Emmerson Mnangagwa anayetarajiwa kumrithi Mugabe ataapishwa Ijumaa

Emmerson Mnangagwa

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionEmmerson Mnangagwa alikuwa mshirika wa Mugabe wakati mmoja lakini pia hasimu mkubwa wa Grace Mugabe ambaye pia alitarajia kumrithi Mugabe
Makamu wa zamani wa rais wa Zimbabwe, ambaye kufutwa kwake kazi kulishababisha kujiuzulu kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, ataapishwa rasmi Ijumaa, limesema shirika la utangazaji la Zimbabwe (ZBC)
Emmerson Mnangagwa, aliyetorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo Jumatano nchini , kulingana na Zanu-PF.
Robert Mugabe
Image captionAliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Kuondoshwa kwake madarakani kulisababisha chama na jeshi kwa pamoja kuingilia kati na kulazimisha kumalizika kwa utawala wa miaka 37 wa Bwana Mugabe.
Taarifa kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amejiuzulu zilikuja kwa njia ya barua iliyosomwa bungeni Jumanne , bunge likalazimika kuahirisha mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa dhidi yake.
Taarifa hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane:
Raia wa Zimbabwe wakisherekea kujiuzulu kwa MugabeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTaarifa ya kujiuzulu kwa Bwana Mugabe iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane
Rais wa Zimbabwe walishangilia kujiuzulu kwa Mugabe mjini HarareHaki miliki ya pichaAFP
Image captionIlikuwa ni vifijo, nderemo na nyimbo za shangwe katika mji mkuu Harare usiku kucha kufuatia kujiuzulu kwa kiongozi wa taifa hilo wa muda mrefu Robert Mugabe
Baadhi ya rais walipeperusha bendera ya ZimbabweHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBaadhi ya raia wenye furaha walipeperusha bendera ya taifa la Zimbabwe
Asakari wa Zimbabwe pia walisherehekea kujiuzulu kwa Bwana MugabeHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wa Zimbabwe pia waliungana na raia kwenye mitaa ya mji mkuu Harare kusherehekea kujiuzulu kwa Robert Mugabe
Katika barua hiyo , Bwana Mugabe alisema kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kuruhusu ukabidhianaji wa mamlaka wa amani, na kwamba uamuzi umetokana na utashi wake mwenyewe.
Msemaji wa Zanu-PF alisema kuwa Bwana Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 71, atahudumu katika kipindi kilichokuwa kimebakia cha utawala wa Mugabe hadi utakapofanyika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Septemba 2018.
Emmerson Mnangagwa anayetarajiwa kumrithi Mugabe ataapishwa Ijumaa Emmerson Mnangagwa anayetarajiwa kumrithi Mugabe ataapishwa Ijumaa Reviewed by RICH VOICE on Novemba 22, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni

Chapisho Lililoangaziwa

Thursday, September 15, 2016 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Septemba 15 ...