Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Makongoro Mahanga Akamatwa kwa Amri ya Mahakama Kuu


Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani.

Mahakama iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba Msemakweli Sh14 milioni.

Fedha hizo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada ya kushinda kesi ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja kwenye kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”.

Katika kitabu hicho anamtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye shahada za udaktari wa kughushi.

Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6 milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.
Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Makongoro Mahanga Akamatwa kwa Amri ya Mahakama Kuu Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Makongoro Mahanga Akamatwa kwa Amri ya Mahakama Kuu Reviewed by RICH VOICE on Agosti 31, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...