Nisher na Gabo kufanya filamu



Kama unakumbuka mwaka 2016 Nisher alitoa filamu fupi iliyokwenda kwa jina la Alex, Director huyo wa video za muziki Bongo amefunguka mipango ya kufanya filamu na muigizaji Gabo Zigamba.

Nisher amesema hana mpango wa kuingia kwenye Bongo Movie ila ana mpango wa kufanya filamu refu yenye urefu wa kuanzia dakika 100.
“Bado tupo kwenye malumbano na kaka yangu Gabo Zegamba, siku hiyo amenicheki nipo Arusha akasema Nisher naitwa Gabo tukapiga stori. Kwangu mimi amenionyesha ni mtu myenyekevu, msikivu, ameniheshimu sana, mpaka leo tupo close sana japo hapa kati amekuwa buys kidogo lakini ni mtu poa sana” Nisher ameiambia Bongo5.
“Kwa hiyo tunaangalia ni kitu gani tunaweza kukifanya kupitia yeye na wenzake kwa sababu ana connection nyingi sana na Bongo Movie, mimi sitaki kufanya Bongo Movie nataka kufanya filamu na ndio hicho tunajaribu kufanya na Gabo,” amesisitiza.

Nisher na Gabo kufanya filamu Nisher na Gabo kufanya filamu Reviewed by RICH VOICE on Aprili 04, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...