Utafiti: Ngono haichangii sana mshutuko wa moyo

Couples feet in bed

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUtafiti: Ngono haiwezi kusababisha mshutuko wa moyo
Mshutuko wa ghafla wa moyo unaotokana na tendo la ngono unaweza kutokea zaidi miongoni mwa wanaume kuliko kwa wanawake, kwa mujibu wa utafiti.
Lakini hata hivyo pia kuna uwezekano mdogo kwa ngono kusababisha mshutuko wa moyo
Ni asilimia 34 ya visa 4,557 vya mshutuko wa moyo vilivytokea wakati wa tendo la au baada ya saa moja ya ngono na 32 kati ya wale walioathiriwa walikuwa ni wanaume.
Dr Sumeet Chugh, kutoka taasisi ya moyo ya Cedars-Sinai, anasema utafiti huo ndio wa kwanza kubaini ikiwa tendo la ngono linaweza kusababisha mshtuko wa moyo.
Hali hiyo hutokea wakati moyo unakumbwa matatizo na kuacha kupiga.
Dr Chugh na wenzake huko California walikagua rekodi za hospitali kuhusu kesi za mshutuko wa moyo kwa watu wazima kati ya mwaka 2002 na 2015 huko Portland, Oregon.
Ngono ilichangia chini ya asilimia moja ya visa hivyo. Wengi walikuwa ni wanaume walio katika umri wa makamo.
Utafiti: Ngono haichangii sana mshutuko wa moyo Utafiti: Ngono haichangii sana mshutuko wa moyo Reviewed by RICH VOICE on Novemba 13, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...