Liverpool waanza mazungumzo kuhusu Oxlade-Chamberlain


 Alex Oxlade-Chamberlain

Liverpool wameanza mazungumzo na Arsenal kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Alex Oxlade-Chamberlain.
Mchezaji huyo wa miaka 24 alikataa kuhamia Chelsea Jumanne hata baada ya klabu hizo kuafikiana kuhusu uhamisho wake wa £40m.
Oxlade-Chamberlain anayechezea timu ya taifa ya England anataka kucheza kama kiungo katika safu ya kati na anahisi kwamba anaweza akapata nafasi Anfield.
Alikataa kuhamia Chelsea baada ya kugundua kwamba huenda wakataka kumtumia katika upande wa kushoto uwanjani.
Bado haijabainika iwapo Liverpool watafikia dau ambayo Chelsea walikuwa wamewasilisha.
Oxlade-Chamberlain anatumikia mkataba wake wa mwisho Emirates na amechezea mechi zote nne za Arsenal msimu huu licha yake kumwambia meneja Arsene Wenger kwamba hatatia saini mkataba mpya.
Alishangiliwa na wachezaji wa Liverpool alipoondolewa uwanjani wakati wa mechi ya Jumapili ambayo Arsenal walilazwa 4-0 uwanjani Anfield Jumapili.
Liverpool waanza mazungumzo kuhusu Oxlade-Chamberlain Liverpool waanza mazungumzo kuhusu Oxlade-Chamberlain Reviewed by RICH VOICE on Agosti 30, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...