Mustakabali wa Syria kujadiliwa Uturuki


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatazamia kuwapokea leo Jumatano marais wenzake kutoka Irani, Hassan Rohani, na Urusi, Vladimir Putin, washirika wawili muhimu wa Syria. Viongozi hao watajadili mustakabali wa Syria iliyoharibiwa na vita kwa muda wa miaka saba.
Viongozi hao watatu ni washirika muhimu wa rais wa Syria Bashar Al Assa. Mkutano huo ni uendelezaji wa mchakato wa Astana, ambao haujumuishi Washington na unakinzana na mazungumzo ya Umoja wa Mataifa.
Mchakato huu, uliozinduliwa na nchi hizi tatu mnamo mwezi Januari 2017, ulipelekea kufikiwa makubaliano kuhusu kutengwa kwa "maeneo manne yanayokabiliwa na vita" nchini Syria. Lakini kama vurugu zitasambaa katika baadhi ya maeneo, zoezi la hivi karibuni la kuwaondoa raia waliokwama katika eneo la Ghouta Mashariki, linalokabiliwa na mashambulizi ya Urusi na Syria, na kuendelea kwa mashambulizi ya anga katika mkoa wa Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria, linaweza kusitishwa mara moja, kwa mujibu wa chanzo cha usalama kutoka Syria.
"Maswali haya yote yatawekwa kwenye meza," chanzo rasmi kutoka Uturuki kimesema. Uturuki, ambayo ina msimamo wake wa dhidi ya Assad, pia inatarajia "kushinikiza Urusi kutoa ulinzi katika zoezi la kuhamisha watu waliokwama katika maeneo yanayokabiliwa na vita vinavyoendelea," chanzo hicho kimeongeza. Kwa mujibu wa chanzo hiki, suala la kuundwa kwa "kamati ya kikatiba", ambayo tayari lilijadiliwa katika mkutano wa mwisho uliofanyika katika mji wa Sochi, nchini Urusi, limo kwenye ajenda ya mkutano huo. "Tulijadili suala la kuundwa taasisi ya watu 150 kutoka Syria, ambapo kila nchi tatu zilitoa majina ya watu 50," chanzo hiki kimeendelea.
Mgawanyiko wa maslahi
Lakini suala la kutafuta suluhu ya mgogoro wa Syria, ambapo upinzani wa Syria umeendelea kugawanyika na kuwa dhaifu, limeendelea kuzua tofauti ya maslahi kati ya Moscow, Ankara na Tehran.
media
Mustakabali wa Syria kujadiliwa Uturuki Mustakabali wa Syria kujadiliwa Uturuki Reviewed by RICH VOICE on Aprili 04, 2018 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...