JERRY TEGETE ATOA NENO KUHUSU MAJIMAJI KUSHUKA DARAJA


Licha ya kuwa Majimaji inaelekea kubaya na ikiwa na dalili za kushuka daraja kutoka Ligi Kuu ya Vodacom, straika wa timu hiyo, Jerry  Tegete amefunguka kuwa
anaamini wataendelea kupigana na ikiwezekana kuikoa timu hiyo.
Katika mchezo uliopita, Majimaji ilifungwa mabao 3-2, wikiendi iliyopita jana, ilipokutana na Mwadui FC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo ibaki mkiani ikibaki na pointi 16 baada ya kucheza mechi 23.
“Kwa kweli anko hali ni mbaya lakini bado hatujakata tamaa, tutaendelea kupigana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha tunainusuru timu isishuke,” alisema straika huyo wa zamani wa Yanga ambaye ni mwenyeji wa Mwanza.
JERRY TEGETE ATOA NENO KUHUSU MAJIMAJI KUSHUKA DARAJA  JERRY TEGETE ATOA NENO KUHUSU MAJIMAJI KUSHUKA DARAJA Reviewed by RICH VOICE on Aprili 09, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...