Thursday, September 15, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15

SeeBait

\

Thursday, September 15, 2016

Waziri wa Ujenzi atoa miezi sita kumaliza upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza

SeeBait

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mkandarasi Nyanza Road Construction inayojenga barabara ya Furahisha hadi Pasiansi KM 2.8 wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo, jijini Mwanza.


*****

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya Beijing Construction Engineering Group anayejenga uwanja wa ndege wa Mwanza kumaliza kazi ya upanuzi wa uwanja huo ifikapo mwezi Februari Mwakani.


Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo alipokuwa akikagua kazi ya ujenzi na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza pamoja na daraja la watembea kwa miguu lililopo maeneo ya furahisha, jijini Mwanza.


Profesa Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi na upanuzi wa uwanja huo kutaimarisha hali ya usafiri wa anga kwa wakazi wa Mwanza na mikoa mingine na hivyo kukuza shughuli za kibiashara nchini.


“Hakikisheni upanuzi wa uwanja wa ndege huu unakamilika haraka ili kurahisisha na kuboresha huduma za usafirishaji kiwanjani hapa”, alisema Waziri Mbarawa.


Aidha, Profesa Mbarawa amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Nyanza Road Construction kumaliza kwa wakati upanuzi wa barabara ya ‘Mwanza-Airport’ eneo linaloanzia Ghana Quarters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza KM 9.15 pamoja na daraja la watembea kwa miguu la furahisha ili kukuza uchumi na kupunguza kero ya msongamano wa magari katika jiji la Mwanza.


Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amewataka wananchi wa Mwanza kutoharibu miundombinu ya barabara na madaraja ambayo Serikali inatumia gharama kubwa katika utengenezaji wake.


“Naomba muitunze na kuithamini miundombinu hii kwani Serikali inatumia gharama kubwa katika kutengeneza na kukarabati”, alisisitiza Prof. Mbarawa.


Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza ni mkakati wa Serikali kuhakikisha ujenzi wa uwanja huo unaboreshwa kuwa wa kisasa na wa kimataifa ili kuwezesha ndege kubwa kutua kwa wingi na kuwa kiungo muhimu kwa mikoa 10 ya kanda ya Ziwa na Kati.

Mkandarasi wa kampuni ya Nyanza Road Construction inayojenga barabara ya Furahisha hadi Pasiansi akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo jijini Mwanza.


Thursday, September 15, 2016

Serikali yatoa majibu ya hatua iliyofikia kuhusu viwanda ilivyovibinafsisha

SeeBait

Serikali inatekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli la kuhakikisha viwanda vilivyobinafsishwa vinafanya kazi linatekelezwa tangu mwezi Novemba mwaka 2015.


Hayo yalibanishwa jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Manyoni Mhe. Yahaya Massare lililohusu utekelezaji wa ahadi ya Rais kuvirudisha viwanda vyote vilivyobinafsishwa lakini havifanyi kazi.


Waziri Mwijage alisema kuwa Serikali kupuitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inaendelea na zoezi la kuchambua mikataba ya mauzo kwa viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo ama havifanyi vizuri au vimesimamisha uzalishaji kabisa.


Waziri alibainisha kuwa timu ya wataalamu toka Wizara ya Viwanda na Ofisi ya Usajili wa Hazina walifuatilia na kufanya tathimini kwa kutembelea kiwanda baada ya kiwanda hatua ambayo inasaidia kutafuta ufumbuzi wa matatizo yaliyopelekea kiwanda kutofanya kazi.


Aidha, Waziri Mwijage alisema kuwa uchambuzi wa mikataba ya viwanda hivyo unafanyika kwa ushirikiano na Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na Wizara za kisekta ikiwemo Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Nishati na Madini, pamoja na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.


Hata hivyo, Waziri Mwijage alisema kuwa katika kutekeleza ahadi hiyo ya Rais, Serikali imetwaa Kiwanda cha Chai Mponde kilichopo wilaya ya Lushoto mkoani Tanga ambacho mwekezaji amekiuka makubaliano ya mkataba.


Mbali na hayo, akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Emmanuel Mwakasaka lililohusu mpango wa Serikali kujenga maabara ya kupima ubora na kiwango cha asali inayozalishwa hapa nchini.


Waziri Mwijage alisema kuwa Serikali inaendelea kuhimiza ujenzi wa viwanda nchini ikiwemo viwanda vya asali na kuhakikisha vinakuwa na maabara zinazoweza kupima viwango vya msingi.


Waziri Mwijage aliongeza kuwa kuhusu ujenzi wa maabara mkoani Tabora, Wizara itahakikisha wawekezaji wanaofuatilia ujenzi wa viwanda vya asali wanakuwa na maabara za kupima viwango vya msingi vya msingi na kuiachia TBS kuweka viwango vya kitaifa na kudhibiti viwango hivyo.


Na Beatrice Lyimo, MAELEZO, Dodoma

 

 

Thursday, September 15, 2016

Kompyuta zenye majibu ya waliopima ukimwi zaibwa

SeeBait


Kompyuta mpakato zenye majibu ya watu waliopima ukimwi pamoja na majina yao zimeibwa mkoani Tabora.


Kompyuta hizo zipatazo 30 zenye thamani ya Sh70 milioni, zimeibwa kwenye ofisi ya shirika lisilo la kiserikali la Jhpiego linaloshughulika na masuala ya Ukimwi na tohara.


Kompyuta hizo zimeibwa mwishoni mwa wiki kwenye ofisi hiyo iliyo jirani na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa amesema tayari taarifa za tukio hilo zimewafikia  na wanaendelea na uchunguzi wa kina kufahamu kilichotokea.


Inadaiwa kuwa kompyuta hizo, zina majina ya watu waliopima VVU na majibu yao.


“Kinachotatiza ni kwamba kama majina ya watu wenye virusi yakijulikana itakuwa ni utata mkubwa kwani ofisi hiyo itakuwa imewaweka katika wakati mgumu pasipo wao kupenda,” kilisema chanzo chetu cha habari.


Mkurugenzi wa Jhipego, Dk Albert Komba amethibitisha kutokea kwa wizi huo.

 

 

Thursday, September 15, 2016

JK Atoa Ya Moyoni Kuhusu Rais Magufuli Kutokwenda Zambia

SeeBait

Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ameunga mkono uamuzi wa Rais John Magufuli kuahirisha safari kwenda nje ya nchi ili kushiriki katika maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.


Kikwete amesema uamuzi huo ni wa busara kwa kuwa Serikali inatakiwa kufanya juhudi za makusudi kushughulikia tatizo hilo.


Kikwete aliyemtumia salamu za pole Dk Magufuli na waathirika wa tukio hilo, amesema misaada ya haraka na dharura inahitajika ili waathirika waendelee kupata huduma zote muhimu hasa za kibinadamu.


Kiongozi huyo mstaafu ameyasema hayo  katika hafla ya makabidhiano ya nyumba 22 za watumishi wa afya, 10 zikiwa Chalinze, mbili Bagamoyo na nyingine 10 Mafia zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa mkoani Pwani.


“Ndugu zangu pamoja na leo hii tunakabidhiana nyumba 22 za watumishi wa afya mkoani kwetu, naomba tusimame tuwakumbuke wenzetu waliopoteza maisha katika tetemeko la ardhi huko Bukoba na pia natumia fursa hii kutoa pole kwa waathirika wote na Rais Dk Magufuli,” amesema.


Ameongeza kuwa: “kiukweli amefanya uamuzi wa busara kuahirisha safari yake ili kushiriki katika maafa haya.”


Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika Kituo cha Afya Msoga, Chalinze.

 

 

Thursday, September 15, 2016

Serikali Yabariki Wenye Jinsia Mbili Kuchunguzwa

SeeBait

 

Mamlaka  ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali itakuwa na uwezo na mamlaka ya kuchunguza watu waliozaliwa na jinsi mbili na kubaini jinsi tawala yenye nguvu zaidi. 


Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2016, uliopitishwa juzi usiku saa nne bungeni unampa Mkemia Mkuu mamlaka ya kuchunguza na kubaini jinsi ya mtu na kutatua utata kwa mtu atakayekuwa amezaliwa na jinsi mbili.


“Waheshimiwa wabunge naona wengi wenu mnadhani mkemia mkuu kazi yake ni kuchunguza vinasaba kubaini uhalali wa mzazi na mtoto, maana naona wabunge wengi wamelishabikia hilo, lakini katika teknolojia ya vinasaba yanahusu pia utambuzi wa jinsi, watu unakuta wanawake au wanaume wanazaliwa jinsi ya kike na kiume, kwa hiyo tunaangalia jinsi tawala ni ipi ina nguvu,” alisema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.


Ummy alikuwa akijibu michango ya wabunge waliochangia wakati wa kujadili Muswada wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu 2016 kabla ya kuupitisha juzi usiku, waliotaka mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu kutoa elimu kwa wananchi juu ya shughuli zake.


Alisema kwa sheria hiyo, sasa mkemia mkuu kupitia maabara yake anaweza kusema jinsi ya kike au ya kiume ndio yenye nguvu, lakini pia kuna suala la kuhakikisha utambuzi wa mwanadamu hasa wakati yanapotokea majanga pamoja na watu wanaosafiri kwa makundi.


Alikubaliana na wabunge kuwa iko haja ya kuwaelimisha wananchi juu ya kazi za maabara ya mkemia mkuu ambao wengi wao wanadhani inafanya kazi hiyo tu ya kubaini vinasaba vya mzazi na mtoto, lakini sasa wafahamu hata waliozaliwa na jinsi mbili wanaweza kutegua utata huo kwa kubaini jinsi tawala au jinsi yenye nguvu zaidi kama ni ya kiume au ya kike.


Alisema Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekuwepo kihistoria tangu mwaka 1890 na imekuwa chombo cha kiserikali cha uchunguzi cha kikemia wa kimaabara kwa bidhaa mbalimbali na kuongeza kuwa imekuwa ikifanya uchunguzi wa kikemia wa vyakula, dawa na vipodozi hasa pale inapotokea utata au kuhusisha masuala ya kesi za jinai.


Akifafanua zaidi, alisema kwa upande wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wao wanafanya udhibiti wa ubora wa chakula, dawa na vipodozi na maabara hii inafanya uchunguzi wa kikemia.


“Maabara ya Mkemia Mkuu kazi yake ni kufanya uchunguzi wa kikemia, vinasaba, kesi za jinai na sayansi jinai. Chombo hiki hakipimi kudhibiti ila kufanya uchunguzi kwa ajili ya vitu vyenye maslahi ya taifa au masuala yenye utatanishi na ushindanishi,” alisema waziri huyo.


Akitoa mfano wa mahindi, alisema kulikuwa na tatizo la sumu kuvu, kwa hiyo mkemia mkuu anafanya uchunguzi wa kimaabara na kusema wamekuta mahindi yana sumu au la, au anaweza mfanyabiashara kuleta maziwa ya mtoto TFDA ikapata mashaka, mkemia mkuu atayafanya uchunguzi wa maabara atasema kama kuna sumu ama kuna kemikali isiyo salama kwa matumizi wa binadamu.


“Baada ya uchunguzi wa kimaabara mwenye jukumu la kusema mahindi haya yasiuzwe au maziwa haya yasiuzwe ni TFDA na sio maabara ya mkemia mkuu. Vile mfanyabiashara anaweza kuleta bidhaa, TFDA ikaitilia mashaka, kwa hiyo huyu mwenye bidhaa anaweza kukata rufaa kwa mkemia mkuu ili apimiwe bidhaa yake kuithibitishia TFDA kuwa bidhaa yake ni salama,” alisema.


Waziri Ummy alikuwa akijibu hoja za wabunge, ambao walikuwa wana hofu kuwa Maabara ya Mkemia Mkuu inaweza kuingilia kazi za taasisi kama TFDA na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).


Alizungumzia pia kuhusu kuipa mamlaka ya mwisho maabara hiyo, akisema katika nchi zote duniani zenye maabara hizo, lazima serikali iwe na msemaji wa mwisho wa uchunguzi wa masuala ya kimaabara na kikemia, vinasaba, sayansi jinai na kesi za jinai, lakini pia haifuti sheria wala maabara zingine za uchunguzi zilizoanzishwa kwa mujibu wa sheria mbalimbali.


Kuhusu kutenga bajeti ya kutosha, Ummy alisema serikali imepokea maoni ya wabunge na kuwa baada ya kupitisha muswada huo maabara hiyo imepewa hadhi ya mamlaka na sasa imepewa hadhi na hivyo fungu lake lazima liwe zuri kwa ajili kuendesha shughuli za maabara lakini pia kuajiri watumishi 400 kwani waliopo sasa 192 hawatoshi.


Waziri Ummy alisema wamepokea ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, kufanya uchunguzi wa matumizi ya shisha na kuongeza kuwa tayari mkemia mkuu alifanya uchunguzi na kubaini watumiaji wa shisha wanachanganya bangi, heroine na kokeni na ndio maana serikali ilipiga marufuku kuitumia.


Hata hivyo, alisema sasa itajikita zaidi kuchunguza ili kubaini viambata kiasi gani vilivyopo katika shisha na kwa nini serikali iendelee kupiga marufuku matumizi ya shisha nchini.



Thursday, September 15, 2016

Gavana BOT afichua siri ya kilio cha fedha kupotea mtaani

SeeBait


Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa.


Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema kuwa kwakuwa taasisi hiyo ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa hakuna fedha iliyopotea bali fedha zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa njia ya udanganyifu kwakuwa sasa Serikali imebana mianya hiyo.


“Hakuna fedha iliyopotea, Serikali imebana shughuli za watu na ‘mission town’ sasa shughuli zote zinafanywa na Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea, lakini kwetu hazijapotea,” alisema Profesa Ndulu.


Hata hivyo, Profesa Ndulu alikiri kupungua kwa fedha katika mabenki nchini hali iliyopelekea kupunguza kasi ya utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za mashirika ya umma na taasisi kutoka benki za biashara kwenda BoT.


“Fedha hizo zitarudi katika benki hizo wakati zitakapopelekwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali,” Profesa Ndulu aliahidi.


Katika hatua nyingine, Gavana huyo wa Benki Kuu alisema kuwa uchumi unatarajiwa kukuwa kwa asilimia 7.2 mwaka huu, huku akibainisha kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea ukuaji huo ni  ongezeko la uzalishaji wa umeme na saraju.


Akizungumzia hali ya deni la taifa, alisema kuwa deni la taifa la ndani limeongezeka kutoka shilingi  trilioni 8.6 Mwezi Desemba mwaka jana hadi shilingi trilioni 10 mwezi Juni mwaka huu.


Profesa Ndulu alibainisha kuwa wakati deni linalotokana na kukopa ndani likipaa, deni linatokana na ukopaji wa limepungua baada ya Serikali kupunguza ukopaji nje ya nchi.

 

Thursday, September 15, 2016

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Beno Ndulu Atoa Taarifa Kuhusu Hali Halisi ya Uchumi wa Tanzania

SeeBait


1.0    Hali ya Uchumi wa tanzani

1.1  Ukuaji wa Uchumi

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, hali ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania imeendelea kuwa ya kuridhisha. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ukuaji wa Pato la Taifa unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 5.5 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.7 kipindi kama hicho mwaka 2015 (Kielelezo Na. 1).

Kielelezo Na. 1: Mwenendo wa Ukuaji wa Uchumi Robo ya Kwanza ya Mwaka (Asilimia)

Chanzo: NBS, Ukokotoaji - Benki Kuu


Shughuli zilizochangia ukuaji huu wa uchumi kwa kiasi kikubwa ni pamoja na kilimo (asilimia 11.7), biashara (asilimia 10.6), uchukuzi (asilimia 10.1), sekta ya fedha (asilimia 10.1) na mawasiliano (asilimia 10.0). Shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi ya juu zaidi katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ni sekta ya fedha (asilimia 13.5), mawasiliano (asilimia 13.4), na utawala wa umma (asilimia 10.2) (Kielelezo Na. 2).


Kielelezo Na. 2a: Ukuaji wa Shughuli Mbalimbali za Uchumi Robo ya Kwanza ya Mwaka (Asilimia)








Kielelezo Na. 2b: Mchango wa Shughuli Mbalimbali za Uchumi katika Ukuaji wa Uchumi Robo ya Kwanza ya Mwaka (Asilimia)






1.2 Matazamio ya Ukuaji wa Uchumi Mwaka 2016

Kwa kuangalia viashiria mbalimbali inaonekana kuwa hali ya uchumi wetu itaendelea kuimarika katika mwaka 2016. Kwa mfano:


Uzalishaji wa umeme nchini katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 umeongezeka kwa asilimia 14.5 kufikia kWh milioni 3,454.2 ikilinganishwa na kWh milioni 3,016.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. Ongezeko hili limetokana kwa kiasi kikubwa na jitihada za serikali katika kutumia nishati ya gesi kwenye uzalishaji umeme kufuatia kukamilika kwa bomba la gesi kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam pamoja na mtambo wa Kinyerezi I.
 Umeme unaozalishwa kwa kutumia nishati ya gesi umeongezeka kwa asilimia 52.2 (Kielelezo Na. 3). Hali hii itasaidia kuongezeka kwa uzalishaji viwandani pamoja na sekta nyingine zinazotegemea nishati ya umeme, na hivyo kuchangia katika kuongeza kwa pato la Taifa.  Gharama ya umeme itashuka pia.


Kielelezo Na. 3: Mwenendo wa Uzalishaji Umeme Nchini

Januari - Juni


Uzalishaji wa saruji katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 umeongezeka kwa asilimia 7 kufikia tani elfu 725.4 ikilinganishwa na tani elfu 680.1 zilizozalishwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2015. Hali hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la uzalishaji wa kampuni ya Dangote ambayo ina uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka (Kielelezo Na. 4).  
Ni matarajio yetu kwamba uzalishaji katika kiwanda cha Dangote chenye uwezo wa tani milioni 3 na katika viwanda vingine vya saruji nchini utaongezeka katika kipindi kilichobaki cha mwaka 2016 kwani mahitaji ya nchi bado ni makubwa kuliko uzalishaji ulivyo hivi sasa.  Aidha kuna miradi mikubwa mingi ya hapo baadaye itakayokuwa na mahitaji makubwa ya saruji kama vile mradi wa reli ya kati.


Kielelezo Na. 4: Mwenendo wa Uzalishaji Sarujii

Januari – Machi


Uagizaji wa malighafi za viwandani kutoka nje umeongezeka kwa asilimia 19.4 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 kufikia Dola za Marekani milioni 520.2 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2015 (Kielelezo Na. 5)
Hali hii imechangiwa na kuendelea kukua kwa shughuli za uzalishaji viwandani. Ukuaji huu utaendelea kuchangia pato la Taifa kiujumla katika mwaka 2016.


Kielelezo Na. 5: Mwenendo wa Uagizaji Malighafi za Viwandani

Januari – Juni


Mauzo ya bidhaa za viwanda nje ya nchi yameendelea kukua kwa kasi ya kuridhisha. Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 mauzo ya bidhaa nje ya nchi yalifikia kiasi cha Dola za Marekani milioni 728.5, sawa na ongezeko la asilimia 15.6 ikilinganishwa na kiasi kilichouzwa kipindi kama hicho mwaka 2015 (Kielelezo Na. 6).


Kielelezo Na. 6: Mwenendo wa Uuzaji wa Bidhaa za Viwandani Nje ya Nchi

Januari – Juni



Makusanyo ya kodi katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 yameendelea kuwa bora zaidi ikilinganishwa na nusu ya kwanza ya mwaka 2015, ikiashiria kuimarika kwa usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya serikali na kuendelea kuimarika kwa hali ya

uchumi wa nchi.


Mikopo itolewayo na mabenki ya biashara kwenye sekta binafsi, imeendelea kuongezeka kwa kasi ya kuridhisha katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 kwa Shilingi bilioni 1,167.2, japo ni pungufu ikilinganishwa na ongezeko la Shilingi bilioni 1,577.5 la mwaka 2015. Ongezeko hili linaendana na malengo ya sera ya mwaka 2015/16 ambayo yanajumuisha utulivu wa mfumuko wa bei (Kielelezo Na. 7).


Kielelezo Na. 7: Mwenendo wa Ongezeko la Mikopo kwa Sekta Binafsi

Januari - Juni


Chanzo: Benki kuu


Miradi mikubwa ya viwanda na miundombinu inayoendelea na inayotarijiwa kuanza kazi siku za usoni itachangia katika kuimarisha uchumi. Hii ni pamoja na:

  1. Ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha  kisasa (Standard gauge)

  2. Ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda ambalo litahusu vile vile upanuzi wa bandari  ya Tanga

  3. Ujenzi wa Export Processing Zone ya Kurasini – itakayokuwa mhimili wa biashara kati ya China na Ukanda huu wa Afrika

  4. Mradi wa kuzalisha megawati 240 za umeme wa Kinyerezi II unaoendelea kujengwa.

  5. Miradi ya kupanua viwanja vya ndege nchini kwa mfano- Dodoma, na mingine inayoendelea -katika viwanja vya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya n.k.

  6. Ujenzi wa maghala ya taifa ya kuhifadhi chakula yenye uwezo wa kuhifadhi tani 350 yatakayojengwa kwa msaada wa Serikali ya Hungary katika sehemu mbalimbali nchini hususan katika mikoa inayozalisha mazao ya nafaka kwa wingi.

  7. Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara ambacho kipo mbioni kuzalisha kulingana na uwezo wake (full capacity);

  8. Kiwanda cha kutengeneza marumaru cha Mkuranga, Pwani ambacho ujenzi wake unaendelea

  9. Kiwanda cha kuzalisha mbolea mkoani Lindi - kinajengwa

  10. Kiwanda cha bidhaa za chuma – mkoani Pwani ambacho kiko mbioni kukamilika.

Kwa kuzingatia mwenendo wa viashiria mbalimbali vya shughuli za uchumi, ni dhahiri kwamba hali ya uchumi wa Tanzania ni nzuri na inatoa matumaini makubwa kwamba shughuli halali za kiuchumi zinaendelea kutekelezwa kama ilivyotarajiwa hapo awali hivyo lengo la ukuaji wa pato la Taifa la asilimia 7.2 kwa mwaka 2016 litafanikiwa. 
Hii inachangiwa pia na ukweli kwamba serikali ya awamu ya tano imejipanga katika kuimarisha uchumi endelevu usiokuwa na mianya ya rushwa; usimamizi thabiti wa rasilimali za umma; na ujenzi wa miundombinu bora kwa lengo la kujenga uchumi wa viwanda chini ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.


1.3  Mwenendowa Mfumuko wa bei

Wastani wa mfumuko wa bei katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016 umeendelea kuwa mzuri ukiendelea kushuka hadi kufikia asilimia 5.5 mwezi Juni 2016 na asilimia 4.9 mwezi Agosti 2016 kutoka asilimia 6.8 mwezi Desemba 2015 (Kielelezo Na. 8). 
Kushuka huku kwa wastani wa mfumuko wa bei kulichangiwa zaidi na bei zisizojumuisha bei za vyakula na nishati (core inflation) zikifuatiwa na zile za nishati na mafuta. Wastani wa mfumuko wa bei usiojumuisha bei za vyakula na nishati (core inflation), ambao ni kiashiria sahihi zaidi cha utekelezaji wa sera ya fedha, umeendelea kubaki katika viwango vya chini (wastani wa asilimia 2.8 katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2016) kutokana na hatua mbalimbali thabiti za sera ya fedha na bajeti katika kudhibiti ujazi wa fedha na ukwasi katika uchumi.


Mfumuko wa bei unatarajiwa kuendelea kubakia katika viwango vya tarakimu moja katika siku zijazo na kufikia lengo la muda wa kati la asilimia 5. 
Hii ni kutokana na matarajio ya hali nzuri ya hewa itakayochangia kupungua kwa kasi ya kuongezeka kwa bei za vyakula, pamoja na ongezeko dogo la bei ya mafuta nchini inayotokana na mwenendo wa bei ya mafuta katika soko la dunia, na utulivu wa thamani ya Shilingi. 
Pia, mwendelezo wa sera thabiti ya fedha, usimamizi mzuri wa matumizi na mapato ya Serikali, na upatikanaji wa umeme utokanao na gesi ambao utasaidia kupunguza gharama za uzalishaji viwandani vitaendelea kuimarisha utulivu wa mfumuko wa bei. 
Hata hivyo ni muhimu kuzingatia kuwa upungufu wa mavuno ya mazao ya chakula uliojitokeza kwa baadhi ya nchi za ukanda wa kusini mwa Afrika unaweza kusababisha shinikizo la mfumuko wa bei katika siku za usoni.



Kielelezo Na. 8: Mwenendo wa Mfumuko wa Bei (Badiliko la Miezi 12)


Chanzo: Benki kuu

1.4 Utekelezaji wa Sera ya Fedha

Ili kufikia malengo ya serikali ya kuimarisha uchumi na kudumisha utulivu wa mfumuko wa bei, Benki Kuu imeendelea kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti ukwasi ili uendane na mahitaji halisi ya uchumi. Ongezeko la fedha taslimu (reserve money) ambacho ni kipimo cha ukwasi kwenye uchumi limeendelea kubakia ndani ya malengo katika kipindi chote cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016. 
Katika kipindi hicho ujazi wa fedha taslimu ulikua kwa wastani wa asilimia 11.6; wakati ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) ulikua kwa wastani wa asilimia 14.4, ikiwa ni ndani ya makadirio ya ukuaji usiozidi asilimia 16.0 kwa mwaka 2015/16.

Wakati huohuo sekta ya fedha imeendelea kuchangia ukuaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kasi nzuri ya kutoa mikopo kwa wakati na kwa kiwango cha kutosha. Mikopo kwa sekta binafsi ilikua kwa wastani wa asilimia 21.3 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016, sawa na kiwango kilichopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2015. 
Mikopo mingi kwa sekta binafsi ilielekezwa kwenye shughuli za biashara kwa wastani wa asilimia 19.3 ya jumla ya mikopo yote, shughuli za watu binafsi wastani wa asilimia 19.0, uzalishaji viwandani wastani wa asilimia 10.6, uchukuzi na mawasiliano wastani wa asilimia 7.9, na shughuli za kilimo asilimia 7.8.

Benki Kuu inaendelea kutekeleza sera madhubuti ya fedha kwa kutumia zana mbalimbali za sera ili kuhakikisha kwamba mahitaji ya ukwasi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi yanafikiwa bila ya kuchochea mfumuko wa bei.


1.5     Mwenendo wa Thamani ya Shilingi ya Tanzania

Thamani ya Shilingi imeendelea kuwa tulivu katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, kufuatia hatua mbalimbali za sera ya fedha zilizochukuliwa na Benki Kuu katika kusimamia hali ya ukwasi kwenye uchumi pamoja na mwenendo wa uchumi ndani na nje ya nchi. 
Kuimarika kwa sekta ya nje kulikotokana na ongezeko la mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi na kupungua kwa thamani ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje kumechangia katika utulivu wa thamani ya shilingi. 
Kupungua kwa thamani ya bidhaa kutoka nje kumechangiwa zaidi na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. Katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mwaka 2016 Shilingi imekuwa ikibadilishwa kwa kati shilingi 2,180 hadi 2,190 kwa dola moja ya Marekani (Kielelezo Na. 9).


Kielelezo Na. 9: Mwenendo wa Thamani ya Shilingi


Chanzo:Benki kuu


Hali hii ya utulivu wa thamani ya Shilingi kwenye soko huru la fedha inadhihirisha kuwa sera thabiti za uchumi pamoja na mwenendo mzuri wa urari wa mapato ya fedha za kigeni, ndio jawabu la kulinda thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni na sio kudhibiti matumizi ya dola kama ambayo imekuwa ikidaiwa mara kwa mara. 
Nchi zenye udhibiti mkubwa wa fedha za kigeni mfano Afrika Kusini imeshuhudia kuyumba sana kwa thamani ya fedha yake tofauti na shilingi ya Tanzania.


Hivyo nguvu kubwa inapaswa ielekezwe katika kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta mbalimbali hususan zile zinazoboresha urari wa malipo ya nje kama vile utalii, viwanda, uchimbaji madini, kilimo n.k. Ikumbukwe kuwa uhuru wa kumiliki na kutumia fedha za kigeni nchini Tanzania uliwekwa kama hatua ya kukabiliana na hali iliyokuwepo miaka ya 1980 ya kuadimika sana kwa fedha za kigeni na mchango wa uhuru huo tumeuona katika kuwepo kwa fedha za kigeni za kutosha. 
Nchi zilizojaribu kuondoa uhuru huo, mfano Zambia, zimeshuhudia kutoweka kwa fedha za kigeni kwenda nje. Hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuhimiza na kuweka mazingira mazuri ya uzalishaji na kuondokana na fikra za kuingilia soko huru kama jawabu la kulinda thamani ya shilingi.


1.6  Mwenendo wa Sekta ya Kibenki

Katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016, sekta ya kibenki imeendelea kukua ikichangiwa na uanzishwaji wa taasisi mpya za kifedha ikiwemo Benki ya Waalimu Tanzania (Mwalimu Commercial Bank Plc) na Canara Bank (Tanzania) Limited. Takwimu za awali za tathmini ya hali ya mabenki yetu zinaonesha kuwa mabenki yetu ni imara na salama, yakiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha. Kufikia mwezi Juni 2016, kulikuwa na jumla ya benki na taasisi za fedha zinazosimamiwa na Benki Kuu zipatazo 65 zenye matawi 739 nchini kote.


Kiwango cha mitaji kikilinganishwa na mali iliyowekezwa (total capital to total risk weighted assets and off-balance sheet exposures) kilikuwa asilimia 17.17 kikilinganishwa na kiwango cha chini kinachotakiwa kisheria cha asilimia 12.0. Hali ya ukwasi ambayo hupimwa kwa kuangalia uwiano kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu na amana zinazoweza kuhitajika katika muda mfupi (liquid assets to demand liabilities) ulikuwa asilimia 37.03 ukilinganishwa na uwiano wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia 20 (Jedwali Na. 1).


Amana za wateja katika mabenki zilipungua kutoka shilingi trilioni 20.52 mwezi Desemba 2015 kufikia shilingi trilioni 20.24 mwezi June 2016. Miongoni mwa sababu zilizochangia kupungua kwa amana kwenye mabenki ni pamoja na uamuzi wa Serikali kuhamisha sehemu ya fedha za taasisi na mashirika ya umma kutoka mabenki ya biashara kwenda Benki Kuu ya Tanzania. Aidha mikopo (loans and overdafts) iliongezeka kutoka shilingi trilioni 15.28 mwezi Desemba 2015 hadi kufikia shilingi trilioni 15.67 mwezi Juni 2016.


Upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wasiofikiwa na mabenki umeendelea kuongezeka kutokana na ubunifu wa mipango ya utoaji wa huduma za malipo ya rejareja kupitia simu za mikononi, pamoja na huduma za uwakala wa mabenki (agent banking services).


Kiujumla kwa kuangalia viashiria vyote vya msingi hali ya ukwasi wa benki imeendelea kuwa ya kuridhisha. Benki Kuu katika kusimamia majukumu yake ya kisera, imeendelea kutoa mikopo ya muda mfupi kupitia “reverse repos” pamoja na kununua fedha za kigeni zinazotokana na mauzo ya bidhaa nje ya nchi kutoka kwenye benki. Kwa viashiria hivi ni dhahiri kwamba uamuzi wa serikali wa kuagiza fedha zake zote kuwekwa kwenye akaunti maalum Benki Kuu hakujasababisha sekta ya kibenki kutokuwa na ukwasi wa kutosha na kuacha kukopesha kwa sekta binafsi kama inavyofikiriwa na baadhi yetu.


Ni vyema jamii ya Watanzania ikafahamu kwamba akaunti ambazo fedha za mashirika zimehamishiwa Benki Kuu ni akaunti za kukusanya mapato tu. Akaunti za matumizi bado ziko katika benki za biashara ili kuyawezesha mashirika kufanya malipo kupitia akaunti hizo. Hivyo, bado benki za biashara ni kiungo muhimu kati ya mashirika ya umma na watoa huduma kwa mashirika hayo. Pia hali ya utoaji mikopo kama tulivyoona awali ni nzuri na watanzania wanaendelea kuhudumiwa na benki zetu kama inavyotarajiwa.


Jedwali Na. 1: Viashiria vya Uimara wa Sekta ya Fedha



1.7 Sekta ya Nje na Akiba ya Fedha za Kigeni

Katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2016, nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamisho mali nchi za nje (current account deficit) ilipungua kwa asilimia 61.7 na kufikia nakisi ya dola za Kimarekani milioni 970.4, kutoka nakisi ya dola za Kimarekani milioni 2,532.5 mwaka 2015. Kupungua huko kulitokana zaidi na ongezeko la thamani ya bidhaa za viwandani, mapato yatokanayo na utalii na huduma za usafirishaji nje ya nchi, pamoja na kupungua kwa thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ya nchi hususan bidhaa za mitaji, na bidhaa za matumizi ya kawaida. 
Katika kipindi cha miezi sita iliyoishia Juni 2016, kikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliotangulia, thamani ya bidhaa na huduma zilizouzwa nje ya nchi ziliongezeka kwa asilimia 14.2 na kufikia dola za Kimarekani milioni 4,473.2 wakati thamani ya bidhaa na huduma toka nje zilipungua kwa asilimia 18.3 na kufikia dola za Kimarekani milioni 5,360.7


Hazina ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha na kuendelea kukidhi mahitaji ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuongeza imani kwa wawekezaji katika uchumi wetu; japo kumekuwepo na ucheleweshwaji wa fedha za wahisani na mikopo ya kibiashara kutoka nje ya nchi.
 Hadi mwezi June 2016, akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Kimarekani milioni 3,870.3 ambazo zinatosheleza kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa takriban miezi 4. Wakati huo huo, rasilimali za fedha za kigeni za mabenki (gross foreign assets) zilikuwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 835.0

1.8  Deni la Taifa

Deni la Taifa limeendelea kuongezeka na kufikia dola za Kimarekani milioni 20,851 mwishoni mwa mwezi Juni 2016, kutoka dola za Kimarekani milioni 19,861 mwezi Desemba 2015. Deni la nje liliongezeka kwa asilimia 2.6 na kufikia dola za Kimarekani milioni 16,281 mwezi Juni 2016 (sawa na asilimia 77.8 ya deni la taifa), kutoka dola za Kimarekani milioni 15,864 mwezi Desemba 2015. Hii ilitokana na kuongezeka kwa mikopo mipya pamoja na malimbikizo ya malipo ya madeni. 
Katika deni hilo la nje, asilimia 83.4 ni deni la Serikali na taasisi za umma. Pamoja na ongezeko hilo, takwimu zinaonyesha kuwa deni letu bado ni stahimilivu. Kwa mfano, deni la nje kwa thamani ya sasa (Net Present Value) ni karibu ya asilimia 20 ya Pato la Taifa, ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 50 ya Pato la Taifa (Sept-15 DSA). Hii inaonyesha kuwa bado kuna nafasi kubwa ya kukopa bila kuhatarisha ustahimilivu wa deni letu.


Deni la ndani liliongezeka kufikia shilingi bilioni 10,038.4 mwishoni mwa mwezi Juni 2016 kutoka shilingi bilioni 8,597.0 mwezi Desemba 2015.
 Ongezeko hilo lilitokana na Serikali kukopa kupitia dhamana na hati fungani ajili ya kugharamia bajeti ya Serikali kwa mwaka 2015/16, ikichangiwa pia na kupungua kwa misaada na mikopo kutoka nje.


Jedwali Na 2 linaonyesha vyanzo vya fedha za Serikali na matumizi yake katika kipindi cha miezi 6 kuanzia Januari hadi Juni 2016. Kama inavyoonekana jumla ya mapato ya ndani ilikuwa shilingi bilioni 7,267 wakati matumizi ya kawaida (ukiondoa riba) yalikuwa shilingi bilioni 6,488, hivyo mapato yalitosha kulipia matumizi ya kawaida ya Serikali. Hii ni kuonyesha kwamba madeni ya nje na ndani yalitumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na kurejesha madeni yaliyopita.


Jedwali Na. 2: Vyanzo vya Fedha vya Serikali na Matumizi Yake (Shilingi bilioni)

 

Thursday, September 15, 2016

Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

SeeBait

VIJANA watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli na Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi wanne waliouawa na majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es Salaam hivi karibuni.


Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Salum Mohammed.


Walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, Huruma Shahidi, Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage.


Akisomewa mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24, mwaka huu eneo la Ubungo External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka maoni katika group linaloitwa Dsm 11 4u Movement, akisema ‘JPM sijui anawaza nini kichwani… hata samahani hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu mmoja aliyeamua kujilipua ufahamu wake’, ‘sijaona tatizo kwa hilo, ila kwa huyu bwana misimamo ambaye amesema msinijaribu na ilhali kajaribiwa na ubwabwa wa jubilee kusema yote’.


‘Siasa si chuki wala upinzani si uadui, ajifunze kushindana kwa hoja sio mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo na kichwa wala miguu ya polisi’.


Mshtakiwa Suleiman Saidi anadaiwa Agosti 25, mwaka huu maeneo ya Kigogo, kwa kutumia mtandao wa Facebook, aliandika ‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.


Katika kesi nyingine, mshtakiwa Juma Mtatuu akiwa eneo la Ocean Road, Agosti 24, mwaka huu anadaiwa kuwa alituma ujumbe katika Facebook akisema ‘Huyu hata akifa ataenda peponi, na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala, mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana  kule Kahama, tarehe moja naelekea Kahama kwa Ukuta, mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta, kifo kipo tuu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha’

 

KATIKA HABARI ZA KIMATAIFAA 

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Waasi wanaotaka kujitenga nchini Ukraine na vikosi vya serikali wanalaumina juu ya ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha vita yaliyotakiwa kuanza usiku wa kuamkia leo huko mashariki mwa nchi hiyo.Siku ya Jumanne waasi walitangaza hatua ya upande mmoja ya kusitisha vita ambapo waziri wa amambo ya nje wa Ujerumani aliyeitembelea nchi hiyo alisema siku iliyofuatia kwamba serikali pia imekubali kusitisha mapigano.Hii leo Televisheni ya Urusi imenukuu maafisa wa waasi wakisema kwamba vikosi vyao vilishambuliwa kwa makombora mapema asubuhi.Msemaji wa jeshi la Ukraine Ivan Arefyev amesema mapigano yalizuka usiku wa manane lakini waasi walitumia silaha ndogo ndogo na mabomu ya kurusha kwa mkono majira ya asubuhi.Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa na Ujerumani ambao ndio wasuluhishi wakuu katika mgogoro huo wa Ukraine walikutana jana na rais wa nchi hiyo na wanatarajiwa kuelekea upande wa mashariki hii leo.

 

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Hatua ya kusitisha mapigano nchini Syria imeendelea kuheshimiwa hii leo licha ya kuripotiwa mara kadhaa kutokea ukiukaji. Hata hivyo msaada wa kibinadamu haujaweza kufika katika nchi hiyo na umezuiwa katika eneo la mpakani na Uturuki. Shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria limesema kwamba tangu kuanza kwa usitishaji huo wa mapigano Jumatatu usiku hakujakua na dalili za malori ya msaada kuingia ndani ya Syria.Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kiasi malori 20 ya msaada yameegesha katika eneo la mpaka na Uturuki yakisubiri kuingia Syria.Mamia kwa maelfu ya wasyria bado wanakabiliwa na hali ya kuzingirwa au kuwepo katika maeneo yasioyoweza kufikika nchini humo.Serikali ya Syria inapinga hatua ya kuingizwa msaada nchini humo bila ridhaa yake wakati waasi wanataka msaada huo usiingizwe kupitia maeneo kadhaa yaliyoko chini ya vikosi vya rais Bashar al Assad.

 

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Kiasi wakimbizi milioni 3.8 na wanaoomba hifadhi ya uhamiaji walizikimbia nchi zenye mizozo na kuingia katika nchi nyingine zenye mizozo. Hayo yamesemwa na shirika la msaada la Oxfam katika ripoti yake iliyochapishwa hii leo.Shirika hilo limetowa mfano wa Yemen nchi inayokumbwa na vita na iliyo masikini katika Mashariki ya kati kwamba kuna kiasi watu milioni 2 wanaoishi kama wakimbizi wa ndani lakini nchi hiyo vile vile inawahifadhi wakimbizi kutoka nchi nyingine zenye  mizozo kama Eritrea,Ethiopia na hata Syria.Ripoti ya Oxfam imetolewa wiki moja kabla ya rais Barack Obama kuongoza mkutano wa kwanza wa kilele wa Umoja wa Mataifa juu ya wakimbizi mjini New-York.Obama anatarajiwa kuwatolea mwito viongozi wa dunia kuchukua hatua zaidi kuwasaidia wakimbizi katika nchi kama Lebanon,Uturuki,Kenya na Jordan.

 

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

 Serikali ya Uingereza imesema leo kwamba imetoa ruhsa ya kuendelea kwa mradi wenye utata wa nyuklia wa Hinkley baada ya Waziri Mkuu Theresa May kutoa maagizo ya kufanyika tathmini juu ya mradi huo.Katika taarifa waziri wa biashara Greg Clark ameeleza kwamba baada ya mapendekezo ya mradi huo wa Hinkley kufanyiwa mapitio  kitakachofuatia ni kuanzishwa msururu wa hatua za kuhakikisha usalama na kuhakikisha kwamba mradi huo haufanyiwi mabadiliko bila ya ridhaa ya serikali.Awali bodi ya kampuni ya umeme inayomilikiwa na serikali ya Ufaransa EDF iliidhinisha hatua ya kushiriki kwake katika mradi huo wa kusini magharibi mwa England na baadae serikali mpya ya Uingereza ikiongozwa na Theresa May ilitangaza kwamba inataka kuutathmini upya mradi huo.China inahodhi robo ya hisa za mjradi huo,na wachambuzi walionya kwamba Uingereza ingehatarisha uhusiano wake na nchi hiyo endapo ingeufutilia mbali mradi huo wa nyuklia.

 

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Benki ya Dunia imesema kwamba  fedha zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza  ni chini ya nusu ya kiwango kilichoahidiwa kutolewa na wafadhili hao baada ya vita kati ya kundi la Hamas na Israel mwaka 2014. Upungufu huo ni miongoni mwa sababu kadhaa zinazochangia kuulemaza uchumi wa Palestina ambako kiwango cha wasiokuwa na ajira katika Ukanda huo wa Gaza kimefikia asilimia 42 na asilimia 18 upande wa Ukingo wa Magharibi.Benki hiyo ya dunia pia imesema kwamba vizuizi vya Israel vinachangia kuurudisha nyuma uwezo wa Palestina kushindana kiuchumi na kuwafukuza wawekezaji wa kibinafasi.Taasisi hiyo ya fedha ya dunia imeshauri kwamba Israel iruhusu ujenzi zaidi wa majengo katika ukingo wa Magharibi na kupunguza vizuizi vyake Gaza.Ripoti hiyo iliyotolewa leo itawasilishwa kwa kamati maalum ya nchi wafadhili kwa ajili ya Palestina huko New-York wiki ijayo.

 

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema Ujerumani inahitaji mpango unaotekelezeka wa kuwajumuisha  wakimbizi katika mfumo wa nguvu kazi haraka iwezekanavyo. Hayo Bi Merkel ameyasema leo katima mkutano na makambuni muhimu ya Ujerumani, ambayo yamewaajiri wakimbizi 100 miongoni mwa zaidi ya milioni moja waliowasili nchini Ujerumani mwaka uliopita. Kansela Angela Merkel ambaye umaarufu wake umeshuka kutokana na sera yake ya kuwafungulia mlango wakimbizi, hapo jana alikutana mjini Berlin na wakurugenzi wa makampuni muhimu, akitaka kujua kwa nini hawachukui hatua, na kujadiliana nao juu ya namna ya kurekebisha hali hiyo. Makampuni mengi yanasema vikwazo vikubwa vya kuwaajili wakimbizi ni ufahamu haba wa lugha ya kijerumani, na kushindwa kwa wakimbizi hao kuthibitisha uhalali wao wa kuishi nchini Ujerumani kwa muda mrefu.

 

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic nchini Marekani Hillary Clinton amerudi tena katika kampeini ya uchaguzi baada ya kutibiwa maradhi ya homa ya mapafu yaliyomzuia kuonekana kwenye kampeini hizo kwa siku tatu na kusababisha kuibuka maswali juu ya kwa kiasi gani wagombea wa vyama vyote viwili Democratic na Republican wanavyoweza kuzungumzia juu ya afya zao.Kambi ya kampeini ya Clinton imejibu kwa kutangaza barua mpya ya daktari wake inayosema mgombea huyo ana afya ya kuweza kuongoza taifa.Kwa upande mwingine mgombea wa Republican Donuld Trump amesema hata yeye anapanga kutangaza hali yake ya kiafya ingawa haifahamiki lini atatoa maelezo hayo na kwa kiwango gani.

 

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Waandamanaji wameingia mitaano kote nchini Ufaransa hii leo katika hatua mpya ya maandamano ya kupinga  mageuzi ya sheria ya kazi yanayopendekezwa na serikali ya kisosholisti ingawa wapinzani wa mageuzi hayo wanaonekana kuishiwa nguvu.

Kadhalika waandamanaji wameingia mitaani katika mji wa mashariki wa Belfort ambako serikali imejikuta iko katika mvutano na kampuni kubwa ya ujenzi wa Treni la Alstom kuhusiana na hatma ya kiwanda hicho kinachokabiliwa na kitisho.Katika miezi ya nyuma maandamano mengi nchini humo yalikabiliwa na vurugu zilizozuka kati ya waandamanaji na polisi wa kupambana na ghasia ambapo kiasi watu 40 walijeruhiwa na wengine kukamatwa.Hata hivyo vyama vya wafanyakazi leo vimeitisha maandamano hayo mapya ingawa mwitikio wa waliojitokeza  umeonekana kuwa mdogo.Makampuni kadhaa ya ndege kama Rynair yametangaza kufuta safari zake kadhaa za ndege za kutoka au kuingia Ufaransa kufuatia mgomo huo

 ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

KATIKA HABARI ZA KIMICHEZO KWA HAPA NYUMBANI 

 

Wakati pambano la timu ya Mwadui dhidi ya Yanga likizidi kupamba moto, Kocha Mkuu wa Mwadui ya mkoani Shinyanga, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema atahakikisha anashinda mchezo wake dhidi ya wapinzani wake hao keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani humo.

Kocha Julio amesema kuwa kutokana na yeye kutangaza kustaafu soka mara baada ya msimu huu kumalizika atahakikisha kuwa anaifunga Yanga ili astaafu soka kwa heshima, kitu ambacho kinaweza kuwapa hasira zaidi Yanga kuelekea mchezo huo.




“Nimejipanga kuhakikisha kuwa Yanga wanapata kipigo na nitahakikisha kuwa tunawapa kipigo kikali ili watambue kuwa makocha wazawa ni wazuri kuliko Wazungu.

“Ifahamike tangu timu yangu ipande daraja Yanga haijawahi kunifunga kwenye uwanja wa nyumbani hivyo sitaruhusu historia ivunjwe bali nitahakikisha kuwa Yanga haondoki na pointi katika mchezo huo.

“Mimi sitishwi na ubora wa wachezaji wa Yanga bali nitahakikisha malengo niliyojiwekea yanatimia kwani kila mchezaji wangu nimempa majukumu maalumu ya kuhakikisha kuwa wachezaji wa Yanga hawaleti madhara kwenye lango letu hivyo lazima walifahamu hilo,” alisema Julio.

 

 

Katika kile kinachoonekana presha kuwa kubwa kuelekea mechi dhidi ya Simba, wikiendi hii, benchi la ufundi la Azam FC ambalo linaongozwa na makocha kutoka Hispania limekataa mazoezi yao kushuhudiwa na waandishi wa habari.

Leo asubuhi ikiwa ni siku mbili kabla ya mchezo huo ripota wa SALEHJEMBE alifika kwenye Uwanja wa Azam Complex kwa ajili ya kushuhudia kilichokuwa kikiendelea lakini akakutana na ukuta wa chuma.







Baada ya kufika uwanjani hapo aripota huyo aliambiwa hataruhusiwa kuingia ndani kushuhudia mazoezi hayo kwa kuwa tayari kocha ameanza mazoezi maalum kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru.

Imeelezwa kuwa kocha huyo aliwakubalia watu wa habari wa klabu hiyo pekee lakini wengine wote kutoka nje ya Azam FC hawakuruhusiwa kushuhudia kilichokuwa kikiendelea.

Mchezo huo ni mmoja wa mchezo mkubwa kwa kuwa Azam imekuwa ikitoa ushindani mkali katika miaka ya hivi karibuni tofauti na zamani ambapo ilionekana mechi kubwa ni za Yanga na Simba pekee.

 

 

 

Kikosi cha Yanga kimeondoka alfajiri ya leo jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza kisha Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC.

 







Yanga na Mwadui zanatarajiwa kukutana Jumamosi ya keshokutwa kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, mchezo ambao unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na upinzani wa timu hizo licha ya kuwa Yanga ndiyo ambayo inaonekana kuwa vizuri zaidi uwanjani kutokana na matokeo yake ya hivi karibuni.

Yanga iliondoka Dar es Salaam kwa ndege ya Fast Jet na tayari imetua Mwanza ambapo asubuhi hii ilikuwa ikifanya mchakato wa kuelekea Shinyanga.

Mwadui inanolewa na Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye tayari amesikika akijinadi kuwa lazima ataifanyia Yanga kwa kuifunga na kuwataka wale wanaodhani kuwa mabingwa hao watetezi wa Ligi kuu Bara watapata pointi tatu kirahisi mkoani humo, wanajidanganya.

Mwadui ipo katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 4 katika michezo minne wakati Yanga ina pinti saba katika michezo mitatu.



YANGA SC WAWASILI SHINYANGA, ILIBIDI WAPANDE HADI DALA DALA ILI KUWAHI

 

  KIKOSI cha Yanga SC kimewasili salama Shinyanga baada ya safari ya tangu asubuhi kutoka Dar es Salaam kuanzia angani hadi barabarani. Yanga walipanda ndege kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ambako walipanda basi hadi Shinyanga, tayari kwa mchezo wao wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Hata hivyo, baada ya kufika Mwanza, Yanga walilazimika kukodi Hiece mbili daladala za Uwanja wa Ndege, kwenda Mwanza mjini kupanda basi walilokodi kuwapeleka Shinyanga.

Basi la Yanga baada ya kuwasili hotelini mjini Shinyanga

Wachezaji wa Yanga wakiwa ndani ya ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza 

Kipa Deo Munishi 'Dida' nje ya basi leo wakati wa safari ya Shinyanga

Hapa wachezaji wa Yanga wanapanda daladala kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza kulifuata basi katikati ya mji kwa safari ya Shinyanga

Katibu Mkuu wa Yanga; Baraka Deusdedit amesema; “Nachoweza kusema basi lilichelewa kufika Uwanja wa Ndege kuchukua wachezaji, na hatukuona sababu ya kupoteza muda mwingi kulisubiri,”. “Tukaona tuchukue usafiri wowote wa haraka tulifikie kuliko kuwaacha wachezaji wanazagaa ovyo Uwanja wa Ndege, ndiyo tukakodi dala dala,”amesema Deusdedit akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo.   Yanga SC watakuwa wenyeji wa Mwadui FC Jumamosi Uwanja wa Kambarage, Shinyanga katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Kwa ujumla Ligi Kuu inaendelea wikiendi hii, mbali ya Yanga na kuwa wageni wa Mwadui Shinyanga – Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Azam FC watamenyana na Simba SC na Mbeya City na Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Mtibwa Sugar na Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Ruvu Shooting na Mbao FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Maji Maji na Ndanda FC Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Jumapili kutakuwa na michezo miwili, Stand United wakiikaribisha JKT Ruvu Stars Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na African Lyon wakimenyana na Toto Africans Uwanja wa Uhuru.

 

 

STARS YAPOROMOKA VIWANGO VYA
Kikosi cha Taifa Stars


Shirikisho la soka Duniani, FIFA limetoa orodha ya viwango vya ubora kwa mataifa mbalimbali duniani kwa mwezi Septemba.

Orodha inaonesha kwamba, Tanzania imeporomoka kwa nafasi nne kutoka 124 hadi kushika nafasi ya 132.

Kufungwa dhidi ya Nigeria katika mchezo uliokuwa wa kusaka tiketi ya kufuzu Afcon mwaka 2017 pengine ndiyo sababu kubwa ya Tanzania kuporomoka.

Uganda bado wameendelea kuwa bora Afrika Mashariki na ukanda wote wa CECAFA kwa ujumla wakishika nafasi ya 65 duniani na 15 barani Afrika.

Rwanda wanafuata kwa karibu baada ya kupanda mpaka nafasi ya 107 kutoka nafasi ya 121.

Barani Afrika, Ivory Coast wameendelea kuwa kileleni, huku wakishika nafasi ya 34 duniani, wakifuatiwa na Waarabu wa Algeria, Senegal na Ghana.

Kinara wa ulimwengu wanabaki kuwa Argentina wakfuatiwa kwa karibu na Ubelgiji, Ujerumani, Colombia na Brazil.

 

KIMATAIFA MICHEZO 

 

EUROPA LIGI: LEO MAN UNITED KUANZA BILA ROONEY!

,

==MOU - HATUKUTAKA TUWEMO ILA TUTAWANIA UBINGWA!

MOU-CARRINGTONKEPTENI wa Manchester United Wayne Rooney hayumo kwenye Kikosi cha Timu hiyo kilichoruka kwenda Rotterdam kucheza na Klabu ya Netherlands Feyenoord katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI.

Wengine ambao hawamo kwenye Kikosi hicho cha Wachezaji 20 ni Luke Shaw, Antonio Valencia na Jesse Lingard.

Maneja Jose Mourinho amesema Rooney amecheza Mechi zote za England na Man United na hivyo amepumzishwa ile awe freshi kwa ajili ya tripu yao ya Ugenini hapo Jumapili wakicheza kwenye EPL, Ligi Kuu England na Watford.

Kuhusu ushiriki wao kwenye Mashindano haya, Morinho amekiri Klabu haikutaka kuwemo lakini maadamu wamo basi watawania kutwaa Ubingwa.

Ameeleza: "Si ndoto ya kila Mchezaji mkubwa lakini hatumo CHAMPIONZ LIGI. Lazima tuyatizame Mashindano haya kwa heshima. Tunataka tufanye vyema!"

Mbali ya Marcus Rashford kuanza Mechi hii kama Mourinho alivyodokeza, wengine wanaotarajiwa kucheza ni Marcos Rojo atakaechukua nafasi ya Luke Shaw pamoja na Michael Carrick, Matteo Darmian, Timothy Fosu-Mensah na Memphis Depay.

=============

JE WAJUA?

Man United imeshacheza na Feyenoord mara 2, kwenye Kundi lao la UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 1997/98, na Man United kushinda Mechi zote mbili ikiwemo 3-1 huko Uwanjani De Kuip ambako Andy Cole alipiga Hetitriki.

==============

Wakati huo huo, Feyenoord wamelazimika kupunguza uwezo wa Uwanja De Kuip na kuwa na Watazamaji 30,000 tu ili kukwepa Adhabu zaidi toka UEFA kwani kwa sasa wapo kwenye Angalizo baada ya fujo za Mashabiki wao Msimu uliopita na kupunguzwa huko kutasaidia udhibiti wa fujo za Mashabiki. 

Manchester United - Kikosi cha Wachezaji 20: De Gea, Romero, Johnstone, Darmian, Bailly, Blind, Fosu-Mensah, Rojo, Smalling, Carrick, Fellaini, Herrera, Mata, Memphis, Pogba, Schneiderlin, Young, Ibrahimovic, Martial, Rashford.

UEFA EUROPA LIGI

Mechi za Ufunguzi

Alhamisi Septemba 15

KUNDI A: Feyenoord v Manchester United, Zorya Luhansk v Fenerbahçe

KUNDI B: Young Boys v Olympiacos, APOEL v Astana

KUNDI C: Mainz v St-Étienne, Anderlecht v Qäbälä

KUNDI D: AZ Alkmaar v Dundalk, Maccabi Tel-Aviv v Zenit

KUNDI E: Viktoria Plzeň v Roma, Astra Giurgiu v Austria Wien

KUNDI F: Rapid Wien v Genk, Sassuolo v Athletic Club

KUNDI G: Standard Liège v Celta Vigo, Panathinaikos v Ajax

KUNDI H: Konyaspor v Shakhtar Donetsk, Braga v Gent

KUNDI I: Salzburg v Krasnodar, Nice v Schalke

KUNDI J: QarabaÄŸ v Slovan Liberec, PAOK v Fiorentina

KUNDI K: Inter Milan v Hapoel Beer-Sheva, Southampton v Sparta Praha

KUNDI L: Osmanlıspor v Steaua Bucureşti, Villarreal v Zürich

 

 

MABINGWA REAL WANUSURIKA, SPURS YALALA KWAO, LEICESTER WASHINDA, CITY WALA KIPORO!

,

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Jumatano 14 Septemba 2016

Matokeo:

KUNDI E

Bayer Leverkusen 2 CSKA 2        

Tottenham 1 Monaco 2                  

KUNDI F

Legia Warsaw 0 Borussia Dortmund 6             

Real Madrid 2 Sporting Lisbon 1               

KUNDI G

Club Brugge 0 Leicester City 3               

FC Porto 1 FC Copenhagen 1        

KUNDI H

Juventus 0 Sevilla 0          

Lyon 3 Dinamo Zagreb 0

KUNDI C

Man City 4 Borussia Monchengladbach 0                      

++++++++++++++++++++++++++++++          

UCL-2016-17-1-2Mechi za kwanza za Makundi ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI ziliendelea Jana na Mabingwa Watetezi Real Madrid kuponyoka kipigo toka Timu ya zamani ya Staa wao Cristiano Ronaldo Sporting Lisbon ya Ureno kwenye Mechi ya Kundi F.

Real walitanguliwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 48 la Bruno Cesar lakini Ronaldo akawasawazishia Dakika ya 89 na Alvaro Morata kuwapa ushindi wa 2-1 kwa Bao la Dakika ya 94.

Nayo ile Mechi ya Kundi C iliyoahirishwa Juzi kutokana na Mvua kubwa Uwanjani Etihad Jijini Manchester ilichezwa Jana na Man City kuitwanga Borussia Monchengladbach 4-0.

Bao za City zilipigwa na Sergio Aguero, Bao 3 moja likiwa la Penati, na Kelechi Iheanacho.

Nayo Tottenham, ikiwa Kundi E na ikicheza 'kwao' Wembley Stadium badala ya White Hart Lane unaofanyiwa ukarabati, ilichapwa 2-1 na AS Monaco.

Monaco walitangulia 2-0 kwa Bao za Dakika za 16 na 31 za Bernardo Silva na Thomas Lemar na Spurs kupata Bao lao Dakika ya 45 kupitia Toby Alderweireld.

Nao Mabingwa wa England Leicester City wameanza Ulaya kwa kushinda Ugenini walipoichapa Club Brigge ya Belgium 3-0.

Bao za Leicester zilufungwa dakika za 5, 29 na 61 ambazo zilifungwa na Marc Albrighton na 2 za Riyad Mahrez moja likiwa la Penati.

Ule mtanange wa Kundi H uliochezwa huko Turin, Italy kati ya Juventus na Sevilla uliisha 0-0.

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Matokeo:

Jumanne 13 Septemba 2016

KUNDI A

Basel 1 Ludo Razgrad 1                 

Paris St Germain 1 Arsenal 1                  

KUNDI B

Benfica 1 Besiktas 1           

Dynamo Kiev 1 Napoli 2               

KUNDI C

Barcelona 7 Celtic 0            

Man City v Borussia Monchengladbach [ILIAHIRISHWA]           

KUNDI D

Bayern Munich 5 FC Rostov 0                   

PSV Eindhoven 0 Atletico Madrid 1

Ratiba:

Jumanne 27 Septemba 2016

KUNDI E

CSKA v Tottenham           

Monaco v Bayer Leverkusen                  

KUNDI F

Borussia Dortmund v Real Madrid          

Sporting v Legia Warsaw            

KUNDI G

FC Copenhagen v Club Brugge              

Leicester City v FC Porto             

KUNDI H

Dinamo Zagreb v Juventus          

Sevilla v Lyon                   

Jumatano 28 Septemba 2016

KUNDI A

Arsenal v Basel                

Ludo Razgrad v Paris St Germaine                   

KUNDI B

Besiktas v Dynamo Kiev             

Napoli v Benfica               

KUNDI C

Borussia Monchengladbach v Barcelona           

Celtic v Man City              

KUNDI D

Atletico Madrid v Bayern Munich            

FC Rostov v PSV Eindhoven        

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MAKUNDI:

Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba

Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba

Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba

Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba

Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba

Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba

MECHI ZA MTOANO:

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

 

 

Wadukuzi wa Urusi wafichua faili zaidi za Wada


Wadukuzi wanaoaminika kutoka Urusi wametoa faili zaidi ya wanariadha zilizoibwa kutoka kwa mamlaka kuu duniani ya kudhibiti utumiaji wa dawa za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha (Wada).

Wanariadha hao wanajumuisha muendeshaji baiskeli wa Uingereza Sir Bradley Wiggins, mwanariadha wa Olimpiki mwenye hadhi kubwa zaidi nchini humo, na bingwa mara nne wa mashindano ya Tour de France Chris Froome.

Hakuna dalili zozote zinazowahusisha wanariadha hao na uhalifu.

Wada inasema kuwa udukuzi wa kimitandao ni jaribio la kudhoofisha mfumo mzima wa dunia wa kukabiliana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha.

Mkurugenzi mkuu wa Wada Olivier Niggli, anakosoa ufujaji wa taaarifa hizo na kusema kwamba "hakuna shaka" udukuzi huo ulikuwa tendo la kulipiza kisasi dhidi ya ripoti ya Wada kwa wanariadha wa Urusi kwamba taifa hilo iliwasaidia wanariadha wake kudanganya huku akiomba utawala nchini Urusi kuzima udukuzi huo.

Rekodi hiyo ilitolewa na kundi moja linalojiita "Fancy Bears" mara nyingi ikishinikiza kile kinachojulikana kama "Therapeutic Use Exemptions" (TUEs) na kukubalia dawa zilizopigwa marufuku kutumika na "wanariadha" ili kuthibitishwa mahitaji ya matibabu.

Kundi hilo linasema kuwa TUEs "imeidhinishwa kutumika" na kwamba Wada "ni fisadi na inaeneza udanganyifu".

Taarifa hiyo inahusisha Wamarekani 10, Waingereza 5 na Wajerumani 5 kwa pamoja na mwanaridha mmoja mmoja kutoka Denmark, Urusi, Poland, Romania na Jamhuri ya Czech.

Miongoni mwa majina hayo kutoka Jamhuri ya Czech ni bingwa mara mbili wa mchezo wa Tennis wa Wimbledon Petra Kvitova na mshindi wa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya olimpiki ya London mwaka 2012, Robert Harting, raia wa Ujerumani.

Orodha hiyo pia inajumuisha majina 11 washindi wa medali mbali mbali katika mashindano ya mbio zilizomalizika hivi majuzi mjini Rio De Jeneiro, likiwemo jina la mmarekani Bethanie Mattek-Sands, ambaye alishinda dhahabu katika mashindano ya tennis inayojumuisha wachezaji wawili.

Ufujaji huu mpya unafuatia mwingine uliotokea hapo awali ambapo taarifa inayohusiana na wanariadha wa Marekani ilitolewa akiwemo mshindi wa dhahahu wa mazoezi ya viungo Simone Biles.

 SHUKRANI ZANGU KWA BBC SWAHILI ,MPEKUZI,MAMBOMOTOMOTO YA SOKA ,SHAFF DAUDA,SALEHE JEMBE NA BIN ZUBERY AMBAO NDIO CHANZO CHA HABARI HIZI ZOTE ZA KIMICHEZO HABARI ZA KIJAMII  LAKINI PIA NA DW HABARI ZA ULIMWENGU ,

 USISAHAU KUTEMBELEA BLOG HII ILI UWEZE  KUHABARIKA ,

Reviewed by RICH VOICE on Septemba 15, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...