Donald Trump amuonya Kim Jong-Un moja kwa moja
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un katika hotuba ndani ya bunge la Korea Kusini.
''Usitudharau, Usitujaribu," alisema, huku akishutumu hali ilivyo nchini Korea Kaskazini.
Bwana Trump alimzungumzia moja kwa moja rais Kim akisema kuwa ''silaha unazojilimbikia hazikufanyi wewe kuwa salama lakini zinakuweka katika hali hatari''.
Kiongozi huyo wa Marekani yuko katika ziara ya siku mbili nchini Korea Kusini katika ziara ya bara Asia.
Kwengineko katika hotuba yake amesema kuwa huku Korea Kaskazini ikiona uvumilivu kuwa udhaifu sasa kuna utawala mpya nchini Marekani.
Bwana Trump pia ameutaka ulimwengu hususan China na Urusi kuiwekea shinikizo kali Pyongyang kusitisha utengenezaji wake wa silaha za kinyuklia.
Dunia haiwezi kuvumilia hatari inayosababishwa na taifa linaloongozwa na utawala usioaminika ambao unaitishia na silaha za kinyuklia.
Mataifa yote yaliowajibika yanafaa kuungana kuangamiza utawala wa kikatili wa Korea Kaskazini kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeuunga mkono, kupata usaidizi wowote ama hata kukubalika, alisema.
Donald Trump amuonya Kim Jong-Un moja kwa moja
Reviewed by RICH VOICE
on
Novemba 08, 2017
Rating:
Hakuna maoni