NABII MKUU MH DK GEODAVIE AMEWATAKA WATU KUWA NA UWEZO MZURI WA AKILI ZA ROHONI NA AKILI ZA MWILINI.





Watu wametekiwa kuwa na akili za rohoni na mwilini ili waweze kufanikiwa katika maeneo mbalimbali maishani.

Nabii mkuu Mh Dk GeoDavie  ameyasema hayo katika ibada ya jiji chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika hema la kukutania kisongo arusha ambapo amesema kila kitu kilichofanyika vizuri huwa kinakuwa na maandalizi mazuri.

Pia amesema kuwa katika maisha watu wanatakiwa waendeshe akili mbili za rohoni na akili za mwilini ili waweze kufanikiwa katika mambo mbalimbali maishani.
Katika ibada hiyo Nabii mkuu Mh Dk GeoDavie  ametangaza kuwepo hemani jumapili ijayo ambapo amesema itakuwa ni jumapili ya kusanyiko huku akiwagiza watu kuja na sadaka maalumu  kwa ajili ya kufanyika kichwa kwa akili za rohoni na akili za mwilini.
Nabii mkuu Mh Dk GeoDavie  ametoa wito kwa watu wote kuhudhuria ibada hiyo kwani itakuwa ni siku ya muhimu kwa kila Mtu


Kwa upande wa watu waliohudhuria ibada ya chuo kikuu cha manabii wamesema kuwa wamebarikiwa sana.
NABII MKUU MH DK GEODAVIE AMEWATAKA WATU KUWA NA UWEZO MZURI WA AKILI ZA ROHONI NA AKILI ZA MWILINI. NABII MKUU MH DK GEODAVIE  AMEWATAKA WATU KUWA NA UWEZO MZURI WA AKILI ZA ROHONI NA AKILI ZA MWILINI. Reviewed by RICH VOICE on Agosti 30, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...