Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 23.11.2017
Arsene Wenger anatamka mkufunzi wa Feyenoord Giovanni van Bronckhorst kuwa mrithi wake kama mkufunzi wa Arsenal. (Daily Star)
Real Madrid wanatumai wataishinda Manchester City katika kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28. (Don Balon, via Daily Express)
Paris St-Germain huenda ikamtaka Sanchez katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku kandarasi ya mshambuliaji huyo wa Chile ikitarajiwa mwishoni mwa msimu(Daily Mirror)
Everton hawana matumaini tena ya kumsajili mkufunzi wa Warford Marco Silva kama mkufunzi wake mpya. (Independent)
The Toffees wanataka kumuajiri mkurugenzi wa michezo wa klabu ya RB Lipzig Ralf Rangnick badala yake (Express)
West Brom huenda wakafeli katika harakati zao za kutaka kumuajiri Sam Allardyce kama mkufunzi wake mpya.Mkufunzi huyo ana hamu ya kurudi kufunza timu za kimataifa.. (Daily Mirror)
Mkufunzi wa klabu ya Hull Leonid Slutsky anajaribu kuokoa kazi yake baada ya klabu hiyo kurekodi matokeo mabaya katika ligi hiyo ya mabingwa. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 24, na kiungo wa kati Dele Alli, 21, ni miongoni mwa wachezaji watano wanaosakwa na rais wa klabu hiyo Florentino Perez. (Diario Gol, via Daily Mail)
Manchester City wanapanga kumnunua winga wa Leicester City Riyad Mahrez, 26. (Don Balon, kupitia Manchester Evening News)
The Foxes watamuuza mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa, 25,mshambuliaji wa Argentina Leonardo Ulloa, 31, pamoja na beki wa Tunisia Yohan Benalouane, 30, mnamo mwezi Januari. (Daily Mirror)
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amezuia hatua ya klabu hiyo kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 29. (Diario Gol, via Daily Star)
Liverpool imewasiliana na PSG kuhusu uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Ujerumani Julian Draxler, 24. (L'Equipe, via Talksport)
Mkufunzi wa zamani wa West Ham, Newcastle na Crystal Palace boss Alan Pardew ndio anayepigiwa upato kumrithi Tony Pulis katika klabu ya West Brom. (Birmingham Mail)
Arsenal huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ureno Joao Mario kwa kitita cha £26m mnmao mwezi Januari. (Tuttosport, via Sun)
Sampdoria haitamuuza kiungo wake wa kati mwenye umri wa miaka 21 Lucas Totteira kueleka Everton mwezi Januari. (La Repubblica via Talksport)
Mchezaji anayelengwa na Manchester City Joshua Kimmich, kiungo wa kati mwenye umri wa 22 kutoka Ujerumani anaendelea na majadiliano na klabu yake ya sasa Bayern Munich. (Bild, via Sun)
Liverpool na Tottenham ni miongoni mwa vilabu vinavyomsaka kinda wa timu ya Stevenage katika ligi ya daraja la pili ya Uingereza Ben Wilmot. (Daily Mail)
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 23.11.2017
Reviewed by RICH VOICE
on
Novemba 23, 2017
Rating:
Hakuna maoni