Mamilioni Yemen yamkini wakafariki kutokana na mzingiro uliowekwa na Saudia
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Dunaini, WFP, limeonya kuwa mamilioni ya watu wa Yemen wanakabiliwa na hatari ya mauti kufuatia mzingiro uliowekwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo na hivyo kuzuia misaada kuwafikia wanaohitajia.
Katika taarifa mkuu wa WFP amesema mamilioni ya watu Yemen sasa wanategemea misaada ya kibinadamu ili kuendelea kuishi.
Ameongeza kuwa kati ya watu wote milioni 26 wa Yemen, milioni 17 hawajui mlo wao ujao utatoka wapi huku milioni saba kati yao wakitegemea kikamilifu misaada ya chakula.
Novemba 6 Saudi Arabia ilitangaza kufunga mipaka yote ya anga, nchi kavu na baharini ya Yemen baada ya wapiganaji wa Yemen kuvurumisha kombora hadi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Riyadh ikiwa ni katika oparesheni ya kulipiza kisasi jinai za Saudia dhidi ya Wayemen.
Saudia ilianzisha hujuma yake dhidi ya Yemen mnamo Machi mwaka 2015 kwa uungaji mkono wa Marekani kwa lengo la kuirejesha madarakani serikali kibaraka ya Abdu Rabuh Mansour Hadi aliyejiuzulu urais na kukimbilia mji mkuu wa Saudia, Riyadh. Hivi sasa Saudia inadhibiti mipaka yote ya Yemen na kutumia uwezo huo kuzuia misaada kuwafikia mamilioni ya watu wa nchi hiyo wanaokabiliwa na njaa.
Raia zaidi ya elfu 13 wa Yemen wameuawa, hasa wanawake na watoto, na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika uvamizi huo wa kijeshi huku Umoja wa Mataifa ukishindwa kuchukua hatua yoyote ya kuzuia jinai hizo za Saudia huko Yemen. Aidha watu zaidi ya laki sita wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kote Yemen huku wengine zaidi ya 2,000 wakifarikia dunia tokea mwezi Aprili mwaka huu.
Mamilioni Yemen yamkini wakafariki kutokana na mzingiro uliowekwa na Saudia
Reviewed by RICH VOICE
on
Novemba 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni