Baada ya wigi kumvuka ghafla hadharani, Lady Jaydee anena


Mwanamuziki Lady Jaydee amezungumza ishu ya wigi kumvuka ghafla wakati akicheza.

Kitu hicho kinaonekana katika video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Anaweza ambao amemshirikisha msanii mkongwe kutoka nchini Jamaica, Luciano.
“Lilianguka, (anacheka) ilikuwa kwamba lilianguka chini, ni ajali kazini,” Lady Jaydee ameiambia Bongo5.
Hata hivyo ukitazama video ya wimbo huo kwa makini utagundua ulikuwa ni mpango wa makusudi ili Lady Jadee kuondoka katika scene hiyo na kupisha madansa katika video hiyo kuendelea na shughuli yao.
Video Player
00:00
00:14
Katika hatua nyingine Lady Jaydee alizungumza kuhusu project mpya baada ya Anaweza.
“Kwa sababu ndio kwanza project imetoka hautakiwi kuongelea project ya mbele wanatakiwa wafurahie hii baada ya kuwa wamechoka basi tutazungumza kuhusiana na projet mpya,” alisema.
Baada ya wigi kumvuka ghafla hadharani, Lady Jaydee anena Baada ya wigi kumvuka ghafla hadharani, Lady Jaydee anena Reviewed by RICH VOICE on Aprili 10, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...