uchimbaji madini na rasilimali za misitu.

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

habari z kimachezooo

 BALOTELLI ATINGISHA DABI YA RIVIERA, KOCHA WAKE APIGWA BUT

BALOTELLI-Nice2BOSI wa Nice Lucien Favre ameungama kwamba Mario Balotelli sasa amezidi matarajio yao baada ya Jana kupiga tena Bao 2 kwenye Mechi na Monaco ya Ligi 1 huko France.
Hiyo ni Mechi ya pili mfululizo kwa Balotelli kufunga Bao baadavya Jana Nice kuwachapa Monaco 4-0 katika Dabi ya Riviera na kukaa kileleni mwa Ligi 1 wakiwa juu ya Mabingwa Watetezi Paris Saint-Germain.
Baada ya Gemu hiyo Kocha Favre alisema: "2-0 toka kwa Balotelli zilikuwa ni muhimu na zilitupa morali ya kujiamini. Mario ni muhimu kwetu kwani anatoa kina kwenye Gemu yetu. Sasa anapaswa kuendelea hivi hivi."
Kocha huyo aliendelea: "Baada ya Miaka kadhaa migumu kwake sasa anaweza kurejea kileleni. Tutajaribu kumsaidia ili aimarike zaidi!"

EPL: JUMAMOSI KUANZA OLD TRAFFORD MAN UNITED v LEICESTER, KWISHA EMIRATES ARSENAL v CHELSEA!


EPL-2016-17-LOGO2EPL, Ligi Kuu England, Wikiendi hii itaanza mapema Mchana Jumamosi huko Old Trafford wakati Manchester United watakapowakaribisha Mabingwa Watetezi Leicester City.zipo Mechi 8 na ya mwisho Usiku ni mtanange mkali huko Emirates Jijini London kati ya Arsenal na EPL-SEP23Chelsea.
Katikati ya Mechi hizo mbili za mwanzo na za mwisho kwa Jumamosi zipo Mechi nyingine 6, zote zikianza Saa 11 Jioni, na miongoni mwao ni ya Swansea City kuwakaribisha Vinara wa EPL Man City.
Raundi hii ya 6 ya EPL itaendelea Jumapili na Jumatatu kwa Mechi moja moja.
Kwa sasa Vinara wa Ligi hii ni Man City ambao wameshinda Mechi zao zote 5 na wana Pointi 15 wakifuata Everton ambao wana Pointi 13 baada ya kushinda Mechi 4 na Sare 1 na ya 3 ni Tottenham wenye Pointi 11 baada ya kushinda Mechi 3 na Sare 2.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
Jumamosi Septemba 24
1430 Man United v Leicester City          
1700 Bournemouth v Everton               
1700 Liverpool v Hull City           
1700 Middlesbrough v Tottenham         
1700 Stoke v West Brom            
1700 Sunderland v Crystal Palace          
1700 Swansea v Man City           
1930 Arsenal v Chelsea              
Jumapili Septemba 25
1800 West Ham v Southampton            
Jumatatu Septemba 26
2200 Burnley v Watford


LA LIGA: REAL SARE, BARCA SARE, MESSI NJE WIKI 3!



LALIGA-2016-17MABINGWA wa La Liga Jana huko kwao Nou Camp walitoka Sare 1-1 na Atletico Madrid na pia kumpoteza Lionel.Messi ambae alitoka baada ya kuumia.
Taarifa toka Barca zimedokeza kuwa Messi atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 3 akiuguza Nyonga yake.
Kwenye Mechi hiyo, Barca walitangulia kufunga kwa Bao la Kipindi cha Kwanza la Ivan Rakitic aliefunga kwa Kichwa akiunganisha krosi ya Iniesta.
Kipinďi cha Pili Majeruhi yakawafanya Barca wawapoteze Sergio Busquets na kisha Messi na kutoa mwanya kwa Correa kusawazisha kutokana na kosa la Javier Mascherano.
Matokeo hayo yamewaweka Barca Nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Vinara Real Madrid kwa Pointi 3 huku Nafasi ya Pili ikishikwa na Sevilla walio Pointi 2 nyuma ya Real na Atletico wapo Nafasi ya 4 Pointi 1 nyuma ya Barcam
Mapema Jana Real walibanwa na kutoka 1-1 na Villareal.
Villareal walitangulia kufunga kwa Penati ya Bruno Soriano ya Kipindi cha Kwanza ya baada ya Sergio Ramos kuunawa Mpira lakini mwanzoni Kipindi cha Pili Ramos akafuta makosa yake kwa kusawazisha.
LA LIGA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Jumanne Septemba 20
Malaga CF 2 SD Eibar 1
Sevilla 1 Real Betis 0
Jumatano Septemba 21
Celta de Vigo 2 Sporting Gijon 1    
Real Madrid CF 1 Villarreal CF 1
FC Barcelona 1 Atletico de Madrid 1
Real Sociedad 4 Las Palmas 
Granada CF 1 Athletic de Bilbao 2  
Alhamisi Septemba 22
2100  Deportivo La Coruna v CD Leganes        
2100  Osasuna v RCD Espanyol  
2300  Valencia C.F v Deportivo Alaves   
Ijumaa Septemba 23         
2145  Real Betis v Malaga CF     
Jumamosi Septemba 24
1400  SD Eibar v Real Sociedad
1715  Sporting Gijon v FC Barcelona
1930  Athletic de Bilbao v Sevilla FC     
2145  Las Palmas v Real Madrid CF

WAYNE ROONEY AJIBU WAPONDAJI MAN UNITED - MENGI YAO NI TAKATAKA!


ROONEY-TRAININGKEPTENI wa Manchester United Wayne Rooney Leo amewajibu Watu wanaoiponda Timu yake hasa baada ya kufungwa Mechi 3 ndani ya Siku 8 mikononi mwa Manchester City, Feyenoord na Watford.
Akiongea kwenye Kipindi cha MUTV, Kituo cha TV cha Man United, Rooney alikiri ni kawaida wao kupondwa kutokana na hadhi yao na kusema: “Hiyo ndio Soka, nadhani. Hatukushinda Gemu 3 na ni wazi kila Mtu ataongea hilo. Tulikuwa na Wiki mbaya, Siku 8 mbaya na tulipoteza Gemu 3 na muhimu ni jinsi tutakavyoibuka upya.”
Kuhusu yeye binafsi kupondwa kwa madai kiwango chake kushuka, Rooney alisema: “Ndio, nimeandamwa na hilo maisha yangu yote ya Soka na nadhani hilo ndio Soka la sasa. Mie nasikiliza Makocha wangu na Wachezaji wenzangu, Watu wa karibu yangu, na sisikilizi vitu wanavyoongea Watu wengi kwani mengi ni takataka!”
“Inabidi nitie mkazo, nifanye kazi kwa bidii, kama nilivyokuwa nikifanya maisha yangu yote ya Soka nikifanya juhudi na kujaribu kila kitu kwa faida ya Timu.”
Pia Rooney aligusia ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Northampton kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya EFL CUP, Kombe la Ligi, na kusema: “Jana Usiku tulishinda na sasa tuna Gemu 3 za Nyumbani kabla ya mapumziko ya Mechi za Kimataifa na ni muhimu tushinde zote ili Msimu wetu urudi kwenye Reli.”
Kuhusu kupangwa kucheza na Mahasimu wao Man City kwenye Raundi ya 4 ya EFL CUP, Rooney ameeleza: “Kwangu mimi ni Droo safi. Baada ya kilichotokea kwenye Ligi, hii ni nafasi safi kulipa kisasi. Ni Mechi safi Old Trafford!”
Pia Rooney amesema ana hakika Man United itakuwemo kwenye mbio za Mataji Msimu huu hasa kwa vile Meneja wao ni Jose Mourinho.
Rooney ametamka: “Yeye amekuwa bora tangu aje. Mazoezi yamebadilika mno. Kila kitu kuelekea Mechi, mbinu, mwelekeo, ni mzuri sana! Nina hakika tutarudi kupigania Taji Msimu huu!”


SAMATTA AUMIA GOTI, GENK YAIBUTUA 4-0 EENDRACHT AALST


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta yuko nje kwa wiki moja sasa kutokana na maumivu ya goti. Samatta aliumia katika mchezo wa kwanza wa Kundi F Europa League dhidi ya Rapid Viena Alhamisi iliyopita Uwanja wa Allianz, Viena, Austria, KRG Genk ikifungwa 3-2. Na Nahodha huyo wa Taifa Stars amekosa mechi mbili hadi sasa, moja ya Ligi ya Ubelgiji wakifungwa 2-0 na Anderlecht Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk Jumapili na jana katika kombe la Ligi ya Ubelgiji, wakishinda 4-0 ugenini dhidi ya Eendracht Aalst Uwanja wa Het Pierre Cornelisstadion, Aalst.
Mbwana Samatta yuko nje kwa wiki moja sasa kutokana na maumivu ya goti
Samatta anatakiwa kuwa nje kwa angalau wiki mbili, lakini taarifa nyingine zinasema maumivu yake ni ya kupumzika kwa wiki moja tu, maana yake anaweza kuanza mazoezi wakati wowote kuanzia leo. Tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, Samatta amecheza jumla ya mechi 25 za mashindano yote, 18 msimu uliopita na saba msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita. Katika mechi hizo, ni 14 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tatu msimu huu, wakati 11 alitokea benchi nane msimu uliopita na tatu msimu huu – na mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu.
Nikolaos Karelis alifunga mabao yote jana KRC Genk ikishinda 4-0 
Genk watashuka tena uwanjani Jumapili kumenyana na Kortrijk Uwanja wa Guldensporen mjini Kortrijk katika Ligi ya Ubelgiji, kabla ya Alhamisi wiki ijayo kurejea kwenye Europa League watakapoikaribisha Sassuolo ya Italia katika mchezo wa pili wa Kundi F. Katika mchezo wa jana, mabao yote ya Genk yalifungwa na mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis dakika za 14, 22, 45 na 55.

AZAM WAIFUATA NDANDA FC NA STAILI TOFAUTI


AZAM FC imeondoka leo mchana kwenda Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Ndanda FC Jumamosi Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Na Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, Zeben Hernandez Rodriguez, amekiweka sawa kikosi chake kukabiliana na kila hali katika mchezo huo. Azam FC itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo moja tu la kuhakikisha inaibuka na ushindi kutokana na kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Simba (1-0) licha ya kuonyesha kiwango bora kwa asilimia kubwa ya mechi hiyo.
Rodriguez (katikati) akiwa na Wasaidizi wake katika moja ya michezo ya Ligi Kuu
“Tutabadilisha aina yetu ya mpira kwa sababu uwanja tutakaochezea ni mbaya sana, tunauchukulia kwa uzito mkubwa sana mchezo huo, tutacheza soka la mipira mirefu sana lakini kwa urahisi, hili ni jambo la muhimu sana kutokana na aina ya uwanja tutakaochezea,” alisema. Ili kuonyesha amepania kukabiliana na uwanja huo pamoja na wapinzani wake, Kocha huyo raia wa Hispania kwa siku mbili hizi tokea jana hadi kesho asubuhi, amekuwa akikipika kikosi chake katika uwanja wa nyasi za kawaida unaoendana kidogo na Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Zeben alisema kuwa jambo la muhimu kwa leo na kesho ni baadhi ya wachezaji waliocheza mchezo uliopita kufanya mazoezi ya kurudisha miili yao vizuri kabla ya kuamua kikosi kitakachokwenda kuikabili Ndanda, kitakachosafiri kesho Alhamisi mchana. “Kwangu mimi mchezo uliopita (Simba) ulikuwa mzuri kwa timu yangu, tulikuwa bora mchezoni zaidi ya Simba, lakini kwa kosa moja tulilolifanya Simba waliweza kulitumia na kufunga bao, kwa sasa ninachofanya ni kuwaweka sawa wachezaji wangu na muhimu kwangu kwa sasa ni kuweka akili yetu kwa mchezo ujao na kuachana na habari za mchezo uliopita,” alisema. Mpaka sasa katika msimamo wa ligi hiyo hadi raundi ya tano inamalizika, Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB na kinywaji safi cha Azam Cola kinachosisimua koo, inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 10 sawa na Yanga iliyo nafasi ya pili huku Simba ikiwa kileleni kwa pointi 13 ilizojikusanyia.

HOMA YA PAMBANO LA WATANI… MAMA LORAA AWAAHIDI ‘MADOLA’ WACHEZAJI YANGA WAKIUA MNYAMA


SHABIKI na mwanachama maarufu wa Yanga, Catherine Ambakisye ‘Mama Loraa’ amewaahidi dola za Kimarekani wachezaji wa Yanga wakiifunga Simba wiki ijayo. Watani wa jadi katika soka la Tanzania, Simba na Yanga watakutana Oktoba 1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Na Mama Loraa katika kuwahamasisha wachezaji wa Yanga, ametenga dola 600 za Kimarekani, zaidi ya Sh. Milioni 1.2 kwa ajili ya zawadi wachezaji iwapo watamfunga mtani.
Mama Loraa (kushoto) akiwa na Baby Madaha (katikati) na Isabella Mpanda (kulia)
“Mimi ni shabiki wa Yanga damu. Nimeona umuhimu wa mechi ya Oktoba 1 (2016 dhidi ya Simba). Hivyo nikaona nitoe chochote kidogo kuchochea morali. Nina imani hiki kidogo nimeahidi, lakini morali inaweza kuwa kubwa. Ninaomba Yanga washinde,”amesema.
Akifafanua, Mama Loraa alisema kwamba ametenga dola 600 kununua hadi mabao matatu yatakayofungwa na wachezaji wa Yanga, kila moja kwa dola 200. Lakini Mama Loraa amesema atatoa zawadi hiyo iwapo tu Yanga itashinda au kutoa sare, lakini hatatoa hata senti moja iwapo itafungwa hata 2-1, 3-2, 4-3. “Washinde hata iwe 3-2 nitanunua kila bao kwa dola 200,”amesema na kuwataka wapenzi wengine na wanachama wa Yanga kujitokea kuongeza ofa zao ilio kuwahamasisha wachezani wa timu yao wawafunge mahasimu Oktoba 1, Uwanja wa Taifa.

KOCHA ARSENE WENGER ALITUA ARSENAL MIAKA 20 ILIYOPITA, ILIKUWA NI MWAKA 1996 WAKATI HUO AKITOKEA NAGOYA GRAMPUS EIGHT YA NCHINI JAPAN.






























 

 



ONGALA


Majimaji ya Songea wako jijini Dar es Salaam, tayari kuivaa Simba Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.

Pamoja na kuonekana kusua katika mechi zote za mwanzo, Majimaji wanaonekana wamepania kuifunga Simba.

Wamepolekewa vizuri na wadau mbalimbali ambao wangependa Simba ishindwe na kupewa huduma bora kabisa.

Majimaji wamefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana, hali inayoonyesha kuwa wana maandalizi makini hasa.

Kama hiyo haitoshi, wamekamilisha mipango yao ya kumrejesha kocha wao wa zamani, Kali Ongala.

Ongala ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Abajalo ya Sinza na Yanga, aliondoka baada ya kuiwezesha kubaki Ligi Kuu Bara msimu huu.



Lakini taarifa kutoka ndani ya Majimaji, zinaeleza amerejea na ataanza kuonekana kwenye benchi la timu hiyo Jumamosi.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017



SeeBait



Kuona Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Chuo Kikuu 2016/2017,



Kwa Chuo  Kikuu Cha Udom  <<bonyeza Hapa>>



Kwa Chuo  Kikuu Cha Ifm <<bonyeza Hapa>>



Kwa Chuo Kikuu Marian << Bonyeza Hapa>>



Kwa Chuo Kikuu Cbe        << Bonyeza Hapa>>



Kwa Tumaini-mbeya     << Bonyeza Hapa>> & <<hapa>>



Kwa Chuo Kikuu Mum         << Bonyeza Hapa>>



Kwa Chuo Mum(Diploma) <<Bonyeza Hapa>>



Kwa Chuo- Stella Maris   << Bonyeza Hapa>>



Kwa Chuo- Kampala-kiu  << Bonyeza Hapa>>

Orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na UDOM mwaka wa masomo 2016/2017

SeeBait
Kupata majina ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma ngazi ya Shahada, katika mwaka wa masomo 2016/2017, <<Bonyeza hapa>>
Reviewed by RICH VOICE on Septemba 22, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...