Papa Francis aanza ziara Myanmar
Papa Francis ameanza ziara yake nchini Myanmar, ambapo amekutana na mkuu wa jeshi katika siku ya kwanza ya ziara yake katika nchi inatuhumiwa kutokana na vitendo wanavyofanyiwa watu wa jamii ya Kiislam ya Rohingya.
Generali Aung Hlaing ametupilia mbali madai kuwa kuna ubaguzi wa kidini katika operesheni za kijeshi zinazoendelea katika jimbo la Rakhine.
Hata hivyo maofisa wengi kutoka jamii wa watu wa Budha nchini humo wanasubiria kuona kama Papa atazungumzia vipi mgogoro wa Rohingya.
Kumekuwa na msukumo mkubwa dhidi ya papa Francis kutoka serikali za mataifa mengine na makundi ya haki za binadamu kuhakikisha anaweka msukumo kuhusiana na suala la Rohingya.
Zaidi ya watu laki sita wamekimbia kutoka Myanmar na kwenda nchi jirani Burma na Bangaladesh tangu mwezi Agosti kutokana na mauajia yanayodaiwa kufanywa na jeshi.
Papa Francis aanza ziara Myanmar
Reviewed by RICH VOICE
on
Novemba 28, 2017
Rating:
Hakuna maoni