Raia 2 wa Tanzania na 10 wa Iran wakamatwa kwa dawa za kulevya

Maboti yanayojulikana kama dhow huonekana katika pwani ya bahari ya Tanzania

Image captionMaboti yanayojulikana kama dhow huonekana katika pwani ya bahari ya Tanzania
Raia 10 wa Iran na wawili wa Tanzania wameshtakiwa kwa kuingiza kinyume na sheria takriban kilo 100 za dawa za kulevya aina ya heroine kupitia bahari hindi kulingana na gazeti la The Citizen nchini tanzania.
Kulingana na gazeti hilo 12 hao walikamatwa wakiabiri boti kwa jina dhow lililobeba dawa hiyo katika pwani ya Zanzibar Jumanne iliopita wakati maafisa wa shirika la kukabiliana na mihadarati wakishirikiana na maafisa wa usalama walipokuwa wakipiga doria za vita dhidi ya dawa za kulevya.
Mahakama ya eneo la Kisutu iliambiwa kwamba washukiwa hao walikamatwa katika maji ya Tanzania mnamo tarehe 25 mwezi Novemba walipokuwa wakipenyeza kilo 111.2 za dawa ya heroine , iliochanganywa na bangi .
Hakimu wa mahakama hiyo alikataa ombi la washukiwa hao kuachiliwa kwa dhamana.
Wakati wa kukamatwa kwao katika maji makuu , washukiwa hao walidaiwa kutaka kubadili mwelekeo baada ya kubaini kwamba wamenaswa lakini hawakuweza kutoroka mbali kabla ya meli ya wanamaji kuwakamata.
Gazeti hilo limesema kuwa ni kiwango kikubwa cha dawa za kulevya ambazo zimepatikana tangu shirikisho hilo la kubaliana na dawa za kulevya kubuniwa mnamo mwezi Aprili.
Mkuu wa shirika hilo la kukabiliana na dawa za kulevya liliambia gazeti hilo kwamba dawa hizo zilikuwa zikipakiwa wakati meli hiyo ya wanamaji ilipowasili
Raia 2 wa Tanzania na 10 wa Iran wakamatwa kwa dawa za kulevya Raia 2 wa Tanzania na 10 wa Iran wakamatwa kwa dawa za kulevya Reviewed by RICH VOICE on Novemba 01, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...