Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran: Saudi Arabia ni mhimili wa shari katika eneo
Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran ameitaja Saudi Arabia kuwa mhimili wa Shari na kusisitiza juu ya ulazima wa kusimama kidete mbele ya njama mbovu na za kifisadi za Marekani na waitifaki wake katika eneo hili la Mashariki ya Kati kwa kuwepo umoja na kushikamana zaidi watu wa eneo hili.
Akizungumza leo katika kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa Idara ya Mahakama, Ayatullah Sadiq Amoli Larijani ameshiria hali mbaya waliyonayo wananchi wa Yemen na kuongeza kuwa mauaji ya kinyama yanayofanywa na Saudi Arabia dhidi ya wananchi wanaodhulimika wa Yemen ni mfano wa wazi wa jinai za kivita na natija ya kuzingirwa nchi hiyo kama zilivyokiri taasisi za kimataifa na Umoja wa Mataifa kuwa kinachojiri Yemen ni maafa ya kibinadamu na jinai dhidi ya binadamu.
Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran ameashiria pia kimya cha Jumuiya za Kutetea Haki za Binadamu kuhusu jinai za Saudi Arabia huko Yemen na kueleza kuwa nchi za Magharibi ikiwemo Marekani zinaunga mkono jinai hizo dhidi ya wananchi wa Yemen; kwani uuzaji silaha chungu nzima kwa Saudia unathibitisha kuwa Marekani ndiyo inayotekeleza jinai hizo.
Ayatullah Larijani amezipongeza serikali, wananchi na marjaa wa Iraq na vile vile wananchi na serikali ya Syria kwa kuondoa magaidi wa Daesh katika miji ya Iraq na Syria na kueleza kuwa, shari ya kundi hilo la kigaidi ambalo Marekani inadai kuwa imekuwa ikipambana dhidi yake imepungua katika kipindi kifupi kwa raia wa eneo hilo kutokana na misaada na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu na mhimili wa muqawama.
Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran: Saudi Arabia ni mhimili wa shari katika eneo
Reviewed by RICH VOICE
on
Novemba 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni