Wanachuo Zimbabwe waandamana dhidi ya Mugabe

Wanachuo nchini Zimbabwe wamefanya maandamano katika kuonyesha upinzani wao kwa rais wa nchi hiyo.Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Harare mji mkuu wa Zimbabwe wameandamana dhidi ya Mugabe aliye na miaka 93 huku wakipiga nara dhidi ya kiongozi huyo wakimtaka aondoke madarakani. Viongozi wa chuo hicho kikuu cha mjini Harare wamesema kuwa wameakhrisha mitihani iliyotazamiwa kufanywa chuoni hapo hadi wakati mwingine. Jeshi la Zimbabwe Jumatano tarehe 15 mwezi huu lilitangaza kuwa Mugabe na familia yake wapo katika kifungo cha nyumbani na kisha kumuondoa uongozini. Jeshi la Zimbabwe lilichukua hatua hiyo kama radiamali kwa hatua ya siku kadhaa zilizopita iliyochukuliwa na Mugabe ya kumuuzulu aliyekuwa Makamu wake Emmerson Mnangagwa ili aweze kumrithisha nafasi hiyo mkewe  Bi Grace Mugabe. 
Grace Mugabe, Mke wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe 
Ilitazamiwa kuwa Robert Mugabe angetangaza kujiuzulu kiti cha urais baada ya kuwa madarakani kwa miaka 37 kupitia hotuba yake ya jana usiku, hata hivyo hakuashiria suala hilo katika hotuba hiyo. 
Wanachuo Zimbabwe waandamana dhidi ya Mugabe Wanachuo Zimbabwe waandamana dhidi ya Mugabe Reviewed by RICH VOICE on Novemba 20, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...